Fifa-CWC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 16 Jul 2025 07:41:06 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Fifa-CWC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Chelsea yabeba taji la dunia https://www.greensports.co.tz/2025/07/15/chelsea-yabeba-taji-la-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2025/07/15/chelsea-yabeba-taji-la-dunia/#respond Tue, 15 Jul 2025 19:57:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13729 New Jersey, MarekaniChelsea imefanikiwa kubeba taji la michuano ya Fifa ya Klabu ya Dunia baada ya kuilaza PSG mabao 3-0 katika mechi ya fainali iliyopigwa Jumapili hii Julai 13, 2025.Ushindi wa Chelsea ni tukio ambalo halikutarajiwa kwani timu hiyo haikuwa kati ya timu zilizopewa nafasi ya kubeba taji la michuano hiyo iliyoshirikisha timu kadhaa kubwa […]

The post Chelsea yabeba taji la dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
New Jersey, Marekani
Chelsea imefanikiwa kubeba taji la michuano ya Fifa ya Klabu ya Dunia baada ya kuilaza PSG mabao 3-0 katika mechi ya fainali iliyopigwa Jumapili hii Julai 13, 2025.
Ushindi wa Chelsea ni tukio ambalo halikutarajiwa kwani timu hiyo haikuwa kati ya timu zilizopewa nafasi ya kubeba taji la michuano hiyo iliyoshirikisha timu kadhaa kubwa zikiwamo, Real Madrid na Bayern Munich.
Shujaa wa Chelsea katika mechi hiyo alikuwa ni kiungo Cole Palmer ambaye alifunga mabao mawili dakika za 22 na 30 kabla ya kuwa mpishi wa bao la tatu lililofungwa na Joao Pedro dakika chache kabla ya timu kwenda mapumziko.
PSG ndiyo iliyopewa nafasi kubwa ya kubeba taji hilo hasa baada ya kubeba taji la Ligi 1 ya Ufaransa na Ligi ya Mabingwa Ulaya na matarajio yaliyokuwa kwa timu hiyo kubeba taji la tatu.
Matumaini ya PSG chini ya kocha Luis Enrique hata hivyo yalizimwa na Chelsea ambao sasa wameweka historia ya kubeba taji hilo katika michuano ambayo inafanyika mara ya kwanza katika mfumo mpya unaoshirikisha timu nyingi.
Katika mechi hiyo, kocha wa Chelsea, Enzo Maresca alifanya mabadiliko ya wachezaji wawili katika kikosi kilichocheza nusu fainali, akiwapa nafasi Levi Colwill na Reece James badala ya Tosin Adarabioyo na Christopher Nkunku.
Mabadiliko hayo yaliipa faida timu hiyo ambayo ilionekana kuwa tishio zaidi huku Palmer akionesha mapema alivyopania kuipa ushindi timu yake katika dakika ya saba baada ya mpira alioupiga kwa mguu wa kushoto kutoka nje.
PSG nao walianza kuja juu baada ya kushtuliwa na kama si umahiri wa beki Marc Cucurella kuzuia pasi hatari iliyopigwa na Desire Doue kwenda kwa Achraf Hakimi mambo yangekuwa mabaya kwa Chelsea.

“Tunajisikia vizuri, kocha alikuja na mpango mzuri, alijua wapi kulikuwa na nafasi na alijitahidi kunifanya niwe huru kadri ilivyowezekana, nami nikamjibu kwa kufunga mabao,” alisema Palmer.


Naye kocha Maresca alisema kwamba hana la kusema zaidi kwa wachezaji wake na kilichotokea ni kwamba walishinda mechi hiyo katika dakika kumi za kwanza na walijua jinsi walivyotaka kucheza.
Mechi hiyo ya fainali ilihudhuriwa na Rais wa Marekenia, Donald Trump ambaye ndiye aliyewakabidhi Chelsea taji hilo na alitajwa kama mgeni wa Rais wa Fifa, Gianni Infantino.
Fainali za michuano hiyo ya Fifa zimekamilika nchini Marekani kukiwa na malalamiko ya baadhi ya klabu kutaka zifutwe kwa kuwa zinavuruga ratiba za soka na kuwachosha wachezaji huku mechi zake zikishindwa kuvutia mashabiki wengi.

The post Chelsea yabeba taji la dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/07/15/chelsea-yabeba-taji-la-dunia/feed/ 0
Klopp aponda Kombe la Dunia la Klabu https://www.greensports.co.tz/2025/06/29/klopp-aponda-kombe-la-dunia-la-klabu/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/29/klopp-aponda-kombe-la-dunia-la-klabu/#respond Sun, 29 Jun 2025 17:48:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13683 Florida, MarekaniAliyekuwa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema anaamini wazo la kuanzishwa michuano ya Fifa ya Kombe la Dunia la Klabu inayoshirikisha timu nyingi ni la hovyo.Klopp mara kwa mara amekuwa akilalamikia kuhusu ratiba za msimu mmoja zinavyokuwa na mzigo wa mechi nyingi na jinsi mechi hizo zinavyochosha wachezaji.Siku kadhaa kabla ya kuanza kwa michuano […]

The post Klopp aponda Kombe la Dunia la Klabu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Florida, Marekani
Aliyekuwa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema anaamini wazo la kuanzishwa michuano ya Fifa ya Kombe la Dunia la Klabu inayoshirikisha timu nyingi ni la hovyo.
Klopp mara kwa mara amekuwa akilalamikia kuhusu ratiba za msimu mmoja zinavyokuwa na mzigo wa mechi nyingi na jinsi mechi hizo zinavyochosha wachezaji.
Siku kadhaa kabla ya kuanza kwa michuano ya Fifa ya Kombe la Dunia la Klabu, Umoja wa Wanasoka Profesheno ulitioa ripoti na kusema kwamba wachezaji wanahitaji walau kuwa na wiki nne za mapumziko katika msimu mmoja.
Mwaka huu kwa mara ya kwanza michuano hiyo inayosimamiwa na Fifa imeshirikisha timu 32 na inahusisha mechi 48 ambapo timu ya Salzburg Red Bull, moja ya timu ambazo Klopp ni kiongozi tayari imetolewa katika hatua ya makundi.
Akizungumzia ubaya wa michuano hiyo, Klopp alisema kinachoangaliwa ni mechi tu na si mazingira ya matukio husika na ndio maana anaamini michuano hiyo ni wazo la hovyo kuwahi kufanywa katika soka.

“Watu ambao hata mara moja hawajawahi kuwa na kitu cha kufanya katika shughuli za kila siku ndio wanaokuja na mawazo yao, kuna ukichaa wa pesa katika ushiriki lakini pia si kwa kila timu,” alisema Klopp.


Akifafanua zaidi Klopp alisema mwaka jana kulikuwa na Copa America na michuano ya Ulaya na mwaka huu ni Kombe la Dunia la Klabu na mwakani ni Kombe la Dunia.
Klopp anaamini kuwapo kwa ratiba ya aina hiyo maana yake ni kwamba kwa wachezaji hakuna kupumzika kimwili na hata kiakili.

The post Klopp aponda Kombe la Dunia la Klabu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/29/klopp-aponda-kombe-la-dunia-la-klabu/feed/ 0
Alaba kukosa michuano ya Klabu Fifa https://www.greensports.co.tz/2025/06/28/alaba-kukosa-michuano-ya-klabu-fifa/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/28/alaba-kukosa-michuano-ya-klabu-fifa/#respond Sat, 28 Jun 2025 10:54:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13675 Florida, MarekaniBeki wa kati wa Real Madrid, David Alaba (pichani) amepata matatizo ya misuli na huenda akakosa kuiwakilisha timu yake kwenye michuano ya Fifa ya Klabu ya Dunia inayoendelea nchini Marekani.Habari kuhusu matatizo ya Alaba zimethibitishwa na klabu hiyo Ijumaa hii na imeelezwa kuwa beki huyo mkongwe mwenye miaka 33 ataanza kwa kuikosa mechi ya […]

The post Alaba kukosa michuano ya Klabu Fifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Florida, Marekani
Beki wa kati wa Real Madrid, David Alaba (pichani) amepata matatizo ya misuli na huenda akakosa kuiwakilisha timu yake kwenye michuano ya Fifa ya Klabu ya Dunia inayoendelea nchini Marekani.
Habari kuhusu matatizo ya Alaba zimethibitishwa na klabu hiyo Ijumaa hii na imeelezwa kuwa beki huyo mkongwe mwenye miaka 33 ataanza kwa kuikosa mechi ya Jumanne dhidi ya Juventus.
Matatizo ya beki huyo ni mwendelezo wa majanga yanayomuandama kwani tayari alishazikosa mechi tatu za michuano hiyo wakati akiuguza maumivu ya goti la kushoto aliyoyapata mwezi Aprili.
Kama mambo yatakwenda vizuri baada ya mechi hiyo ya Jumanne, Real Madrid itacheza mechi ya robo fainali Julai 5 na kufuatiwa na nusu fainali Julai 9 na fainali Julai 13.

“David anachukua muda mrefu kidogo, baada ya kufanyiwa operesheni tunahitaji kuwa makini na wenye kusubiri, hatua moja hadi nyingine, tutasubiri zaidi,” alisema kocha wa Real Madrid, Xabi Alonso.


Katika michuano hiyo ya Fifa, Real Madrid inashiriki bila ya wachezaji wake tegemeo wa kikosi cha kwanza ambao ni Eder Militao, Dani Carvajal na Eduardo Camavinga ambao wanaendelea na mazoezi ya kujiweka fiti.
Wachezaji wengine ambao ni majeruhi ambao pia inaelezwa wanatarajiwa kupona na kurudi uwanjani ni Ferland Mendy na Endrick ambao kwa sasa wapo Madrid wakipambana kujiweka fiti.
Akiwazungumzia wachezaji hao, Alonso hata hivyo alisema Ferland bado ana muda mrefu hadi kupona wakati matumaini makubwa ya kupona na kuwa fiti yapo kwa Eduardo.

The post Alaba kukosa michuano ya Klabu Fifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/28/alaba-kukosa-michuano-ya-klabu-fifa/feed/ 0
Benfica yaiduwaza Bayern https://www.greensports.co.tz/2025/06/25/benfica-yaiduwaza-bayern/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/25/benfica-yaiduwaza-bayern/#respond Wed, 25 Jun 2025 13:02:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13661 Charlotte, MarekaniBenfica ya Ureno imewaduwaza vinara wa Bundesliga, Bayern Munich kwa kuwachapa bao 1-0 katika mechi ya michuano ya Fifa ya Kombe la Dunia la Klabu inayoendelea Marekani.Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumatano hii, bao hilo pekee la Benfica lilipatikana dakika ya 13 mfungaji akiwa Andreas Schjelderup akiitumia krosi ya beki Fredrik Aursnes.Bayern ambao tayari wamefuzu […]

The post Benfica yaiduwaza Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Charlotte, Marekani
Benfica ya Ureno imewaduwaza vinara wa Bundesliga, Bayern Munich kwa kuwachapa bao 1-0 katika mechi ya michuano ya Fifa ya Kombe la Dunia la Klabu inayoendelea Marekani.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumatano hii, bao hilo pekee la Benfica lilipatikana dakika ya 13 mfungaji akiwa Andreas Schjelderup akiitumia krosi ya beki Fredrik Aursnes.
Bayern ambao tayari wamefuzu hatua ya pili ya michuano hiyo, hawakupanga kikosi chao bora na hivyo haikushangaza timu hiyo kuonekana dhaifu na kushindwa kufanya shambulizi la maana hasa kipindi cha kwanza.
Kocha wa Bayern, Vincent Kompany hata hivyo hakuzungumzia udhaifu wa kikosi chake kuwa sababu ya kushindwa badala yake alilaumu hali ya hewa ya joto na aina ya uwanja.

“Nilijua kikosi changu kitapata tabu, nafikiri kipindi cha kwanza hatukuwa bora kabisa, kutokana na hali ya joto na aina ya uwanja, nilihofu kwamba jambo hilo lingeathiri kasi yetu uwanjani,” alisema Kompany.


Baada ya matokeo hayo, timu hizo zitajiandaa kwa hatua ya 16 bora mechi zitakazochezwa siku tano zijazo kwa Bayern kuikabili Flamengo ya Brazil na Benfica kuumana na Chelsea.
Katika mechi nyingine, Chelsea ilitoka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya ES Tunis ya Tunisia.
Ushindi huo umekuwa neema kwa nyota mpya wa Chelsea, Liam Delap ambaye alifunga bao lake la kwanza na timu yake hiyo mpya.
Mabao mengine ya washindi yalifungwa na Tosin Adarabioyo na hiyo mpya kabla ya kuongeza la pili wakati bao jingine lilifungwa na Tyrique George.

The post Benfica yaiduwaza Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/25/benfica-yaiduwaza-bayern/feed/ 0
Alonso aomba muda Real Madrid https://www.greensports.co.tz/2025/06/19/alonso-ataka-uvumilivu-real-madrid/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/19/alonso-ataka-uvumilivu-real-madrid/#respond Thu, 19 Jun 2025 12:12:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13639 Miami, MarekaniKocha wa Real Madrid, Xabi Alonso ametaka kuwapo uvumilivu baada ya timu yake kutoka sare ya bao 1-1 na Al Hilal katika mechi ya kwanza ya michuano ya Fifa ya Kombe la Dunia la Klabu.Alonso ambaye ndio kwanza amejiunga na timu hiyo akitokea Bayer Leverkusen ya Ujerumani amesema itachukua muda kufanyia kazi mabadiliko anayoyataka […]

The post Alonso aomba muda Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Miami, Marekani
Kocha wa Real Madrid, Xabi Alonso ametaka kuwapo uvumilivu baada ya timu yake kutoka sare ya bao 1-1 na Al Hilal katika mechi ya kwanza ya michuano ya Fifa ya Kombe la Dunia la Klabu.
Alonso ambaye ndio kwanza amejiunga na timu hiyo akitokea Bayer Leverkusen ya Ujerumani amesema itachukua muda kufanyia kazi mabadiliko anayoyataka katika timu hiyo.
Real Madrid ilikuwa na wakati mgumu mapema katika nusu ya kwanza ya mechi hiyo kabla ya mshambuliaji wao mpya, Gonzalo Garcia kuipatia timu hiyo bao la kuongoza dakika ya 34.
Ruben Neves aliisawazishia Al Hilal kwa mkwaju wa penalti na Real Madrid nayo ilipata fursa kama hiyo ya kuongeza bao la pili ilipopata penalti lakini mkwaju uliopigwa na Federico Valverde uliokolewa na kipa Yassine Bouno.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Alonso alisema kipindi cha pili timu yake ilikuwa bora lakini kipindi cha kwanza walikosa mambo mengi ikiwamo uwiano na tayari wamelizungumza jambo hilo.
“Nilipenda jinsi wachezaji walivyobadilika, tulikuwa na uwezo wa kubadili kasi yetu na kuutawala zaidi mchezo huku tukicheza kwenye eneo lao zaidi, hii ni hatua ni lazima tuichukue vizuri na kuendelea kutafuta ubora,” alisema Alonso.
Alonso alifanya mazoezi kwa mara ya kwanza na kikosi cha Real Madrid, Juni 9 kabla ya kuelekea Marekani kwa ajili ya michuano ya klabu ya dunia inayoendelea nchini humo.

“Nilijua itachukua muda, kuna mambo ambayo tunahitaji kubadilika, kwa pamoja tunahitaji kubadili mambo na tutaendelea kufanya hivyo, kila kitu kinahitaji muda, tuna siku tisa na baadhi ya wachezaji wamefanya mazoezi mara tatu, tuko katika mashindano lakini pia tunataka kujifunza na tunachotaka kukifanya kitachukua muda,” alisema Alonso.


Kipa wa timu hiyo, Thibaut Courtois alisema awali walikuwa na kocha Carlo Ancelotti kwa miaka minne na walimzoea na sasa wanalazimika kubadilika na kufuata anachotaka kocha mpya na hilo halikamilishwi kwa siku nne.
Katika mechi hiyo, Real Madrid ilimkosa mshambuiaji wao nyota, Kylian Mbappe ambaye anasumbuliwa na homa, Mbappe msimu uliopita wa 2024-25 aliifungia timu hiyo mabao 43 katika mashindano yote.

The post Alonso aomba muda Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/19/alonso-ataka-uvumilivu-real-madrid/feed/ 0
Bayern yashinda 10-0 https://www.greensports.co.tz/2025/06/16/bayern-yashinda-10-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/16/bayern-yashinda-10-0/#respond Mon, 16 Jun 2025 14:34:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13620 California, MarekaniBayern Munich imeanza kwa kishindo michuano ya Fifa ya Klabu ya Dunia kwa kuweka rekodi ya ushindi wa mabao 10-0 dhidi ya Auckland City katika mechi iliyochezwa Jumapili hii Juni 15, 2025.Vinara hao wa Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga waliutawala vyema mchezo huku Jamal Musiala akifunga mabao matatu (hat trick) na Thomas Muller akipachika […]

The post Bayern yashinda 10-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
California, Marekani
Bayern Munich imeanza kwa kishindo michuano ya Fifa ya Klabu ya Dunia kwa kuweka rekodi ya ushindi wa mabao 10-0 dhidi ya Auckland City katika mechi iliyochezwa Jumapili hii Juni 15, 2025.
Vinara hao wa Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga waliutawala vyema mchezo huku Jamal Musiala akifunga mabao matatu (hat trick) na Thomas Muller akipachika mawili.
Bayern chini ya kocha Vincent Kompany walianza kuziona nyavu za wapinzani wao kutoka New Zealand katika dakika ya sita ya mchezo kwa bao la Kingsley Coman.
Dakika sita baadaye Bayern waliongeza bao la pili lililofungwa na Sacha Boey kabla Michael Olise hajapahika bao la tatu alipoinasa krosi ya Muller.
Wakati Auckland City wakitafakari, Coman kwa mara nyingine alitupia mpira kambani na kuifanya Bayern ifikishe mabao manne huku yeye akiwa amefunga la pili.
Muda mfupi kabla ya timu kwenda mapumziko, Muller alifunga bao la tano akiitumia krosi ya Olise kabla Olise hajakamlisha bao la sita na kuzifanya timu ziende mapumzko Bayern wakiwa mbele kwa mabao 6-0.
Kasi ya Bayern kupachika mabao ilipungua kidogo kipindi cha pili lakini hatimaye dakika ya 67 Musiala aliongeza bao la saba .
Musiala ambaye alizikosa mechi sita za Bayern za mwishoni mwa msimu kutokana na kuwa majeruhi, aliandika bao la nane kwa mkwaju wa penalti dakika ya 73 na kukamilisha bao lake la tisa na la tatu kwenye mechi hiyo katika dakika ya 84.
Bao la 10 na la mwisho kwa Bayern lilifungwa na Muller zikiwa zimebakia dakika mbili kumalizika kwa mchezo huo.
Ushindi wa Bayern unaingia kwenye rekodi ya kuwa ushindi wa mabao mengi zaidi katika mashindano hayo baada ya ule wa mwaka 2022 wa Al Hilal kuichapa Al Jazira mabao 6-1.
Katika mechi nyingine vinara wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, PSG ya Ufaransa waliilaza Atletico Madrid mabao 4-0 huku mabao ya washindi yakifungwa na Fabián Ruiz,
Vitinha, Mayulu kwa mkwaju wa penalti na Lee Kang-In.

The post Bayern yashinda 10-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/16/bayern-yashinda-10-0/feed/ 0