Fei Toto - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 29 May 2024 12:36:05 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Fei Toto - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Fei ampongeza Aziz Ki https://www.greensports.co.tz/2024/05/29/fei-ampongeza-aziz-ki/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/29/fei-ampongeza-aziz-ki/#respond Wed, 29 May 2024 12:36:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11157 Na mwandishi wetuBaada ya kushindwa kunyakua kiatu cha ufungaji bora, kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amempongeza kinara wa mabao Stephane Aziz Ki wa Yanga japo na yeye anafurahia timu yao kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika.Fei Toto aliyemaliza Ligi Kuu NBC akiwa na mabao 19, amempongeza kiungo wa Yanga Aziz Ki aliyefunga mabao […]

The post Fei ampongeza Aziz Ki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya kushindwa kunyakua kiatu cha ufungaji bora, kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amempongeza kinara wa mabao Stephane Aziz Ki wa Yanga japo na yeye anafurahia timu yao kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika.
Fei Toto aliyemaliza Ligi Kuu NBC akiwa na mabao 19, amempongeza kiungo wa Yanga Aziz Ki aliyefunga mabao 21 ambapo Fei pia amekiri kuwa mchezaji huyo alistahili kwa namna ambavyo alipambana.
“Hata kama nimekosa kiatu lakini najisikia vizuri tu, unajua jambo la kwanza ni timu na mengine baadaye. Kwa hiyo nampongeza sana (Aziz Ki) kwa kuwa mfungaji bora na pia tuna furaha tumefuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kama timu.
“Maana jambo la kwanza lilikuwa kufuzu na mengine baadaye, tuangalie hayo baadaye,” alisema Fei aliyejiunga na Azam msimu huu akitokea Yanga.
Fei ambaye pia ametoa pasi za mabao saba, akizidiwa mbili na Kipre Junior (Azam) mwenye tisa ameeleza kuwa anaamini huu ndio msimu wake bora zaidi tangu aanze kucheza Ligi Kuu NBC alipotua Yanga msimu wa 2018-19.

“Niseme kweli, ni wazi huu ndio msimu wangu bora tangu nianze kucheza Ligi ya Tanzania Bara kwa hiyo namshukuru Mungu kwa kumaliza msimu salama salmini bila ya majeraha na najiskia furaha,” alisema Fei.


Fei aliongeza kwamba kwake yeye hiyo ni historia kubwa na la muhimu zaidi ni kujitunza, kufanya mazoezi kwa bidii, kumsikiliza kocha na mambo mengine yataaenda vizuri.

The post Fei ampongeza Aziz Ki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/29/fei-ampongeza-aziz-ki/feed/ 0
Aziz Ki amfunika Fei Toto https://www.greensports.co.tz/2024/05/28/aziz-ki-amfunika-fei-toto/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/28/aziz-ki-amfunika-fei-toto/#respond Tue, 28 May 2024 19:41:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11142 Na mwandishi wetuKiungo wa Yanga, Stephanie Aziz Ki ameibuka kinara wa mabao Ligi Kuu NBC akimfunika kiungo wa Azam FC, Feisal Salum wakati ndoto za Simba kushika nafasi ya pili katika ligi hiyo zikiota mbawa.Aziz Ki na Feisal au Fei Toto wamekuwa katika mpambano wa kusaka kiatu cha mfungaji bora na kabla ya mechi za […]

The post Aziz Ki amfunika Fei Toto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo wa Yanga, Stephanie Aziz Ki ameibuka kinara wa mabao Ligi Kuu NBC akimfunika kiungo wa Azam FC, Feisal Salum wakati ndoto za Simba kushika nafasi ya pili katika ligi hiyo zikiota mbawa.
Aziz Ki na Feisal au Fei Toto wamekuwa katika mpambano wa kusaka kiatu cha mfungaji bora na kabla ya mechi za leo Jumanne za kufunga pazia la ligi hiyo, kila mmoja alikuwa na mabao 18.
Mabao ya mechi za leo ndiyo yaliyombeba Aziz Ki na kumfanya amalize ligi hiyo akiwa na mabao 21 baada ya Yanga kuinyuka Prisons mabao 4-1 wakati Fei amefikisha mabao 19 baada ya kufunga bao moja dhidi ya Geita Gold.
Aziz Ki leo amefunga mabao matatu peke yake na hivyo kuondoka na mpira hali ambayo si tu imedhihirisha uwezo wake katika kuzifumania nyavu bali pia amewanyamazisha waliokuwa na fikra kwamba Fei leo angeweza kumpiku kwa mabao.
Fei ambaye amewahi kucheza pamoja na Aziz Ki katika kikosi cha Yanga hata hivyo naye ana kila sababu ya kujivunia mabao aliyofunga msimu huu kwani ndiyo yaliyoiwezesha Azam kushika nafasi ya pili.
Kwa kushika nafasi ya pili, Azam itaungana na Yanga katika ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakati Simba iliyoangukia nafasi ya tatu itashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho pamoja na Coastal Union.
Yanga iliyotwaa taji hilo imemaliza ligi na pointi 80, Simba na Azam zimemaliza kila moja ikiwa na pointi 69, Simba imezipata pointi hizo baada ya kuifunga JKT Tanzania mabao 2-0 na Azam imeilaza Geita Gold mabao 2-0.
Azam imeshika nafasi ya pili kutokana na wastani mzuri wa mabao, imefunga mabao 63 dhidi ya 53 ya Simba wakati Azam pia imefungwa mabao 21, Simba imefungwa mabao 29.
Wakati hali ikiwa hivyo katika nafasi nne za juu, mambo si mazuri kwa Mtibwa Sugar ambayo tayari imeshuka daraja ikiungana na Geita Gold katika mkumbo huo wa kuelekea ligi ya Championship.
Matokeo ya mechi za mwisho za ligi hiyo…
Simba 2-0 JKT Tanzania
Coastal Union 0-0 KMC
Mashujaa FC 3-0 Dodoma Jiji
Ihefu 5-1 Mtibwa Sugar
Yanga 4-1 Prisons
Namungo FC 3-2 Tabora United
Geita Gold 0-2 Azam FC
Singida FG 2-3 Kagera Sugar

The post Aziz Ki amfunika Fei Toto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/28/aziz-ki-amfunika-fei-toto/feed/ 0
Chirwa: Fei ni zaidi ya Aziz Ki https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/chirwa-fei-ni-zaidi-ya-aziz-ki/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/chirwa-fei-ni-zaidi-ya-aziz-ki/#respond Fri, 10 May 2024 07:59:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10912 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa Kagera Sugar, Obrey Chirwa amesema anaamini kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ni mchezaji mzuri zaidi ya Stephanie Aziz Ki wa Yanga, isipokuwa Fei anashushwa chini kutokana na uhalisia wa nchi yake, Tanzania.Chirwa ambaye anatokea nchini Zambia amezungumza hayo na kufafanua kwamba amekuwa akiiona hali ya wachezaji wa Kitanzania […]

The post Chirwa: Fei ni zaidi ya Aziz Ki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Kagera Sugar, Obrey Chirwa amesema anaamini kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ni mchezaji mzuri zaidi ya Stephanie Aziz Ki wa Yanga, isipokuwa Fei anashushwa chini kutokana na uhalisia wa nchi yake, Tanzania.
Chirwa ambaye anatokea nchini Zambia amezungumza hayo na kufafanua kwamba amekuwa akiiona hali ya wachezaji wa Kitanzania kutokukubalika nchini na badala yake wadau huvutiwa zaidi na wanaotoka nje.
Alisema hali hiyo huwakuta wachezaji hao hata kama wana viwango vya kawaida lakini yeye binafsi anaamini ni nchi yenye wachezaji wenye viwango vikubwa mno tofauti na watu wanavyodhani.
“Ukiachana na Diarra (Djigui wa Yanga), nilishakutana na makipa wengi wakali wa Tanzania kama Aishi Manula au Beno Kakolanya, wale wana hatari ujue ila shida ni kwamba Watanzania mnawadharau wenzenu, mnapenda vipya lakini Watanzania wana uwezo mkubwa kushinda ‘maforena’,” alisema Chirwa ambaye timu yake ilifungwa bao 1-0 na Yanga.


“Mnaona mabeki wa kati wa Yanga, wale ni Watanzania lakini watu wanawadharau wanawaona wa kawaida tu. Mfano viungo yaani ina wale kina Mudathir (Yahya), Feisal ni hatari wale siwezi kusema sana lakini mambo yanaelweka.

“Hata Fei na Aziz, Fei yupo juu lakini sababu ni Mtanzania watu wanamchukulia poa mbele ya wageni,” alisema Chirwa ambaye pia aliwahi kukipiga Yanga.


Chirwa aliyewahi pia kukipiga Nogoom FC ya nchini Misri ameongelea ushindani wa Fei na Aziz Ki kwa kuwa pia wanachuana msimu huu msimu huu.


Wachezaji hao ambao walikuwa na ushirikiano mzuri wakati wakiwa Yanga kabla ya Fei kutimkia Azam kwa sasa wamefungana kileleni kwa mabao 15 huku Aziz akiwa juu kwa kutoa pasi za mabao nane na Fei akitoa pasi saba mpaka sasa (kabla ya mechi ya Simba na Azam).

The post Chirwa: Fei ni zaidi ya Aziz Ki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/chirwa-fei-ni-zaidi-ya-aziz-ki/feed/ 0
Tuzo ya mfungaji bora haimsumbui Fei Toto https://www.greensports.co.tz/2024/04/20/tuzo-ya-mfungaji-bora-haimsumbui-fei-toto/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/20/tuzo-ya-mfungaji-bora-haimsumbui-fei-toto/#respond Sat, 20 Apr 2024 12:37:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10689 Na mwandishi wetuKiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ameendelea kusisitiza kuwa hajali kupitwa idadi ya mabao na kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki katika mbio za kuwania kiatu cha ufungaji bora kwa kuwa anaangalia zaidi mafanikio ya kikosi chake.Fei amezungumza hayo leo Ijumaa baada ya kupitwa na Aziz Ki kwa idadi ya […]

The post Tuzo ya mfungaji bora haimsumbui Fei Toto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ameendelea kusisitiza kuwa hajali kupitwa idadi ya mabao na kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki katika mbio za kuwania kiatu cha ufungaji bora kwa kuwa anaangalia zaidi mafanikio ya kikosi chake.
Fei amezungumza hayo leo Ijumaa baada ya kupitwa na Aziz Ki kwa idadi ya mabao akiwa amefunga mara 14 na kumuacha Fei akiwa na mabao 13.
Fei hajafunga bao hata moja katika mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu NBC tangu alipofunga mara ya mwisho dhidi ya Yanga waliposhinda kwa mabao 2-1 wiki kadhaa zilizopita.

“Mimi katika ufungaji nafunga ili kusaidia timu yangu, kwa hiyo ninapopata nafasi ya kufunga nafanya hivyo si kwa kushindana na mtu kwamba yeye kanizidi nianze kumuangalia sana, mimi naangalia timu yangu kuipambania ili kupata matokeo zaidi,” alisema Fei mchezaji wa zamani wa Yanga.


Fei pia aligusia ushindani wao wa ubingwa dhidi ya Yanga akifafanua kuwa licha ya wao kuwa wa pili kwa pointi 51 baada ya mechi 23 dhidi ya vinara Yanga wenye pointi 55 kwa mechi 21 lakini mechi saba zilizosalia kabla ya pazia la ligi kufungwa, zinaweza kutoa tafsiri halisi ya nani bingwa.
“Kwa sare yetu ya 0-0 na Mashujaa bado haiwezi kueleza kwamba tumemaliza mbio za ubingwa, bado kuna michezo ipo mbele, bado zimebakia mechi saba sasa hivi kwa hiyo tutaendelea kupambana katika michezo ya mbele iliyosalia ili tufike kwenye nafasi nzuri sababu mbio za ubingwa bado ziko wazi,” alisema Fei.

The post Tuzo ya mfungaji bora haimsumbui Fei Toto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/20/tuzo-ya-mfungaji-bora-haimsumbui-fei-toto/feed/ 0
Fei Toto aizamisha Yanga https://www.greensports.co.tz/2024/03/18/fei-toto-aizamisha-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/18/fei-toto-aizamisha-yanga/#respond Mon, 18 Mar 2024 07:16:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10242 Na mwandishi wetuFeisal Salum au Fei Toto ameidhihirishia timu yake ya zamani ya Yanga kwamba bado yuko vizuri baada ya kuifungia Azam FC bao la pili lililoipa timu hiyo ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga.Fei ataendelea kufurahia ushindi huo hasa akikumbuka jinsi alivyojikuta katika mgogoro na uongozi wa Yanga kutokana na uamuzi wake wa […]

The post Fei Toto aizamisha Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Feisal Salum au Fei Toto ameidhihirishia timu yake ya zamani ya Yanga kwamba bado yuko vizuri baada ya kuifungia Azam FC bao la pili lililoipa timu hiyo ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga.
Fei ataendelea kufurahia ushindi huo hasa akikumbuka jinsi alivyojikuta katika mgogoro na uongozi wa Yanga kutokana na uamuzi wake wa kuvunja mkataba na timu hiyo uliomfanya awe nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.
Mgogoro huo hata hivyo ulifikia mwisho baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwaomba viongozi wa Yanga kulimaliza suala hilo na hatimaye mchezaji huyo kuruhusiwa kujiunga na Azam.
Yanga kwa matokeo ya mechi hiyo ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa Jumapili hii usiku yanaifanya timu hiyo iwe na unyonge wa kufungwa na Fei Toto lakini pia kupunguzwa kasi yake ya ushindi kwenye ligi hiyo msimu huu.
Yanga ambayo imekuwa ikiinyanyasa Azam katika mechi zao za hivi karibuni pamoja na timu nyingine za ligi hiyo msimu huu, hata hivyo inaendelea kubaki kileleni ikiwa na pointi zake 52.
Kwa upande wa Azam inakuwa imerudi katika nafasi yake ya pili ikiwa na pointi 47 na kuizidi Simba kwa tofauti ya pointi mbili ingawa Azam imecheza michezo 21 ikiwa ni michezo miwili zaidi ya ile ya Simba.
Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Clement Mzize katika dakika ya 10 lakini ikawachukua Azam dakika tisa kusawazisha kupitia kwa Gibril Sillah na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Dakika sita baada ya kuanza kipindi cha pili, Azam walifanya shambulizi kali langoni mwa Yanga na Fei Toto kuuwahi mpira kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa wa Yanga Djigui Diarra.
Yanga katika mechi hiyo ilipata pigo katika kipindi cha kwanza baada ya kiungo wake, Pacome Zouazoua kuumia na nafasi yake kuingia Joseph Guede.

The post Fei Toto aizamisha Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/18/fei-toto-aizamisha-yanga/feed/ 0
Ufungaji bora haumsumbui Fei Toto https://www.greensports.co.tz/2024/03/05/ufungaji-bora-haumsumbui-fei-toto/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/05/ufungaji-bora-haumsumbui-fei-toto/#respond Tue, 05 Mar 2024 06:28:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10033 Na mwandishi wetuBaada ya kuongoza kwenye mbio za ufungaji bora Ligi Kuu NBC, kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema hatolei macho tuzo ya ufungaji bora badala yake lengo lake namba moja ni kuisaidia timu yake kubeba taji la ligi kuu.Mabao mawili aliyoyafunga Jumapili katika mechi dhidi ya Dodoma Jiji FC, yamemfanya kiungo […]

The post Ufungaji bora haumsumbui Fei Toto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya kuongoza kwenye mbio za ufungaji bora Ligi Kuu NBC, kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema hatolei macho tuzo ya ufungaji bora badala yake lengo lake namba moja ni kuisaidia timu yake kubeba taji la ligi kuu.
Mabao mawili aliyoyafunga Jumapili katika mechi dhidi ya Dodoma Jiji FC, yamemfanya kiungo huyo kufikisha mabao 11 na kumpita kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki mwenye mabao 10.
Akizungumza baada ya mchezo huo kiungo huyo alisema siri ya kiwango chake kupanda ni kujituma na kufuata maelekezo ya kocha wake na lengo kubwa ni kuona Azam inabeba ubingwa wa ligi msimu huu.

“Mabao ninayofunga ni kwa ajili ya kuisaidia timu yangu na si kwamba nataka kushindana na mtu hapa, namheshimu Aziz Ki ni mchezaji mkubwa lakini watu wajue kila zuri ninalofanya lengo ni kuipigania timu yangu,” alisema Fei Toto.


Kiungo huyo wa zamani wa Yanga, alisema anajua ligi imekuwa na ushindani mkubwa lakini wataendelea kupambana ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri na kutimiza lengo hilo ambalo wamekusudia kulifikia msimu huu.
Azam ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikikusanya pointi 43 sawa na vinara Yanga, lakini Azam ipo mbele kwa michezo mitatu dhidi ya Yanga na michezo minne dhidi ya wanaoshika nafasi ya tatu Simba SC.

The post Ufungaji bora haumsumbui Fei Toto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/05/ufungaji-bora-haumsumbui-fei-toto/feed/ 0
Fei Toto: Tutaiheshimisha Tanzania https://www.greensports.co.tz/2024/01/11/fei-toto-tutaiheshimisha-tanzania/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/11/fei-toto-tutaiheshimisha-tanzania/#respond Thu, 11 Jan 2024 07:58:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9259 Na mwandishi wetuKiungo wa timu ya taifa, Taifa Stars, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema wapo tayari kuiheshimisha Tanzania kwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Afcon inayotarajia kuanza Jumamosi nchini Ivory Coast.Katika michuano hiyo, Taifa Stars imepangwa Kundi F na timu za Morocco, DR Congo na Zambia na itaanza kampeni ya kusaka taji hilo kwa kucheza […]

The post Fei Toto: Tutaiheshimisha Tanzania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo wa timu ya taifa, Taifa Stars, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema wapo tayari kuiheshimisha Tanzania kwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Afcon inayotarajia kuanza Jumamosi nchini Ivory Coast.
Katika michuano hiyo, Taifa Stars imepangwa Kundi F na timu za Morocco, DR Congo na Zambia na itaanza kampeni ya kusaka taji hilo kwa kucheza na vinara wa soka Afrika, Morocco Januari 17, mwaka huu.
Akizungumza akiwa nchini Ivory Coast, kiungo huyo alisema maandalizi wanayofanya chini ya kocha, Adel Amrouche yamewaongezea ari ya kupambana na kulipa heshima taifa lao licha ya kwamba watu wengi hawawapi nafasi.

“Ukweli kila mchezaji amepania kuipa heshima Tanzania kwa kufanya vizuri kwenye mashindano haya, najua tupo kundi gumu lakini hakuna kinachoshindikana hata hao waliokuwa juu walianza kama sisi kwa hiyo Watanzania waondoe hofu tupo kwa ajili yao,” alisema Fei.


Akijizungumzia yeye binafsi alisema tofauti na ilivyokuwa fainali za mwaka 2019 ambapo alikuwa kijana mdogo kwa sasa yupo fiti na yupo tayari kwa mapambano ya kuipigania nchi yake.
Alisema ana uzoefu wa kutosha kutokana na kucheza mashindano mengi kwenye ngazi ya klabu hivyo matarajio yake mbali na kuiheshimisha Tanzania lakini pia anataka kuitumia michuano hiyo kuonesha kipaji alichonacho.

The post Fei Toto: Tutaiheshimisha Tanzania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/11/fei-toto-tutaiheshimisha-tanzania/feed/ 0
Wachezaji Yanga wampongeza Fei Toto https://www.greensports.co.tz/2023/10/24/wachezaji-yanga-wampongeza-fei-toto/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/24/wachezaji-yanga-wampongeza-fei-toto/#respond Tue, 24 Oct 2023 09:50:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8214 Na mwandishi wetuWachezaji nyota wa Yanga wamempongeza kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwa kiwango kikubwa alichokionesha timu hizo zilipokutana jana Jumatatu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na Azam kufungwa mabao 3-2.Wachezaji hao walioongozwa na kiungo wa Uganda, Khalid Aucho walitoa pongezi zao hizo kwenye chapisho la Fei aliloliweka jana kwenye […]

The post Wachezaji Yanga wampongeza Fei Toto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Wachezaji nyota wa Yanga wamempongeza kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwa kiwango kikubwa alichokionesha timu hizo zilipokutana jana Jumatatu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na Azam kufungwa mabao 3-2.
Wachezaji hao walioongozwa na kiungo wa Uganda, Khalid Aucho walitoa pongezi zao hizo kwenye chapisho la Fei aliloliweka jana kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kwa kuweka picha ya mechi hiyo ya juzi.
Kwa upande wake Aucho aliandika kwenye maoni ya chapisho hilo: “Mchezo mzuri jana kaka endelea kupambana.”
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki alimsifia Fei kwa kumwita mchezaji mkubwa, ambapo Fei aliujibu ujumbe huo kwa kushukuru na yeye kumpongeza Ki kwa uwezo wake akimwita “Master Ki”.
Wengine waliompongeza Fei ambaye msimu uliopita alikuwa akikipiga Yanga ni beki Ibrahim Bacca na mshambuliaji wa Pyramids ya Misri ambaye aliandika: “Zanzibar Finest ni mmoja tu.”
Mechi hiyo ya juzi ni mechi ya pili, Fei anakutana na waajiri wake hao wa zamani ambapo mechi ya kwanza ilikuwa ya Ngao ya Jamii mwanzoni mwa msimu huu na Azam ikafungwa mabao 2-0, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Hata hivyo, katika mechi hiyo ya juzi, Fei alionesha kiwango kikubwa na alionekana kuisumbua mno safu ya kiungo ya Yanga kiasi cha Aucho na Mudathir kuadhibiwa kwa kadi ya njano kutokana na kumchezea madhambi kiungo huyo.

The post Wachezaji Yanga wampongeza Fei Toto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/24/wachezaji-yanga-wampongeza-fei-toto/feed/ 0
Mudathir: Nilikabidhiwa Fei Toto https://www.greensports.co.tz/2023/08/11/mudathir-nilikabidhiwa-fei-toto/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/11/mudathir-nilikabidhiwa-fei-toto/#respond Fri, 11 Aug 2023 05:05:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7327 Kiungo wa kati wa Yanga, Mudathir Yahya amesema upinzani mkubwa ulioibuka kati yake na Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam FC, ulitokana na maelekezo maalumu kutoka kwa kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi.Katika mchezo huo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii, Fei Toto, alishindwa kutamba kama yale mashuti yake aliyokuwa akiyapiga wakati akiichezea […]

The post Mudathir: Nilikabidhiwa Fei Toto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Kiungo wa kati wa Yanga, Mudathir Yahya amesema upinzani mkubwa ulioibuka kati yake na Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam FC, ulitokana na maelekezo maalumu kutoka kwa kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi.
Katika mchezo huo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii, Fei Toto, alishindwa kutamba kama yale mashuti yake aliyokuwa akiyapiga wakati akiichezea Yanga huku mara kadhaa wawili wakionekana kugongana, kukamiana na kukabana kwa nguvu.
Kiungo huyo alisema kabla ya kwenda kwenye mchezo huo walifanya kikao maalumu na kuwachambua wapinzani ikiwemo kufatilia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ikiwemo kubaini uwezo na madhara yao na yeye alikabidhiwa kumkaba Fei Toto.

“Kocha alinikabidhi Fei Toto akaniambia asicheze yeye wala kuichezesha timu na mimi nilitimiza jukumu alilonipa kocha wangu ndio maana Azam hawakufanya shambulizi lolote la hatari kwenye lango letu,” alisema Mudathir.


Kiungo huyo alisema anajivunia kutimiza majukumu yake vizuri kwani imemuongezea uhakika wa kupata nafasi ya kucheza chini ya kocha huyo lakini pia anaamini ameisaidia timu yake kupata ushindi katika mchezo muhimu kama huo.
Alisema mbali na yeye kufanikiwa kumdhibiti Fei lakini kilichowasaidia kushinda mchezo huo ni timu nzima kucheza kwa umakini na kufuata vyema mbinu na maelekezo waliyopewa na kocha wao.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kutinga fainali ya Ngao ya Jamii itakayochezwa Jumapili hii.

The post Mudathir: Nilikabidhiwa Fei Toto first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/11/mudathir-nilikabidhiwa-fei-toto/feed/ 0
Fei atua Azam, amshukuru Rais Samia https://www.greensports.co.tz/2023/06/08/fei-atua-azam-amshukuru-rais-samia/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/08/fei-atua-azam-amshukuru-rais-samia/#respond Thu, 08 Jun 2023 15:08:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6521 Na mwandishi wetuKiungo mpya wa Azam FC, Feisal Salum, ‘Fei Toto’ amemshukuru Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kulimaliza suala lake na kufanikiwa kujiunga na kikosi cha Azam.Hayo ameyasema leo Alhamisi kwenye makao makuu ya klabu hiyo Mzizima, wakati akitambulishwa baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia timu hiyo ambayo amekuwa akihusishwa nayo […]

The post Fei atua Azam, amshukuru Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo mpya wa Azam FC, Feisal Salum, ‘Fei Toto’ amemshukuru Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kulimaliza suala lake na kufanikiwa kujiunga na kikosi cha Azam.
Hayo ameyasema leo Alhamisi kwenye makao makuu ya klabu hiyo Mzizima, wakati akitambulishwa baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia timu hiyo ambayo amekuwa akihusishwa nayo kwa muda mrefu.

“Namshukuru sana Rais Samia kwa kuliingilia suala hili Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi katika majukumu yake, nafurahi kujiunga na Azam na nitahakikisha napiga kazi kuwapa furaha pia naishukuru Yanga, ingawa nimeondoka lakini bado naipenda,” alisema Fei Toto.


Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin ‘Popat’ alisema usajili wa Fei Toto unakwenda kuimarisha kikosi chao ambacho msimu ujao wamedhamiria kufanya makubwa katika mashindano ya ndani na nje ya Tanzania.
Alisema wana imani kubwa na mchezaji huyo ambaye kwenye kikosi chao atarahisisha kufikia malengo ambayo wamekuwa nayo kwa misimu kadhaa nyuma kwa kushirikiana na wachezaji wengine wapya wanaotarajia kuwasajili kwenye dirisha kubwa na wale waliopo kwenye kikosi chao.
Azam imekamilisha dili hilo baada ya kuelezwa kukutana na Yanga tangu juzi ikiwa ni siku chache tangu Rais Samia kupeleka ombi kwa Yanga akiwataka wamalize mgogoro wao na mchezaji huyo.
Fei Toto alishinikiza kuvunja mkataba wake na Yanga tangu Desemba, mwaka jana kabla ya Yanga kuamua kudai haki yake na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likaamuru mchezaji huyo arejee Yanga kabla ya kiungo huyo kupinga na kujipanga kwenda Mahakama ya Kimataifa ya Michezo (CAS).
Kitendo cha Fei kutua Azam pia kimezima safari ya kwenda Cas ambako alichangisha kiasi cha pesa kwa Watanzania takriban Sh milioni 109 ambazo amesema atazipeleka nyumba za ibada na nyingine atazipeleka kwenye nyumba za kulea watoto yatima.
Fei ametambulishwa Azam na kukabidhiwa jezi namba sita ambayo ni jezi yake pendwa aliyokuwa akiitumia tangu alipokuwa Yanga na hata timu ya taifa, Taifa Stars.
Awali Yanga walitoa taarifa ya kuachana na mchezaji huyo baada ya wao kufikia makubaliano na klabu ya Azam ingawa hawakutaja kiasi cha fedha walicholipwa hadi kumuachia mchezaji huyo ambaye awali walionekana kutokuwa tayari kuvunja naye mkataba.

The post Fei atua Azam, amshukuru Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/08/fei-atua-azam-amshukuru-rais-samia/feed/ 0