FA - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 21 Feb 2024 19:00:31 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg FA - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Yanga yaitandika Polisi 5-0 https://www.greensports.co.tz/2024/02/21/yanga-yaitandika-polisi-5-0/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/21/yanga-yaitandika-polisi-5-0/#respond Wed, 21 Feb 2024 19:00:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9828 Na mwandishi wetuYanga imeendelea kudhihirisha ubabe katika soka la Tanzania kwa kuinyuka Polisi Tanzania mabao 5-0 katika mechi iliyopigwa Jumanne hii usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.Ushindi huo mnono katika mechi ya Kombe la Shirikisho Azam (FA) licha ya kuendeleza ubabe wa Yanga, pia ilikuwa nafasi ya kipekee kwa mshambuliaji mpya wa […]

The post Yanga yaitandika Polisi 5-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imeendelea kudhihirisha ubabe katika soka la Tanzania kwa kuinyuka Polisi Tanzania mabao 5-0 katika mechi iliyopigwa Jumanne hii usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Ushindi huo mnono katika mechi ya Kombe la Shirikisho Azam (FA) licha ya kuendeleza ubabe wa Yanga, pia ilikuwa nafasi ya kipekee kwa mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Joseph Guede kuanza kuzifumania nyavu.
Guede aliyesajiliwa hivi karibuni ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzitikisa nyavu za Polisi katika dakika ya 13 kabla Farid Mussa hajaongeza bao la pili katika dakika ya 33.
Guede alikamilisha bao lake la pili na la tatu kwa Yanga katika dakika ya 45 na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko Yanga ikiwa mbele kwa mabao 3-0.
Mabao mengine mawili ya Yanga yalifungwa na Clement Mzize dakika ya 82 na Shekhan Khamis kwa mkwaju wa penalti dakika ya 86.
Timu nyingine za Ligi Kuu NBC ambazo zimewahi kukumbana na kipigo cha mabao matano mbele ya Yanga ni pamoja na mahasimu wao Simba, KMC na JKT Tanzania.

The post Yanga yaitandika Polisi 5-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/21/yanga-yaitandika-polisi-5-0/feed/ 0
Yanga yabeba taji la FA https://www.greensports.co.tz/2023/06/12/yanga-yabeba-taji-la-fa/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/12/yanga-yabeba-taji-la-fa/#respond Mon, 12 Jun 2023 19:50:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6568 Na mwandishi wetu, TangaYanga imezima ndoto za Azam kubeba taji msimu huu baada ya kuichapa bao 1-0 katika mechi ya fainali ya Kombe la FA (ASFC) iliyopigwa kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga, leo Jumatatu.Kwa ushindi huo Yanga sasa imemaliza msimu na mataji mawili baada ya kubeba lile la Ligi Kuu NBC na sasa timu […]

The post Yanga yabeba taji la FA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu, Tanga
Yanga imezima ndoto za Azam kubeba taji msimu huu baada ya kuichapa bao 1-0 katika mechi ya fainali ya Kombe la FA (ASFC) iliyopigwa kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga, leo Jumatatu.
Kwa ushindi huo Yanga sasa imemaliza msimu na mataji mawili baada ya kubeba lile la Ligi Kuu NBC na sasa timu hiyo inajiandaa kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao wakati Azam itaangukia kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Kennedy Musonda ndiye aliyeacha kilio Azam baada ya kufunga bao hilo pekee katika dakika ya 16 kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Tuisila Kisinda au TK Master.
Dakika nne baada ya kuingia bao hili, Musonda nusura aipatie Yanga bao la pili baada ya kuinasa pasi ya Benard Morisson na kufumua shuti ambalo hata hivyo lilitoka nje.
Dakika saba baada ya Musonda kukosa bao, Azam walijibu mapigo na kufanya shambulizi lililozaa mpira wa adhabu baada ya Khalid Aucho kumchezea rafu James Akaminko lakini shuti lililopigwa na Ayoub Lyanga lilidakwa na kipa wa Yanga, Djigui Diarra.


Dakika 10 kabla ya timu hizo kwenda mapumziko, Yanga nao walipata mpira wa adhabu baada ya Kisinda ambaye baadaye alitolewa na kuingia Mudathir Yahya, kuchezewa rafu lakini shuti la Morisson halikuweza kuipatia bao timu hiyo.
Makocha wa timu zote walifanya mabadiliko katika mchezo huo lakini mabadiliko hayo hayakuweza kuleta matokeo tofauti kwani hadi mwisho wa mchezo Yanga walitoka uwanjani na bao lao moja lililowawezesha kubeba kombe.
Yanga inakuwa imelibeba taji hilo kwa mara ya pili mfululizo, ikifanya hivyo msimu uliopita ilipokutanana Coastal Union katika hatua ya fainali na kushinda kwa penalti 4-1 baada ya sare ya mabao 3-3.

The post Yanga yabeba taji la FA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/12/yanga-yabeba-taji-la-fa/feed/ 0
Man City yabeba taji FA https://www.greensports.co.tz/2023/06/04/man-city-yabeba-taji-fa/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/04/man-city-yabeba-taji-fa/#respond Sun, 04 Jun 2023 07:32:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6435 London, EnglandMan City imepiga hatua nyingine muhimu katika azma yake ya kubeba mataji matatu msimu huu baada ya kuibwaga Man United kwa mabao 2-1 katika mechi ya fainali ya Kombe la FA na kubeba taji hilo.Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumamosi hii kwenye dimba la Wembley, Man City ilipata ushindi huo kwa mabao ya nahodha Ilkay […]

The post Man City yabeba taji FA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Man City imepiga hatua nyingine muhimu katika azma yake ya kubeba mataji matatu msimu huu baada ya kuibwaga Man United kwa mabao 2-1 katika mechi ya fainali ya Kombe la FA na kubeba taji hilo.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumamosi hii kwenye dimba la Wembley, Man City ilipata ushindi huo kwa mabao ya nahodha Ilkay Gundogan katika dakika ya kwanza na ya 51, yote yakitokana kazi nzuri ya Kevin De Bruyne wakati bao pekee la United likifungwa kwa penalti na Bruno Fernandes katika dakika ya 33.
Man City tayari ina mataji mawili baada ya kubeba lile la Ligi Kuu England (EPL) na sasa inasubiri Juni 10 itakapoumana na Inter Milan katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Iwapo Man City itaibwaga Inter katika fainali hiyo itakayopigwa mjini Istanbul, Uturuki itakuwa imeweka rekodi ambayo mara ya mwisho kwa England iliwekwa na Man United mwaka 1999 ilipobeba mataji matatu yaani EPL, FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Gundogan ambaye hivi karibuni kocha wake Pep Guardiola ameelezea umuhimu wake ndani ya kikosi cha Man City, aliweka rekodi kwa kufunga bao la mapema katika Kombe la FA akiwa amefunga katika sekunde ya 12.
Bao hilo linamfanya awe ameipiku rekodi ya Luois Saaha ambaye mwaka 2009 akiwa mchezaji wa Everton alifunga bao la mapema katika sekunde ya 25 katika mechi dhidi ya Chelsea.
Kwa majirani zao katika jiji la Manchester, Man United, matarajio yao ya kubeba taji la pili msimu huu yametoka kapa na sasa wanabaki na taji moja tu la Carabao ambalo ni la kwanza katika kipindi cha miaka sita.
Kocha Erik ten Hag bila shaka atakuwa na kazi nzito ya kufanya msimu ujao hasa baada ya kuonyesha matumaini makubwa msimu huu akifanikiwa kuingia top four na msimu ujao atashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika mipango ya msimu ujao ya Man United, jina la kiungo wa Chelsea, Mason Mount limo kwenye mpango wa Ten Hag na haitashangaza akiichezea timu hiyo msimu ujao kama ilivyo kwa mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane ambaye pia yumo kwenye hesabu za Ten Hag kwa ajili ya msimu ujao.

The post Man City yabeba taji FA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/04/man-city-yabeba-taji-fa/feed/ 0
Yanga yafuzu fainali FA https://www.greensports.co.tz/2023/05/21/mayele-aipeleka-yanga-fainali-fa/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/21/mayele-aipeleka-yanga-fainali-fa/#respond Sun, 21 May 2023 15:31:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6243 Na mwandishi wetuBao pekee la Fiston Mayele, leo Jumapili limetosha kuipeleka Yanga fainali ya Kombe la FA (ASFC) na sasa inasubiri kuumana na Azam ili kumpata kinara wa michuano hiyo msimu huu wa 2022-23.Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Liti, Singida, Mayele alifunga bao hilo dakika ya 82 baada piga nikupige kwenye lango la […]

The post Yanga yafuzu fainali FA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Bao pekee la Fiston Mayele, leo Jumapili limetosha kuipeleka Yanga fainali ya Kombe la FA (ASFC) na sasa inasubiri kuumana na Azam ili kumpata kinara wa michuano hiyo msimu huu wa 2022-23.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Liti, Singida, Mayele alifunga bao hilo dakika ya 82 baada piga nikupige kwenye lango la Singida na kumalizia shuti la Nkane ambalo kwanza liliokolewa na kipa Benedict Haule.
Mayele alifunga bao hilo takriban dakika mbili baada ya kocha wa Yanga, Nassredine Nabi kufanya mabadiliko akiwatoa Clement Mzize, Aziz Ki na Jesus Moloko na nafasi zao kuingia, Mayele, Tuisila Kisinda na Kennedy Musonda ambao walibadili mchezo.
Ni katika kipindi hicho hicho, Singida nao waliwatoa Francis Kazadi na Deus Kaseke na nafasi zao kuingia Meddie Kagere na Aziz Andabwile. Kaseke na Kazadi hawakufurahia mabadiliko hayo hasa Kaseke ambaye alidhihirisha hali hiyo wazi wazi.
Mabadiliko ya Nabi ndiyo kwa kiasi kikubwa yaliwapa wakati mgumu Singida ambao kwa muda mrefu walionekana kukabiliana na kasi ya Yanga, wakizuia hatari langoni mwao ingawa nao walifanya mashambulizi machache.
Katika dakika 45 za mwanzo, Yanga walionekana kufika katika lango la Singida mara kwa mara lakini umahiri wa kipa Benedict Haule ulikuwa kikwazo kwa timu hiyo kupata bao.
Mfano dakika ya 32 aliokoa vizuri shuti la mguu wa kushoto lililopigwa na Mzize, kabla ya kuokoa shuti lingine la mguu wa kushoto lililopigwa na Aziz Ki.
Katika kuiimarisha timu yake, Nabi alianza kwa kuwatoa Doumbia ambaye aliumia na Farid Mussa na kuwaingiza Nkane na Dickson Job mabadiliko ambayo hayakuisumbua sana Singida kabla ya mabadiliko ya pili yaliyozaa bao la ushindi.
Yanga ambao pia ni vinara wa Ligi Kuu NBC msimu huu, sasa wanakuwa wamefuzu fainali ya pili baada ya kufanya hivyo katika Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuitoa Marumo Gallant ya Afrika Kusini na mambo yakiwaendea vizuri watamaliza msimu na mataji matatu au treble.

The post Yanga yafuzu fainali FA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/21/mayele-aipeleka-yanga-fainali-fa/feed/ 0
Robertinho ataka ushindi FA https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/robertinho-ataka-ushindi-fa/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/robertinho-ataka-ushindi-fa/#respond Wed, 01 Mar 2023 12:38:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5356 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya African Sports kesho Alhamisi ili kutinga robo fainali ya Kombe la FA (ASFC).Simba itakuwa kibaruani kesho kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam dhidi ya timu hiyo inayoshiriki Ligi ya Championship kwenye mchezo huo wa hatua ya 16 […]

The post Robertinho ataka ushindi FA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya African Sports kesho Alhamisi ili kutinga robo fainali ya Kombe la FA (ASFC).
Simba itakuwa kibaruani kesho kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam dhidi ya timu hiyo inayoshiriki Ligi ya Championship kwenye mchezo huo wa hatua ya 16 bora.
Robertinho amesema siku zote malengo ya Simba ni kushinda kila taji la michuano wanayoshiriki kwa hiyo wametoa macho pia katika michuano hiyo ambayo msimu uliopita Simba ilitoka katika nusu fainali kwa kufungwa bao 1-0 na Yanga.
Pia amefunguka kuwa kesho anategemea kuwatumia wachezaji ambao hawapati nafasi kubwa kikosini kwa kuwa wiki ijayo wana mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers, hivyo ni muhimu kuhakikisha wanachanga karata zao vyema na kupata ushindi kote.
“Tumejipanga kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho wa ASFC dhidi ya African Sports, Simba ni timu kubwa na tunahitaji kushinda kila taji na tupo tayari,” amesema kocha huyo.
“Tunategemea kuwatumia wachezaji ambao hawajapata nafasi kubwa kikosini kwa kuwa tuna mchezo wa marudiano nyumbani dhidi ya Vipers kwa hiyo tunaziangalia mechi zote,” amesema Robertinho.

The post Robertinho ataka ushindi FA first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/robertinho-ataka-ushindi-fa/feed/ 0
FA wachunguza kadhia ya De Bruyne https://www.greensports.co.tz/2023/02/17/fa-wachunguza-kadhia-ya-de-bruyne/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/17/fa-wachunguza-kadhia-ya-de-bruyne/#respond Fri, 17 Feb 2023 09:45:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5188 London, EnglandChama cha Soka England (FA), kimeanzisha uchunguzi baada ya mchezaji wa Man City, Kevin de Bruyne kurushiwa vitu uwanjani katika mechi na Arsenal ambayo City ilishinda kwa mabao 3-1.De Bruyne alikumbana na kadhia hiyo wakati akitoka uwanjani na inaaminika mwamuzi wa mchezo huo uliochezwa juzi Jumatano, Anthony Taylor amelitaja tukio hilo katika ripoti yake.Arsenal […]

The post FA wachunguza kadhia ya De Bruyne first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Chama cha Soka England (FA), kimeanzisha uchunguzi baada ya mchezaji wa Man City, Kevin de Bruyne kurushiwa vitu uwanjani katika mechi na Arsenal ambayo City ilishinda kwa mabao 3-1.
De Bruyne alikumbana na kadhia hiyo wakati akitoka uwanjani na inaaminika mwamuzi wa mchezo huo uliochezwa juzi Jumatano, Anthony Taylor amelitaja tukio hilo katika ripoti yake.
Arsenal wanachunguza tukio hilo kupitia picha za CCTV na kuahidi kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kuhusika. “Hili jambo halikubaliki na halivumiliki,” alisema msemaji wa Arsenal.
De Bruyne katika mechi hiyo alifunga goli na kutoa pasi iliyozaa goli na kuipa City matokeo ambayo yameifanya iiengue Arsenal kileleni ingawa timu hizo zinalingana kwa pointi zote zikiwa na pointi 51 City ikineemeka na idadi ya mabao ya kufunga na City imecheza mechi moja kuizidi Arsenal.
Katika kinachoonekana kudhihaki tukio hilo, De Bruyne alitupia picha yake kwenye mtandao wa kijamii ikiwa na maneno, ‘asanteni’ na nyingine yenye ujumbe unaozungumzia unywaji wa bia.

The post FA wachunguza kadhia ya De Bruyne first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/17/fa-wachunguza-kadhia-ya-de-bruyne/feed/ 0