Euro 2024 - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 15 Jul 2024 07:12:56 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Euro 2024 - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Euro 2024, Ni Hispania https://www.greensports.co.tz/2024/07/15/euro-2024-ni-hispania/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/15/euro-2024-ni-hispania/#respond Mon, 15 Jul 2024 07:12:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11609 Berlin, UjerumaniNani kubeba taji la Euro 2024, ni kitendawili kilichotatiza mashabiki wa soka kwa siku kadhaa lakini Jumapili hii kimeteguliwa kwa Hispania kubeba taji hilo baada ya kuilaza England mabao 2-1.Ushindi wa Hispania unaendeleza maumivu makali ya England ambayo ilikuwa na matumaini ya kubeba taji hilo na hivyo kufuta unyonge wa taifa hilo wa miaka […]

The post Euro 2024, Ni Hispania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Berlin, Ujerumani
Nani kubeba taji la Euro 2024, ni kitendawili kilichotatiza mashabiki wa soka kwa siku kadhaa lakini Jumapili hii kimeteguliwa kwa Hispania kubeba taji hilo baada ya kuilaza England mabao 2-1.
Ushindi wa Hispania unaendeleza maumivu makali ya England ambayo ilikuwa na matumaini ya kubeba taji hilo na hivyo kufuta unyonge wa taifa hilo wa miaka 58 bila taji lolote kubwa la soka.
Mechi iliyozikutanisha timu ambazo awali hazikupewa nafasi ya kufika mbali lakini zilivuka hatua moja hadi nyingine na kukutana katika fainaili iliyopigwa mjini Berlin kwenye dimba la Olimpiki.
Aliyepeleka msiba England alikuwa ni Mikel Oyarzabal ambaye alifunga bao la ushindi dakika ya 86 akiunganisha krosi ya Marc Cucurella na Hispania kulilinda bao hilo hadi mwamuzi anapuliza filimbi ya kumaliza mchezo.
Kocha wa England, Gareth Southgate na wachezaji wake hawakuamini kilichotokea baada ya filimbi ya kumaliza mchezo kupulizwa, wakabaki vichwa chini kama watu wasiojua hatma yao baada ya matokeo hayo.
Hispaniam vinara wa taji hilo 2012, walianza kuzichana nyavu za England dakika mbili baada ya kuanza kipindi cha pili kwa bao la Nico Williams aliyeitumia pasi ya Lamine Yamal kufumua shuti lililomshinda kipa wa England, Jordan Pickford.
England walipambana na dakika 25 baadaye walisawazisha bao hilo kupitia Cole Palmer ambaye aliitumia pasi ya Jude Bellingham na hivyo kuibua matumaini mapya kwa mashabiki wa England ambao waliwazidi kila kitu wenzao wa Hispania.
Baada ya bao la kusawazisha kukawa na kila dalili hasa nje ya uwanja kwa mashabiki kwamba huu ulikuwa mwaka wa England hasa baada ya kupindua meza katika mechi zilizopita dhidi ya Slovakia, Switzerland na Uholanzi.


Katika mechi hizo England ilionesha kila dalili za kushindwa lakini ilifanikiwa kubadili matokeo na kusonga mbele hadi kufikia hatua ya fainali, imani iliendelea kuwa hivyo kwa mashabiki wa timu hiyo kabla ya kutulizwa na bao la Oyarzabal.
Maumivu ya England ambayo yamekuja baada ya kuwapo matumaini makubwa yanabadili mambo mengi kuhusu mambo ya baadaye ya timu hiyo moja kati ya hayo ni kuhusu kocha Southgate na nahodha wake Harry Kane.
Kane ameshindwa kuonesha ubora ambao amekuwa nao katika kikosi cha Bayern Munich na hata katika mechi ya fainali alilazimika kutupwa benchi na hoja inayoibuka sasa ni je ataendelea kuwa nahodha wa timu hiyo.
Kuhusu Southgate, hatma yake muda mrefu sasa imekuwa mjadala lakni baada ya timu hiyo kufikia hatua ya fainali kulikuwa na hoja ya kumtaka aendelee kikonoa kikosi hicho hadi kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026, je msimamo huo bado upo vile vile?

The post Euro 2024, Ni Hispania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/15/euro-2024-ni-hispania/feed/ 0
Kocha Uholanzi: VAR inaua soka https://www.greensports.co.tz/2024/07/11/kocha-uholanzi-var-inaua-soka/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/11/kocha-uholanzi-var-inaua-soka/#respond Thu, 11 Jul 2024 08:25:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11589 Dortmund, UjerumaniBaada ya Uholanzi kutolewa na England katika nusu fainali Euro 2024 kwa mabao 2-1, kocha wa timu hiyo, Ronaldo Koeman amelalamikia matumizi ya VAR akidai teknolojia hiyo inaua soka.Koeman alichukizwa na bao la England lililotokana na penalti iliyopigwa na Harry Kane baada ya mchezaji huyo kuchezewa rafu na mwamuzi kutumia VAR kujiridhisha kuhusu rafu […]

The post Kocha Uholanzi: VAR inaua soka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Dortmund, Ujerumani
Baada ya Uholanzi kutolewa na England katika nusu fainali Euro 2024 kwa mabao 2-1, kocha wa timu hiyo, Ronaldo Koeman amelalamikia matumizi ya VAR akidai teknolojia hiyo inaua soka.
Koeman alichukizwa na bao la England lililotokana na penalti iliyopigwa na Harry Kane baada ya mchezaji huyo kuchezewa rafu na mwamuzi kutumia VAR kujiridhisha kuhusu rafu hiyo na hatimaye England kupewa penalti.
Katika mechi hiyo, Uholanzi waliandika bao la kwanza kupitia Xavi Simons kabla ya England kupata penalti dakika ya 18 baada ya Denzel Dumfries kumkaba ndivyo sivyo Kane ambaye pamoja na hilo alifanikiwa kupiga mpira ambao ulipaa.
England iliendelea kupambana na kupata bao la pili na la ushindi lililofungwa katika dakika ya 90 na Ollie Witson ambaye aliingia akitokea benchi.
Awali mwamuzi wa mechi hiyo, Felix Zwayer hakutoa penalti lakini baadaye alitoa penalti hiyo aliposhauriwa kuangalia picha za VAR na ndipo alipotoa ishara ya penalti ambayo hatimaye iliipa England bao la kusawazisha.

“Kwa mtazamo wangu ile haikutakiwa kuwa penalti, aliupiga mpira, nafikiri sasa hatutoweza kucheza soka kwa katika namna nzuri na hii ni kwa sababu ya VAR, hakika inaharibu soka,” alisema Koeman.


Naye beki wa Uholanzi, Virgil van Dijk alisema kwamba penalti waliyopewa England ilibadili kila kitu katika mchezo huo.
“Nafikiri penalti ilikuwa tukui kubwa, England walipata hali ya kujiamini kupitia penalti, nafikiri maamuzi mengi hayakuwa mazuri kwetu, lakini sitaki kumzungumzia mwamuzi,” alisema Van Dijk ambaye pia ni beki wa Liverpool.
Kwa upande wake beki wa zamani wa Man United na England ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka, Gary Neville alisema kwamba Uholanzi wana kila sababu ya kuona wameumizwa.
“Nikiwa kama beki nafikiri ni uamuzi usiofdaa, hakuna namna unaweza kusema ile ilikuwa penalti, alikwenda kuzuia mpira, kwangu mimi ile si penalti,” alisema Neville.
Akizungumzia tukio hilo hilo, mshambuliaji wa zamani wa Newcastle na England ambaye kwa sasa pia ni mchambuzi, Alan Shearer alisema ni wazi kulikuwa na kugusana lakini beki wa Uholanzi alikuwa akijaribu kuzuia mpira.

The post Kocha Uholanzi: VAR inaua soka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/11/kocha-uholanzi-var-inaua-soka/feed/ 0
Ni England, Hispania fainali Euro 2024 https://www.greensports.co.tz/2024/07/11/ni-england-hispania-fainali-euro-2024/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/11/ni-england-hispania-fainali-euro-2024/#respond Thu, 11 Jul 2024 08:21:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11586 Dortmund, UjerumaniEngland imeilaza Uholanzi mabao 2-1 na sasa itaumana na Hispania Jumapili ijayo kwenye dimba la Olimpiki katika mechi ya fainali Euro 2024, mechi ambayo mshindi atakuwa bingwa wa fainali hizo.Ushindi wa England katika mechi hiyo ya nusu fainali iliyopigwa Jumatano hii unaifanya timu hiyo kusogea hatua zaidi katika mbio za kuliwania taji hilo ililolikosa […]

The post Ni England, Hispania fainali Euro 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Dortmund, Ujerumani
England imeilaza Uholanzi mabao 2-1 na sasa itaumana na Hispania Jumapili ijayo kwenye dimba la Olimpiki katika mechi ya fainali Euro 2024, mechi ambayo mshindi atakuwa bingwa wa fainali hizo.
Ushindi wa England katika mechi hiyo ya nusu fainali iliyopigwa Jumatano hii unaifanya timu hiyo kusogea hatua zaidi katika mbio za kuliwania taji hilo ililolikosa mwaka 2020 baada ya kulala mbele ya Italia kwa mikwaju ya penalti katika mechi ya fainali.
Uholanzi ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao mapema dakika ya saba Xavi Simons, kabla ya Harry Kane kusawazisha kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 18.
England ilipambana kwa hali na mali na kukawa na kila dalili kwamba timu hizo zingeenda katika dakika 30 za nyongeza lakini Ollie Witson aliyeingia akitokea benchi alibadili matokeo katika dakika ya 90 na kuipeleka England katika hatua ya fainali.
Hii sasa itakuwa mechi ya tatu kwa England dhidi ya Hispania kwenye fainali za Euro ikikumbukwa kuwa katika mechi mbili zilizopita England iliibuka na ushindi mara zote na swali ni je safari hii Hispania itakubali kuendeleza uteja wake kwa England?
Mwaka 1980 England iliifunga Hispania mabao 2-1 katika hatua ya makundi, fainali zilizopigwa nchini Italia na mwaka 1996, England ikiwa nyumbani katika Euro 96 iliitoa Hispania kwa mikwaju ya penalti katika hatua ya mtoano.

The post Ni England, Hispania fainali Euro 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/11/ni-england-hispania-fainali-euro-2024/feed/ 0
Mbappe: Nimefeli Euro 2024 https://www.greensports.co.tz/2024/07/11/mbappe-nimefeli-euro-2024/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/11/mbappe-nimefeli-euro-2024/#respond Thu, 11 Jul 2024 08:16:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11582 Munich, UjerumaniNahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe amekiri kufeli katika mbio zake kwenye fainali za soka za Euro 2024 baada ya timu hiyo kutolewa na Hispania katika nusu fainali kwa kipigo cha mabao 2-1.Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumanne, Mbappe alitoa pasi kwa Kolo Muani na kuipatia Ufaransa bao la kwanza […]

The post Mbappe: Nimefeli Euro 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe amekiri kufeli katika mbio zake kwenye fainali za soka za Euro 2024 baada ya timu hiyo kutolewa na Hispania katika nusu fainali kwa kipigo cha mabao 2-1.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumanne, Mbappe alitoa pasi kwa Kolo Muani na kuipatia Ufaransa bao la kwanza lakini Hispania ilijibu mapigo kwa mabao yaliyofungwa na Lamine Yamal na Dani Olmo.
Kwa ushindi huo, Hispania sasa itaumana na mshindi wa mechi kati ya England na Uholanzi katika mechi ya fainali itakayopigwa Jumapili mjini Berlin katika dimba la Olimpiki.
Mbappe ambaye anatarajia kutangazwa rasmi na klabu ya Real Madrid hivi karibuni, amemaliza fainali hizo akiwa na bao moja tu la penalti ambalo alifunga katika mechi dhidi ya Poland katika hatua ya makundi kabla ya kuumia pua.
:”Kuhusu mashindano, kwa upande wangu yalikuwa magumu, nilifeli, tulikuwa na matamanio ya kuwa mabingwa wa Ulaya, nilikuwa na matamanio ya kuwa bingwa Ulaya, haikuwa hivyo, kwa hiyo ni kufeli,” alisema Mbappe.

“Hayo ndiyo mambo ya soka, ni lazima sasa tuangalie mbele, kimekuwa kipindi kirefu cha mwaka mzima, na sasa nakwenda likizo na kupata muda wa kupumzika hilo litakuwa jambo zuri kwangu na baada ya hapo nitajitahidi nirudi nikiwa imara,” alisema Mbappe.


Mbappe amepitia kipindi kigumu katika fainali za Euro 2024 baada ya kuumia pua katika mechi ya kwanza ya Ufaransa dhidi ya Austria na kukosa mechi dhidi ya Uholanzi ingawa baadaye alicheza mechi zilizofuata akiwa amevaa kifaa maalum cha kulinda pua iliyoumia.

The post Mbappe: Nimefeli Euro 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/11/mbappe-nimefeli-euro-2024/feed/ 0
Ronaldo hana mpango kustaafu https://www.greensports.co.tz/2024/07/08/ronaldo-hana-mpango-kustaafu/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/08/ronaldo-hana-mpango-kustaafu/#respond Mon, 08 Jul 2024 19:10:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11569 Porto, UrenoWinga wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo amesema kwamba ataendelea kuichezea timu yake ya taifa licha ya kutolewa kwenye fainali za Euro 2024.Ronaldo, 39, amekuwa akihusishwa na mipango ya kustaafu kuichezea timu hiyo ingawa hivi karibuni alisema kwamba fainali za Euro 2024 ni za […]

The post Ronaldo hana mpango kustaafu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Porto, Ureno
Winga wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo amesema kwamba ataendelea kuichezea timu yake ya taifa licha ya kutolewa kwenye fainali za Euro 2024.
Ronaldo, 39, amekuwa akihusishwa na mipango ya kustaafu kuichezea timu hiyo ingawa hivi karibuni alisema kwamba fainali za Euro 2024 ni za mwisho kwake kwamba hatokuwamo kwenye fainali za 2028 ingawa hajasema lolote kuhusu fainali za Kombe la Dunia 2026 akiwa na miaka 41.
Kabla ya Ureno kutolewa kwenye fainali za Euro 2024 zinazoendelea nchini Ujerumani, Ronaldo alicheza mechi tano za michuano hiyo akitumia wastani wa dakika 97 kwa kila mechi.
Safari hii hata hivyo Ronaldo aliweka rekodi mpya ya kutotoka na bao katika michuano mikubwa ya kimataifa na hivyo hadithi ya kustaafu kwake ikazidi kupamba moto.
Ronaldo ambaye pia ndiye nahodha wa timu ya Ureno mara baada ya timu hiyo kutolewa kwenye Euro 2024 na Ufaransa kwa penalti 5-3, alitumia mitandao ya kijamii kuonesha kwamba huo si mwisho wake.
“Tunahitaji zaidi, tunastahili zaidi, ni kwa ajili yetu na kwa kila mmoja wenu, kwa ajili ya Ureno,” alisema nyota huyo wa zamani wa timu za Man United na Real Madrid.
Kocha wa timu ya taifa ya Ureno, Roberto MartĂ­nez mara baada ya timu yake kutolewa kwenye Euro 2024 alisema ni mapema mno kusema kwamba Ronaldo amecheza mechi yake ya mwisho akiwa na timu ya taifa lake.
Ronaldo alianza kuichezea timu ya Ureno mwaka 2003 na anashikilia rekodi ya kipekee akiwa ameifungia mabao 130 katika mechi 212, mwaka 2016 aliiwezesha kubeba taji la Euro 2016, michuano ambayo pia ameiwakilisha nchi yake katika fainali sita tofauti.

The post Ronaldo hana mpango kustaafu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/08/ronaldo-hana-mpango-kustaafu/feed/ 0
England, Uholanzi nusu fainali Euro https://www.greensports.co.tz/2024/07/07/england-uholanzi-nusu-fainali-euro/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/07/england-uholanzi-nusu-fainali-euro/#respond Sun, 07 Jul 2024 09:50:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11545 Berlin, UjerumaniUholanzi na England zimefuzu nusu fainali Euro 2024 na sasa zinasubiri kuumana katika mechi ambayo bingwa atacheza mechi ya fainali ya michuano hiyo dhidi ya mshindi wa mechi kati ya Ufaransa na Hispania.England iliibuka na ushindi wa mabao ya penalti 5-3 Jumamosi hii mbele ya Switzerland baada ya sare ya 1-1 katika dakika 90 […]

The post England, Uholanzi nusu fainali Euro first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Berlin, Ujerumani
Uholanzi na England zimefuzu nusu fainali Euro 2024 na sasa zinasubiri kuumana katika mechi ambayo bingwa atacheza mechi ya fainali ya michuano hiyo dhidi ya mshindi wa mechi kati ya Ufaransa na Hispania.
England iliibuka na ushindi wa mabao ya penalti 5-3 Jumamosi hii mbele ya Switzerland baada ya sare ya 1-1 katika dakika 90 za kawaida na 30 za nyongeza wakati Uholanzi imeibugiza Uturuki mabao 2-1.
Switzerland ndio waliokuwa wa kwanza kuzitikisa nyavu za England dakika ya 75 kwa bao la Breel Embolo ambalo lilitosha kuwaweka vichwa chini mashabiki wa England wasiamini kilichotokea.
England ambao katika mechi ya mtoano dhidi ya Slovakia waliokolewa kwa bao la kusawazisha la Jude Bellingham lililosaidia kuwafikisha robo fainali safari hii wameokolewa na bao la Bukayo Saka la dakika ya 80 na kuwapeleka nusu fainali.
Baada ya matokeo hayo, timu hizo zilipambana na kumaliza dakika 90 matokeo yakiwa hivyo hivyo na hata katika dakika 30 za nyongeza hakuna timu iliyopata bao na ndipo sheria ya mikwaju ya penalti ilipotumika na England kutoka na ushindi.
Katika mikwaju ya penalti, England walifunga kupitia Cole Palmer, Jude Bellingham, Saka, Ivan Toney na penalti ya mwisho ya ushindi ilifungwa na Trent Alexander-Arnold.
Aliyewaangusha Switzerland alikuwa ni Manuel Akanji ambaye shuti lake liliokolewa na kipa wa England, Jordan Pickford.
Nao Uholanzi wakiwa nyuma kwa bao 1-0 walifanikiwa kipindua matokeo na kutoka uwanjai na ushindi wa mabao 2-1.


Katika mechi hiyo Uturuki ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 35 lililofungwa kwa kichwa na beki wa kati ya timu hiyo Samet Akaydin akiunganisha krosi ya Arda Guler.
Kipindi chote cha kwanza kilitoa dalili njema kwa Uturuki hasa baada ya kupata bao hilo lakini dakika ya 70 Uholanzi ilisawazisha kupitia kwa Stefan de Vrij aliyeujaza mpira wavuni kwa kichwa.
Dakika saba baadaye mambo yaliwaharibikia, Uturuki baada ya Mert Muldur kujifunga na hivyo kuwazawadia bao la bure Uholanzi.
Mechi za nusu fainali Euro 2024
Jumanne Julai 9, 2024
Ufaransa vs Hispania
Jumatano Julai 10, 2024
England vs Uholanzi

The post England, Uholanzi nusu fainali Euro first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/07/england-uholanzi-nusu-fainali-euro/feed/ 0
Ujerumani, Ureno waaga Euro 2024 https://www.greensports.co.tz/2024/07/06/ujerumani-ureno-waaga-euro-2024/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/06/ujerumani-ureno-waaga-euro-2024/#respond Sat, 06 Jul 2024 07:07:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11538 Stuttgart, UjerumaniWenyeji Ujerumani wameaga fainali za Euro2 2024 baada ya kufungwa mabao 2-1 na Hispania katika mechi ya robo fainali kama ambavyo Ureno nayo imeaga fainali hizo baada ya kulala kwa penalti 5-3 mbele ya Ufaransa.Kwa matokeo ya mechi hizo zilizopigwa Ijumaa hii jioni, Ufaransa na Hispania baada ya kushinda sasa zitakutana Jumanne katika nusu […]

The post Ujerumani, Ureno waaga Euro 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Stuttgart, Ujerumani
Wenyeji Ujerumani wameaga fainali za Euro2 2024 baada ya kufungwa mabao 2-1 na Hispania katika mechi ya robo fainali kama ambavyo Ureno nayo imeaga fainali hizo baada ya kulala kwa penalti 5-3 mbele ya Ufaransa.
Kwa matokeo ya mechi hizo zilizopigwa Ijumaa hii jioni, Ufaransa na Hispania baada ya kushinda sasa zitakutana Jumanne katika nusu fainali ambayo mshindi wake atacheza mechi ya fainali.
Ushindi wa Hispania ulikuja baada ya mechi hiyo kupigwa kwa dakika 120 baada ya dakika 90 za kawaida kumalizika kwa sare ya 1-1 na ndipo Hispania waliponeemeka kwa bao la Mikel Merino katika dakika ya 119.
Hispania walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya sita ya kipindi cha pili mfungaji akiwa Dani Olmo ambaye aliujaza wavuni mpira uliotokana na krosi ya kinda wa miaka 16, Lamine Yamal.
Ujerumani baada ya kupambana walisawazisha bao hilo dakika ya 89 mfungaji akiwa Florian Wirtz, bao lililoamsha shangwe za mashabiki wa timu hiyo mwenyeji ambao walianza kukata tamaa.
Ufaransa yaitoa Ureno
Nayo Ufaransa ilifanikiwa kuitoa Ureno kwa mikwaju ya penalti 5-3 baada ya dakika 120 za kukata na shoka ambazo ziliisha kwa sare ya 0-0.
Ureno ambao waliitoa Slovenia katika hatua ya mtoano kwa mikwaju ya penalti walishindwa kuonesha ubora huo na kujikuta wakiziaga fainali hizo ambazo mwaka 2016 walibeba taji.


Macho ya mashabiki walio wengi yalikuwa kwa nyota wa Ureno mwenye miaka 39, Cristiano Ronaldo ambaye alisema kwamba fainali za Euro 2024 ni za mwisho kwake hivyo hatokuwapo kwenye fainali za 2028.
Ronaldo hata hivyo hakuweka wazi hatma yake kwenye timu ya taifa kwa ujumla kama ataendelea kuichezea kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 au la.
Mbali na Ronaldo, mchezaji mwingine ambaye aliteka hisia za mashabiki kabla ya mechi hiyo ni Kylian Mbappe wa Ufaransa lakini si yeye wala Ronaldo aliyeweza kuwa msaada kwa timu yake.
Kwa Mbappe ambaye anavaa kifaa maalum cha kuzuia pua iliyovunjika katika mechi ya kwanza dhidi ya Austria, hali ilikuwa mbaya zaidi kwani alitolewa na hivyo kutokuwamo katika mikwaju ya penalti.

The post Ujerumani, Ureno waaga Euro 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/06/ujerumani-ureno-waaga-euro-2024/feed/ 0
Mbappe afurahia kumkabili Ronaldo https://www.greensports.co.tz/2024/07/05/mbappe-afurahia-kumkabili-ronaldo/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/05/mbappe-afurahia-kumkabili-ronaldo/#respond Fri, 05 Jul 2024 05:37:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11530 Hamburg, UjerumaniNahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe amesema ni heshima kwake kucheza dhidi ya Cristiano Ronaldo katika mechi ya robo fainali ya Euro 2024 itakayopigwa leo Ijumaa.Mbappe, 25, nyota wa zamani wa PSG na ambaye tayari ameshasaini kuichezea Real Madrid, timu ambayo Ronaldo ameichezea kwa mafanikio na kushinda mataji manne […]

The post Mbappe afurahia kumkabili Ronaldo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Hamburg, Ujerumani
Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe amesema ni heshima kwake kucheza dhidi ya Cristiano Ronaldo katika mechi ya robo fainali ya Euro 2024 itakayopigwa leo Ijumaa.
Mbappe, 25, nyota wa zamani wa PSG na ambaye tayari ameshasaini kuichezea Real Madrid, timu ambayo Ronaldo ameichezea kwa mafanikio na kushinda mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Akiizungumzia mechi hiyo, Mbappe alisema kwamba ni jambo la kufurahia kucheza dhidi ya mchezaji huyo ambaye pia ametwaa tuzo za Ballon d’Or mara tano.
“Kwa wakati wote ni mchezaji ambaye nimekuwa nikivutiwa naye, nimewahi pia kupata nafasi ya kujuana naye na kuzungumza mara kadhaa, huwa tunawasiliana,” alisema Mbappe.
“Wakati wote amekuwa akijaribu kunipa ushauri na kuniarifu mambo mbalimbali yanayoendelea, kucheza dhidi yake ni heshima kutokana na kila kitu ambacho amewahi kukifanya katika soka,” alisema Mbappe.

“Bila ya kujali nini kitatokea kabla au baada ya mchezo, Ronaldo wakati wote atabaki kuwa gwiji lakini mwisho wa yote matumaini yetu Ufaransa ni kushinda na kufikia hatua ya nusu fainali,” alisema Mbappe.


Mbappe pia alisema kwamba Ronaldo ataendelea kuwa mmoja tu na anajiona mwenye bahati kwa kupata fursa ya kuendelea kuzipigania ndoto zake akiwa mchezaji wa Real Madrid kama ilivyokuwa kwa Ronaldo.
Ronaldo, 39, ameshasema kwamba anaamini fainali hizi za Euro 2024 ni za mwisho kwake na haamini kama atashiriki michuano hiyo kwa siku zijazo na hivyo mechi ya leo kwa mujibu wa Mbappe ni kama tukio la wachezaji mahiri kuagana.
Naye kiungo wa Man City, Bernando Silva ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Ureno na aliwahi kuwa pamoja na Mbappe katika timu ya Monaco amesema Mbappe wakati wote ni bora kwenye kundi la wachezaji.


“Kylian ni mchezaji wa kipekee na alianza nasi pale AS Monaco wakati huo akiwa na miaka 16, nakumbuka baada ya wiki ya kwanza tu tulianza kuulizana dogoo huy ni nani,” alisema Silva.
Silva aliwasifia Ronaldo na Mbappe kwa umahiri lakini alikataa kuingia katika hoja ya wachezaji hao kwenye mechi ya leo badala yake alisema kwamba ni mechi inayozihusu Ufaransa na Ureno na si Ronaldo na Mbappe. Mechi ya Ufaransa na Ureno itatanguliwa na mechi nyingine ya robo fainali kati ya wenyeji Ujerumani dhidi ya Hispania.

The post Mbappe afurahia kumkabili Ronaldo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/05/mbappe-afurahia-kumkabili-ronaldo/feed/ 0
Mendes amsubiri Mbappe kwa hamu https://www.greensports.co.tz/2024/07/04/mendes-amsubiri-mbappe-kwa-hamu/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/04/mendes-amsubiri-mbappe-kwa-hamu/#respond Thu, 04 Jul 2024 07:14:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11511 Munich, UjerumaniBeki wa kushoto wa timu ya taifa ya Ureno, Nuno Mendes (pichani) ameelezea furaha na shauku aliyonayo kukutana na mshambuliaji nyota wa Ufaransa, Kylian Mbappe katika mechi ya robo fainali ya Euro 2024 kesho Ijumaa.Mendes. 22, pia amewahi amecheza na Mbappe misimi miwili katika kikosi cha PSG kabla ya Mbappe kutangaza kuhamia Real Madrid […]

The post Mendes amsubiri Mbappe kwa hamu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Beki wa kushoto wa timu ya taifa ya Ureno, Nuno Mendes (pichani) ameelezea furaha na shauku aliyonayo kukutana na mshambuliaji nyota wa Ufaransa, Kylian Mbappe katika mechi ya robo fainali ya Euro 2024 kesho Ijumaa.
Mendes. 22, pia amewahi amecheza na Mbappe misimi miwili katika kikosi cha PSG kabla ya Mbappe kutangaza kuhamia Real Madrid akiwa mchezaji huru hivi karibuni.
Alisema kwamba yuko tayari kukabiliana na Mbappe kama mchezaji huyo atakuwa kwenye eneo lake kwani wakati wote huwa anafanya mazoezi ya kukabiliana na watu wa aina hiyo.

“Sina hakika kama atacheza katika eneo langu lakini kama itatokea hivyo nimeshajiandaa, huwa nafanya mazoezi mara kwa mara kwa matukio haya, tuko tayari kukabiliana nao,” alisema Mendes.


Mendes pia alikiri Ufaransa ina wachezaji wa hadhi ya juu lakini hapo hapo akasisitiza hata wao Ureno wana wachezaji wa aina hiyo na wanahitaji kufanya kila liwezekanalo ili kuizuia nguvu ya Ufaransa ili wao Ureno wacheze soka lao.
Katika kikosi cha Ureno kwenye fainali za Euro 2024 zinazoendelea nchini Ujerumani, Mendes pia yuko timu moja na Cristiano Ronaldo, staa wa zamani wa timu za Man United na Real Madrid na mshindi mara tano wa tuzo za Ballon d’Or.
Akiwazungumzia Mbappe na Ronaldo, Mendes alisema ni wachezaji wa kiwango cha juu duniani wenye uwezo wa kubadili matokeo katika mazingira yoyote.


“Wote hawa nimekuwa nao pamoja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na ni jambo la kufurahia kucheza na MbappĂ© na Cristiano. Ni wachezaji wa kipekee, kutoka tukio moja hadi jingine wana uwezo wa kuleta utofauti,” alisema Mendes.
Alipoulizwa kati ya wachezaji hao anaweza kumchagua yupi, Mendes alisema kwamba hilo kwake ni swali gumu na kama angekuwa kocha basi angewachagua wote wawili.

The post Mendes amsubiri Mbappe kwa hamu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/04/mendes-amsubiri-mbappe-kwa-hamu/feed/ 0
Ronaldo: Euro 2024 ndio mwisho https://www.greensports.co.tz/2024/07/03/ronaldo-euro-2024-ndio-mwisho/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/03/ronaldo-euro-2024-ndio-mwisho/#respond Wed, 03 Jul 2024 06:29:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11493 Munich, UjerumaniWinga wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amethibitisha kuwa fainali za soka Euro 2024 ni za mwisho kwake akiwa na timu yake ya taifa na hakuna ubishi kwamba zitakuwa zenye kuvutia.Hii ni mara ya sita kwa Ronaldo kushiriki fainali hizo maarufu Euro ambazo hufanyika kila baada ya miaka minne zikishirikisha timu za […]

The post Ronaldo: Euro 2024 ndio mwisho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Winga wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amethibitisha kuwa fainali za soka Euro 2024 ni za mwisho kwake akiwa na timu yake ya taifa na hakuna ubishi kwamba zitakuwa zenye kuvutia.
Hii ni mara ya sita kwa Ronaldo kushiriki fainali hizo maarufu Euro ambazo hufanyika kila baada ya miaka minne zikishirikisha timu za mataifa ya Ulaya.
Fainali zijazo za Euro yaani Euro 2028 zitafanyika Uingereza na Jamhuri ya Ireland na wakati huo, Ronaldo, nyota wa zamani wa timu za Man United, Real Madrid na Juventus atakuwa na miaka 43.
“Hakuna ubishi kwamba hizi ni fainali za mwisho kwangu za Euro, lakini si kwamba ninazungumza kwa sababu ya hamasa tu, hapana ni masuala ya soka na mapenzi yangu kwa kila kitu kwenye mchezo huu,” alisema.
“Mvuto nilionao katika mchezo huu, namna ninavyoupenda, nawaona mashabiki, familia yangu na watu waliojaa mapenzi ya soka, hivyo si suala la kutengana na soka moja kwa moja, kwani ni nini kingine kwangu ninachoweza kukifanya ili nishinde?” alihoji Ronaldo.
Ronaldo ambaye alianza kuichezea timu ya taifa ya Ureno mara ya kwanza mwaka 2003, aliisaidia kubeba taji la michuano hiyo mwaka 2016 na ndiye kinara wa mabao kwa sasa akiwa ameifungia timu hiyo mabao 130.

“Jambo muhimu zaidi katika safari hii ni ule mvuto ambao bado ninao wa kuendelea kuwa hapa, ni miaka 20 ya kuiwakilisha na kuichezea timu ya taifa, kuwapa watu, familia yangu na watoto wangu furaha, hilo ndilo linalonihamasisha zaidi,” alisema Ronaldo.


Juzi Jumatatu Ronaldo alikuwa katika majaribu baada ya mkwaju wa penalti alioupiga kuokolewa na kipa wa Slovenia Jan Oblak katika dakika ya 114 ingawa Ureno walishinda katika penalti tano tano na kufuzu kucheza robo fainali.


Baada ya kukosa penalti hiyo, Ronaldo ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia alijikuta akimwaga chozi kabla ya kutulizwa na wachezaji wenzake.
“Ni mambo ya soka, wale ambao hushindwa ndio hao hao ambao hujaribu, wakati wote nitakuwa mwenye kufanya katika ubora wangu niwapo na jezi hii, bila kujali iwe ni kushindwa au kushinda,” alisema Ronaldo.

The post Ronaldo: Euro 2024 ndio mwisho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/03/ronaldo-euro-2024-ndio-mwisho/feed/ 0