Eto'o - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 30 May 2024 06:51:26 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Eto'o - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Eto’o amuweka kando kocha mkuu Cameroon https://www.greensports.co.tz/2024/05/30/etoo-amuweka-kando-kocha-mkuu-cameroon/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/30/etoo-amuweka-kando-kocha-mkuu-cameroon/#respond Thu, 30 May 2024 06:51:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11177 Yaounde, CameroonHali bado tete katika soka Cameroon baada ya shirikisho la soka nchini humo, Facefoot ambalo linaongozwa na mwanasoka wa zamani, Samuel Eto’o kumuweka kando kocha mkuu, Marc Brys (pchani) .Uongozi wa Facefoot umekuja na azimio hilo baada ya kuibuka mzozo kati ya kocha huyo na Eto’o na tayari shirikisho hilo limemteua Martin Ndtoungou kuwa […]

The post Eto’o amuweka kando kocha mkuu Cameroon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Yaounde, Cameroon
Hali bado tete katika soka Cameroon baada ya shirikisho la soka nchini humo, Facefoot ambalo linaongozwa na mwanasoka wa zamani, Samuel Eto’o kumuweka kando kocha mkuu, Marc Brys (pchani) .
Uongozi wa Facefoot umekuja na azimio hilo baada ya kuibuka mzozo kati ya kocha huyo na Eto’o na tayari shirikisho hilo limemteua Martin Ndtoungou kuwa kocha wa muda wa timu hiyo.
Brys, kocha kutoka Ubelgiji ambaye aliteuliwa na serikali, juzi Jumanne alizozana na Eto’o na sasa hatokuwa na timu hiyo inayojiandaa kwa mechi za kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026.
Habari za ndani zinadai kwamba viongozi Facefoot hawakukubaliana na uteuzi wa kocha huyo ambao ulifanywa Aprili mwaka huu na serikali kupitia wizara ya michezo bila ya kuwashirkisha viongozi wa shirikisho hilo.
Katika mzozo wa Jumanne, Brys alialikwa katika ofisi za Facefoot kwenye kikao cha kupanga mikakati ya kazi lakini baadhi ya wasaidizi wake walizuiwa kuingia kwenye jengo la ofisi za shirikisho hilo mjini Yaounde.
Baada ya tafrani hiyo, Eto’o na kamati yake katika Facefoot wakaitisha kikao cha dharura na ndicho kilichofikia uamuzi wa kumuweka kando Brys jambo ambalo ni wazi litaliingiza shirikisho hilo katika mgogoro na serikali.
Timu ya Cameroon au Indomitable Lions, katika mbio za kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026, hadi sasa ina pointi nne baada ya kushinda mechi moja na kutoka sare moja, Juni 8 itaumana na Cape Verde kabla ya kucheza na Angola siku tatu baadaye.

The post Eto’o amuweka kando kocha mkuu Cameroon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/30/etoo-amuweka-kando-kocha-mkuu-cameroon/feed/ 0
Usajili wa Eto’o Chelsea wachunguzwa https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/usajili-wa-etoo-chelsea-wachunguzwa/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/usajili-wa-etoo-chelsea-wachunguzwa/#respond Wed, 01 Nov 2023 19:52:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8331 London, EnglandUsajili wa wachezaji Samuel Eto’o na Willian katika klabu ya Chelsea mwaka 2013 ni kati ya matukio ya Ligi Kuu England yanayochunguzwa yakihusishwa na ukiukwaji wa taratibu za matumizi ya fedha.Julai mwaka huu, Umoja wa Vyama vya Soka Ulaya (Uefa) ulitangaza kuitoza Chelsea faini ya Dola 10.65 milioni kwa kutoa taarifa za fedha zilizoonekana […]

The post Usajili wa Eto’o Chelsea wachunguzwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Usajili wa wachezaji Samuel Eto’o na Willian katika klabu ya Chelsea mwaka 2013 ni kati ya matukio ya Ligi Kuu England yanayochunguzwa yakihusishwa na ukiukwaji wa taratibu za matumizi ya fedha.
Julai mwaka huu, Umoja wa Vyama vya Soka Ulaya (Uefa) ulitangaza kuitoza Chelsea faini ya Dola 10.65 milioni kwa kutoa taarifa za fedha zilizoonekana kuwa na utata zikihusisha biashara zilizofanyika kati ya mwaka 2012 hadi 2019.
Habari zaidi zilidai kwamba katika matumizi ya fedha yaliyofanyika katika kipindi hicho na ambayo yanafanyiwa uchunguzi yamo yale yaliyohusisha usajili wa winga Willian pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Barcelona, Samuel Eto’o.
Chelsea ilimsajili Willian huku habari zaidi zikidai kwamba mchezaji huyo alikuwa mbioni kusajiliwa na Tottenham kabla ya Chelsea kuvuruga mpango huo na siku chache baadaye alisajiliwa Eto’o ambaye pia alikuwa nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Cameroon.
Wachezaji wote hao waliosajiliwa mwaka 2013 walitokea klabu ya Anzhi Makhachkala ya nchini Urusi, wakati Willian kwa sasa anaichezea Fulham, Eto’o alistaafu soka miaka minne iliyopita na sasa ni rais wa chama cha soka nchini Cameroon.
Wakati matukio hayo yakitokea Chelsea ilikuwa ikimilikiwa na bilionea wa Urusi, Roman Abramovich ambaye aliinunua mwaka 2003 lakini mwaka jana alilazimika kuiuza baada ya Serikali ya Uingereza kudai kuwa alikuwa na ukaribu na rais wa Urusi, Vladimir Putin ambaye alikuwa akipigwa vita kwa kuivamia kijeshi Ukraine.

The post Usajili wa Eto’o Chelsea wachunguzwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/usajili-wa-etoo-chelsea-wachunguzwa/feed/ 0