Eric ten Hag - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 24 Feb 2023 12:40:18 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Eric ten Hag - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ushindi wampa jeuri Ten Hag https://www.greensports.co.tz/2023/02/24/ushindi-wampa-jeuri-ten-hag/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/24/ushindi-wampa-jeuri-ten-hag/#respond Fri, 24 Feb 2023 07:43:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5290 Manchester, EnglandUshindi wa mabao 2-1 ambao Man United imeupata jana Alhamisi usiku dhidi ya Barca, umempa jeuri kocha wa timu hiyo Erik ten Hag ambaye amesema sasa wanaweza kuifunga timu yoyote.Man United ikiwa nyumbani Old Trafford iliibuka na ushindi huo katika mechi ya Europa Ligi na sasa inajiandaa kucheza hatua nyingine ya michuano hiyo huku […]

The post Ushindi wampa jeuri Ten Hag first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Ushindi wa mabao 2-1 ambao Man United imeupata jana Alhamisi usiku dhidi ya Barca, umempa jeuri kocha wa timu hiyo Erik ten Hag ambaye amesema sasa wanaweza kuifunga timu yoyote.
Man United ikiwa nyumbani Old Trafford iliibuka na ushindi huo katika mechi ya Europa Ligi na sasa inajiandaa kucheza hatua nyingine ya michuano hiyo huku ikiwa imeitoa Barca katika mashindano hayo.
Ushindi huo ni tukio jingine kubwa la timu hiyo kuwaangusha baadhi ya vigogo wa soka barani Ulaya msimu huu ikiwa tayari imeshazipa vipigo, Arsenal na Liverpool za England.
Ten Hag katika kudhihirisha anavyojiamini alisema kwamba kuanzia sasa hadi mwezi Mei hawatoiogopa timu yoyote, “Unahitaji matokeo mazuri ili uamini una nguvu,” alisema kocha huyo Mholanzi.
“Nafikiri hii ni hatua nyingine muhimu kwani unapoifunga Barcelona (Barca), moja ya timu bora katika hatua hii ya Ulaya, hapo unakuwa unajiamini kwamba uko imara na kuwa tayari kumfunga yeyote.”

“Ulikuwa ni usiku wa kipekee, nafikiri ni jambo ‘bab kubwa’ unapoifunga Barcelona, inaongoza La Liga ikiwa mbele ya Real Madrid kwa pointi nane na tumeona Real ilivyocheza wiki hii (imeifunga Liverpool 5-2),” alisema Ten Hag ambaye huu ni msimu wake wa kwanza Man United.


“Tumecheza katika kiwango kizuri na tunatakiwa kuendelea hivyo msimu huu, kuendelea na kiwango hiki katika kuamini kwamba tunaweza kushinda mechi kubwa,” alisema.
Katika mechi hiyo, Barca ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 18 lililofungwa na Robert Lowandowski kwa penalti iliyotolewa baada ya Bruno Fernandes kumchezea rafu Alejandro Balde.
Man United iliandika bao la kusawazisha dakika ya 47 lililofungwa na Fred kabla Mbrazil mwenzake Antony hajamalizia bao la pili dakika ya 72.
Katika mechi ya awali baina ya timu hizo iliyopigwa Nou Camp, matokeo yalikua sare ya mabao 2-2 na hiyo maana yake ni kwamba Man United sasa inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3.
Matokeo mechi za Europa Ligi Alhamisi hii…
Nantes 0-3 Juventus
PSV Eindhoven 2-0 Sevilla
Man Utd 2-1 Barcelona
FC Midtjylland 0-4 Sporting
Monaco 2-3 B Leverkusen
(B Leverkusen 5-3 Monaco-penalti)
Union Berlin 3-1 Ajax
Rennes 2-1 Shakhtar Donetsk
(Shakhtar Donetsk 5-4 Rennes-penalti)
Roma 2-0 RB Salzburg

The post Ushindi wampa jeuri Ten Hag first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/24/ushindi-wampa-jeuri-ten-hag/feed/ 0
Ten Hag atoa angalizo mechi ya Barca https://www.greensports.co.tz/2023/02/23/ten-hag-atoa-angalizo-mechi-ya-barca/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/23/ten-hag-atoa-angalizo-mechi-ya-barca/#respond Thu, 23 Feb 2023 06:28:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5271 Manchester, EnglandMan United leo Alhamisi inaumana na Barca katika mechi ya Europa Ligi, mechi ambayo kocha wa timu hiyo, Eric ten Hag amesema ili washinde ni lazima wacheze katika kiwango bora cha msimu huu.Katika mechi iliyopita ambayo Man United walikuwa ugenini timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 na leo Man United watakuwa nyumbani Old […]

The post Ten Hag atoa angalizo mechi ya Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Man United leo Alhamisi inaumana na Barca katika mechi ya Europa Ligi, mechi ambayo kocha wa timu hiyo, Eric ten Hag amesema ili washinde ni lazima wacheze katika kiwango bora cha msimu huu.
Katika mechi iliyopita ambayo Man United walikuwa ugenini timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 na leo Man United watakuwa nyumbani Old Trafford.
“Unapokutana na timu kubwa kama hizo unalazimika kucheza katika ubora wako vinginevyo huna nafasi,” alisema Ten Hag.
Baada ya mechi ya leo ambayo ni ya hatua ya 16 bora, Jumapili Man United wana mechi nyingine ya fainali ya kukata na shoka dhidi ya Newcastle kuwania taji la Carabao kwenye dimba la Wembley.
Wakifanikiwa kulibeba taji hilo, itakuwa mara ya kwanza kwa kocha Ten Hag kubeba taji akiwa na timu hiyo lakini pia litakuwa taji la kwanza kwa timu hiyo tangu mwaka 2017.
Kama hiyo haitoshi Machi Mosi, timu hiyo itakuwa na mechi ya Kombe la FA raundi ya tano dhidi ya West Ham, mechi ambayo wakishinda pia watakuwa wamepiga hatua muhimu katika mbio za kusaka taji hilo.
Katika Ligi Kuu England (EPL) pia huwezi kuitoa Man United katika mbio za kuliwania taji hilo msimu huu, inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 49, imezidiwa na vinara Arsenal kwa pointi tano na pointi tatu dhidi ya Man City inayoshika nafasi ya pili.

“Tuna fursa lakini fikra za kwanza wakati wote ni katika mechi inayofuata, na hatuwezi kubeba taji la Europa Ligi wiki hii, ni lazima tujiweke katika mtazamo kwamba kila siku tunatakiwa kuwa na malengo yaliyo bora kwa ajili yetu,” alisema Ten Hag.


Ten Hag pia alizungumzia kitendo cha yeye kupata chakula cha jioni na kocha wa zamani wa Man United, Sir Alex Ferguson aliyeweka rekodi ya kubeba mataji 13 akisema kwamba jambo hilo lilikuwa na maana kubwa kwake.
“Wakati wote nafurahia kuzungumza na watu ambao wana uelewa wa mambo, uzoefu mkubwa, anataka kushirikisha watu, anataka kukusaidia na kukuunga mkono,” alisema Ten Hag.
“Unaona kama vile Manchester United ni klabu yake, anaona anatakiwa kujitoa kwa klabu na anataka kuona tunafanya vizuri, ulikuwa usiku mzuri na nafikiria siku nyingine ya kukutana naye kwa chakula cha jioni,” alisema.
Winga wa Man United, Antony na beki Harry Maguire wako fiti kwa mechi hiyo baada ya kuwa majeruhi wakati mshambuliaji Anthony Martial bado majeruhi na beki Lisandro Martinez na kiungo Marcel Sabitzer wamemaliza adhabu.
Barca leo itawakosa viungo Pedri ambaye ni majeruhi na Gavi anayetumikia adhabu huku mshambuliaji Mfaransa Ousmane Dembele hatokuwapo kwa kuwa bado anasumbuliwa na misuli ingawa kiungo mkongwe, Sergio Busquets aliyekuwa na matatizo ya enka kwa sasa yuko fiti.
Kocha wa Barca Xavi akiizungumzia mechi hiyo alisema: “Hakika itakuwa mechi ngumu, Manchester United ni moja ya timu bora za Ulaya na hilo wamekuwa wakilithibitisha.
Mechi za Europa Ligi leo Alhamisi ni kama ifutavyo…
Man Utd v Barcelona
FC Midtjylland v Sporting
Monaco v B Leverkusen
Nantes v Juventus
PSV Eindhoven v Sevilla
Union Berlin v Ajax
Rennes v Shakhtar Donetsk
Roma v RB Salzburg

The post Ten Hag atoa angalizo mechi ya Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/23/ten-hag-atoa-angalizo-mechi-ya-barca/feed/ 0