Enzo Fernandez - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 08 Aug 2024 13:06:35 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.5 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Enzo Fernandez - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kocha Chelsea amtetea nahodha Enzo https://www.greensports.co.tz/2024/08/08/kocha-chelsea-amtetea-nahodha-enzo/ https://www.greensports.co.tz/2024/08/08/kocha-chelsea-amtetea-nahodha-enzo/#respond Thu, 08 Aug 2024 13:06:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11738 Chicago, MarekaniKocha wa Chelsea, Enzo Maresca ametetea uamuzi wa kumpa unahodha Enzo Fernandez katika mechi ya kirafiki na Real Madrid akisema suala hilo liko wazi kwa kuwa mchezaji huyo anaheshimika katika kikosi cha timu hiyo.Fernandez (pichani juu), ambaye pia ni kiungo wa timu ya taifa ya Argentina, alipewa kitambaa cha unahodha wakati wa kipindi cha […]

The post Kocha Chelsea amtetea nahodha Enzo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Chicago, Marekani
Kocha wa Chelsea, Enzo Maresca ametetea uamuzi wa kumpa unahodha Enzo Fernandez katika mechi ya kirafiki na Real Madrid akisema suala hilo liko wazi kwa kuwa mchezaji huyo anaheshimika katika kikosi cha timu hiyo.
Fernandez (pichani juu), ambaye pia ni kiungo wa timu ya taifa ya Argentina, alipewa kitambaa cha unahodha wakati wa kipindi cha pili, mechi ambayo Chelsea ililala kwa mabao 2-1.
Uamuzi wa kumpa mchezaji huyo kitambaa cha unahodha umeacha maswali kwani anakumbukwa kwa kuandamwa na kashfa ya ubaguzi wa rangi iliyoibuka katika timu yake ya taifa.
Wakati akishangilia ushindi wa Argentina kwenye Copa America, Enzo, 23, alitupia picha ya video iliyomuonesha akiwa na wachezaji wenzake wa timu ya taifa wakiimba nyimbo ya kuwadhihaki wachezaji wa Ufaransa wenye asili ya Afrika.
Zaidi ya hilo, Fernandez pia amepewa jukumu hilo kutoka kwa Reece James ambaye hapo kabla alinukuliwa akisema kwamba alichokifanya Fernandez kinaweza kusababisha matatizo miongoni mwa wachezaji wa Chelsea.
Beki wa Chelsea, Wesley Fofana alichukizwa na video hiyo wakati klabu ya Chelsea ilitoa taarifa ya kulaani kitendo kilichofanywa na Fernandez.
Baada ya kitendo hicho Fernandez aliomba radhi ingawa Maresca alimtetea akisema kwamba mchezaji huyo hakuwa na nia mbaya katika tukio hilo.

“Niwe tu mkweli nafikri tulipombadili Reece tuliamua kumpa kitambaa cha unahodha Enzo, na hii inaonesha jinsi anavyoheshimika katika kikosi, nafikiri hilo lipo wazi,” alisema Maresca.


Chelsea Jumapili inatarajia kucheza na Inte Milan katika mechi ya kirafiki ambayo inatarajia kuwa ya mwisho kabla ya kuanza rasmi msimu wa 2024-25 ambapo itauanza kwa mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Man City.

The post Kocha Chelsea amtetea nahodha Enzo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/08/08/kocha-chelsea-amtetea-nahodha-enzo/feed/ 0
Chelsea yamtangazia ofa kubwa Fernandez https://www.greensports.co.tz/2023/01/30/chelsea-yamtangazia-ofa-kubwa-fernandez/ https://www.greensports.co.tz/2023/01/30/chelsea-yamtangazia-ofa-kubwa-fernandez/#respond Mon, 30 Jan 2023 20:22:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4925 London, EnglandChelsea imetoa ofa ya Pauni 105 milioni ili kumsajili kiungo wa Benfica na timu ya Taifa ya Argentina, Enzo Fernandez dau ambalo likikamilika litamfanya mchezaji huyo aweke rekodi ya uhamisho.Hadi sasa bado hakuna uhakika kama ofa hiyo itakubaliwa na ikikubaliwa, itakuwa kubwa kuliko ile ya mwaka 2021 ambapo Man City ilitoa Pauni 100 milioni […]

The post Chelsea yamtangazia ofa kubwa Fernandez first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Chelsea imetoa ofa ya Pauni 105 milioni ili kumsajili kiungo wa Benfica na timu ya Taifa ya Argentina, Enzo Fernandez dau ambalo likikamilika litamfanya mchezaji huyo aweke rekodi ya uhamisho.
Hadi sasa bado hakuna uhakika kama ofa hiyo itakubaliwa na ikikubaliwa, itakuwa kubwa kuliko ile ya mwaka 2021 ambapo Man City ilitoa Pauni 100 milioni kumsajili Jack Grealish kutoka Aston Villa.
Fernandez amejipatia umaarufu zaidi wakati wa fainali za Kombe la Dunia akiwa na timu ya Argentina ambayo hatimaye ilibeba taji hilo huku mchezaji huyo akitangazwa kuwa nyota mwenye umri mdogo.
Benfica iliwahi kuituhumu Chelsea kwa kumsumbua kiungo huyo ambapo kocha wake, Roger Schmidt aliwahi kunukuliwa akisema kwamba ‘wameufunga’ mpango wa Chelsea kumsajili mchezaji huyo.
Ni dhahiri kwamba uamuzi wa Chelsea kutangaza dhamira ya kumtaka mchezaji huyo huenda wana uhakika mpango wao unaelekea kufanikiwa.
Fernandez alijiuunga na Benfica akitokea klabu ya River Plate ya Argentina August mwaka jana kwa ada ya Pauni 10 milioni na hadi sasa ameifungia timu hiyo mabao manne katika mechi 29 za Ligi Kuu ya Ureno.
Iwapo usajili wa mchezaji huyo ambaye Januari 17 mwaka huu alifikisha miaka 22, utafanikiwa utaifanya Chelsea kushika nafasi ya kwanza kwa kutumia pesa nyingi za usajili kwa msimu mmoja.
Tangu majira ya kiangazi klabu hiyo imetumia Pauni 270 milioni ikiwa imezidiwa na Real Madrid pekee hadi sasa ambayo mwaka 2019 ilitumia Pauni 292 milioni.

The post Chelsea yamtangazia ofa kubwa Fernandez first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/01/30/chelsea-yamtangazia-ofa-kubwa-fernandez/feed/ 0