Emerse Fae - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 21 Feb 2024 06:37:40 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Emerse Fae - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Fae sasa kocha mkuu Ivory Coast https://www.greensports.co.tz/2024/02/21/fae-sasa-kocha-mkuu-ivory-coast/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/21/fae-sasa-kocha-mkuu-ivory-coast/#respond Wed, 21 Feb 2024 06:37:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9817 Abidjan, Ivory CoastAliyekuwa kocha wa muda wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Emerse Fae (pichani) hatimaye ameteuliwa kuwa kocha mkuu baada ya kuiwezesha timu ya taifa hilo kubeba taji la mataifa ya Afrika au Afcon.Fae, 42, alikuwa kocha msaidizi wakati fainali za Afcon 2023 zikianza nchini Ivory Coast lakini akateuliwa kuwa kocha wa muda […]

The post Fae sasa kocha mkuu Ivory Coast first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Abidjan, Ivory Coast
Aliyekuwa kocha wa muda wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Emerse Fae (pichani) hatimaye ameteuliwa kuwa kocha mkuu baada ya kuiwezesha timu ya taifa hilo kubeba taji la mataifa ya Afrika au Afcon.
Fae, 42, alikuwa kocha msaidizi wakati fainali za Afcon 2023 zikianza nchini Ivory Coast lakini akateuliwa kuwa kocha wa muda baada ya kutimuliwa kwa Mfaransa, Jean-Louis Gasset timu hiyo ilipopoteza mechi mbili kati ya tatu za hatua ya makundi.
Pamoja na matokeo mabaya ya awali, Ivory Coast iliweza kupenya hadi kwenye hatua ya mtoano inayoshirikisha timu 16 na kusonga mbele hadi fainali kabla ya kubeba kombe.

“Emerse Fae ambaye ni kocha wa muda, sasa anathibitishwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Ivory Coast,” ilieleza taarifa ya raia wa Shirikisho la Soka Ivory Coast, Idriss Diallo.


Mafanikio ya Fae yamewashtua wengi kwani hakuwa na uzoefu wowote katika kazi ya ukocha kabla ya hapo, alianza kwa kuinoa timu ya vijana wadogo ya Nice ya Ufaransa na hapo hapo akawa kocha wa wachezaji wa akiba wa Clermont Foot.
Fae pia enzi zake za kucheza soka la ushindani aliwahi kuzichezea klabu za Nice ya Ufaransa na Reading ya England na timu ya taifa ya Ivory Coast aliyoiwakilisha kwenye fainali tatu za Afcon pamoja na Kombe la Dunia 2006 nchini Ujerumani.

The post Fae sasa kocha mkuu Ivory Coast first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/21/fae-sasa-kocha-mkuu-ivory-coast/feed/ 0