Diego Simeone - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 25 Jan 2026 11:06:24 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Diego Simeone - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Vini amchokoza Simeone mitandaoni https://www.greensports.co.tz/2026/01/10/vini-amchokoza-simeone-mitandaoni/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/10/vini-amchokoza-simeone-mitandaoni/#respond Sat, 10 Jan 2026 18:13:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14268 Mdrid, HispaniaWinga wa Real Madrid, Vinícius Júnior ametumia mitandao ya kijamii kumdhihaki kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone kwa kumwambia kuwa amepoteza pambano jingine la mtoano.Kauli hiyo ya Vinicius, ‘Vinicius Jr’ au ‘Vini’ imeambatana na picha ya video ikihusisha mechi baina ya timu hiyo iliyochezwa Alhamisi Januari 8, 2026 na Real Madrid kushinda kwa mabao […]

The post Vini amchokoza Simeone mitandaoni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Mdrid, Hispania
Winga wa Real Madrid, Vinícius Júnior ametumia mitandao ya kijamii kumdhihaki kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone kwa kumwambia kuwa amepoteza pambano jingine la mtoano.
Kauli hiyo ya Vinicius, ‘Vinicius Jr’ au ‘Vini’ imeambatana na picha ya video ikihusisha mechi baina ya timu hiyo iliyochezwa Alhamisi Januari 8, 2026 na Real Madrid kushinda kwa mabao 2-1.
Katika mechi hiyo ya nusu fainali ya Spanish Supercopa iliyopigwa mjini Jeddah, Saudi Arabia, mjadala wa baada ya mechi ulihusisha utata uliojitokeza baina ya Vini na Simeone wakati wa mechi.
Kamera za televisheni ziliwaonesha wawili hao wakizozana katika kipindi cha kwanza kuhusu madai ya Atletico kutaka wapewe penalti huku Simeone akimwambia Vini zaidi ya mara moja kwamba ataachwa na Real Madrid.
Baadaye, Simeone na Vini wote walipewa kadi za njano kutokana na mzozo huo wa maneno kabla ya kocha wa Real Madrid, Xabi Alonso na wasaidizi wake kuingilia kati na baadaye Vini kufanyiwa mabadiliko.
Simeone alipotakiwa kutoa maoni yake baada ya mechi alisema hakumbuki nini alikisema kwa kuwa ya uwanjani yanabaki uwanjani.

“Sina la kusema, mambo yanayotokea uwanjani yanabaki uwanjani, sina kumbukumbu, mimi si mtu mwenye kumbukumbu nzuri,” slisema Simeone.


Kwa upande wake Alonso alisema hakufurahishwa na tabia za Simeone na hakulipenda tukio zima baina ya Vini na Simeone hasa kauli za Simeone.
“Sijapenda kilichotokea, hayo mambo yamevuka mipaka katika suala zima la kuheshimu mwenzako, alichokisema (Simeone) si mfano wa tabia za mwanamichezo mstaarabu, kuna mipaka,” alisema Alonso.
Baadaye ndipo Vini alipotumia mtandao wa Instgram kutoa maoni yalioonekana kumdhihaki Simeone akidai kocha huyo amepoteza pambano jingine la mtoano, maoni yaliyoambatana na picha ya tukio la mzozo wake na Simeone.
Real Madrid ambao sasa watacheza mechi ya fainali na mahasimu wao Barca, ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Federico Valverde kwa mpira wa adhabu na baadaye Rodrygo akaongeza la pili wakati bao pekee la Atletico lilifungwa na Alexander Sorloth.

The post Vini amchokoza Simeone mitandaoni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/10/vini-amchokoza-simeone-mitandaoni/feed/ 0
Arteta ampamba Diego Simeone https://www.greensports.co.tz/2025/10/21/arteta-ampamba-diego-simeone/ https://www.greensports.co.tz/2025/10/21/arteta-ampamba-diego-simeone/#respond Tue, 21 Oct 2025 15:15:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14020 London, EnglandWakati Arsenal ikisubiri kuivaa Atletico Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amemsifia kocha wa Atletico, Diego Simeone (pichani) akidai anaamini kocha huyo anaweza kuchukua nafasi ya kocha yeyote England.Simeone amekuwa kocha wa Atletico tangu Desemba 2011 akiwa sasa anafikisha miaka 14 na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Hispania maarufu […]

The post Arteta ampamba Diego Simeone first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Wakati Arsenal ikisubiri kuivaa Atletico Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amemsifia kocha wa Atletico, Diego Simeone (pichani) akidai anaamini kocha huyo anaweza kuchukua nafasi ya kocha yeyote England.
Simeone amekuwa kocha wa Atletico tangu Desemba 2011 akiwa sasa anafikisha miaka 14 na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Hispania maarufu La Liga.
Hakuna kocha wa timu ya Ligi Kuu England (EPL) aliyedumu kwa kipindi kirefu na timu yake kama ilivyo kwa Simeone, kwa England kocha anayeongoza kwa kuwa muda mrefu kwenye timu moja ni Pep Guardiola aliyejiunga na Man City mwaka 2016.
Aneyeshika nafasi ya pili baada ya Pep kwa kudumu muda mrefu na timu moja ni Arteta ambaye alijiunga na Arsenal mwaka 2019 na hadi sasa yuko na timu hiyo.
Arteta alikuwa akijibu swali la waandishi wa habari baada ya kuulizwa kama kuna kitu kinamhamasisha kwa Simeone kutokana na muda ambao amekaa akiwa na Atletico.
“Ni kweli yupo Simeone ambaye namuangalia na kujifunza kutoka kwake katika mazingira mengi na kinachonigusa zaidi ni hamasa aliyonayo,” alisema Arteta kabla ya mechi hiyo.

“Nafikiri kwa kipindi ambacho amekuwa katika soka na katika timu hiyo hiyo na wachezaji hao hao na hapo unajiuliza unakuwaje na mkono na nguvu ya kubadilika na kuwa na utayari wa kupata ushindi,” aliongeza Arteta.


Arteta alisema kwamba makocha wanaishi katika mazingira magumu na kitendo cha kuwaza kuwashawishi wachezaji unatakiwa pia kuwa mtu wa kipekee.
“Simjui yeye (Simeone) binafs lakini kila kitu ninachokisikiti kuhusu yeye ni kwamba yuko vizuri mno katika kazi yake na hiyo ndiyo sababu hasa ya kumfanya adumu katika kiwango hicho,” alisema Arteta na kuongeza kuwa kocha huyo ana sifa zote zinazomfaa kocha wa kuwa kwenye Ligi Kuu England.
“Kama anafanya kazi kwenye Ligi ya Mabingwa, michuano ambayo ni mikubwa zaidi Ulaya, maana yake ni kwamba anaweza kufanya kazi popote,” alisema Arteta ambaye timu yake leo Jumanne, Oktoba 21, inaumana na Atletico

The post Arteta ampamba Diego Simeone first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/10/21/arteta-ampamba-diego-simeone/feed/ 0