David de Gea - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 19 Nov 2023 15:04:41 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg David de Gea - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 De Gea akataa ofa ya Saudi Arabia https://www.greensports.co.tz/2023/11/19/de-gea-akataa-ofa-ya-saudi-arabia/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/19/de-gea-akataa-ofa-ya-saudi-arabia/#respond Sun, 19 Nov 2023 15:04:40 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8534 Madrid, HispaniaKipa wa zamani wa Man United, David de Gea inadaiwa amekataa ofa ya kuungana nyota mwenzake wa zamani wa Man United Cristiano Ronaldo katika klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia.De Gea, kipa wa Hispania amekuwa bila timu tangu akatae kuongeza mkataba Man United na habari zaidi zinadai kwamba Al Nassr wapo tayari kumlipa […]

The post De Gea akataa ofa ya Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kipa wa zamani wa Man United, David de Gea inadaiwa amekataa ofa ya kuungana nyota mwenzake wa zamani wa Man United Cristiano Ronaldo katika klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia.
De Gea, kipa wa Hispania amekuwa bila timu tangu akatae kuongeza mkataba Man United na habari zaidi zinadai kwamba Al Nassr wapo tayari kumlipa Pauni 500,000 kwa wiki lakini amekataa ofa hiyo.
Kipa huyo pia amekuwa akihusishwa na mipango ya kuungana na nyota wa zamani wa Barcelona, Lionel Messi katika klabu ya Inter Miami FC ya Marekani lakini hadi sasa hajaonesha utayari wowote wa kuichangamkia ofa hiyo.
De Gea alizua hali ya mshangao baada ya kukaa kimya wakati akisubiriwa kusaini mkataba mpya Man United lakini hadi ilipofika majira ya kiangazi mwaka jana aligoma moja kwa moja kwa kilichodaiwa kuwa alitaka maslahi zaidi.
Tangu hapo amekuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na klabu mbalimbali za barani Ulaya lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika na haishangazi kuona habari zake zimehamia katika klabu za Marekani na Saudi Arabia.

The post De Gea akataa ofa ya Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/19/de-gea-akataa-ofa-ya-saudi-arabia/feed/ 0
Man United kumrudisha De Gea https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/man-united-kumrudisha-de-gea/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/man-united-kumrudisha-de-gea/#respond Thu, 26 Oct 2023 20:49:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8251 Manchester, EnglandMan United inadaiwa kutaka kumrudisha aliyekuwa kipa wake, David de Gea kwa kumpa mkataba wa muda mrefu ikiwa ni miezi minne tangu imruhusu kipa huyo aondoke.De Gea aliondoka katika klabu hiyo baada ya mabosi wake kutokuwa tayari kumpa mkataba mpya kwa kile kilichodaiwa kwamba kipa huyo alikuwa akitaka maslahi makubwa.Baada ya kuondoka kwa De […]

The post Man United kumrudisha De Gea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Man United inadaiwa kutaka kumrudisha aliyekuwa kipa wake, David de Gea kwa kumpa mkataba wa muda mrefu ikiwa ni miezi minne tangu imruhusu kipa huyo aondoke.
De Gea aliondoka katika klabu hiyo baada ya mabosi wake kutokuwa tayari kumpa mkataba mpya kwa kile kilichodaiwa kwamba kipa huyo alikuwa akitaka maslahi makubwa.
Baada ya kuondoka kwa De Gea, Man United ilimsajili aliyekuwa kipa namba moja wa Inter Milan, Andre Onana ambaye hata hivyo amekuwa katika lawama kwa makosa yaliyoigharimu timu hiyo kwenye mechi kadhaa.
Katika kuhakikisha wanakuwa na kipa mahiri, macho yameelekezwa kwa De Gea ambaye kuondoka kwake Man United kuliacha maswali ingawa kilichokuwa wazi ni kwamba kipa huyo mwenye umri wa miaka 32 alikataa kusaini mkataba mpya.
Onana ambaye amekuwa lawamani hata hivyo katika mechi mbili zilizopita ameonekana kuwa kama mwenye kurudi katika ubora wake hasa katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Copenhagen.
Katika mechi hiyo, Onana mbali na kuokoa michomo kadhaa, kipa huyo pia aliokoa penalti na kuifanya timu yake itoke na ushindi wa bao 1-0, ushindi ambao umefufua matumaini mapya kwa timu hiyo baada ya kuwa katika kipindi kigumu.

The post Man United kumrudisha De Gea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/man-united-kumrudisha-de-gea/feed/ 0
Ten Hag amkingia kifua De Gea https://www.greensports.co.tz/2023/05/08/ten-hag-amkingia-kifua-de-gea/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/08/ten-hag-amkingia-kifua-de-gea/#respond Mon, 08 May 2023 06:42:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6052 London, EnglandKocha wa Man United, Erik ten Hag hana wasiwasi na kipa wake David de Gea licha ya kipa huyo kufanya kosa lililoipa West Ham bao jana Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL).De Gea (pichani) alifanya kosa ambalo Said Benrahma alilitumia na kuipa West Ham ushindi wa bao 1-0, matokeo ambayo yameifanya Man […]

The post Ten Hag amkingia kifua De Gea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Man United, Erik ten Hag hana wasiwasi na kipa wake David de Gea licha ya kipa huyo kufanya kosa lililoipa West Ham bao jana Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL).
De Gea (pichani) alifanya kosa ambalo Said Benrahma alilitumia na kuipa West Ham ushindi wa bao 1-0, matokeo ambayo yameifanya Man United ijikwaze katika mbio za kuwania ‘top four’ ya EPL.
Na ingawa Man United inashika nafasi ya nne kushindwa kupata pointi mbele ya West Ham kunaifanya ishindwe kuongeza tofauti ya pointi kati yake na Liverpool inayoshika nafasi ya tano ikiwa na pointi 62 wakati Man United ina pointi 63 ingawa Man United imecheza mechi 34 na Liverpool 35. Man United pia ingeweza kupanda hadi nafasi ya tatu na kuipiku Newcastle iliyopoteza mechi yake na Arsenal.
Siku kadhaa zilizopita kumekuwa na mjadala kuhusu majaliwa ya De Gea ndani ya kikosi cha Man United na nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo lakini Ten Hag ameendelea kusisitiza kuwa bado ana imani na kipa huyo raia wa Hispania.

“Ni kipa mwenye ‘clean sheets’ nyingi katika ligi kuu kwa hiyo tusingeweza kuwa hapa tulipo bila ya yeye,” alisema Ten Hag katika mkutano na waandishi wa habari.


“Kwa hiyo ana imani yangu kwa asilimia zote, sina wasiwasi naye, makosa yanatokea lakini katika timu ni lazima mkabiliane nayo, ni lazima muonyeshe ubora, utulivu na kujirudi na hicho ndicho ambacho hii timu itakifanya,” aliongeza Ten Hag.
Mkataba wa De Gea na Man United unafikia ukomo majira ya kiangazi baadaye mwaka huu ingawa mazungumzo ya kumuongezea mkataba yanaendelea.
Katika siku za karibuni Man United imekuwa ikihusishwa na mipango ya kusajili makipa kadhaa lakini akimzungumzia De Gea, Ten Hag alisema kwamba kipa huyo mwenye umri wa miaka 32 ataendelea kuwa katika klabu hiyo msimu ujao.

The post Ten Hag amkingia kifua De Gea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/08/ten-hag-amkingia-kifua-de-gea/feed/ 0