Copa America - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 16 Jul 2024 07:10:55 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Copa America - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Rais wa soka Colombia akamatwa https://www.greensports.co.tz/2024/07/16/rais-wa-soka-colombia-akamatwa/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/16/rais-wa-soka-colombia-akamatwa/#respond Tue, 16 Jul 2024 07:10:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11624 Miami, MarekaniRais wa Shirikisho la Soka Colombia, Ramon Jesurun (pichani) na mtoto wake wa kiume, Ramon Jamil wamekamatwa na polisi kufuatia vurugu za Jumapili wakati wa mechi ya fainali ya Copa America dhidi ya Argentina.Taarifa ya idara ya polisi wa Miami ilieleza kuwa Ramon, 71 na mwanawe Jamil, 43 wamekamatwa wakihusishwa na vurugu za kwenye […]

The post Rais wa soka Colombia akamatwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Miami, Marekani
Rais wa Shirikisho la Soka Colombia, Ramon Jesurun (pichani) na mtoto wake wa kiume, Ramon Jamil wamekamatwa na polisi kufuatia vurugu za Jumapili wakati wa mechi ya fainali ya Copa America dhidi ya Argentina.
Taarifa ya idara ya polisi wa Miami ilieleza kuwa Ramon, 71 na mwanawe Jamil, 43 wamekamatwa wakihusishwa na vurugu za kwenye mechi hiyo iliyoisha kwa Argentina kuilaza Colombia bao 1-0 na kubeba taji la Copa America.
Katika taarifa hiyo ilieleza kwamba makosa waliyoshtakiwa wawili hao yanahusisha vurugu zilizotokea uwanjani baada ya mechi ingawa Ramon na Jamil bado hawajasema lolote kuhusu mashtaka hayo.
Vurugu hizo zinadaiwa kufanywa baada ya kumalizika kwa mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Hard Rock ambapo Ramon na Jamil awali walikuwa wakielekea uwanjani lakini ghafla hali ilibadilika na kuonekana waliojawa hasira.
Katika hali ambayo haikutarajiwa, wawili hao hapo hapo walianza kuwapigia makelele maofisa usalama ambao walielekezwa kuwazuia watu kusogea zaidi eneo la uwanjani.
Mmoja wa maofisa usalama alionekana akimzuia Jamil kifuani na kumtaka asisogee zaidi eneo la uwanjani na ndipo vurugu zilipoanza baada ya Ramon kumsukuma ofisa huyo wakati huo Jamil naye akamkaba shingo ofisa huyo na kumuangusha chini kabla ya kuanza kumpiga mateke kichwani.
Baadaye Ramon naye alimkaba ofisa usalama mwanamke aliyekuwa akitoa msaada huku habari nyingine zikidai kwamba Ramon na mwanawe pia walimpiga ngumi meneja wa maofisa hao.
Habari nyingine zinadai kwamba Ramon na mwanawe walikuwa wakielekea kwenye eneo la uwanja kwa ajili ya kushiriki katika hafla ya utoaji tuzo kabla ya kuingia katika tafrani hiyo.

The post Rais wa soka Colombia akamatwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/16/rais-wa-soka-colombia-akamatwa/feed/ 0
Argentina yabeba Copa America https://www.greensports.co.tz/2024/07/15/argentina-yabeba-copa-america/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/15/argentina-yabeba-copa-america/#respond Mon, 15 Jul 2024 07:35:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11616 Miami, MarekaniArgentina wana kila sababu ya kujivunia soka lao, baada ya Kombe la Dunia 2022, wamebeba taji la Copa America kwa kuilaza Colombia bao 1-0 katika mechi ya fainali iliyopigwa Jumapili hii.Mechi hiyo ya fainali ililazimika kuchelewa kuanza kutokana na vurugu za nje ya uwanja na baadaye kuchezwa kwa dakika 120 baada ya dakika 90 […]

The post Argentina yabeba Copa America first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Miami, Marekani
Argentina wana kila sababu ya kujivunia soka lao, baada ya Kombe la Dunia 2022, wamebeba taji la Copa America kwa kuilaza Colombia bao 1-0 katika mechi ya fainali iliyopigwa Jumapili hii.
Mechi hiyo ya fainali ililazimika kuchelewa kuanza kutokana na vurugu za nje ya uwanja na baadaye kuchezwa kwa dakika 120 baada ya dakika 90 za kawaida kushindwa kumpata mshindi.
Alikuwa ni Lautaro Martinez aliyefunga bao pekee la Argentina katika dakika ya 112 akiitumia pasi ya Giovani lo Celso na hivyo kuiwezesha timu hiyo kubeba taji la Copa America kwa mara ya 16.
Mechi hiyo hata hivyo ilikuwa ngumu kidogo kwa nahodha wa Argentina, Lionel Messi ambaye alijikuta akitokwa machozi alipotolewa kipindi cha pili baada ya kuumia wakati akiwania mpira.
Majeraha haya hata hivyo hayakumzuia Messi kufurahia ushindi wa taji hilo kwa Argentina mara baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya kumaliza mchezo.
Vurugu zilizotokea nje ya Uwanja wa Hard Rock ilipochezwa mechi hiyo zinadaiwa kusababishwa na mashabiki ambao hawakuwa na tiketi lakini walikuwa wakihaha kutaka kuingia uwanjani.
Hali hiyo ilisababisha hata wale wenye tiketi kuchelewa kuingia wakisubiri nje ya uwanja kwa muda mrefu ili kupata nafasi ya kuingia ndani.
Katika tukio hilo polisi walilazimika kupambana na mashabiki hao ambao baadhi yao walikamatwa na wengine kulazimika kupatiwa matibabu hasa ya huduma ya kwanza.
Katika hali ambayo pia haikutarajiwa muda wa mapumziko ulichelewa kwa takriban dakika 25 kwa sababu ya burudani ya muziki kutoka kwa nyota wa miondoko ya pop, Shakira ambaye pia anatokea nchini Colombia.


Kitendo cah mwanamuziki huyo kuchelewesha mechi kilionekana kumkera kocha wa Colombia, Nestor Lorenzo na baadhi ya mashabiki waliokuwa uwanjani hapo.
Kwa Messi taji hilo ni mwendelezo wa kufuta ukame wa mataji na timu yake ya taifa kwani kwa muda mrefu alikuwa hana taji la kujivunia na timu hiyo kabla ya kubeba taji lake la kwanza mwaka 2021 la Copa America wakati huo akiwa na miaka 34.
Mafanikio hayo yanamfanya awe amebeba mataji yote makubwa akiwa na timu yake ya taifa kwa miaka ya karibuni, kwani baada ya mwaka 2021, mwaka uliofuata wa 2022 alibeba Kombe la Dunia.
Messi ambaye kwa sasa ana miaka 37 kabla ya kuanza fainali hizi za Copa America alisema kwamba bado hajaamua ni lini atastaafu kuichezea timu yake ya taifa hivyo huenda kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 akaendelea kuiwakilisha timu hiyo.

The post Argentina yabeba Copa America first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/15/argentina-yabeba-copa-america/feed/ 0
Nunez, mashabiki Colombia wachunguzwa https://www.greensports.co.tz/2024/07/13/nunez-mashabiki-colombia-wachunguzwa/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/13/nunez-mashabiki-colombia-wachunguzwa/#respond Fri, 12 Jul 2024 21:40:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11603 North Carolina, MarekaniShirikisho la Soka nchi za Marekani Kusini (Conmebol) limeanza uchunguzi unaohusisha tukio lisilo la kiuanamichezo lililomhusisha mshambuliaji wa Uruguay, Darwin Nune ambaye alipambana na mashabiki wa Colombia.Tukio hilo lilitokea Jumatano katika mechi ya nusu fainali ya Copa America baina ya timu hizo mbili, mechi ambayo ilimalizika kwa Colombia kutoka na ushindi wa bao […]

The post Nunez, mashabiki Colombia wachunguzwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

North Carolina, Marekani
Shirikisho la Soka nchi za Marekani Kusini (Conmebol) limeanza uchunguzi unaohusisha tukio lisilo la kiuanamichezo lililomhusisha mshambuliaji wa Uruguay, Darwin Nune ambaye alipambana na mashabiki wa Colombia.
Tukio hilo lilitokea Jumatano katika mechi ya nusu fainali ya Copa America baina ya timu hizo mbili, mechi ambayo ilimalizika kwa Colombia kutoka na ushindi wa bao 1-0.
Katika tukio hilo, Nunez ambaye pia ni mshambuliaji wa Liverpool alionekana akipambana na mashabiki jukwaani katika eneo ambalo familia za wachezaji wengi wa Colombia walikuwa wamekaa.
Nunez alionekana akiruka kutoka upande mmoja na kuelekea sehemu ya mashabiki kabla ya kuanza kupambana nao.
“Ni jambo lisilokubalika, tukio kama hili limegeuza hali ya utulivu kuwa vurugu,” ilieleza taarifa ya Conmebol.
Taarifa hiyo pia iliwahakikishia mashabiki na wadau wa soka kuwa hakuna tukio ambalo linaharibu taswira nzuri ya soka kwa kuhusisha mashabiki na wachezaji uwanjani halafu likavumiliwa.
Katika uchunguzi huo, Conmebol watataka kufahamu kiini cha tukio hilo lililotokea baada ya ushindi wa Colombia ambao Jumapili wataumana na Argentina katika mechi ya fainali.

“Hakukuwa na polisi na hivyo tulilazimika kuzilinda familia zetu, haya ni matatizo ya watu wawili au watatu ambao walipata pombe kidogo na hawajui namna ya kunywa pombe,” alisema nahodha wa Uruguay, Jose Maria Gimenez.


Nunez ambaye hajasema lolote kuhusiana na tukio hilo, mara baada ya hali ya utulivu kurejea, alionekana uwanjani akimbusu mtoto wake wa kiume.

The post Nunez, mashabiki Colombia wachunguzwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/13/nunez-mashabiki-colombia-wachunguzwa/feed/ 0
Kocha Brazil akubali lawama Copa America https://www.greensports.co.tz/2024/07/07/kocha-brazil-akubali-lawama-copa-america/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/07/kocha-brazil-akubali-lawama-copa-america/#respond Sun, 07 Jul 2024 20:41:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11556 Las Vegas, MarekaniKocha wa timu ya taifa ya Brazil, Dorival Junior amesema anabeba lawama zote za timu hiyo kutolewa na Uruguay kwa mikwaju ya penalti 4-2 katika mechi ya robo fainali ya Copa America jana Jumamosi.Uruguay iliyolazimika kucheza na wacheza 10 uwanjani kwa takriban dakika 25 baada ya Nahitan Nandez kupewa kadi nyekundu lakini ilifanikiwa […]

The post Kocha Brazil akubali lawama Copa America first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Las Vegas, Marekani
Kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Dorival Junior amesema anabeba lawama zote za timu hiyo kutolewa na Uruguay kwa mikwaju ya penalti 4-2 katika mechi ya robo fainali ya Copa America jana Jumamosi.
Uruguay iliyolazimika kucheza na wacheza 10 uwanjani kwa takriban dakika 25 baada ya Nahitan Nandez kupewa kadi nyekundu lakini ilifanikiwa kulazimisha sare ya 0-0 na hatimaye kwenda kwenye mikwaju ya penalti.
“Kazi ya aina hii inahitaji kiwango cha juu cha uvumilivu, najua kwamba haya si matekeo ambayo yalitarajiwa, na hivyo nawajibika kwa lawama zote lakini pia nadhani timu hii ina nafasi kubwa ya kukua na kuwa bora zaidi,” alisema Dorival.
Katika penalti, Douglas Luiz na Eder Militao walishindwa kuifungia Brazil ambayo ilicheza bila ya mshambuliaji wake nyota, Vinicius Junior anayetumikia adhabu wakati kwa Uruguay aliyekosa ni Jose Marta Gimenez.
Uruguay sasa imefuzu nusu fainali ambapo Jumatano ijayo itaikabili Colombia wakati Brazil ikiaga fainali hizo kwa rekodi isiyovutia katika hatua ya makundi baada ya kuambulia ushindi katika mechi moja tu ingawa ilifuzu hatua ya mtoano na hatimaye kukwama mbele ya Uruguay.

“Huu ni kama mchakato, kwa ujumla unapokuwa katika hatua ya kujenga timu unapitia magumu, haya ni mashindano yetu rasmi ya kwanza na matokeo ni ya haki kutokana na kile tulichokitarajia, lengo letu kuu kwa sasa ni kufuzu Kombe la Dunia,” alisema Dorival.


Dorival ambaye tangu akabidhiwe jukumu la kuinoa Brazil hadi sasa ameiongoza katika mechi nane, aliwatetea wachezaji wake akisema wengi wao wameingia katika mashindano hayo baada ya kutoka katika kampeni ngumu na klabu zao.
Kwa Brazil hiki ni kipigo cha pili mfululizo mbele ya Uruguay, Oktoba mwaka jana timu hiyo pia ilifungwa na Uruguay mabao 2-0 katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026.

The post Kocha Brazil akubali lawama Copa America first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/07/kocha-brazil-akubali-lawama-copa-america/feed/ 0
Brazil kama haisomeki Copa America https://www.greensports.co.tz/2024/07/03/brazil-kama-haisomeki-copa-america/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/03/brazil-kama-haisomeki-copa-america/#respond Wed, 03 Jul 2024 19:46:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11499 California, MarekaniBrazil imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya soka ya Copa America inayoendelea Marekani baada ya sare ya bao 1-1 na Colombia jana Jumanne ingawa matokeo hayo yameibua hofu kuhusu ubora wa timu hiyo.Kwa matokeo hayo Colombia imeshika usukani Kundi D na sasa inasubiri kuumana na Panama katika robo fainali wakati Brazil iliyoshika […]

The post Brazil kama haisomeki Copa America first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

California, Marekani
Brazil imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya soka ya Copa America inayoendelea Marekani baada ya sare ya bao 1-1 na Colombia jana Jumanne ingawa matokeo hayo yameibua hofu kuhusu ubora wa timu hiyo.
Kwa matokeo hayo Colombia imeshika usukani Kundi D na sasa inasubiri kuumana na Panama katika robo fainali wakati Brazil iliyoshika nafasi ya pili itaumana na Uruguay ambao ni vinara wa Kundi C.
Brazil ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Raphinha katika dakika ya 12 kwa mpira wa adhabu lakini dakika chache kabla ya timu kwenda mapumziko Colombia walisawazisha bao hilo mfungaji akiwa ni Daniel Munoz.
“Ni mechi ambayo sote tulitaka kuicheza ili kuipima timu kwenye tukio kubwa, nafikiri tumepiga hatua mbele,” alisema kocha wa Colombia Nestor Lorenzo.
Lorenzo alisema kwamba unapocheza na Brazil huwezi kupuuza hata sekunde moja, na hivyo kwa mtazamo wao wameridhika na sasa wanaifikiria mechi yao dhidi ya Panama.
Brazil pia ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake, Vinícius Júnior kupewa kadi ya njano dakika ya saba na hivyo ataikosa mechi dhidi ya Uruguay kutokana na kuwa na kadi nyingine hapo kabla.
Matokeo hayo kwa ujumla yameshangaza wengi akiwamo beki wa Brazil Marquinhos ambaye amekiri kwamba wanahitaji kuwa katika ubora.

“Ni lazima tuwe wakweli sisi wenyewe kwamba tuna kazi ya kufanya ili tuwe bora zaidi hasa katika mashindano makubwa kama haya,” alisema Marquinhos .


The post Brazil kama haisomeki Copa America first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/03/brazil-kama-haisomeki-copa-america/feed/ 0
Argentina yasaka taji la tatu https://www.greensports.co.tz/2024/06/22/argentina-yasaka-taji-la-tatu/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/22/argentina-yasaka-taji-la-tatu/#respond Sat, 22 Jun 2024 12:46:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11405 Atlanta, MarekaniUshindi wa mabao 2-0 ilioupata Argentina dhidi ya Canada kwenye Copa America unatoa dalili za timu hiyo kubeba taji la tatu kubwa mfululizo baada ya Copa America 2021, Kombe la Dunia 2022 na sasa inataka tena Copa America 2024.Ijumaa hii kwenye dimba la Mercedes-Benz nchini Marekani, nahodha wa Argentina, Lionel Messi aliiongoza vyema timu […]

The post Argentina yasaka taji la tatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Lionel Messi mara baada ya kushinda Kombe la Dunia

Atlanta, Marekani
Ushindi wa mabao 2-0 ilioupata Argentina dhidi ya Canada kwenye Copa America unatoa dalili za timu hiyo kubeba taji la tatu kubwa mfululizo baada ya Copa America 2021, Kombe la Dunia 2022 na sasa inataka tena Copa America 2024.
Ijumaa hii kwenye dimba la Mercedes-Benz nchini Marekani, nahodha wa Argentina, Lionel Messi aliiongoza vyema timu hiyo kuanza mbio za kulitetea taji hilo ambalo huenda timu yake ikalibeba kwa mara nyingine.
Kwa Messi ambaye Jumatatu alifikisha umri wa miaka 37 hiyo inakuwa mechi yake ya 35 kwenye fainali za Copa America na hivyo kumzidi mechi moja, Sergio Livingtone wa Chile.
Katika mechi hiyo Messi ndiye aliyekuwa mpishi wa bao la kwanza la Argentina baada ya kutoa pasi ya kichwa iliyomkuta Alexis Mac Allister kabla ya Alvarez kumalizia kazi ya kuujaza mpira wavuni.
Bao la pili la Argentina lilifungwa na Martinez na kwa mara nyingine lilitokana na mchango wa Messi aliyeunasa mpira katika eneo la kati la uwanja kabla ya kutoa pasi kwa mfungaji.
Baada ya ushindi huo, Argentina itajitupa uwanjani kwa mara nyingine Jumanne kuumana na Chile na kumalizia mzunguko wa kwanza kwa kuumana na Peru wakati Jumanne Canada itaumana na Peru kabla ya kumalizia mzunguko wa kwanza kwa kuivaa Chile.

The post Argentina yasaka taji la tatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/22/argentina-yasaka-taji-la-tatu/feed/ 0