Clara Luvanga - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 21 May 2024 19:26:14 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Clara Luvanga - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ronaldo, Clara Luvanga, wakutana Saudi Arabia https://www.greensports.co.tz/2024/05/21/ronaldo-clara-luvanga-wakutana-saudi-arabia/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/21/ronaldo-clara-luvanga-wakutana-saudi-arabia/#respond Tue, 21 May 2024 19:26:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11055 Na mwandishi wetuMshambuliaji hatari wa Tanzania wa timu ya wanawake ya Al Nassr ya Saudi Arabia, Clara Luvanga amekutana kwa mara ya kwanza na nyota wa klabu hiyo kwa timu ya wanaume, Cristiano Ronaldo.Clara ambaye amekuwa tishio tangu atue Nassr msimu huu akitokea Dux Logrono ya Hispania, ameelezea furaha aliyokuwa nayo baada ya kukutana na […]

The post Ronaldo, Clara Luvanga, wakutana Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji hatari wa Tanzania wa timu ya wanawake ya Al Nassr ya Saudi Arabia, Clara Luvanga amekutana kwa mara ya kwanza na nyota wa klabu hiyo kwa timu ya wanaume, Cristiano Ronaldo.
Clara ambaye amekuwa tishio tangu atue Nassr msimu huu akitokea Dux Logrono ya Hispania, ameelezea furaha aliyokuwa nayo baada ya kukutana na mchezaji huyo bora duniani aliyewahi kutamba na timu za Man United, Real Madrid na nyinginezo.
Katika kuonesha furaha aliyokuwa nayo, Clara ameweka picha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akiwa ameshikana mkono na nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno huku nyuma yao kukiwa na nembo kubwa ya Al Nassr.

“likuwa ndoto kukutana naye na kupiga picha naye, hatimaye ndoto yangu imetimia. Nina furaha sana kukutana naye” ameandika Clara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.


Kama ilivyo kwa Ronaldo, 39 ambaye ni kinara wa mabao wa timu hiyo na ligi ya wanaume ya Saudi Arabia akiwa na mabao 33, Clara pia ni miongoni mwa washambuliaji tishio wa timu hiyo akiwa amepachika mabao 11.
Clara hata hivyo anashika nafasi ya nne kwenye orodha ya wafungaji wa ligi ya wanawake lakini ni wa pili kwa timu yake, akizidiwa na Mualgeria, Lina Boussaha aliyefunga mabao 12.
Wakati Al Nassr ya wanaume ikiwa ni ya pili dhidi ya wababe Al Hilal, Clara ambaye makabrasha yake yanaonesha amezaliwa mwaka 2005, ameiongoza Al Nassr ya wanawake kutwaa ubingwa wa nchi hiyo.

The post Ronaldo, Clara Luvanga, wakutana Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/21/ronaldo-clara-luvanga-wakutana-saudi-arabia/feed/ 0
Clara apiga hat trick Saudi Arabia https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/clara-apiga-hat-trick-saudi-arabia/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/clara-apiga-hat-trick-saudi-arabia/#respond Thu, 04 Apr 2024 19:36:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10501 Na mwandishi wetuMshambuliaji nyota wa kimataifa wa Tanzania, Clara Luvanga anayekipiga Al Nassr ya Saudi Arabia ameendeleza moto baada ya usiku wa kuamkia leo Alhamisi kufunga ‘hat-trick’ (mabao matatu).Clara ambaye pia ni mchezaji wa timu ya wanawake ya Tanzania, alifunga mabao hayo kwenye ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya timu ya taifa ya Singapore katika […]

The post Clara apiga hat trick Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Tanzania, Clara Luvanga anayekipiga Al Nassr ya Saudi Arabia ameendeleza moto baada ya usiku wa kuamkia leo Alhamisi kufunga ‘hat-trick’ (mabao matatu).
Clara ambaye pia ni mchezaji wa timu ya wanawake ya Tanzania, alifunga mabao hayo kwenye ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya timu ya taifa ya Singapore katika mchezo wa kirafiki.
Nyota huyo wa zamani wa Yanga Princess amekuwa na muendelezo mzuri kwenye ligi ya nchini Saudia akifunga mabao 11 kwenye ligi hadi sasa na kuisaidia Nassr kuchukua ubingwa msimu huu.
Aidha, zimesalia mechi mbili kuamua hatma ya Mtanzania huyo kuchukua kiatu cha ufungaji bora akiwa kinara huku akifungana na Ibtissam Jraidi wa Al Ahli iliyopo nafasi ya pili kwenye msimamo.
Hata hivyo, Nassr imecheza mechi 12, ikipoteza mechi moja pekee na kushinda michezo 11, ikiwa imetwaa ubingwa wa nchi hiyo kwa pointi 31 ikiwa ni tofauti ya pointi 10 dhidi ya Al Ahli na Al Shabab zenye pointi 21 kila moja.

The post Clara apiga hat trick Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/clara-apiga-hat-trick-saudi-arabia/feed/ 0
Clara Luvanga azidi kung’ara Saudia https://www.greensports.co.tz/2023/11/19/clara-luvanga-azidi-kungara-saudia/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/19/clara-luvanga-azidi-kungara-saudia/#respond Sun, 19 Nov 2023 14:58:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8531 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa timu ya Al Nassr ya wanawake ya Saudi Arabia, Clara Luvanga, ameendelea kung’ara katika Ligi Kuu Saudi Arabia akiwa kinara wa mabao kwenye ligi hiyo. Clara amekuwa na muendelezo mzuri tangu alipotua Al Nassr akitokea Ludogrono ya nchini Hispania hadi sasa akiwa amepachika mabao sita katika […]

The post Clara Luvanga azidi kung’ara Saudia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa timu ya Al Nassr ya wanawake ya Saudi Arabia, Clara Luvanga, ameendelea kung’ara katika Ligi Kuu Saudi Arabia akiwa kinara wa mabao kwenye ligi hiyo.

Clara amekuwa na muendelezo mzuri tangu alipotua Al Nassr akitokea Ludogrono ya nchini Hispania hadi sasa akiwa amepachika mabao sita katika michezo mitano aliyoshuka dimbani.

Katika orodha hiyo ya vinara wa mabao, Clara anafuatiwa kwa karibu na Mtanzania mwenzake, Enekia Kasonga anayekipiga Eastern Flames akiwa na mabao matano kibindoni.

Akizungumza leo Jumapili juu ya mafanikio yake hayo, Clara alisema kwamba anafurahia kiwango chake hivi sasa kwani malengo yake ni kucheza kwenye ligi bora zaidi ya aliyopo hivi sasa.

“Nafurahi kuwa hapa, mazingira yake pamoja na sapoti ninayoipata kwa wachezaji wenzangu na benchi la ufundi inanifanya nizidi kuimarika zaidi na kufanya vizuri kwenye michezo ninayopata nafasi,” alisema Clara.

“Malengo yangu ni kuisaidia timu yangu kushinda ubingwa lakini pia mimi binafsi nahitaji kushinda kiatu cha ufungaji bora kama nitamaliza msimu salama bila kupata majeraha,” alisema Clara nyota wa zamani wa Yanga Princess.

The post Clara Luvanga azidi kung’ara Saudia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/19/clara-luvanga-azidi-kungara-saudia/feed/ 0
Clara Luvanga aanza vyema Saudia https://www.greensports.co.tz/2023/11/05/clara-luvanga-aanza-vyema-saudia/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/05/clara-luvanga-aanza-vyema-saudia/#respond Sun, 05 Nov 2023 13:48:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8360 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, Clara Luvanga ameanza vyema katika klabu yake mpya ya Al Nassr ya Saudi Arabia baada ya kuifungia mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Eastern Flames Ijumaa hii.Luvanga amejiunga na timu hiyo hivi karibuni akitokea klabu ya Dux Logrono ya Hispania ambako […]

The post Clara Luvanga aanza vyema Saudia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, Clara Luvanga ameanza vyema katika klabu yake mpya ya Al Nassr ya Saudi Arabia baada ya kuifungia mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Eastern Flames Ijumaa hii.
Luvanga amejiunga na timu hiyo hivi karibuni akitokea klabu ya Dux Logrono ya Hispania ambako hajadumu muda mrefu tangu auzwe mwanzoni kwa msimu huu kutokana na kiwango chake kuzivutia timu mbalimbali.
Tangu ajiunge na Nassr huo ni mchezo wa pili anacheza baada ya ule wa awali kutofunga ingawa alitajwa kuwa miongoni mwa wachezaji walioonesha kiwango cha kuvutia.
Katika mchezo huo pia ulimuhusisha Mtanzania mwngine, Enekia Kasongo ambaye anacheza klabu ya Eastern Flames ambaye naye pia alipata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza.
Katika hatua nyingine, Luvanga ameshinda tuzo ya Outstanding Women in Sports, kwenye sherehe za utoaji wa tuzo za wanawake katika Sanaa na Michezo zilizoandaliwa na mwigizaji Yvonne Cherrie ‘Monalisa’ jana Ijumaa.
Miongoni mwa aliowashinda Clara katika kiny’ang’anyiro cha tuzo hiyo ni Fatuma Issa ‘Fetty Densa’ wa Simba SC, Irene Kisisa ‘Rodrygo’ wa Yanga Princess na wengine kutoka michezo mingine mbali na soka.

The post Clara Luvanga aanza vyema Saudia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/05/clara-luvanga-aanza-vyema-saudia/feed/ 0
‘Clara Luvanga ni mwanzo tu’ https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/clara-luvanga-ni-mwanzo-tu/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/clara-luvanga-ni-mwanzo-tu/#respond Wed, 30 Aug 2023 17:09:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7588 Na mwandishi wetuKlabu ya Yanga imeeleza kukamilika kwa dili la Clara Luvanga aliyetimkia Dux Logrono ya Hispania, ni mwanzo wa wachezaji wengi watakaowauza hivi karibuni kutoka timu yao ya wanawake ya Yanga Princess.Clara aliyevuma akiwa na kikosi cha timu ya U17 ya Tanzania kwenye fainali za Kombe la Dunia India 2022, amejiunga na Dux inayoshiriki […]

The post ‘Clara Luvanga ni mwanzo tu’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Yanga imeeleza kukamilika kwa dili la Clara Luvanga aliyetimkia Dux Logrono ya Hispania, ni mwanzo wa wachezaji wengi watakaowauza hivi karibuni kutoka timu yao ya wanawake ya Yanga Princess.
Clara aliyevuma akiwa na kikosi cha timu ya U17 ya Tanzania kwenye fainali za Kombe la Dunia India 2022, amejiunga na Dux inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa mkataba wa miaka mitatu.
Mkurugenzi wa Mashindano Yanga, Saad Kawemba alisema wanafurahia kuwa na maendeleo ya namna hiyo katika klabu akisisitiza kuwa wapo wachezaji wengi wa Princess ambao wameshafanyiwa mipango na muda si mrefu wataweka wazi wanakoelekea nyota wao hao.
“Ni maendeleo kwa kweli na ni jambo jema kwa klabu, tuna idadi ndefu kidogo kuhusu uhamisho wa wachezaji wetu kwenda nje na hivi karibuni klabu itatoa taarifa rasmi kuhusiana na hilo.
“Nasema hivyo kwa sababu orodha ni ndefu kidogo ndio maana klabu itatoa taarifa rasmi kwa wanaoondoka, ni mipango mikubwa tuliyonayo kuhusiana na hilo na muda si mrefu itawekwa wazi,” alifafanua Kawemba.
Timu ya Dux Logrono ina miaka 15 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008 kabla ya Julai Mosi, mwaka juzi kuuzwa kwa Dux Gaming ambapo washirika wake ni DJ Mariio na kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois.
Timu hiyo kwa sasa inanolewa na Gerardo Leon, beki wa zamani wa timu za Villarreal, Valencia na Real Sociedad za Hispania.

The post ‘Clara Luvanga ni mwanzo tu’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/clara-luvanga-ni-mwanzo-tu/feed/ 0