Christophe Galtier - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 06 Jun 2023 20:11:42 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Christophe Galtier - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 PSG yamtimua kocha Galtier https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/psg-yamtimua-kocha-galtier/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/psg-yamtimua-kocha-galtier/#respond Tue, 06 Jun 2023 20:11:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6480 Paris, UfaransaKlabu ya PSG imemfuta kazi kocha Christophe Galtier huku kukiwa na habari kwamba mazungumzo na aliyekuwa kocha wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann yanaendelea vizuri.Galtier pamoja na kuiwezesha PSG kutwaa taji la Ligi 1 nchini Ufaransa, alikwama kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu baada ya kutolewa kwenye michuano hiyo na Bayern Munich katika hatua […]

The post PSG yamtimua kocha Galtier first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Klabu ya PSG imemfuta kazi kocha Christophe Galtier huku kukiwa na habari kwamba mazungumzo na aliyekuwa kocha wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann yanaendelea vizuri.
Galtier pamoja na kuiwezesha PSG kutwaa taji la Ligi 1 nchini Ufaransa, alikwama kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu baada ya kutolewa kwenye michuano hiyo na Bayern Munich katika hatua ya 16 bora.
Mkurugenzi wa michezo wa PSG, Luis Campos alimuarifu Galtier leo Jumanne kuhusu kutimuliwa kwake na awali klabu hiyo ilikuwa ikimuwinda kocha wa zamani wa Barca, Luis Enrique kabla ya kuamua kumgeukia Nagelsmann.
Matarajio ya Nagelsmann kupewa jukumu la kuinoa timu hiyo ni makubwa na inadaiwa kocha huyo atapenda kusaidiwa kazi na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry.
Galtier alijiunga na PSG mwaka jana majira ya kiangazi akitokea klabu ya Nice aliyoiwezesha kushika nafasi ya tisa katika Ligi 1 msimu wa 2021-22 lakini pia aliwahi kuzinoa klabu za Lille na Saint-Etienne.
PSG tayari imeondokewa na wachezaji wake nyota akiwamo Lionel Messi na Sergio Ramos ambao mikataba yao imekwisha lakini pia mshambuliaji Neymar naye yuko mbioni kuihama timu hiyo ambayo pia ipo tayari kumruhusu aondoke.

The post PSG yamtimua kocha Galtier first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/psg-yamtimua-kocha-galtier/feed/ 0