Chole - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 04 Jun 2026 17:25:34 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Chole - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Chole wa Serengeti Boys mchezaji bora Afcon-17 https://www.greensports.co.tz/2026/06/04/chole-wa-serengeti-boys-mchezaji-bora-afcon-17/ https://www.greensports.co.tz/2026/06/04/chole-wa-serengeti-boys-mchezaji-bora-afcon-17/#respond Thu, 04 Jun 2026 17:25:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14682 Rabat, MoroccoKiungo wa Serengeti Boys, Issa Chole ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa vijana chini ya miaka 17 zilizofikia tamati Jumanne, Juni 2, 2026 nchini Morocco.Sambamba na Chole mchezaji mwingine wa Serengeti Boys, Dismas Shida alitwaa tuzo ya kiatu cha dhahabu Golden Boot, mshambuliaji huyo aliifungia […]

The post Chole wa Serengeti Boys mchezaji bora Afcon-17 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rabat, Morocco
Kiungo wa Serengeti Boys, Issa Chole ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa vijana chini ya miaka 17 zilizofikia tamati Jumanne, Juni 2, 2026 nchini Morocco.
Sambamba na Chole mchezaji mwingine wa Serengeti Boys, Dismas Shida alitwaa tuzo ya kiatu cha dhahabu Golden Boot, mshambuliaji huyo aliifungia Serengeti mabao matatu katika michuano hiyo.
Serengeti Boys iliweka rekodi kwa kufikia hatua ya fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza lakini ilishindwa na Senegal walioibuka vinara kwa penalti 4-2 baada ya sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida.
Timu hiyo chini ya kocha Elieneza Nsanganzelu ilianza mbio zake hadi fainali ikiongoza katika kundi lake kabla ya kuibwaga Algeria katika robo fainali na baada ya hapo kuitoa Misri katika nusu fainali kwa mikwaju ya penalti.
Wakati huo huo, kipa wa timu ya taifa ya vijana ya Senegal au The Young Lions of Teranga, Assane Sarr ametwaa tuzo ya kipa bora wa fainali hizo baada ya kuiwezesha timu yake kubeba taji la michuano hiyo.
Umahiri wa Sarr ambaye pia ndiye nahodha wa timu hiyo ulionekana kwa kipindi kirefu cha fainali hizo akiokoa michomo kadhaa iliyoelekezwa langoni mwake ikiwamo mikwaju ya penalti.

C

The post Chole wa Serengeti Boys mchezaji bora Afcon-17 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/06/04/chole-wa-serengeti-boys-mchezaji-bora-afcon-17/feed/ 0