China - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 13 Sep 2024 08:34:44 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg China - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 43 wafungiwa maisha China kwa kupanga matokeo https://www.greensports.co.tz/2024/09/13/wachezaji-38-wafungiwa-maisha-china-kwa-kupanga-matokeo/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/13/wachezaji-38-wafungiwa-maisha-china-kwa-kupanga-matokeo/#respond Fri, 13 Sep 2024 08:22:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11898 Beijing, ChinaWanasoka 38 na maofisa watano wa klabu za soka nchini China wamefungiwa kujihusisha na soka kwa maisha yao yote baada ya kukutwa na hatia ya upangaji matokeo, rushwa na uchezaji kamari.Ofisa Mwandamizi Wizara ya Usalama wa Ndani nchini China, Zhang Xiaopeng alisema uchunguzi walioufanya kwa miaka miwili ulibaini matukio 128 ya upangaji matokeo ukihusisha […]

The post 43 wafungiwa maisha China kwa kupanga matokeo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Beijing, China
Wanasoka 38 na maofisa watano wa klabu za soka nchini China wamefungiwa kujihusisha na soka kwa maisha yao yote baada ya kukutwa na hatia ya upangaji matokeo, rushwa na uchezaji kamari.
Ofisa Mwandamizi Wizara ya Usalama wa Ndani nchini China, Zhang Xiaopeng alisema uchunguzi walioufanya kwa miaka miwili ulibaini matukio 128 ya upangaji matokeo ukihusisha watuhumiwa 128 na maofisa 41 na klabu za soka.
Miongoni mwa waliokumbana na adhabu hiyo wamo wanasoka wa zamani wa kimataifa wa China, Guo Tianyu, Gu Chao na Jin Jingdao na mchezaji wa Korea Kusini, Son Jun-ho ambao sasa hawana ruhusa ya kujihusisha na masuala yoyote ya soka kwa maisha yao yote.
Son alikamatwa akiwa China na kutiwa ndani kwa miezi 10 kabla ya kuachiwa Machi mwaka huu na kurejea kwao Korea Kusini na kwa sasa anaichezea klabu ya Suwon kwa kile ambacho uongozi wa klabu hiyo unadai kwamba adhabu ya mchezaji huyo inafanya kazi China pekee.
Rais wa Chama cha Soka China (CFA), Song Kai (pchani) alisema kuwa watu hao wanakabiliwa na adhabu zinazotokana na makosa ya jinai na wamefungiwa maisha kujihusisha na masuala ya soka.
Kwa mujibu wa Kai miongoni mwa waliokumbwa na adhabu hiyo wapo wachezaji 17 na maofisa wawili wa klabu waliofungiwa kwa miaka mitano akiwamo mchezaji wa kimataifa wa Cameroon, Ewolo Donovan ambaye anaichezea klabu ya Heilongjiang Ice City.
Kai pia alimtaja mchezaji wa zamani wa timu ya Hangzhou Greentown, Shen Liuxi ambaye licha ya kuwa ni mtuhumiwa lakini hayumo kwenye adhabu ya kifungo cha maisha kwa sababu tayari anatumikia adhabu hiyo tangu mwaka 2013.
Katika uchunguzi mpya, Kai alisema kwamba mchezaji huyo alikutwa na hatia ya matukio ya upangaji matokeo na kufungua casino kinyume na utaratibu
China imekuwa katika mkakati mzito wa kukabiliana na matukio ya rushwa na upangaji matokeo ambapo Machi mwaka huu rais wa zamani wa CFA alipewa adhabu ya kifungo cha jela maisha kwa kosa la kupokea rushwa na kujihusisha na upangaji wa matokeo.
Takriban miezi mitano baada ya adhabu hiyo makamu rais wa zamani wa CFA alipewa adhabu ya kifo ch jela miaka 11 kwa kosa la kupokea rushwa pamoja na mkurugenzi wa zamani wa mashindano wa CFA naye alifungwa jela miaka saba kwa kosa hilo hilo.

The post 43 wafungiwa maisha China kwa kupanga matokeo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/13/wachezaji-38-wafungiwa-maisha-china-kwa-kupanga-matokeo/feed/ 0
Bosi wa soka China jela maisha kwa rushwa https://www.greensports.co.tz/2024/03/27/bosi-wa-soka-china-jela-maisha-kwa-rushwa/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/27/bosi-wa-soka-china-jela-maisha-kwa-rushwa/#respond Wed, 27 Mar 2024 06:20:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10387 Beijing, ChinaRais wa zamani wa Chama cha Soka China (CFA), Chen Xuyuan (pichani) amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kujihusisha na rushwa.Taarifa za vyanzo vya habari nchini China zinaeleza kuwa Januari mwaka huu kiongozi huyo alikiri kuchukua pesa zinazodaiwa kuwa ni zao la rushwa na ufisadi zinazofikia Dola 11.8 milioni.Hatua ya kiongozi huyo […]

The post Bosi wa soka China jela maisha kwa rushwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Beijing, China
Rais wa zamani wa Chama cha Soka China (CFA), Chen Xuyuan (pichani) amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kujihusisha na rushwa.
Taarifa za vyanzo vya habari nchini China zinaeleza kuwa Januari mwaka huu kiongozi huyo alikiri kuchukua pesa zinazodaiwa kuwa ni zao la rushwa na ufisadi zinazofikia Dola 11.8 milioni.
Hatua ya kiongozi huyo kukamatwa na kushitakiwa imekuja baada ya rais wa China, Xi Jinping kuanzisha kampeni ya kupambana na ufisadi ambayo imeangazia sekta ya michezo, benki na jeshi.
Katika soka habari zinadai kwamba makocha na wachezaji kadhaa wanaendelea kuhojiwa na kuchunguzwa kuhusiana na matukio ya rushwa.
Kuhusu Xuyuan, taarifa za kimahakama zilieleza kuwa kiongozi huyo anadaiwa kujihusisha na ufisadi kati ya mwaka 2010 hadi 2023 ambapo katika kipindi hicho mbali na urais wa CFA pia alikuwa mwenyekiti wa Shanghai International Port Group.
Waendesha mashitaka walidai kuwa Xuyuan alipokea fedha na vitu mbalimbali kwa makubaliano ya kusaidia upatikanaji wa miradi ya ujenzi na kuandaa matukio ya kimichezo.
Mbali na Xuyuan, viongozi wengine waandamizi watatu wa kwenye soka nao walihukumiwa kifungo cha jela kati ya miaka minane hadi 14 kwa makosa tofauti tofauti ya rushwa na ufisadi.
Mapema mwaka huu kiungo wa zamani wa Everton ambaye pia amewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya soka ya China, Lie Tie alikiri kupanga matokeo ya mechi kadhaa na kutoa rushwa kwa baadhi ya watu akiwamo Chen ili apate kazi ya ukocha katika timu ya taifa ya China.
Mwaka 2011 Rais Jinping alinukuliwa akisema kwamba anataka kuifanya China iwe taifa kubwa katika soka na katika hali alitaka kufanikisha mambo matatu ambayo ni kufuzu Kombe la Dunia, kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia na kubeba Kombe la Dunia.
Katika tukio jingine taarifa za Wizara ya Mambo ya Nje zilieleza kuwa mchezaji nyota wa Korea Kusini, Son Jun-ho anayeichezea Shandong Taishan alikamatwa na polisi na kuwekwa kizuizini kwa tuhuma za rushwa lakini baadaye aliachiwa huru.

The post Bosi wa soka China jela maisha kwa rushwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/27/bosi-wa-soka-china-jela-maisha-kwa-rushwa/feed/ 0