Chasambi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 19 Jul 2026 11:34:55 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Chasambi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Chasambi aachwa Simba https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/chasambi-aachwa-simba/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/chasambi-aachwa-simba/#respond Sun, 19 Jul 2026 11:34:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14807 Na mwandishi wetuKlabu ya soka ya Simba imetangaza kuachanana winga wake Ladack Chasambi ambaye sasa ni rasmi hatokuwa na timu hiyo kwa msimu ujao wa 2026-27.Taarifa iliyopatikana Jumamosi Julai 18, 2026 kwenye vyanzo vya habari vya klabu hiyo, imemtaja mchezaji huyo kuwa mmoja wa wachezaji ambao wamepewa nafasi ya kutafuta maisha nje ya Simba.Chasambi alijiunga […]

The post Chasambi aachwa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya soka ya Simba imetangaza kuachanana winga wake Ladack Chasambi ambaye sasa ni rasmi hatokuwa na timu hiyo kwa msimu ujao wa 2026-27.
Taarifa iliyopatikana Jumamosi Julai 18, 2026 kwenye vyanzo vya habari vya klabu hiyo, imemtaja mchezaji huyo kuwa mmoja wa wachezaji ambao wamepewa nafasi ya kutafuta maisha nje ya Simba.
Chasambi alijiunga na Simba Januari 2024 akitokea Mtibwa Sugar ambapo alipandishwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo baada ya kuonesha uwezo wake kwenye timu ya vijana kabla ya Simba kuvutiwa naye.
Alisajiliwa na Simba wakati huo ikiwa chini ya kocha Abdelhak Benchikha akitajwa kuwa mmoja wa wachezaji waliopewa matumaini makubwa ya kutamba kutokana na uwezo alioanza kuuonesha.
Hali hata hivyo imekuwa tofauti kwa mchezaji huyo ambaye hatimaye Simba imetangaza rasmi kuachana naye.
Chasambi sasa anaungana na mshambuliaji wa timu hiyo, Jonathan Sowah ambaye naye alitangaza kuachwa baada ya kuichezea timu hiyo kwa msimu mmoja tu akitokea Singida Black Stars.
Mchezaji mwingine ambaye Simba imetangaza kuachana naye hivi karibuni ni kiungo mkongwe, Muzamir Yassin ambaye amekuwa na timu hiyo akicheza kwa mafanikio kwa takriban miaka 10.

The post Chasambi aachwa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/chasambi-aachwa-simba/feed/ 0
Chasambi halitaki benchi Simba https://www.greensports.co.tz/2024/01/10/chasambi-halitaki-benchi-simba/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/10/chasambi-halitaki-benchi-simba/#respond Wed, 10 Jan 2024 07:03:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9231 Na mwandishi wetuWinga mpya wa Simba, Ladack Chasambi amesema amejiunga na timu hiyo kwa lengo la kucheza na siyo kukaa benchi.Chasambi ameyazungumza hayo muda mchache baada ya kutambulishwa rasmi na timu hiyo Jumatatu, akifafanua kuwa ingawa timu hiyo ina wachezaji wengi mahiri lakini atapambana kumshawishi kocha Abdelhak Benchikha kumpa nafasi.“Najua ukubwa wa timu niliyojiunga nayo […]

The post Chasambi halitaki benchi Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Winga mpya wa Simba, Ladack Chasambi amesema amejiunga na timu hiyo kwa lengo la kucheza na siyo kukaa benchi.
Chasambi ameyazungumza hayo muda mchache baada ya kutambulishwa rasmi na timu hiyo Jumatatu, akifafanua kuwa ingawa timu hiyo ina wachezaji wengi mahiri lakini atapambana kumshawishi kocha Abdelhak Benchikha kumpa nafasi.
“Najua ukubwa wa timu niliyojiunga nayo na changamoto ya nafasi lakini hilo kwangu si tatizo, nitapambana kuhakikisha nacheza kikosi cha kwanza lakini uwepo wa changamoto ni jambo zuri kwangu sababu itafanya niongeze bidii mazoezini,” alisema Chasambi.
Winga huyo alisema pamoja na kipaji alichonacho lakini bado ana mengi ya kujifunza kutoka kwa wachezaji wakongwe aliowakuta Simba na yupo tayari kwa ushirikiano ili kutimiza ndoto zake.
Alisema atahakikisha anashirikiana na wachezaji wenzake pamoja na benchi la ufundi ili kuipigania timu yao kufikia malengo ambayo wamekusudia kuyafikia mwishoni mwa msimu huu.
Chasambi ambaye ni mzawa amekuwa mchezaji wa tatu kutambulishwa Simba kwenye dirisha dogo baada ya Salehe Karabaka na Babacar Sarr raia wa Senegal

The post Chasambi halitaki benchi Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/10/chasambi-halitaki-benchi-simba/feed/ 0