Cedric Kaze - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 19 Aug 2023 19:03:50 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Cedric Kaze - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kaze apigania matokeo Namungo https://www.greensports.co.tz/2023/08/19/kaze-apigania-matokeo-namungo/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/19/kaze-apigania-matokeo-namungo/#respond Sat, 19 Aug 2023 19:03:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7452 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Namungo, Cedric Kaze amesema wanapambana kuhakikisha wanaingiza falsafa ya namna ya kupata matokeo mfululizo na kuirejesha timu hiyo kwenye michuano ya klabu Afrika.Namungo imeanza ligi msimu huu kwa kupoteza dhidi ya JKT Tanzania kwa bao 1-0, lakini Kaze amesisitiza wanalifanyia kazi hilo ili kuhakikisha timu hiyo inaanza kupata matokeo mfululizo.“Malengo […]

The post Kaze apigania matokeo Namungo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Namungo, Cedric Kaze amesema wanapambana kuhakikisha wanaingiza falsafa ya namna ya kupata matokeo mfululizo na kuirejesha timu hiyo kwenye michuano ya klabu Afrika.
Namungo imeanza ligi msimu huu kwa kupoteza dhidi ya JKT Tanzania kwa bao 1-0, lakini Kaze amesisitiza wanalifanyia kazi hilo ili kuhakikisha timu hiyo inaanza kupata matokeo mfululizo.
“Malengo makubwa ya Namungo ni kurudi kucheza mechi za kimataifa na iliwahi kufanya hivyo kwa mafanikio, ni ligi ngumu sana kwa sasa, lakini nafikiri kitu kikubwa ni kujiandaa na kujua tunaenda kucheza vipi.

“Ninachofahamu unaweza kukosa matokeo leo na kesho, keshokutwa ukaanza kupata kwa mfululizo na sasa tunaingiza falsafa kwa wachezaji namna ya kucheza, kuzuia, kuishi nje ya mpira, kupumzika, kula ili uwezo wa mchezaji tuutumie ipasavyo na kupata matokeo,” alisema Kaze.


Kocha huyo raia wa Burundi alisema anaamini bado wako kwenye njia nzuri ingawa wanapaswa kuongeza ubunifu hasa kwenye pasi za mwisho za mabao, mikimbio ya wasio na mpira, namna ya kufunga ili wapate matokeo kila mchezo.
Namungo inashiriki Ligi Kuu NBC kwa msimu wa tano mfululizo, msimu wa 2019-20 ilimaliza nafasi ya nne na kuiwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, msimu uliofuata ilimaliza nafasi ya tisa kabla ya misimu miwili iliyopita kumaliza katika nafasi ya tano.

The post Kaze apigania matokeo Namungo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/19/kaze-apigania-matokeo-namungo/feed/ 0
Kaze adai Yanga ipo tayari https://www.greensports.co.tz/2023/05/31/kaze-adai-yanga-ipo-tayari/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/31/kaze-adai-yanga-ipo-tayari/#respond Wed, 31 May 2023 18:07:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6401 Na mwandishi wetuWakati kikosi cha Yanga kikitarajia kuondoka kesho Alhamisi kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, kocha msaidizi wa timu hiyo, Cedric Kaze amesema wapo tayari kwa vita hiyo.Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Jumapili iliyopita Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Yanga ilifungwa mabao 2-1 hivyo […]

The post Kaze adai Yanga ipo tayari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Wakati kikosi cha Yanga kikitarajia kuondoka kesho Alhamisi kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, kocha msaidizi wa timu hiyo, Cedric Kaze amesema wapo tayari kwa vita hiyo.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Jumapili iliyopita Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Yanga ilifungwa mabao 2-1 hivyo ili kubeba taji hilo inalazimika kushinda kuanzia mabao 2-0.
Kaze (pichani juu) alisema kuwa wametumia vizuri siku mbili za mazoezi kuyafanyia kazi mapungufu ambayo waliyaona kwenye mchezo uliopita ambao walipoteza mbele ya mashabiki wao wa nyumbani.
“Tunatambua uzito wa mchezo wa marudiano kwa kuwa tutakuwa ugenini, kitu kizuri ni kwamba tunakwenda tukiwa tunawajua vizuri wapinzani wetu USM Alger na tumeandaa mbinu mbadala za kuwadhibiti na kupata ushindi,” alisema Kaze.
Kocha huyo alisema wachezaji wao wako fiti akiwemo Stephene Aziz Ki, ambaye katika mchezo wa mkondo wa kwanza alitoka kutokana na kukabiliwa na maumivu ya mguu wa kushoto.
Alisema benchi la ufundi pamoja na wachezaji wote kwa pamoja wameupa uzito mkubwa mchezo huo lengo ni kuhakikisha wanacheza kwa umakini na kupata ushindi ambao utawapa ubingwa na kurudi na kombe hilo Tanzania.
Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu inatarajiwa kuchezwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Julai 5, 1962, mjini Algiers kuanzia saa 4 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

The post Kaze adai Yanga ipo tayari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/31/kaze-adai-yanga-ipo-tayari/feed/ 0
Kaze ajipa matumaini kwa Singida https://www.greensports.co.tz/2023/05/20/kaze-ajipa-matumaini-kwa-singida/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/20/kaze-ajipa-matumaini-kwa-singida/#respond Sat, 20 May 2023 20:18:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6238 Na mwandishi wetuKesho Jumapili Yanga inashuka dimbani kwenye mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Singida Big Stars, ikieleza uwezo na ari waliyonayo itawapa faida ya kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Liti, Singida.Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze ameeleza leo Jumamosi kuwa wanawaheshimu wapinzani wao kwa ubora […]

The post Kaze ajipa matumaini kwa Singida first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kesho Jumapili Yanga inashuka dimbani kwenye mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Singida Big Stars, ikieleza uwezo na ari waliyonayo itawapa faida ya kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Liti, Singida.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze ameeleza leo Jumamosi kuwa wanawaheshimu wapinzani wao kwa ubora walionao msimu huu, wakifahamu wanataka kuvuna chochote kwenye kombe hilo lakini wao wapo tayari kwa mapambano hayo.
“Tunaamini mchezo utakuwa mgumu zaidi ya ile tuliyokutana kwenye ligi, hatutaki kujificha kwenye uchovu tulionao na kutafuta sababu, lakini kiakili tunaamini tuko vizuri, tunamheshimu mpinzani ameonesha kiwango kizuri lakini tutaweka nguvu zote kuhakikisha tunaenda fainali.

“Hamasa ni kubwa sana, siyo tu ya kuchukua makombe yote lakini kuchukua tena kombe hili tulilochukua mwaka jana, tumeona furaha yake kwa mashabiki na kwetu pia. Tunajua Singida haina cha kupoteza kwa sababu hii ni mechi ya mtoano lakini tupo tayari kwa hilo,” alisema Kaze.


Naye kocha mkuu wa Singida BS, Hans Pluijm alisema wanahitaji ushindi lakini wanafahamu uzuri, ubora wa kikosi cha timu wanayokutana nayo, akifahamu mbinu zao nyingi na wao wamejifua vya kukabiliana na hilo.
“Natumaini tumejifunza makosa ya mechi ya mwisho ya nyumbani (dhidi ya Yanga) na hatutaki kuyarudia, Yanga ina kikosi imara na uwezo mkubwa na unapodhani umewakamata ndipo wanapokufunga.
“Hivyo tunahitaji umakini mkubwa kesho tunapaswa kuwa wamoja, nidhamu na kimbinu zaidi, tumejifunza mengi juu ya mechi hii, hatuwezi kueleza kila kitu jinsi tutakavyokwenda kucheza lakini tumejipanga dhidi ya Yanga,” alisema Pluijm.
Kuelekea mechi hiyo itakayopigwa kuanzia saa 9:30 alasiri, Singida itaingia ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 4-1 na kisha 2-1 kwenye mechi mbili ilizokutana na Yanga kwenye ligi ingawa wamejinasibu kupambana kutofungwa tena.
Mshindi wa mechi hiyo, atakutana na Azam kwenye mechi ya fainali itakayopigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Azam ilitinga fainali kwa kuifunga Simba bao 2-1.

The post Kaze ajipa matumaini kwa Singida first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/20/kaze-ajipa-matumaini-kwa-singida/feed/ 0
Kaze: Bado tuna kazi ya kufanya https://www.greensports.co.tz/2023/05/18/kaze-bado-tuna-kazi-ya-kufanya/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/18/kaze-bado-tuna-kazi-ya-kufanya/#respond Thu, 18 May 2023 12:56:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6206 Na mwandishi wetuBaada ya Yanga kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, kocha msaidizi wa timu hiyo, Cedric Kaze amesema walistahili kufika hapo ingawa bado kuna kazi wanapaswa kuimalizia katika fainali.Yanga imetinga fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza jana baada ya kuifunga Marumo Gallants ya Afrika Kusini jumla ya mabao 4-1 na sasa […]

The post Kaze: Bado tuna kazi ya kufanya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya Yanga kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, kocha msaidizi wa timu hiyo, Cedric Kaze amesema walistahili kufika hapo ingawa bado kuna kazi wanapaswa kuimalizia katika fainali.
Yanga imetinga fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza jana baada ya kuifunga Marumo Gallants ya Afrika Kusini jumla ya mabao 4-1 na sasa itakutana na USM Alger ya Algeria iliyoifunga Asec Mimosas ya Ivory Coast mabao 2-0.
Akizungumzia namna walivyoifunga Marumo, Kaze alisema ni mbinu bora walizokuwa nazo ndizo zimewapa matokeo hayo kwani japo walikuwa wanacheza ugenini lakini walijipanga namna ya kupata mabao ya kushtukiza.
“Tulijipanga kimkakati namna ya kucheza na Marumo ugenini na haimaanishi kujipanga kujizuia tu bali tulifahamu mpinzani ukimpa upenyo wa kukushambulia, kuna sehemu atakuwa ameacha nafasi na hivyo tukafanikiwa kuzitumia na kupata ushindi.

“Ni faraja kubwa sana kuingia fainali, msimu ulikuwa mrefu na pia tumetumika sana na tunaamini tulistahili kufika hapa na pia tunafahamu kuna kazi ya fainali pia tunapaswa kuimalizia,” alisema Kaze.


Naye beki wa kati wa Yanga, Dickson Job alisema: “Ni furaha kubwa kama mchezaji mwenye ndoto sababu kwanza tumeingia hatua ya fainali, ni heshima na historia kubwa kwa nchi yote na heshima kwa sisi wachezaji.”
Job alisema kama wachezaji wako tayari kupambana kwa asilimia zote kuhakikisha wanaongeza nguvu ya kuhakikisha wanatwaa ubingwa huo pia kwa mara ya kwanza.
Fainali ya kwanza ya michuano hiyo inatarajiwa kupigwa Mei 28 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kabla ya mechi ya marudiano itakayopigwa nchini Algeria Juni 3, mwaka huu.
Endapo Yanga itafanikiwa kutwaa ndoo hiyo itaondoka na kitita cha Dola za Marekani 2,000,000 (zaidi ya Sh bilioni 4) na ikimaliza nafasi ya pili itajizolea Dola za Marekani 800,000 (zaidi ya Sh bilioni 1).

The post Kaze: Bado tuna kazi ya kufanya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/18/kaze-bado-tuna-kazi-ya-kufanya/feed/ 0
Kaze: Jeshi lipo tayari https://www.greensports.co.tz/2023/04/27/kaze-jeshi-lipo-tayari/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/27/kaze-jeshi-lipo-tayari/#respond Thu, 27 Apr 2023 18:31:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5955 Na mwandishi wetuZikiwa zimesalia siku tatu kabla ya Yanga kurudiana na Rivers United katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema jeshi lao lipo tayari kwa mchezo huo.Yanga itashuka kwenye dimba la Mkapa, Dar es Salaam Jumapili hii kukamilisha mechi hiyo ya mkondo wa pili wa hatua ya robo […]

The post Kaze: Jeshi lipo tayari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya Yanga kurudiana na Rivers United katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema jeshi lao lipo tayari kwa mchezo huo.
Yanga itashuka kwenye dimba la Mkapa, Dar es Salaam Jumapili hii kukamilisha mechi hiyo ya mkondo wa pili wa hatua ya robo fainali huku ikiwa tayari imetanguliza mguu mmoja mbele kufuatia ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa awali uliochezwa Nigeria wiki iliyopita.
Kaze ameeleza kuwa maandalizi yao kuelekea mchezo huo yanakwenda vizuri na wameupa uzito mkubwa mchezo huo licha ya kwamba wanapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele hatua inayofuata.

“Hatuwezi kuidharau Rivers United kwa ushindi ambao tumeupata kwao hata wao wanaweza kufanya hivyo ndio maana tunawasisitiza wachezaji wetu kuongeza umakini na kucheza kwa kujituma sababu bado hatujafuzu nusu fainali,” alisema Kaze.


Kocha huyo ameeleza kuwa wamepanga kucheza kama walivyofanya kwenye mechi za hatua ya makundi walizocheza nyumbani lengo ni kupata mabao ya mapema yatakayowahakikishia safari ya nusu fainali.
Upande wa pili, wapinzani hao wa Yanga, Rivers United wanatarajiwa kuwasili nchini usiku wa kuamkia kesho wakitokea kwao Nigeria.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema wakiwa kama wenyeji, wamewaandalia wageni wao mazingira mazuri ikiwemo usafiri na hoteli nzuri ili wakiwafunga wakose visingizio.
Yanga inahitaji sare ya aina yoyote au ushindi ili kusonga mbele hatua inayofuata ya nusu fainali na kuweka historia ya kufika hatua hiyo.

The post Kaze: Jeshi lipo tayari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/27/kaze-jeshi-lipo-tayari/feed/ 0
Yanga wapo tayari https://www.greensports.co.tz/2023/04/22/yanga-wapo-tayari/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/22/yanga-wapo-tayari/#respond Sat, 22 Apr 2023 17:35:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5911 Na mwandishi wetuWawakilishi wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga SC imeeleza kuwa kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya mechi ya kesho Jumapili kuhakikisha wanapata matokeo dhidi ya Rivers United ya Nigeria.Yanga itashuka ugenini kwenye Uwanja wa Godswill, Uyo kuvaana na Rivers kwenye mechi ya kwanza ya robo fainali ya michuano hiyo itakayopigwa […]

The post Yanga wapo tayari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Wawakilishi wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga SC imeeleza kuwa kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya mechi ya kesho Jumapili kuhakikisha wanapata matokeo dhidi ya Rivers United ya Nigeria.
Yanga itashuka ugenini kwenye Uwanja wa Godswill, Uyo kuvaana na Rivers kwenye mechi ya kwanza ya robo fainali ya michuano hiyo itakayopigwa kuanzia saa 10.00 jioni.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema tangu wamefika juzi nchini Nigeria hali ya hewa imekuwa rafiki kwao na wachezaji wote wamekuwa wakijifua kwa umakini mkubwa kwa ajili ya kupata matokeo mazuri ugenini.
“Kitu cha kwanza hali ya hewa ni nzuri, tumefanya mazoezi ya kujiweka sawa na kimbinu pia, tumetengeneza mikakati yetu namna ya kushambulia na niseme tumemaliza kuweka sawa mipango tuliyonayo kuelekea mechi hiyo.
“Kikubwa hii ni mechi ya kuingia nusu fainali, ni mechi mbili za dakika 180 na wachezaji wako makini na hakuna mchezaji ambaye ana mashaka, kila mtu anaonesha uwanjani kama amehamasika kwenye mechi hii na ya marudiano,” alisema Kaze.
Alisema kikosi hicho bado kimeumia na matokeo ya mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu NBC kwa kufungwa mabao 2-0 na Simba, hivyo wanataka kuutumia mchezo dhidi ya Rivers kujipooza na kuonesha kuwa matokeo yaliyopita yalikuwa kama ajali kwao.
Kuelekea mechi hiyo, Yanga pia inataka kulipa kisasi kwa Rivers kwa kufungwa na kufurushwa kwenye hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikikubali kipigo cha bao 1-0 katika michezo yote miwili ya nyumbani na ugenini.
Timu hizo zinakutana kwenye hatua hiyo baada ya Yanga kufanikiwa kumaliza kinara wa Kundi D kwa pointi 13 sawa na US Monastir ya Tunisia lakini Yanga ikikaa kileleni kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga.
Rivers ilimaliza ya pili kwenye Kundi B ikiwa na pointi 10 nyuma ya Asec Mimosas ya Ivory Coast iliyojikusanyia pointi 13 baada ya mechi sita.

The post Yanga wapo tayari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/22/yanga-wapo-tayari/feed/ 0
Makocha Simba, Yanga full kujiamini https://www.greensports.co.tz/2023/04/06/makocha-simba-yanga-full-kujiamini/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/06/makocha-simba-yanga-full-kujiamini/#respond Thu, 06 Apr 2023 19:40:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5712 Na mwandishi wetuBaada ya Simba na Yanga kuwafahamu wapinzani wao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika, makocha wa timu hizo wamesema wana nafasi ya kufanya vizuri.Katika droo iliyochezeshwa Cairo, Misri Jumatano hii usiku na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Simba ilipangwa kukutana na bingwa mtetezi wa Ligi ya Mabingwa, Wydad […]

The post Makocha Simba, Yanga full kujiamini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya Simba na Yanga kuwafahamu wapinzani wao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika, makocha wa timu hizo wamesema wana nafasi ya kufanya vizuri.
Katika droo iliyochezeshwa Cairo, Misri Jumatano hii usiku na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Simba ilipangwa kukutana na bingwa mtetezi wa Ligi ya Mabingwa, Wydad Casablanca ya Morocco kwenye hatua ya robo fainali huku Yanga ikiangukia kwa Rivers United ya Nigeria.
Kocha wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ alisema kuwa katika hatua hiyo hakuna timu rahisi ila hana wasiwasi na wapinzani wake kutokana na uimara wa kikosi chake.

“Kwenye hatua hii ya Ligi ya Mabingwa hakuna mechi rahisi lakini nina uhakika nitafanya vizuri kutokana na wachezaji nilionao wenye uzoefu na kikosi imara. Nafurahi namna walivyocheza vizuri na kwa muunganiko katika michezo iliyopita,” alisema Robertinho.


Hii ni mara ya tatu katika misimu miwili Simba kukutana na timu za Morocco ambapo katika hatua ya makundi ilikutana na Raja Casablanca na msimu uliopita walicheza na RS Berkane kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze alisema: “Kikubwa sisi wenyewe tunaamini kwamba uwezo wetu ni mkubwa na mzuri na ndio maana tunaamini kuna nafasi pale ya kufanya kazi na kuingia hatua ya nusu fainali.

“Timu zote zilizoingia hatua ya robo fainali ni nzuri, zimejiandaa na zimefanya vizuri hadi kufika hapo hivyo tunapaswa kujipanga vizuri kuwa imara na tayari kwa mapambano,” alisema Kaze.


Mara ya mwisho walikutana katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa mwaka juzi na Yanga kupoteza michezo yote miwili, ikifungwa kila mmoja bao 1-0.
Yanga itaanzia ugenini Aprili 23 kisha itacheza mchezo wa marudiano nyumbani Aprili 30, mwaka huu wakati Simba itavaana na Wydad ikiwa nyumbani Aprili 21 kabla ya mchezo wa marejeano Aprili 28, mwaka huu.


Endapo Simba itamtoa Wydad itakutana na mshindi kati ya CR Belouzidad ya Algeria na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika nusu fainali wakati Yanga itakutana na mshindi wa mechi kati ya Pyramids ya Misri na Marumo Gallants ya Afrika Kusini.

The post Makocha Simba, Yanga full kujiamini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/06/makocha-simba-yanga-full-kujiamini/feed/ 0
Yanga yamsubiri mpinzani robo fainali https://www.greensports.co.tz/2023/03/04/yanga-yamsubiri-mpinzani-robo-fainali/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/04/yanga-yamsubiri-mpinzani-robo-fainali/#respond Sat, 04 Mar 2023 19:24:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5390 Na mwandishi wetuKocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema wapo tayari kupangwa na timu yoyote katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) au Kombe la FA, inayoendelea.Yanga iliungana na Simba, Singida Big Stars na Geita Gold kutinga robo fainali baada ya kuilaza Prisons mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa […]

The post Yanga yamsubiri mpinzani robo fainali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Cedric Kaze

Na mwandishi wetu
Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema wapo tayari kupangwa na timu yoyote katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) au Kombe la FA, inayoendelea.
Yanga iliungana na Simba, Singida Big Stars na Geita Gold kutinga robo fainali baada ya kuilaza Prisons mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa jana Ijumaa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Kocha huyo alisema kuwa juhudi na kujituma kwa wacheaji wao katika mchezo huo kumewapa matumaini ya kupata matokeo mazuri dhidi ya timu yoyote ambayo watapangiwa kwenye hatua hiyo.

“Tulicheza na timu ngumu inayocheza kwa kujilinda na kutumia nguvu nyingi lakini wachezaji wetu walijitahidi kupambana nao na kuonesha uwezo wao, kitu ambacho kimetupa ushindi na kutupeleka hatua inayofuata,” alisema Kaze.


Kaze ameeleza kuwa wataendelea kukiimarisha kikosi chao kwa kufanyia marekebisho mapungufu ambayo yamejitokeza kwenye mchezo huo ikiwemo mipira ya adhabu ndogo ambayo imekuwa ikiwaletea madhara siku za karibuni.
Naye kocha mkuu wa Prisons, Mohamed Abdallah ‘Bares’ amesema kadi nyekundu waliyoipata mwishoni mwa kipindi cha kwanza ndio imesababisha wapoteze mchezo huo kwa idadi kubwa ya mabao.
Bares alisema walikuwa bora kimbinu na kuwadhibiti washambuliaji wa Yanga, katika dakika 45 za kwanza lakini ubora na uzoefu waliokuwa nao wachezaji wa Yanga ilikuwa ni tatizo kwao na kujikuta wanapoteza mchezo.
“Nawapongeza Yanga na tunawatakia safari njema katika safari yao ya kutetea taji hilo lakini niseme kadi nyekundu ilituvurugia mpango wetu na kujikuta tunapoteza mchezo,” alisema Bares.

The post Yanga yamsubiri mpinzani robo fainali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/04/yanga-yamsubiri-mpinzani-robo-fainali/feed/ 0
Yanga, Prisons kupimana mbavu https://www.greensports.co.tz/2023/03/02/yanga-prisons-kupimana-mbavu/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/02/yanga-prisons-kupimana-mbavu/#respond Thu, 02 Mar 2023 16:24:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5368 Na mwandishi wetuYanga kesho inatarajia kushuka kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuumana na Prisons katika mchezo wa Kombe la FA (ASFC) hatua ya 16 bora.Timu hizo zinazoshiriki Ligi Kuu NBC zinakutana katika hatua hiyo zikiwa katika nafasi tofauti ambapo Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 62 wakati Prisons inashika nafasi ya 14 […]

The post Yanga, Prisons kupimana mbavu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga kesho inatarajia kushuka kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuumana na Prisons katika mchezo wa Kombe la FA (ASFC) hatua ya 16 bora.
Timu hizo zinazoshiriki Ligi Kuu NBC zinakutana katika hatua hiyo zikiwa katika nafasi tofauti ambapo Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 62 wakati Prisons inashika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 22.
Mchezo huo hata hivyo unatarajiwa kuwa mkali kutokana na upinzani uliopo baina ya timu hizo kila zinapokutana kama vile zilipokutana mara ya mwisho kwenye mechi ya ligi msimu huu na Yanga kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0.
Kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze (pichani juu) ameeleza kuwa wanafahamu ugumu wa mechi hiyo lakini wao kama mabingwa watetezi wa michuano hiyo wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri na kusonga mbele.
“Sio mchezo mwepesi kulingana na Prisons ilivyo, lakini tumejiandaa, tumejipanga kwa ajili ya mechi hii na ukizingatia sisi ni mabingwa watetezi kwa hiyo tunahitaji kulitetea taji msimu huu na haitakuwa kazi rahisi lakini tutahakikisha tunapambana kupata matokeo hata wachezaji wanalijua hili,” alisema Kaze.
Naye Kocha Mkuu wa Prisons, Mohammed Abdallah ‘Bares’ amesema licha ya timu yao kukosa matokeo mazuri hivi karibuni lakini tayari kuna mabadiliko ndani ya kikosi hicho na wanatarajia kuonesha kitu wapate matokeo na nafasi ya kuiwakilisha nchi kupitia michuano hiyo.

Kocha wa Prisons, Mohammed Abdallah ‘Bares’


“Ni mechi ambayo ni muhimu kwa timu zote, kombe ambalo linaweza kumtoa mshindi kuwakilisha nchi, nafasi ambayo hata sisi tunaitaka kama vile ambavyo Yanga wanaitaka hivyo tumejiandaa vya kutosha, tunakwenda kupambana, kuwadhibiti Yanga na kupata matokeo.

“Mapungufu ya kwenye timu tumeshaanza kuyashughulikia na vijana wanabadilika, nafikiri mipango tuliyonayo dhidi ya Yanga tunaamini itatusaidia kuwakabili Yanga kikamilifu na kupata ushindi,” alisema Bares.


Yanga ilifika hatua hiyo baada ya kufanikiwa kuitungua Rhino Rangers kwa mabao 7-0 wakati Prisons ilipenya hatua hiyo kwa ushindi wa penalti 8-7 dhidi ya Mashujaa FC baada ya sare ya 2-2 baada ya dakika 90 za muda wa kawaida.
Mechi nyingine za hatua hiyo zinazotarajiwa kupigwa kesho itazikutanisha Geita Gold dhidi ya Green Warriors na Singida Big Stars itapepetana na JKT Tanzania.

The post Yanga, Prisons kupimana mbavu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/02/yanga-prisons-kupimana-mbavu/feed/ 0
Kaze akiri, KMC wanawapa upinzani https://www.greensports.co.tz/2023/02/21/kaze-akiri-kmc-wanawapa-upinzani/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/21/kaze-akiri-kmc-wanawapa-upinzani/#respond Tue, 21 Feb 2023 14:57:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5235 Na mwandishi wetuKocha Msaidizi Yanga, Cedric Kaze amekiri timu yake kupata upinzani mkubwa wanapoumana na KMC lakini watapambana kupata ushindi kutokana na hesabu za mbio za ubingwa zilivyo.Yanga itaumana na KMC kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam ambapo Yanga itaingia ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC kwa pointi 56 huku […]

The post Kaze akiri, KMC wanawapa upinzani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Msaidizi Yanga, Cedric Kaze amekiri timu yake kupata upinzani mkubwa wanapoumana na KMC lakini watapambana kupata ushindi kutokana na hesabu za mbio za ubingwa zilivyo.
Yanga itaumana na KMC kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam ambapo Yanga itaingia ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC kwa pointi 56 huku KMC ikiwa nafasi ya 12 kwa pointi 23.
Akizungumza leo Jumanne na waandishi wa habari jijini Dar es Sakaam, Kaze alisema siku zote mchezo wao dhidi ya KMC unakuwa na upinzani mkubwa ndio maana hata mechi yao ya mzunguko wa kwanza walipata ushindi wa bao 1-0 dakika za lala salama.
“Tunapokutana na KMC huwa tunakutana na upinzani ingawa naamini sisi tuko bora zaidi kimwili na kiakili wachezaji wote wako kwenye hali nzuri isipokuwa majeruhi wa muda mrefu Abuutwalib Mshery, Benard Morrison na Denis Nkane ndio watakaokosekana kesho.

“Kikubwa ni kuwafanya wachezaji waondoe furaha ya ushindi wa mchezo uliopita wa Kombe la Shirikisho Afrika, tumetoka kucheza michezo miwili migumu lakini imetusaidia kuwa kwenye hali nzuri ya kiwango chetu kikubwa, tunapaswa kusahau yaliyopita ili tuwe na ari ya kupambana na kuzitafuta pointi tatu dhidi ya KMC,” alisema Kaze.


Kabla ya mechi hiyo na KMC, Yanga imetoka kucheza mechi mbili mfululizo za Kombe la Shirikisho Afrika, ilifungwa ugenini Tunisia mabao 2-0 na US Monastir kabla ya juzi kwenye Uwanja wa Mkapa, kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo.
Kocha Msaidizi wa KMC, Ahmed Ally alisema wanajua wanaenda kucheza na timu bora inayoshiriki mashindano ya kimataifa na ipo kwenye nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu NBC ingawa wamepanga kupambana kwa dakika zote 90 kutafuta matokeo.
“Tunajua tunaenda kucheza mechi ngumu, sisi tunahitaji pointi kutokana na sehemu tuliyopo na wao wanahitaji pointi ili wachukue ubingwa.
“Utakuwa mchezo mzuri na bora, tumejaribu kuangalia sisi benchi la ufundi na wachezaji mipango yetu ya kwenda kucheza na timu ambayo inataka matokeo kwenye kila mchezo lakini ni mechi yenye uhitaji kwa timu zote mbili na mwisho wa siku mwenye kikosi bora ataenda kupata matokeo,” alisema Ally.

The post Kaze akiri, KMC wanawapa upinzani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/21/kaze-akiri-kmc-wanawapa-upinzani/feed/ 0