Casemiro - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 01 May 2026 19:13:45 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Casemiro - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Casemiro akataa ofa ya Saudi Arabia https://www.greensports.co.tz/2026/05/01/casemiro-akataa-ofa-ya-saudi-arabia/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/01/casemiro-akataa-ofa-ya-saudi-arabia/#respond Fri, 01 May 2026 19:12:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14571 Manchester, EnglandKiungo wa Man United anayetajwa kuwa mbioni kuachana na timu hiyo baada ya msimu huu, Casemiro inadaiwa amepanga kujiunga na klabu ya Inter Miami ya Marekani badala ya Saudi Arabia aalipotangaziwa donge nono.Casemiro ambaye amezidi kuwa moto, hivi karibuni alikataa ofa mpya aliyotangaziwa Man United lakini wakati ikidhaniwa atakwenda Saudi Arabia, mwenyewe inadaiwa anataka […]

The post Casemiro akataa ofa ya Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kiungo wa Man United anayetajwa kuwa mbioni kuachana na timu hiyo baada ya msimu huu, Casemiro inadaiwa amepanga kujiunga na klabu ya Inter Miami ya Marekani badala ya Saudi Arabia aalipotangaziwa donge nono.
Casemiro ambaye amezidi kuwa moto, hivi karibuni alikataa ofa mpya aliyotangaziwa Man United lakini wakati ikidhaniwa atakwenda Saudi Arabia, mwenyewe inadaiwa anataka kwenda kucheza na Lionel Messi katika klabu ya Inter Miami.
Mmoja wa wamiliki wa Inter Miami ni nahodha wa zamani wa England na mchezaji wa timu za Man United na Real Madrid, David Beckham ambaye inadaiwa ndiye aliyesaidia kumshawishi Messi ajiunge na timu hiyo na sasa anatarajia kumshawishi Casemiro.
Casemiro hajaweka wazi atakwenda timu gani baada ya Man United lakini kinachojulikana ni kwamba mabilionea wa klabu za Al Nassr na Al Hilal za Saudi Arabia wamemtangazia mchezaji huyo ofa ili acheze soka katika Ligi Kuu Saudi Arabia au Saudi Pro League.
Kiungo huyo kutoka Brazil hata hivyo hayuko tayari kuihamishia familia yake Saudi Arabia badala yake angependa kwenda Marekani hasa katika klabu ya Inter Miami ambayo kwa ushawishi wa Beckham inaendelea kujiimarisha kwa kusajili wachezaji wa hadhi ya juu duniani.
Habari za ndani zinadai kuwa mabosi wa Inter Miami tayari wamemshawishi kiungo huyo kwa mkataba wa kumuweka katika klabu hiyo hadi mwaka 2028 na baada ya hapo wamemtengea ofa nyingine ya mwaka mmoja.
Casemiro licha ya kuwa na miaka 34, anaebdekea kuonesha kiwango bora kiasi cha kuwafanya mashabiki wa Man United kutaka kiungo huyo asiondoke lakini mpango wa klabu kubana matumizi ni sababu tosha ya kumfanya aondoke.
Katika mechi za karibuni za Man United, Casemiro amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu hiyo lakini mmoja wa wamiliki wa klabu, Sir Jim Ratcliffe yuko makini katika kupunguza gharama za mishahara ya wachezaji.
Casemiro analipwa Pauni 400,000 kwa wiki mshahara ambao hauendani na sera za kubana matumizi ambazo kwa sasa zinatekelezwa katika klabu hiyo kwa umakini mkubwa na Sir Jim Ratcliffe.

The post Casemiro akataa ofa ya Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/01/casemiro-akataa-ofa-ya-saudi-arabia/feed/ 0
Casemiro afungiwa milango Man United https://www.greensports.co.tz/2026/03/16/casemiro-afungiwa-milango-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/16/casemiro-afungiwa-milango-man-united/#respond Mon, 16 Mar 2026 16:32:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14448 Manchester, EnglandKlabu ya Manchester United imeweka wazi kuwa haina mpango wa kubadili maamuzi ya awali ya kuachana na kiungo wake mkongwe, Casemiro mwishoni mwa msimu huu.Casemiro mwenye umri wa miaka 34, Januari mwaka huu alitangaza kuwa ataachana na klabu hiyo baada ya mkataba wake wa sasa unaompatia mshahara wa Pauni 350,000 kwa wiki utakapofikia ukingoni.Baada […]

The post Casemiro afungiwa milango Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Klabu ya Manchester United imeweka wazi kuwa haina mpango wa kubadili maamuzi ya awali ya kuachana na kiungo wake mkongwe, Casemiro mwishoni mwa msimu huu.
Casemiro mwenye umri wa miaka 34, Januari mwaka huu alitangaza kuwa ataachana na klabu hiyo baada ya mkataba wake wa sasa unaompatia mshahara wa Pauni 350,000 kwa wiki utakapofikia ukingoni.
Baada ya Casemiro kutoa kauli hiyo kumekuwa na mtazamo tofauti kutokana na kiwango cha mchezaji huyu kuvutia wengi kiasi cha kuibua uvumi kwamba huenda akaongezewa mkataba lakini klabu yake imelikana hilo.
Kutokana na kuibuka mtazamo huo, Man United imeweka wazi kuwa haitokuwa tayari kumpa mkataba mpya kiungo huyo wa zamani wa Real Madrid na kilichopo ni kwamba baada ya msimu huu atakuwa mchezaji huru.
Mmoja wa wamiliki wa klabu hiyo bilionea, Sir Jim Ratcliffe aliwahi kunukuliwa kuhusu Casemiro ambaye mshahara wake kwa mwaka unafikia Pauni 18 milioni ambapo tajiri huyo alielezea mkakati wake wa kupunguza gharama za klabu hiyo.
Habari zinadai kwamba Casemiro mwenyewe ndiye aliyetaka habari kuhusu mkataba wake kuwekwa wazi ili kuepuka kuibuka kauli tata mwishoni mwa msimu ingawa kiwango cha mchezaji huyo kimeibua mtazamo tofauti.
Casemiro ndiye aliyefunga bao la kwanza katika mechi na Aston Villa na baada ya bao hilo alishangilia kwa kuruka juu mbele ya mashabiki na kuibusu jezi ya klabu hiyo zaidi ya mara moja.
Tukio hilo liliwaibua mashabiki ambao walianza kuimba ‘mwaka mmoja zaidi kwa Casemiro’ na kurudia wimbo huo wakati mchezaji huyo akitoka uwanjani baada ya mechi hiyo huku akiibusu jezi zaidi ya mara moja.
Nahodha wa Man United, Bruno Fernandes na beki Leny Yoro nao baada ya mechi walisema wana matumaini Casemiro atabaki katika klabu hiyo ingawa klabu haina mpango wa kubadili uamuzi wa awali wa kuachana na kiungo huyo kutoka Brazil.
Wakati wachezaji wakiwa na mtazamo huo, kocha wa muda wa timu hiyo, Michael Carrick pia amesema kwamba anadhani hakutakuwa na kubadili uamuzi kuhusu mambo yajayo ya Casemiro na klabu hiyo ya Old Trafford.

“Pindi jambo linapokuwa limefanyiwa maamuzi kidogo inakuwa rahisi na kila mmoja anaelewa mazingira, mchango wake kwenye timu umekuwa wa kipekee, na kumekuwa na tukio zuri baada ya mechi kati yake na mashabiki, atafurahia hilo,” alisema Carrick.

The post Casemiro afungiwa milango Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/16/casemiro-afungiwa-milango-man-united/feed/ 0
Casemiro aaga Man Utd https://www.greensports.co.tz/2026/01/23/casemiro-aaga-man-utd/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/23/casemiro-aaga-man-utd/#respond Fri, 23 Jan 2026 19:43:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14275 Manchester, EnglandKlabu ya Manchester United imeeleza kuwa kiungo wake Mbrazil, Casemiro ataachana na klabu hiyo mara baada ya mkataba wake kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu wa 2025-26.Casemiro, 33, alijiunga na Man United mwaka 2022 kwa ada ya Pauni 70 milioni akitokea klabu ya Real Madrid ya Hispania na hadi sasa ameichezea timu hiyo ya […]

The post Casemiro aaga Man Utd first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Klabu ya Manchester United imeeleza kuwa kiungo wake Mbrazil, Casemiro ataachana na klabu hiyo mara baada ya mkataba wake kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu wa 2025-26.
Casemiro, 33, alijiunga na Man United mwaka 2022 kwa ada ya Pauni 70 milioni akitokea klabu ya Real Madrid ya Hispania na hadi sasa ameichezea timu hiyo ya England mara 146.
Kiungo huyo ambaye pia amekuwa akiichezea timu ya taifa ya Brazil, akizungumzia mpango huo alisema kwamba anajivunia kuichezea Man United akisema ataendelea kuikumbuka kwa wakati wote.

“Nitaendelea kuwa na Man United katika maisha yangu yote, huu si wakati wa kusema kwaheri, kwa wakati huu bado kuna mengi ya kutengeneza kumbukumbu nzuri katika kipindi cha miezi minne ijayo,” alisema Casemiro.


Casemiro alisema kwa sasa bado wana wakati wa kupambania mambo mengi pamoja na ataendelea kuwa makini kwa asilimia zote kama ilivyo kawaida yake na kujitoa kwa kila kitu kwa ajlli ya mafanikio ya timu.
“Tuna mengi ya kupambania pamoja, bado kuna muda wa kujitolea kwa hali na mali ili kuisaidia klabu yetu kupata mafanikio,” alisema Casemiro.

The post Casemiro aaga Man Utd first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/23/casemiro-aaga-man-utd/feed/ 0
Ten Hag aponda matumizi ya VAR https://www.greensports.co.tz/2023/03/13/ten-hag-aponda-matumizi-ya-var/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/13/ten-hag-aponda-matumizi-ya-var/#respond Mon, 13 Mar 2023 05:55:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5474 London, EnglandKocha wa Manchester United, Erik ten Hag ameponda matumizi ya VAR katika Ligi Kuu England akidai hayaeleweki baada ya kushuhudia kiungo wake Casemiro akipewa kadi nyekundu kwa mara ya pili.Casemiro (pichani kulia) alipewa kadi hiyo katika mechi ya jana Jumapili na Southampton iliyoisha kwa sare ya 0-0 baada ya kumchezea rafu Carlos Alcaraz na […]

The post Ten Hag aponda matumizi ya VAR first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag ameponda matumizi ya VAR katika Ligi Kuu England akidai hayaeleweki baada ya kushuhudia kiungo wake Casemiro akipewa kadi nyekundu kwa mara ya pili.
Casemiro (pichani kulia) alipewa kadi hiyo katika mechi ya jana Jumapili na Southampton iliyoisha kwa sare ya 0-0 baada ya kumchezea rafu Carlos Alcaraz na mwamuzi Anthony Taylor akaamua kutumia VAR.
Ten Hag alichukizwa na matumizi ya VAR na kutolea mfano tukio la beki wa Leicester City, Ricardo Pereira kutoadhibiwa kwa kumchezea rafu Joao Felix wa Chelsea, rafu inayofanana na ambayo Casemiro anadaiwa kumchezea Alcaraz.
Kocha huyo pia alisema timu yake ilitakiwa kupewa penalti baada ya Armel Bella-Kotchap wa Southampton kuunawa mpira wa krosi uliopigwa na Marcus Rashford katika eneo la penalti.

“Ninachokiona ni kukosekana maamuzi yanayoeleweka, wachezaji hawana tena wanachojua kuhusu sera hii, unaona wiki hii ni Leicester dhidi ya Chelsea, VAR haimuliki ya katikati ya uwanja,” alisema Ten Hag.


Hii ni mara ya pili kwa Casemiro kupewa kadi nyekundu katika mechi mbili kati ya tatu zilizopita za Ligi Kuu England baada ya kuonyeshwa kadi hiyo mara ya kwanza katika mechi dhidi ya Crystal Palace.
Katika mechi na Palace, Casemiro ambaye pia ni kiungo wa timu ya Taifa ya Brazil, picha za VAR zilimkuta na hatia kwa kumkwida kiungo wa Palace, Will Hughes.
Casemiro mwenye umri wa miaka 31 baada ya kupewa kadi hiyo alionekana mnyonge na kutoka uwanjani akilia na sasa atakosa kuiwakilisha timu yake katika mechi nne.

Matokeo ya mechi za Ligi Kuu England zilizochezwa jana Jumapili ni kama ifuatavyo… Fulham 0-3 Arsenal
Man Utd 0-0 Southampton
West Ham 1-1 Aston Villa
Newcastle 2-1 Wolves

The post Ten Hag aponda matumizi ya VAR first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/13/ten-hag-aponda-matumizi-ya-var/feed/ 0
Casemiro wa Madrid atakiwa Old Trafford https://www.greensports.co.tz/2022/08/18/casemiro-wa-madrid-atakiwa-old-trafford/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/18/casemiro-wa-madrid-atakiwa-old-trafford/#respond Thu, 18 Aug 2022 12:13:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2425 Manchester, EnglandKatika mkakati wa kuimarisha safu ya kiungo, Manchester United inadaiwa kuanza mipango ya kumsajili kiungo Mbrazil wa Real Madrid, Casemiro kwa ada inayotajwa kufikia Euro 20 milioni au zaidi.Mpango huo ukikamilika, Casemiro mwenye umri wa miaka 30 atakuwa ni mchezaji anayelipwa pesa ndefu katika klabu hiyo inayotumiwa Uwanja wa Old Trafford ambayo mambo yake […]

The post Casemiro wa Madrid atakiwa Old Trafford first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Katika mkakati wa kuimarisha safu ya kiungo, Manchester United inadaiwa kuanza mipango ya kumsajili kiungo Mbrazil wa Real Madrid, Casemiro kwa ada inayotajwa kufikia Euro 20 milioni au zaidi.
Mpango huo ukikamilika, Casemiro mwenye umri wa miaka 30 atakuwa ni mchezaji anayelipwa pesa ndefu katika klabu hiyo inayotumiwa Uwanja wa Old Trafford ambayo mambo yake bado hayajaanza kuwa mazuri kwenye Ligi Kuu England msimu huu ikiwa tayari imepoteza mechi mbili za mwanzo.
Casemiro amekuwa kwenye kikosi cha Real Madrid tangu mwaka 2013 akibeba mataji matatu ya La Liga na matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, anatakiwa na Man Utd ambayo ilikwama katika mipango yake ya awali ya kumsajili kiungo wa Juventus, Adrienku Rabiot kwa kilichodaiwa kuwa ni mahitaji makubwa ya mchezaji huyo.
Casemiro anaaminika kuwa katika mipango ya kocha Erik ten Hag kuimarisha safu ya kiungo ya Man Utd na imani ya kumpata inatoka na ukweli kwamba nafasi ya mchezaji huyo ndani ya kikosi cha Real Madrid inaweza kuwa njia panda baada ya kusajiliwa kwa Aurelien Tchouameni.
Casemiro ambaye yumo kwenye orodha ya wachezaji 30 wanaowania Ballon D’Or, anatajwa kuwa kati ya viongo wakabaji bora duniani, katika msimu wa 2014/15 aliuzwa kwa mkopo katika klabu ya Porto ya Ureno lakini alirudi Real Madrid msimu uliofuata na hadi sasa ameichezea timu hiyo jumla ya mechi 222 na kufunga mabao 24.

The post Casemiro wa Madrid atakiwa Old Trafford first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/18/casemiro-wa-madrid-atakiwa-old-trafford/feed/ 0