Brazil - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 29 Jun 2024 14:14:03 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Brazil - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Vinicius Jr aipendezesha Brazil https://www.greensports.co.tz/2024/06/29/vinicius-jr-aipendezesha-brazil/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/29/vinicius-jr-aipendezesha-brazil/#respond Sat, 29 Jun 2024 14:14:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11461 Los Angeles, MarekaniBrazil imeichapa Paraguay mabao 4-1 katika fainali za Copa America zinazoendelea nchini Marekani katika mechi ya Kundi D ambayo Vinicius Junior ameibuka shujaa kwa kufunga mabao mawili peke yake.Vinicius Jr ambaye pia ni mshambuliaji wa Real Madrid alifunga bao la kwanza dakika ya 35 kabla Savinho hajaongeza la pili dakika ya 43 na […]

The post Vinicius Jr aipendezesha Brazil first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Los Angeles, Marekani
Brazil imeichapa Paraguay mabao 4-1 katika fainali za Copa America zinazoendelea nchini Marekani katika mechi ya Kundi D ambayo Vinicius Junior ameibuka shujaa kwa kufunga mabao mawili peke yake.
Vinicius Jr ambaye pia ni mshambuliaji wa Real Madrid alifunga bao la kwanza dakika ya 35 kabla Savinho hajaongeza la pili dakika ya 43 na Vinicius kuongeza la tatu katika dakika tano za nyongeza kabla ya mapumziko.
Paraguay wakiwa nyuma kwa mabao matatu walikianza kwa kasi kipindi cha pili na kupata bao lao pekee dakika ya 48 lililofungwa na Omar Alderete lakini walikatishwa tamaa dakika ya 65 baada ya Brazil kufunga bao la nne kwa penalti mfungaji akiwa ni Lucas Paqueta.
Brazil ingeweza kutoka uwanjani na mabao matano lakini Paqueta, kiungo wa West Ham alishindwa kuujaza wavuni mkwaju wa penalti ya awali ambayo ilitolewa dakika ya 30 baada ya beki wa Paraguay kuunawa mpira uliopigwa na Paqueta.
Kwa Vinicius ushindi huo mnono wa jana linakuwa jambo kubwa baada ya kuwataka wachezaji wenzake waboreshe kiwango akionekana kutofurahishwa na matokeo ya sare katika mechi yao iliyopita dhidi ya Costa Rica.
Vinicius kwa mabao hayo anakuwa amefikisha mabao matano akiwa na timu ya Brazil katika mechi 32 na sasa ni kama amefungua ukurasa mpya baada ya kushindwa kuonesha makali yake ya Real Madrid akiwa na timu yake ya taifa.
Katika mechi nyingine ya Copa America ambayo pia ni ya Kundi D iliyochezwa jana Ijumaa, Colombi iliichapa Costa Rica mabao 3-0
Winga wa Liverpool, Luis Diaz ndiye aliyekuwa wa kwanza kuifungia timu hiyo bao kwa mkwaju wa penalti wakati bao la pili la timu hiyo lilifungwa na beki wa Tottenham, Davinson Sanchez kwa kichwa na la tatu lilifungwa na Jhon Cordoba.
Mechi za Copa America Kundi A kesho Jumapili…
Argentina vs Peru
Canada vs Chile

The post Vinicius Jr aipendezesha Brazil first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/29/vinicius-jr-aipendezesha-brazil/feed/ 0
Kiwango Brazil chamtesa Vinicius https://www.greensports.co.tz/2024/06/25/kiwango-brazil-chamtesa-vinicius-jr/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/25/kiwango-brazil-chamtesa-vinicius-jr/#respond Tue, 25 Jun 2024 19:24:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11433 Los Angeles, MarekaniMshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil, Vinícius Júnior hajafurahishwa na kiwango cha soka la Brazil kwenye fainali zinazoendelea za Copa America ingawa amesema wanaweza kuboresha kiwango hicho.Kauli hiyo ya Vinicius Jr imekuja baada ya timu hiyo kuanza mechi yao ya kwanza ya fainali za Copa America ya Kundi D kwa sare ya […]

The post Kiwango Brazil chamtesa Vinicius first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Los Angeles, Marekani
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil, Vinícius Júnior hajafurahishwa na kiwango cha soka la Brazil kwenye fainali zinazoendelea za Copa America ingawa amesema wanaweza kuboresha kiwango hicho.
Kauli hiyo ya Vinicius Jr imekuja baada ya timu hiyo kuanza mechi yao ya kwanza ya fainali za Copa America ya Kundi D kwa sare ya bila kufungana na Costa Rica jana Jumatatu mjini Los Angeles.
Ikiongozwa na safu ya ushambulijai iliyokuwa na washambuliaji wawili mahiri wa Real Madrid Vinicius Jr na mwenzake Rodrygo, Brazil ilipiga mashuti 19 langoni mwa Costa Rica lakini kati ya hayo ni matatu tu yaliyolenga goli.
“Tunajua tunaweza kuboresha soka letu, ni lazima tuwe katika ubora, pia mimi nafahamu nini cha kuboresha na nini cha kufanya kwa ajili ya timu yetu,” alisema Vinicius Jr.
Brazil au Selecao ilipata tabu kuupenya ukuta wa Costa Rica ulioongozwa na mabeki watano hadi kocha wa timu hiyo Dorival Junior kuamua kumtoa Vinícius Jr dakika ya 71 na kumuingiza Endrick.
“Tulijaribu kumtumia Vinicius kwenye winga lakini hatukufanikiwa, baadaye tukamuweka kati lakini bado hatukuweza kupenya, alikabwa vizuri,” alisema Dorival.
Dorival pia alimtoa Raphinha katika dakika ya 71 na kumuingiza Sávio lakini bado timu yake ilipata wakati mgumu kuipenya Costa Rica ingawa alisema ilikuwa lazima kusaka suluhisho na ndio maana alilazimika kufanya mabadiliko.

“Kocha mpya, wachezaji wapya, kila kitu kinahitaji muda, mashabiki wetu wanataka kila kitu kwa haraka lakini tunakwenda kidogo kidogo, mechi ijayo nina hakika tutacheza vizuri zaidi kwa sababu tayari tunaelewa mashindano haya yalivyo,” alisema Vinicius.

The post Kiwango Brazil chamtesa Vinicius first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/25/kiwango-brazil-chamtesa-vinicius-jr/feed/ 0
Brazil, Hispania hakuna mbabe https://www.greensports.co.tz/2024/03/27/brazil-hispania-hakuna-mbabe/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/27/brazil-hispania-hakuna-mbabe/#respond Wed, 27 Mar 2024 06:13:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10382 Madrid, HispaniaBao la penalti la dakika za lala salama la Lucas Paqueta limetosha kuifanya Brazil itoke sare ya mabao 3-3 na Hispania katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyopigwa kwenye dimba la Santiago Berbabeu.Katika mechi hiyo ya Fifa iliyochezwa jana Jumanne, Hispania ndio walioanza kupata bao dakika ya 12 lililofungwa na Rodri kwa mkwaju wa […]

The post Brazil, Hispania hakuna mbabe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Bao la penalti la dakika za lala salama la Lucas Paqueta limetosha kuifanya Brazil itoke sare ya mabao 3-3 na Hispania katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyopigwa kwenye dimba la Santiago Berbabeu.
Katika mechi hiyo ya Fifa iliyochezwa jana Jumanne, Hispania ndio walioanza kupata bao dakika ya 12 lililofungwa na Rodri kwa mkwaju wa penalti kabla Dani Olmo hajaongeza la pili dakika ya 36.
Dakika tano kabla ya mapumziko, Brazil waliandika bao lao la kwanza lililofungwa na Rodrygo na Moreira de Sousa kusawazisha dakika tano baada ya mapumziko na kufanya timu hizo ziwe sare ya mabao 2-2.
Rodri kwa mara nyingine aliifungia Hispania bao la tatu kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 86 na kufanya matokeo yawe 3-2 na hatimaye mkwaju wa penalti wa Paqueta ukatosha kuipa Brazil bao la tatu katika dakika sita za nyongeza na kufanya ubao usomeke 3-3.
England, Ubelgiji zatoka sare
Katika mechi nyingine ya kirafiki, bao la Jude Bellingham liliiwezesha England kutoka sare ya mabao 2-2 na Ubelgiji katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Wembley.
Walikuwa ni Ubelgiji walioanza kupata bao dakika ya 11 lililofungwa na Youri Tielemans lakini Ivan Toney akiichezea England kwa mara ya kwanza akasawazisha kwa mkwaju wa penalti dakika ya 17.
Ubelgiji waliendelea kupambana na kuandika bao la pili dakika ya 36 mfungaji kwa mara nyingine akiwa ni Tielemans hali iliyoiweka England katika wakati mgumu kabla Bellingham hajasawazisha katika dakika tano za nyongeza.
Matokeo ya mechi za kimataifa za kirafiki
England 2-2 Ubelgiji
Ujerumani 2-1 Uholanzi
Jamhuri ya Ireland 0-1 Uswisi
Scotland 0-1 Ireland Kask
Slovenia 2-0 Ureno
Ufaransa 3-2 Chile
Hispania 3-3 Brazil
Zambia 2-1 Malawi
Cayman Islands 0-4 Moldova
Kenya 3-1 Zimbabwe
Uganda 2-2 Ghana
Finland 2-1 Estonia

The post Brazil, Hispania hakuna mbabe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/27/brazil-hispania-hakuna-mbabe/feed/ 0
Kocha mpya Brazil ajipanga bila Neymar https://www.greensports.co.tz/2024/01/12/kocha-mpya-brazil-ajipanga-bila-neymar/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/12/kocha-mpya-brazil-ajipanga-bila-neymar/#respond Fri, 12 Jan 2024 19:43:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9289 Rio de Janeiro, BrazilKocha mpya wa timu ya taifa ya Brazil, Dorival Junior (pichani) amesema Neymar ni kati ya wachezaji watatu bora duniani lakini kwa timu ya taifa ya Brazil inayopitia kipindi kigumu ijifunze kuishi bila ya mchezaji huyo majeruhi.Dorival ambaye mwaka 2010 alitimuliwa katika klabu ya Santos baada ya kumuweka benchi Neymar, Jumatano iliyopita […]

The post Kocha mpya Brazil ajipanga bila Neymar first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Kocha mpya wa timu ya taifa ya Brazil, Dorival Junior (pichani) amesema Neymar ni kati ya wachezaji watatu bora duniani lakini kwa timu ya taifa ya Brazil inayopitia kipindi kigumu ijifunze kuishi bila ya mchezaji huyo majeruhi.
Dorival ambaye mwaka 2010 alitimuliwa katika klabu ya Santos baada ya kumuweka benchi Neymar, Jumatano iliyopita aliteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Brazil akichukua nafasi ya kocha wa muda Fernando Diniz aliyetimuliwa.
Brazil kwa sasa haina mwenendo mzuri ikiwa kwenye mbio za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026, tayari imepoteza mechi tatu kati ya sita ingawa mtihani wa kwanza kwa Dorival utakuwa Juni mwaka huu kwenye fainali za Copa America.
“Brazil lazima ijifunze kuangalia mbele bila ya kuwa na Neymar kwa sababu ni mchezaji majeruhi, tunaye (Neymar) mmoja wa wachezaji watatu bora duniani na hapo tutakuwa tukimtegemea yeye,” alisema Dorival.

Neymar ambaye kwa sasa anashikilia rekodi ya kuifungia timu ya Brazil mabao mengi, aliumia goti la mguu wa kushoto Oktoba mwaka jana wakati akiiwakilisha timu yake ya taifa na tayari amefanyiwa upasuaji akitarajiwa kurudi uwanjani Agosti mwaka huu.
Dorival alisema kwamba Neymar ni mchezaji muhimu sana kama tu atakuwa amepona na kuwa makini na alipoulizwa kama matatizo yao ya siku za nyuma yanaweza kuharibu uhusiano wao kwenye timu ya taifa, kocha huyo alijibu kwa kifupi, “Sina tatizo lolote na Ney.”

“Sijawahi kuwa na tatizo lolote na Neymar, bodi ya klabu ya Santos ilichukua uamuzi wa kunifukuza na niliheshimu hilo na hivyo ndivyo ilivyokuwa lakini sijawahi kuwa na tatizo na Neymar, kila wakati ninapokutana naye tunakuwa vizuri,” alisema Dorival.


The post Kocha mpya Brazil ajipanga bila Neymar first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/12/kocha-mpya-brazil-ajipanga-bila-neymar/feed/ 0
Kocha Brazil atimuliwa https://www.greensports.co.tz/2024/01/06/kocha-brazil-atimuliwa/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/06/kocha-brazil-atimuliwa/#respond Sat, 06 Jan 2024 19:54:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9200 Rio de Janeiro, BrazilShirikisho la Soka Brazil (CBF) hatimaye limeamua kuachana na kocha wa muda wa timu ya taifa, Fernando Diniz (pichani) na sasa linamsaka kocha ambaye atakuwa wa kudumu.Diniz ambaye ana mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo ameiongoza katika mechi sita za kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 na kati ya hizo […]

The post Kocha Brazil atimuliwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Shirikisho la Soka Brazil (CBF) hatimaye limeamua kuachana na kocha wa muda wa timu ya taifa, Fernando Diniz (pichani) na sasa linamsaka kocha ambaye atakuwa wa kudumu.
Diniz ambaye ana mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo ameiongoza katika mechi sita za kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 na kati ya hizo amepoteza tatu, kashinda mbili na sare moja.
Akiwa na timu ya Brazil, Diniz pia ameendelea na kibarua chake cha kuinoa timu ya Fluminense ambao kwa sasa ndio mabingwa wa Copa Libertadores jambo ambalo inadaiwa mabosi CBF hawalifurahii.

“CBF tunamshukuru Fernando Diniz kwa kazi aliyoifanya na kwa namna alivyojitolea na umakini aliouonesha na kwa changamoto za kuiweka sawa timu ya Brazil wakati wa kipindi chake, tunamtakia kila la kheri,” ilieleza taarifa ya CBF.


Rais wa CBF, Ednaldo Rodrigues, juzi Alhamisi alizungumza na rais wa klabu ya Fluminense, Mario Bittencourt kuhusu mpango wa kuajiri kocha wa kudumu kwa maandalizi ya fainali za Kombe la Dunia 2026 ambazo zitafanyika katika nchi za Canada, Mexico na Marekani.
Brazil imekuwa bila ya kocha wa kudumu tangu Tite ang’atuke katika nafasi hiyo baada ya timu hiyo kufungwa na Croatia na kutolewa katika hatua ya robo fainali ya fainali za Kombe la Dunia 2022.
Baada ya Tite kujiuzulu, kocha wa timu ya Brazil ya vijana chini ya miaka 20, Ramon Menezes alikabidhiwa jukumu hilo kwa muda kabla ya kuteuliwa kwa Diniz.
Julai mwaka jana Rodrigues alisema kwamba kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti angepewa nafasi ya kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil jambo ambalo lingemfanya kuwa kocha wa kwanza asiye mzawa kuinoa timu hiyo.
Mpango huo hata hivyo ulizikwa rasmi mwezi uliopita baada ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 64 kusaini mkataba wa miaka miwili na Real Madrid na sasa atakuwa na timu hiyo hadi Juni 2026.

The post Kocha Brazil atimuliwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/06/kocha-brazil-atimuliwa/feed/ 0
Kocha Mario Zagallo afariki dunia https://www.greensports.co.tz/2024/01/06/kocha-mario-zagallo-afariki-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/06/kocha-mario-zagallo-afariki-dunia/#respond Sat, 06 Jan 2024 15:01:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9183 Rio de Janeiro, BrazilKocha wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil, Mario Zagallo mwenye rekodi ya kubeba Kombe la Dunia mara nne akiwa kocha na mchezaji wa timu hiyo, amefariki dunia akiwa na miaka 92.Zagallo, kabla ya kuingia katika ukocha alikuwa mchezaji akicheza nafasi ya winga ambapo akiwa na kikosi cha Brazil walifanikiwa kubeba […]

The post Kocha Mario Zagallo afariki dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil, Mario Zagallo mwenye rekodi ya kubeba Kombe la Dunia mara nne akiwa kocha na mchezaji wa timu hiyo, amefariki dunia akiwa na miaka 92.
Zagallo, kabla ya kuingia katika ukocha alikuwa mchezaji akicheza nafasi ya winga ambapo akiwa na kikosi cha Brazil walifanikiwa kubeba Kombe la Dunia mwaka 1958 na 1962.
Baada ya hapo, Zagalo alikuwa kocha wa timu hiyo, akiwa na kikosi kinachotajwa kuwa bora kikiwa na wachezaji mastaa kina Pele, Carlos Alberto, Jairzinho na wengineo ambao walibeba Kombe la Dunia mwaka 1970.
Baada ya mataji hayo, Zagallo aliibuka katika timu hiyo mwaka 1994 akiwa kocha msaidizi wa Carlos Alberto Parreira, timu ambayo pia ilibeba Kombe la Dunia nchini Marekani na hilo kuwa taji la nne kwa Zagallo.
Zagallo kwa mara nyingine alikabidhiwa jukumu la kuinoa timu ya Brazil akiwa kocha mkuu na mwaka 1998 aliifikisha timu hiyo hatua ya fainali ya Kombe la Dunia nchini Ufaransa lakini ilikwama mbele ya wenyeji waliobeba taji hilo.
Mafanikio hayo yamemfanya Zagallo kuwa mtu wa kwanza duniani mwenye rekodi ya kubeba Kombe la Dunia akiwa mchezaji na baadaye kocha, rekodi ambayo baadaye iliwekwa na Franz Beckenbauer wa Ujerumani na Didier Deschamps wa Ufaransa.
Akizungumzia msiba wa gwiji huyo wa soka, rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva alisema Zagallo alikuwa mmoja wa wanasoka na makocha bora wa wakati wote.

“Ni mfano wa Mbrazili ambaye hakuwahi kuwa mwenye kukata tamaa, ni hulka yake ya kujitoa, kupigania jambo kwa mahaba ndicho kitu anachotuachia katika nchi yetu yote na dunia ya soka kwa ujumla,” alisema Rais Da Silva.


Brazil hadi sasa ndiyo nchi yenye mafanikio zaidi katika soka ikiwa imebeba Kombe la Dunia mara tano na Zagallo ni mmoja wa wanasoka na makocha mahiri aliyehusika kufanikisha historia hiyo ya kipekee.
Katika mahojiano aliyowahi kufanya wakati wa uhai wake, Zagallo alikumbushia tukio la fainali za Kombe la Dunia mwaka 1950 akiwa miongoni mwa watu takriban 200,000 kwenye Uwanja wa Maracana walioshuhudia wenyeji Brazil wakibwagwa na Uruguay katika mechi ya fainali.

The post Kocha Mario Zagallo afariki dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/06/kocha-mario-zagallo-afariki-dunia/feed/ 0
Fifa yachunguza vurugu mechi ya Brazil, Argentina https://www.greensports.co.tz/2023/11/25/fifa-yachunguza-vurugu-mechi-ya-brazil-argentina/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/25/fifa-yachunguza-vurugu-mechi-ya-brazil-argentina/#respond Sat, 25 Nov 2023 05:01:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8620 Rio de Janeiro, BrazilShirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetangaza kufanya uchunguzi baada ya kutokea vurugu katika mechi kati ya Brazil na Argentina na kusababisha mechi hiyo kuchelewa kuanza kwa nusu saa.Mechi hiyo ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 iliyopigwa Jumanne kwenye Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro ilichelewa kuanza baada ya kutokea vurugu […]

The post Fifa yachunguza vurugu mechi ya Brazil, Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetangaza kufanya uchunguzi baada ya kutokea vurugu katika mechi kati ya Brazil na Argentina na kusababisha mechi hiyo kuchelewa kuanza kwa nusu saa.
Mechi hiyo ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 iliyopigwa Jumanne kwenye Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro ilichelewa kuanza baada ya kutokea vurugu zilizosababisha polisi watumie virungu kuwatuliza mashabiki wa Argentina.
Mara tu baada ya kuanza kwa vurugu, nahodha wa Argentina Lionel Mess aliwaongoza wachezaji wake kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na baadaye alinukuliwa akisema kwamba alilazimika kufanya hivyo kwa sababu alihofia hali ingeweza kuwa mbaya zaidi.
Messi aliwalaumu polisi ambao walitumia virungu kuwakabili mashabiki hao ambao nao walivunja viti na kuvitumia kujihami wakati wengine walikimbilia katikati ya uwanja ambapo baadaye shabiki mmoja alionekana akiwa amebebwa kwenye machela na watu wa huduma ya kwanza.
Katika sakata hilo ambalo lilianza wakati nyimbo za taifa zikiimbwa, huenda vyama vya soka vya Brazil na Argentina vyote vikajikuta vikikumbana na adhabu ya Fifa.
Wakati vurugu zikiendelea, wachezaji wa timu zote walionekana kuwafuata mashabiki wao na kuanza kuwatuliza ambapo kipa wa Argentina na klabu ya Aston Villa, Emiliano Martinez alionekana akijaribu kumnyang’anya polisi mmoja kirungu.

“Fifa inathibitisha kwamba kamati ya nidhamu imeanza uchunguzi dhidi ya Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) na Chama cha Soka Argentina (AFA),” ilieleza taarifa ya Fifa iliyopatikana Ijumaa.


Adhabu inayoweza kutolewa kwa kosa hilo ni faini au uwanja kufungiwa, Brazil inahusishwa na kosa la kushindwa kutuliza amani kwenye mechi wakati Argentina inahusishwa na kosa la vurugu za mashabiki.
Baadaye mechi hiyo iliendelea na kuchezwa kwa dakika 90 kama kawaida na Argentina ambao ndio mabingwa wa dunia, walitoka na ushindi wa bao 1-0.

The post Fifa yachunguza vurugu mechi ya Brazil, Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/25/fifa-yachunguza-vurugu-mechi-ya-brazil-argentina/feed/ 0
Virungu vyatembea mechi ya Brazil, Argentina https://www.greensports.co.tz/2023/11/22/virungu-vyatembea-mechi-ya-brazil-argentina/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/22/virungu-vyatembea-mechi-ya-brazil-argentina/#respond Wed, 22 Nov 2023 08:34:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8583 Rio de Janeiro, BrazilMechi ya Brazil na Argentina ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 ambayo Argentina imeshinda kwa bao 1-0 imechelewa kuanza kwa dakika 30 baada ya kutokea vurugu za polisi na mashabiki.Argentina katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Maracana ilipata bao hilo pekee kipindi cha pili lililofungwa na Nicolas Otamendi na […]

The post Virungu vyatembea mechi ya Brazil, Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Mechi ya Brazil na Argentina ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 ambayo Argentina imeshinda kwa bao 1-0 imechelewa kuanza kwa dakika 30 baada ya kutokea vurugu za polisi na mashabiki.
Argentina katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Maracana ilipata bao hilo pekee kipindi cha pili lililofungwa na Nicolas Otamendi na kuifanya Brazil ipoteze kwa mara ya kwanza mechi ya kufuzu ikiwa katika uwanja wa nyumbani.
Vurugu hizo ziliibuka baada ya mashabiki wa Argentina na Brazil kuanza kupambana wakati nyimbo za taifa zikiimbwa hali iliyowafanya polisi kutumia virungu kukabiliana na mashabiki wa Argentina.
Mashabiki wa Argentina nao walijibu mapigo kwa kuwarushia polisi viti hali iliyofanya Uwanja wa Maracana kuwa kama sehemu ya vita baada ya mashabiki wengine kukimbilia katikati ya uwanja ili kukwepa vurugu.
Wakati mapambano hayo yakiendelea, shabiki mmoja aliyejeruhiwa alionekana akiwa amebebwa kwenye machele na kutolewa nje ya uwanja na maofisa wa huduma wa kwanza.
Baadhi ya wachezaji wa Argentina walionekana wakiwataka mashabiki waliokuwa jukwaani kutulia ingawa muda mchache baadaye nahodha wa timu hiyo, Lionel Messi aliwaongoza wenzake kurudi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Kipa wa Argentina, Emiliano Martínez alikimbia hadi karibu na mashabiki wa timu yake kwenye jukwaa huku akiwataka polisi kuhakikisha wanatuliza vurugu.
“Tuliwaona polisi wakipiga watu, na wachezaji wengi hapa ndugu zao wa familia wapo maeneo hayo, hatukuweza kuendelea kucheza mpira,” alisema Messi baada ya mechi hiyo.
Wachezaji wa Argentina inadaiwa waliwaambia wenzao wa Brazil kwamba wangerudi uwanjani baada ya hali kutulia na hatimaye walirudi baada ya dakika 22 na kufanya mazoezi mepesi kwa dakika kama nne kabla ya mechi kuanza.

“Tuliamua kuondoka uwanjani kwa sababu haingewezekana kucheza mpira katika mazingira kama yale, na pia tulidhani kwa sisi kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ingesaidia kutuliza hali,” alisema Messi.


Wakati mechi ikianza kundi kubwa la polisi liliwazingira mashabiki wa Argentina waliokuwa wakishangilia, polisi hao walikuwa wakiwadhibiti mashabiki hao katika eneo ambalo lilikuwa na mashabiki wapatao 3,000.
Tiketi zote 69,000 za mechi hiyo ziliuzwa, mashabiki wa Brazil ambao walionekana wakimzomea na wakati mwingine kumshangilia Messi kabla ya kuanza kwa vurugu, baada ya mechi kuanza walianza kuimba nyimbo za kumsakama.
“Timu hii inaendelea kuweka historia, ushindi mkubwa kwenye dimba la Maracana ingawa umekutana na vipigo kwa mashabiki wa Argentina kwa mara nyingine katika mechi dhidi ya Brazil, ukichaa huu hauwezi kuvumiliwa, na lazima uachwe sasa,” alisema Messi

The post Virungu vyatembea mechi ya Brazil, Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/22/virungu-vyatembea-mechi-ya-brazil-argentina/feed/ 0
Antony aondolewa kikosini Brazil https://www.greensports.co.tz/2023/09/05/antony-aondolewa-kikosini-brazil/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/05/antony-aondolewa-kikosini-brazil/#respond Tue, 05 Sep 2023 07:45:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7662 Sao Paulo, BrazilWinga wa Manchester United, Antony ameondolewa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil baada ya kuwapo tuhuma za udhalilishaji zilizotolewa na aliyekuwa rafiki yake wa kike.Taarifa ya Shirikisho la Soka la Brazil ilieleza kuwa Antony, 23, ameondolewa katika kikosi hicho kwa kuwa kuna tuhuma zinazohitaji uchunguzi na tayari nafasi yake imejazwa na […]

The post Antony aondolewa kikosini Brazil first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Sao Paulo, Brazil
Winga wa Manchester United, Antony ameondolewa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil baada ya kuwapo tuhuma za udhalilishaji zilizotolewa na aliyekuwa rafiki yake wa kike.
Taarifa ya Shirikisho la Soka la Brazil ilieleza kuwa Antony, 23, ameondolewa katika kikosi hicho kwa kuwa kuna tuhuma zinazohitaji uchunguzi na tayari nafasi yake imejazwa na Gabriel Jesus wa Arsenal.
Timu ya Taifa ya Brazil inajiandaa kwa mechi mbili za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 dhidi ya timu za Bolivia na Peru.
Jana Jumatatu, tuhuma zinazomkabili, Antony zilichapishwa na chanzo kimoja cha habari nchini Brazil na tayari polisi wa majiji ya Manchester na Sao Paulo wameanza uchunguzi wa tuhuma hizo ambazo Antony amekana kuhusika.

“Naweza kusema kwamba tuhuma hizi ni za uwongo pamoja na ushahidi ambao tayari umewasilishwa, na ushahidi mwingine ambao utawasilishwa, sina kosa katika tuhuma ninazohusishwa nazo,” alisema Antony.


“Naamini uchunguzi unaoendelea kufanywa na polisi utaweka wazi ukweli kwamba sina kosa lolote,” aliongeza Antony.
Antony anadaiwa kumpiga kichwa hadi kumchana kichwani aliyekuwa rafiki yake wa kike, Gabriela Cavallin hadi kupelekwa hospitali kwa matibabu, tukio analodaiwa kulifanya Januari 15 wakati wakiwa katika chumba cha hoteli moja mjini Manchester.
Akizungumzia kipigo alichopewa, Gabriela alifafanua kuwa, Antony pia alimpiga ngumi kifuani na kwenye maziwa hadi kumuumiza hali ambayo inamfanya ahitaji operesheni ya kumuweka sawa.
Antony alikiri kuwa mahusiano yake na Gabriela hayakuwa mazuri lakini alisisitiza kwamba hakuwahi kumpiga kwa namna yoyote.
Klabu ya Manchester United ilikataa kuzungumzia tuhuma za Antony ikiwa ni siku chache baada ya mchezaji wao mwingine, Mason Greenwood kulazimika kuuzwa kwa mkopo katika klabu ya Getafe baada ya kukabiliwa na tuhuma za udhalilishaji kijinsia licha ya mahakama kumfutia tuhuma hizo.

The post Antony aondolewa kikosini Brazil first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/05/antony-aondolewa-kikosini-brazil/feed/ 0
Brazil, Ujerumani ‘zaua’, Jamaica yafurahia sare https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/brazil-ujerumani-zaua-jamaica-yafurahia-sare/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/brazil-ujerumani-zaua-jamaica-yafurahia-sare/#respond Tue, 25 Jul 2023 08:11:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7100 Sydney, AustraliaWakati Ujerumani ikiilaza Morocco mabao 6-0 na Brazil ikiichapa Panama 4-0, Jamaica inafurahia sare ya 0-0 mbele ya Ufaransa katika mechi za fainali za Kombe la Dunia za Wanawake zinazoendelea Australia na New Zealand.Ujerumani ikiwa mjini Melbourne jana Jumatatu ilineemeka kwa mabao ya Alexandra Popp aliyefunga mawili, Klara Buhl na Lea Schüller pamoja na […]

The post Brazil, Ujerumani ‘zaua’, Jamaica yafurahia sare first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Wachezaji wa Brazil wakishangilia matokeo ya mechi yao ya kwanza ya fainali za Kombe la Dunia za Wanawake. Brazil jana ilianza mechi yake ya kwanza kwa kuichapa Panama mabao 4-0.

Sydney, Australia
Wakati Ujerumani ikiilaza Morocco mabao 6-0 na Brazil ikiichapa Panama 4-0, Jamaica inafurahia sare ya 0-0 mbele ya Ufaransa katika mechi za fainali za Kombe la Dunia za Wanawake zinazoendelea Australia na New Zealand.
Ujerumani ikiwa mjini Melbourne jana Jumatatu ilineemeka kwa mabao ya Alexandra Popp aliyefunga mawili, Klara Buhl na Lea Schüller pamoja na mabao mengine mawili ambayo wachezaji wa Morocco, Hanane Ait El Hajj na Yasmin Mrabet walijifunga.
Katika mechi hiyo Ujerumani iliwakosa wachezaji wake mahiri, Marina Hegering na Lena Oberdorf ambao ni majeruhi lakini ilifanikiwa kuanza vyema fainali hizo. Katika mechi zijazo Ujerumani itaivaa Colombia wakati Morocco itaikabili Korea Kusini.
Nayo Brazil katika mechi nyingine iliyopigwa jana ushindi wao dhidi ya Panama pia ulinogeshwa kwa rekodi ya hat trick (mabao matatu) yaliyofungwa na Ary Borges ambaye pia ndiye aliyetoa pasi iliyozaa bao la nne la timu hiyo lililofungwa na Bia Zaneratto.
Matokeo hayo yanaifanya Brazil kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele katika Kundi F baada ya Ufaransa kuambulia sare ya 0-0 mbele ya Jamaica.
Naye kocha wa Jamaica, Lorne Donaldson akizungumzia sare ya timu yake dhidi ya Ufaransa alisema matokeo hayo yamekuwa ya kipekee kwao katika historia ya soka la wanawake kutokana na ubora wa wapinzani wao, Ufaransa.

Ufaransa inayonolewa na Herve Renard sasa inalazimika kukaa chini na kujipanga upya kabla ya mechi yao ya Julai 29 dhidi ya Brazil ambao ni wababe wengine wa soka la wanawake duniani.
Jamaica ambayo iko nyuma kwa nafasi 38 kwa Ufaransa kwa mujibu wa takwimu za Fifa, ilipambana vizuri na kupata matokeo hayo licha ya nahodha wa timu hiyo, Khadija Shaw kutolewa na kuifanya timu hiyo ibaki na wachezaji 10 uwanjani.
“Naweza kusema kwamba hadi sasa haya ni matokeo makubwa, namba moja, ni matokeo namba moja kwa timu ya wanawake na ya wanaume, ukiangalia tu takwimu za Fifa utayataja matokeo haya kuwa namba moja” alisema Donaldson.
Matokeo mechi za Kombe la Dunia Wanawake…
Colombia 2-0 Korea Kusini
New Zealand 0-1 Philippines
Ufaransa 0-0 Jamaica
Italia 1-0 Argentina
Ujerumani 6-0 Morocco
Brazil 4-0 Panama
Sweden 2-1 Afrika Kusini
Uholanzi 1-0 Ureno

The post Brazil, Ujerumani ‘zaua’, Jamaica yafurahia sare first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/25/brazil-ujerumani-zaua-jamaica-yafurahia-sare/feed/ 0