BFT - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 01 Mar 2024 08:15:50 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg BFT - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ngumi za ridhaa waelekea Ghana https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/ngumi-za-ridhaa-waelekea-ghana/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/ngumi-za-ridhaa-waelekea-ghana/#respond Fri, 01 Mar 2024 08:15:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9952 Na mwandishi wetuTimu ya taifa ya ngumi za ridhaa inatarajia kuondoka nchini Machi 9, mwaka huu kuelekea Ghana kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Afrika.Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Makore Mashaga ameiambia GreenSports kuwa maandalizi yao kuelekea mashindano hayo yanakwenda vizuri na matarajio ya kurudi na medali ni makubwa.“Timu ya […]

The post Ngumi za ridhaa waelekea Ghana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya taifa ya ngumi za ridhaa inatarajia kuondoka nchini Machi 9, mwaka huu kuelekea Ghana kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Afrika.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Makore Mashaga ameiambia GreenSports kuwa maandalizi yao kuelekea mashindano hayo yanakwenda vizuri na matarajio ya kurudi na medali ni makubwa.
“Timu ya ngumi itaondoka Machi 9, tutakuwa na mabondia 11, ambapo kati yao wa kiume ni wanane na watatu wanawake, maandalizi yetu yanakwenda vizuri na matarajio ya kufanya vizuri ni makubwa kwa kweli,” alisema Mashaga.
Alisema mabondia wao wote wa kike na kiume wamepania kufanya vizuri ili kujitangaza na kuipigania nchi yao ili kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.
Mashaga pia ameendelea kuipongeza serikali kwa sapoti iliyoitoa kwa timu hiyo ikiwepo kugharamia kambi, chakula, posho za wachezaji na safari ya kuelekea Ghana kwenye mashindano hayo, akiamini mkono wao una faida kubwa.

The post Ngumi za ridhaa waelekea Ghana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/ngumi-za-ridhaa-waelekea-ghana/feed/ 0
Ngumi waishukuru serikali https://www.greensports.co.tz/2024/02/28/ngumi-waishukuru-serikali/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/28/ngumi-waishukuru-serikali/#respond Wed, 28 Feb 2024 07:14:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9914 Na mwandishi wetuShirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) limeishukuru Serikali ya Tanzania kwa kujitolea kugharamia kambi za timu za taifa za michezo mbalimbali ikiwemo ngumi.Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema hayo Jumanne hii na kufafanua kuwa hatua hiyo imekuwa msaada mkubwa kwao ikiwemo Tanzania kushiriki mashindano mbalimbali bila kukosa.“Huko nyuma tulishindwa kuiweka timu […]

The post Ngumi waishukuru serikali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) limeishukuru Serikali ya Tanzania kwa kujitolea kugharamia kambi za timu za taifa za michezo mbalimbali ikiwemo ngumi.
Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema hayo Jumanne hii na kufafanua kuwa hatua hiyo imekuwa msaada mkubwa kwao ikiwemo Tanzania kushiriki mashindano mbalimbali bila kukosa.
“Huko nyuma tulishindwa kuiweka timu hata kambini kutokana na ukata lakini tulikuwa tunakwenda kwenye mashindano na idadi ndogo ya wachezaji kwa sababu hatukuwa na uwezo wa kusafirisha wachezaji wengi lakini tangu serikali imeweka mkono wake kumekuwa na maendeleo makubwa,” alisema Mashaga.
Mashaga pia alizungumzia maandalizi yao kuelekea mashindano ya Afrika, akisema yanakwenda vizuri na wapo tayari kwa ajili ya kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye michuano hiyo iliyopangwa kufanyika Accra, Ghana.
Mashaga amewataka wadau wa ngumi za ridhaa kuendelea kuwaunga mkono ili wafanye vizuri kwani mabondia wote 11 waliopo kambini wanaendelea vizuri na wana ari kubwa ya kufanya vizuri kutokana na maandalizi wanayoendelea nayo kambini kwao Kibaha, Pwani.

The post Ngumi waishukuru serikali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/28/ngumi-waishukuru-serikali/feed/ 0
Mabondia ngumi za ridhaa kutajwa wiki ijayo https://www.greensports.co.tz/2023/12/24/mabondia-ngumi-za-ridhaa-kutajwa-wiki-ijayo/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/24/mabondia-ngumi-za-ridhaa-kutajwa-wiki-ijayo/#respond Sun, 24 Dec 2023 12:26:26 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9000 Na mwandishi wetuTimu ya taifa ya ngumi za ridhaa inatarajia kutangazwa wiki ijayo kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Mataifa ya Afrika na mashindano ya kufuzu Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa (BFT), Makore Mashaga (pichani) alisema wanaunda timu hiyo wanatoka mashindano ya Bingwa wa Mabingwa yaliyofanyika […]

The post Mabondia ngumi za ridhaa kutajwa wiki ijayo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya taifa ya ngumi za ridhaa inatarajia kutangazwa wiki ijayo kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Mataifa ya Afrika na mashindano ya kufuzu Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa (BFT), Makore Mashaga (pichani) alisema wanaunda timu hiyo wanatoka mashindano ya Bingwa wa Mabingwa yaliyofanyika mkoani Iringa kuanzia Desemba 17-19, mwaka huu.
Alisema katika mashindano ya Bingwa wa Mabingwa uzani wa kg 48, Abdalah Maganga (MMJKT) alimshinda Mtemi Ramadhani (Ngome) kwa pointi na uzani wa kg 51 Iddi Athumani (MMJKT) alimshinda Haji Kudra (MMJKT) kwa pointi.
Uzani wa kg 54 Azizi Chala (Ngome) alimshinda Kaim Said (MMJKT) kwa pointi, kg 57 Stephano Mika (MMJKT) alimshinda John Dominick (Ngome) kwa pointi na kg 60 Hassani Mrutu (Ngome) alimshinda Mwarami Salum.
Katika kg 63.5, King Lucasi (Ngome) alimshinda Sikudhani Simon (Ngome) kwa pointi, kg 67 Addalah Mfaume (Ngome) alimshinda Elias Damson (MMJKT) kwa pointi, kg 71 Joseph Philipo (MMJKT) alimshinda Atanasi Ndiganya (Ngome), kg 75 Eliankunda Daniel (MMJKT) alimshinda Alphonce Abel (MMJKT) kwa pointi.
Katika kg 80 Juma Thabiti (Iringa) alimshinda Kevin Malya (Iringa) kwa pointi., kg 86 Mussa Wambura (Ngome) alishinda kwa W/O baada ya kutopata mpinzani, kg 92 Muhina Moriss (Ngome) alimshinda Fidelis Matonyinga (MMJKT) kwa pointi.
Kwa upande wa wanawake katika kg 52, Aisha Iddi alimshinda Latifa Oloki kwa pointi na Rachel Peter alipewa ushindi wa mezani baada ya kutopata mpinzani.
Pia ulichezwa mchezo wa makocha ambapo Mzonge Hassani (kocha Ngome) alicheza na John Selenge (kocha MMJKT) na matokeo kuwa sare katika uzani wa kg 92.

The post Mabondia ngumi za ridhaa kutajwa wiki ijayo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/24/mabondia-ngumi-za-ridhaa-kutajwa-wiki-ijayo/feed/ 0
BFT yateua mabondia 22 https://www.greensports.co.tz/2023/04/06/bft-yateua-mabondia-22/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/06/bft-yateua-mabondia-22/#respond Thu, 06 Apr 2023 19:48:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5714 Na mwandishi wetuShirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) limeteua mabondia 22 wanaume na wanawake kujiandaa na mashindano ya kimataifa ya kanda ya tatu Afrika yatakayofanyika nchini kuanzia April 18-22, mwaka huu.Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga (pichani) alisema kuwa uteuzi huo umefanyika baada ya mchujo wa mashindano na kuwapata hao waliofanya vizuri watakaochuana na mataifa mengine […]

The post BFT yateua mabondia 22 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) limeteua mabondia 22 wanaume na wanawake kujiandaa na mashindano ya kimataifa ya kanda ya tatu Afrika yatakayofanyika nchini kuanzia April 18-22, mwaka huu.
Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga (pichani) alisema kuwa uteuzi huo umefanyika baada ya mchujo wa mashindano na kuwapata hao waliofanya vizuri watakaochuana na mataifa mengine 13.

“Mchujo huu umefanyika katika ukumbi wa mazoezi wa timu ya ngumi ya JKT Mgulani ambapo kati ya idadi hiyo, wanaume ni 16 na wanawake ni sita waliochaguliwa miongoni mwa 56 waliokuwa katika maandalizi,” alisema Mashaga.


Mashaga alisema mabondia walioteuliwa watafanya mazoezi katika kituo cha JKT Mgulani na kwamba Kamati ya BFT ilichagua kituo hicho kutokana na kuwepo kwa miundombinu mizuri ya kufanya mazoezi ya ngumi kwa ufanisi.
Nchi nyingine zitakazoshiriki mashindano hayo ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Ethiopia, Somalia, DR Congo, Congo Brazaville, Afrika ya Kati, Gabon, Cameroon na Guinea ya Ikweta.
Mabondia walioteuliwa kwa wanaume ni Karim Juma, Yohana Keneth, Abdallah Salum, Hassan Waziri, Rashid Mrema, Alex Isendi, Mohamed Swalehe, Atanas Ndiganya, Joseph Philip, David Chanzi, Joshua Shadrack, Alphonce Abel, Yusuf Changalawe, Nizza Abdalahamani, Jofrey Peter na Alex Sitta.
Kwa upande wa wanawake ni Rahma Maganga, Mariam Richard, Shakila Abdallah, Aisha Idd, Leyla Yazidu na Beatrice Ambrose.
Timu hiyo itaongozwa na walimu Samwel Batman, Hassan Mzonge, Mussin Mohamed, Rogata Damian, Undule Lang’son na Haji Abdallah huku kamati ya ufundi ikiwa chini ya Michael Changarawe kutoka Mwanza na Robert Suluhu wa Dar es Salaam.

The post BFT yateua mabondia 22 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/06/bft-yateua-mabondia-22/feed/ 0