Bellingham - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 13 Nov 2024 07:56:58 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Bellingham - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Bellingham: Tatizo majukumu mapya https://www.greensports.co.tz/2024/11/12/bellingham-tatizo-majukumu-mapya/ https://www.greensports.co.tz/2024/11/12/bellingham-tatizo-majukumu-mapya/#respond Tue, 12 Nov 2024 18:00:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12250 Madrid, HispaniaKiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham amelalamikia mabadiliko ya majukumu kuwa ndiyo yaliyomsababishia ukame wa mabao tangu kuanza kwa msimu huu.Bellingham ambaye pia ni kiungo wa timu ya taifa ya England ametoa kauli hiyo baada ya kufunga bao lake la kwanza msimu huu Jumamosi hii timu yake ikiichapa Osasuna mabao 4-0 katika La Liga.Katika […]

The post Bellingham: Tatizo majukumu mapya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Madrid, Hispania
Kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham amelalamikia mabadiliko ya majukumu kuwa ndiyo yaliyomsababishia ukame wa mabao tangu kuanza kwa msimu huu.
Bellingham ambaye pia ni kiungo wa timu ya taifa ya England ametoa kauli hiyo baada ya kufunga bao lake la kwanza msimu huu Jumamosi hii timu yake ikiichapa Osasuna mabao 4-0 katika La Liga.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Bernabeu, bao la Bellingham lilipatikana dakika ya 42 wakati mabao mengine matatu ya timu hiyo yakifungwa na Vinicius Jr.
Kabla ya bao hilo, Bellingham aliifungia Real Madrid mara ya mwisho mwishoni mwa msimu uliopita wa 2023-24, msimu ambao mchezaji huyo aliumaliza akiwa amefunga mabao 19.
“Najiona ni mwenye kufanya yale yale ninayoyafanya, lakini tofauti pekee ni kwamba nimefunga goli, watu wengi wamekuwa wakizungumzia hilo kwa sababu mwaka jana nilifunga magoli mengi lakini nafikiri sasa nacheza katika majukumu tofauti,” alisema Bellingham.
Bellingham alifafanua kuwa kwa sasa anafanya majukumu tofauti katika sehemu tofauti ya uwanja na kwamba atafanya lolote kwa ajili ya timu.
Mashabiki wa Real Madrid wameendelea kumuunga mkono mchezaji huyo licha ya ukame wa mabao na hata alipotolewa dakika ya 75 walisimama na kumpa heshima yake.

“Bado najiona kama mimi ni mtu wa kipekee katika dunia hii kwa kuichezea hii klabu, hata katika wakati mgumu bado nashukuru kwa kuwa hapa, kutoka nje na kupewa heshima, hilo najivunia,” alisema Bellingham.


Bellingham pia alimpongeza mchezaji mwenzake Vinícius ambaye mabao yake matatu aliyofunga yamemfanya afikishe mabao manane hadi sasa baada ya kucheza mechi 12 za La Liga msimu huu.

The post Bellingham: Tatizo majukumu mapya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/11/12/bellingham-tatizo-majukumu-mapya/feed/ 0
‘Mbappe hatobadili nafasi ya Bellingham Real Madrid’ https://www.greensports.co.tz/2024/08/05/mbappe-kutobadili-nafasi-ya-bellingham-real-madrid/ https://www.greensports.co.tz/2024/08/05/mbappe-kutobadili-nafasi-ya-bellingham-real-madrid/#respond Mon, 05 Aug 2024 11:53:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11715 Charlotte, MarekaniKocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema nafasi na majukumu ya Jude Bellingham katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid hayatobadilika licha ya klabu hiyo kumsajili, Kylian Mbappe.Bellingham, 21, ambaye pia ni kiungo wa timu ya taifa ya England katika msimu wake wa kwanza na Real Madrid wa 2023-24 amebeba vyema majukumu yake akifunga […]

The post ‘Mbappe hatobadili nafasi ya Bellingham Real Madrid’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Charlotte, Marekani
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema nafasi na majukumu ya Jude Bellingham katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid hayatobadilika licha ya klabu hiyo kumsajili, Kylian Mbappe.
Bellingham, 21, ambaye pia ni kiungo wa timu ya taifa ya England katika msimu wake wa kwanza na Real Madrid wa 2023-24 amebeba vyema majukumu yake akifunga mabao 23 katika mechi 42 na timu hiyo kubeba mataji ya La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika msimu mpya wa 2024-25, Real Madrid imemsajili Mbappe, 25, ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ufaransa, usajili ambao inadhaniwa unaweza kumfanya Ancelotti ambadilishie Bellingham majukumu yake kwenye kikosi cha kwanza.
Ancelotti hata hivyo alikana kuwa na mpango wowote wa kumbadilishia majukumu Bellingham kwa kumsogeza mbele zaidi ili Mbappe aingie vyema katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Kocha huyo badala yake alisisitiza kwamba hakuna kitakachobadilika kwa mchezaji huyo ambaye pia aliwahi kunukuliwa akisema kwamba kucheza timu moja na Mbappe litakuwa jambo zuri.

“Msimu wa kwanza tu ameshangaza kweli kwa sababu ameonesha kiwango cha kipekee, amekuwa bora, msimu ujao hautokuwa tofauti, atakuwa mmoja wa wachezaji bora tulio nao, anaisaidia sana timu kwa kiwango chake,” alisema Ancelotti.

Ancelotti pia alimtetea Bellingham baada ya mchezaji huyo kushutumiwa kwa kiwango kisichovutia kwenye fainali za soka za Euro 2024 zilizomalizika hivi karibuni nchini Ujerumani ambapo England ilifikia hatua ya fainali lakini ilishindwa kutamba mbele ya Hispania waliobeba kombe.
“Hayo ni mawazo tu lakini Bellingham alicheza vizuri kwenye Euro, England pia ilicheza vizuri hasa hadi kufikia hatua ya fainali na ilikuwa bado kidogo wabebe kombe,” alisema Ancelotti.
Mbappe na Bellingham ambao wote walikuwa na timu zao za taifa kwenye fainali za Euro 2024 wanasubiriwa kwa hamu kuibeba Real Madrid katika msimu mpya wa 2024-25 unaotarajia kuanza kutimua vumbi baadaye mwezi huu.

The post ‘Mbappe hatobadili nafasi ya Bellingham Real Madrid’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/08/05/mbappe-kutobadili-nafasi-ya-bellingham-real-madrid/feed/ 0
Bellingham nyota wa msimu La Liga https://www.greensports.co.tz/2024/05/30/bellingham-nyota-wa-msimu-la-liga/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/30/bellingham-nyota-wa-msimu-la-liga/#respond Thu, 30 May 2024 05:49:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11168 Madrid, HispaniaKiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya England, Jude Bellingham ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa msimu wa La Liga akiwa katika mwaka wake wa kwanza nchini Hispania.Bellingham, 20, alijiunga na Real Madrid mwanzoni mwa msimu huu akitokea, Borussia Dortmund, hadi sasa ameifungia timu hiyo mabao 19 na kuiwezesha kubeba taji la […]

The post Bellingham nyota wa msimu La Liga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya England, Jude Bellingham ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa msimu wa La Liga akiwa katika mwaka wake wa kwanza nchini Hispania.
Bellingham, 20, alijiunga na Real Madrid mwanzoni mwa msimu huu akitokea, Borussia Dortmund, hadi sasa ameifungia timu hiyo mabao 19 na kuiwezesha kubeba taji la La Liga kwa kuwaacha mahasimu wao Barcelona walioshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi 10.
Nyota huyo mzaliwa wa Stourbridge pia katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ameifungia timu hiyo mabao manne na keshokutwa Jumamosi, timu hiyo itaumana na Dortmund katika mechi ya fainali ya ligi hiyo kwenye dimba la Wembley.
Katika kinyang’anyiro cha kusaka tuzo hiyo, Bellingham aliwashinda mchezaji wenzake wa Real Madrid, Vinicius Jr, Antoine Griezmann wa Atletico Madrid, Artem Dovbyk wa Girona na Robert Lewandowski wa Barcelona.
Mshindi wa tuzo hiyo hupatikana kwa kupigiwa kura na mashabiki, manahodha wa timu pamoja na jopo la wataalam na kwa Bellingham, akiwa Dortmund pia alitwaa tuzo ya mwanasoka bora wa msimu wa 2022-23.

“Ningependa kuitoa tuzo hii kwa wachezaji wenzangu, makocha na zaidi ya yote mashabiki wa klabu hii bora duniani,” alisema Bellingham.


Bellingham hata hivyo hakuweza kuhudhuria hafla ya utoaji tuzo hiyo iliyofanyika Jumanne jioni kwa kuwa anajiandaa kwa mechi ya Jumamosi dhidi ya Dortmund.

The post Bellingham nyota wa msimu La Liga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/30/bellingham-nyota-wa-msimu-la-liga/feed/ 0
Bellingham atwaa tuzo Hispania https://www.greensports.co.tz/2024/04/23/bellingham-atwaa-tuzo-hispania/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/23/bellingham-atwaa-tuzo-hispania/#respond Tue, 23 Apr 2024 14:33:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10721 Madrid, HispaniaKiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya England, Jude Bellingham ametwaa tuzo ya Laureus World Sports kwa namna alivyopata mafanikio akiwa katika msimu wake wa kwanza katika klabu hiyo na kuwa moto kwenye ligi mpya kwake.Bellingham alijiunga na Real Madrid majira ya kiangazi msimu huu kwa ada ya Pauni 89 milioni akitokea […]

The post Bellingham atwaa tuzo Hispania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya England, Jude Bellingham ametwaa tuzo ya Laureus World Sports kwa namna alivyopata mafanikio akiwa katika msimu wake wa kwanza katika klabu hiyo na kuwa moto kwenye ligi mpya kwake.
Bellingham alijiunga na Real Madrid majira ya kiangazi msimu huu kwa ada ya Pauni 89 milioni akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani na tangu wakati huo ameendelea kuwa mchezaji muhimu wa timu hiyo.
Juzi Jumapili, Bellingham alifunga bao la ushindi dhidi ya Barcelona katika El Clasico na hadi sasa ana mabao 17 katika Ligi Kuu Hispania au La Liga.
Bellingham pia ameiwezesha Real Madrid kufuzu hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuwatoa mabingwa watetezi Man City kwa mikwaju ya penalti kwenye hatua ya robo fainali.
Kwa upande mwingine tuzo kuu ya mwaka ya Laureus World Sports imekwenda kwa nyota wa tenisi Novak Djokovic ambaye anakuwa ameibeba tuzo hiyo kwa mara ya tano.
Tuzo aliyotwaa Djokovic kwa upande wa wanawake imekwenda kwa kiungo wa timu ya wanawake ya Barcelona ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania, Aitana Bonmati.
Bonmati ambaye kwa sasa anashikilia tuzo ya Ballon d’Or ameisaidia klabu yake kushinda mataji ya Liga F, Spanish Cup na Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa wanawake msimu wa 2022-23.
Katika vipengele vingine vya tuzo hiyo, timu ya wanawake Hispania imetwaa tuzo ya timu ya mwaka wakati nyota wa tenisi Hispania, Diede de Groot amebeba tuzo ya mwaka kwa upande wa wanamichezo wenye ulemavu.
,

The post Bellingham atwaa tuzo Hispania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/23/bellingham-atwaa-tuzo-hispania/feed/ 0
Madrid kuikatia rufaa kadi ya Bellingham https://www.greensports.co.tz/2024/03/05/madrid-kuikatia-rufaa-kadi-ya-bellingham/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/05/madrid-kuikatia-rufaa-kadi-ya-bellingham/#respond Tue, 05 Mar 2024 06:22:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10029 Madrid, HispaniaKlabu ya Real Madrid ya Hispania inajipanga kukata rufaa dhidi ya kadi nyekundu aliyopewa kiungo wake Jude Bellingham katika mechi dhidi ya Valencia iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2.Katika mechi hiyo iliyochezwa Jumamosi iliyopita, Bellingham alipewa kadi hiyo baada ya kuibuka mzozo baina ya wachezaji na maofisa wa Real Madrid dhidi ya mwamuzi wa […]

The post Madrid kuikatia rufaa kadi ya Bellingham first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Klabu ya Real Madrid ya Hispania inajipanga kukata rufaa dhidi ya kadi nyekundu aliyopewa kiungo wake Jude Bellingham katika mechi dhidi ya Valencia iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2.
Katika mechi hiyo iliyochezwa Jumamosi iliyopita, Bellingham alipewa kadi hiyo baada ya kuibuka mzozo baina ya wachezaji na maofisa wa Real Madrid dhidi ya mwamuzi wa mechi hiyo, Gil Minzano.
Habari zaidi zinadai kwamba ripoti ya Ginzano ilieleza kuwa Bellingham alitoa lugha kali dhidi ya mwamuzi zaidi ya mara moja kwa kile alichoamini kuwa mwamuzi huyo aliinyima timu yake bao ambalo lingewawezesha kutoka na ushindi wa 3-2.
Alichokuwa akikipinga Bellingham ni hatua ya mwamuzi huyo, Gil Minzano kupuliza filimbi ya kumaliza mchezo wakati alipopiga mpira wa kichwa uliotokana na krosi ya Brahim Diaz na kujaa wavuni katika dakika ya tisa ya dakika za nyongeza.
Baada ya mechi hiyo, kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti alimtetea Bellingham akisema kwamba mchezaji huyo hakutamka neno lolote la kumtusi mwamuzi wa mchezo huo.

“Tumeumizwa na kadi nyekundu aliyopewa Bellingham, hakutoa kauli yoyote ya kumtukana mwamuzi, alitoa kauli ya kulalamika kunyimwa goli kama ambavyo sisi sote tulikuwa katika fikra za aina hiyo,” alisema Ancelotti.


Bellingham alipewa kadi hiyo wakati mpira ukiwa umekwisha na kwa mujibu wa Ancelotti, mwamuzi alikosea na kusisitiza kwamba mchezaji wake alikuwa sahihi kwa kile alichokuwa akikilalamikia.

The post Madrid kuikatia rufaa kadi ya Bellingham first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/05/madrid-kuikatia-rufaa-kadi-ya-bellingham/feed/ 0
Bellingham alimwa kadi nyekundu https://www.greensports.co.tz/2024/03/04/bellingham-alimwa-kadi-nyekundu/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/04/bellingham-alimwa-kadi-nyekundu/#respond Mon, 04 Mar 2024 06:13:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10009 Valencia, HispaniaKiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham amelimwa kadi nyekundu baada ya kumlalamikia mwamuzi kwa kumnyima bao ambalo lingeiwezesha timu yake kutoka na ushindi wa mabao 3-2 badala yake timu hiyo iliambulia sare ya 2-2 dhidi ya Valencia.Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumamosi jioni, Real Madrid ililazimika kupambana kusaka mabao ya kusawazisha baada ya kuwa nyuma […]

The post Bellingham alimwa kadi nyekundu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Valencia, Hispania
Kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham amelimwa kadi nyekundu baada ya kumlalamikia mwamuzi kwa kumnyima bao ambalo lingeiwezesha timu yake kutoka na ushindi wa mabao 3-2 badala yake timu hiyo iliambulia sare ya 2-2 dhidi ya Valencia.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumamosi jioni, Real Madrid ililazimika kupambana kusaka mabao ya kusawazisha baada ya kuwa nyuma kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Duro dakika ya 27 na Yaremchuk dakika ya 30.
Real Madrid waliokolewa na mabao mawili ya dakika za 45 za 76 yaliyofungwa na Vinicius Jr ambaye katika hali ya kushangaza inadaiwa alijikuta akikumbana na kadhia ya ubaguzi wa rangi, tukio ambalo pia alikutana nalo msimu uliopita.
Katika dakika ya sita muda wa nyongeza, Belllingham aliujaza mpira wavuni kwa kichwa lakini mwamuzi Gil Manzano alipuliza filimbi kuashiria kumalizika kwa mchezo kabla krosi iliyozaa bao hilo haijapigwa.
Matokeo hayo yameendelea kuiimarisha Real Madrid kileleni mwa msimamo wa La Liga kwa tofauti ya pointi saba lakini tukio hilo lilimkera Bellingham ambaye alijikuta akiingia katika mzozo na mwamuzi huyo.
Wachezaji na maofisa wa Real Madrid walianza kumzonga Manzano na katika tukio hilo mwamuzi huyo alimpa Bellingham kadi nyekundu kwa kinachodhaniwa kuwa ni ushiriki wake katika mzozo huo.

The post Bellingham alimwa kadi nyekundu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/04/bellingham-alimwa-kadi-nyekundu/feed/ 0
Bellingham nje wiki tatu https://www.greensports.co.tz/2024/02/12/bellingham-nje-wiki-tatu/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/12/bellingham-nje-wiki-tatu/#respond Mon, 12 Feb 2024 06:59:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9689 Madrid, HispaniaKlabu ya Real Madrid imethibitisha kuwa kiungo wake, Jude Bellingham atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu baada ya kuumia enka katika mechi ya La Liga dhidi ya Girona iliyochezwa Jumamosi.Katika mechi hiyo ambayo Real Madrid ilitoka na ushindi wa mabao 4-0, Bellingham alifunga mawili kati ya hayo na kuifanya timu yake iongoze ligi […]

The post Bellingham nje wiki tatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Klabu ya Real Madrid imethibitisha kuwa kiungo wake, Jude Bellingham atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu baada ya kuumia enka katika mechi ya La Liga dhidi ya Girona iliyochezwa Jumamosi.
Katika mechi hiyo ambayo Real Madrid ilitoka na ushindi wa mabao 4-0, Bellingham alifunga mawili kati ya hayo na kuifanya timu yake iongoze ligi ikiwa imeizidi Girona inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi tano.
Bellingham alilazimika kutoka nje kabla ya mpira kumalizika ambapo kocha wake, Carlo Ancelloti alinukuliwa baada ya mechi akisema kwamba mchezaji huyo atafanyiwa vipimo kabla ya kuthibitishwa kwamba atakuwa nje wiki tatu.
Kuumia kwa mchezaji huyo kumekuja wakati mbaya kutokana na ratiba ngumu ya timu hiyo ambayo kesho Jumanne itakuwa uwanjani katika mechi ya hatua ya 16 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya RB Leipzig ya Ujerumani.
Real Madrid pia mwishoni mwa wiki itakuwa uwanjani kusaka pointi nyingine tatu muhimu za kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa La Liga itakapoumana na Rayo Vallecano.
Bellingham ambaye huu ni msimu wake wa kwanza na Real Madrid, ndiye kinara wa mabao wa timu hiyo akiwa hadi sasa amezifumania nyavu mara 20 katika mashindao yote huku mabao 16 kati ya hayo akiyafunga kwenye La Liga.

The post Bellingham nje wiki tatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/12/bellingham-nje-wiki-tatu/feed/ 0
Ancelotti awachambua Bellingham, Zizou https://www.greensports.co.tz/2023/11/30/ancelotti-awachambua-bellingham-zizou/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/30/ancelotti-awachambua-bellingham-zizou/#respond Thu, 30 Nov 2023 12:44:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8691 Madrid, HispaniaKiwango cha soka la kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham kimeendelea kumfurahisha kocha wake, Carlo Ancelotti ambaye amechambua sifa za mchezaji huyo na nyota wa zamani wa timu hiyo, Zinedine Zidane au Zizou.Ancelotti alitoa uchambuzi huo jana Jumatano mara baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Napoli, mechi ambayo Real Madrid […]

The post Ancelotti awachambua Bellingham, Zizou first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kiwango cha soka la kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham kimeendelea kumfurahisha kocha wake, Carlo Ancelotti ambaye amechambua sifa za mchezaji huyo na nyota wa zamani wa timu hiyo, Zinedine Zidane au Zizou.
Ancelotti alitoa uchambuzi huo jana Jumatano mara baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Napoli, mechi ambayo Real Madrid ilitoka na ushindi wa mabao 4-2 huku Bellingham akicheza soka la kuvutia.
Katika mechi hiyo iliyopigwa katika dimba la Santiago Bernabeu, Bellingham ndiye aliyefunga kwa kichwa bao la pili la Real Madrid baada ya Napoli kupata bao la kwanza kupitia Giovanni Simeone na Rodrygo kusawazisha.
Napoli walisawazisha kupitia Frank Zambo na kufanya matokeo kuwa 2-2 lakini Madrid waliongeza bao la tatu lililofungwa na Nico Paz na Bellingham kutoa pasi iliyozaa bao la nne mfungaji akiwa Joselu.
“Ni vigumu kulinganisha vizazi viwili tofauti, ninachokiona ni uwezo wa Bellingham kuingia kwenye boksi, Zidane hakuwa na hilo lakini kuna sifa na hadhi ya kipekee ambayo Zidane alikuwa nayo na Bellingham hana,” alisema Ancelotti alipotakiwa na waandishi kutoa tathmini yake kuhusu Bellingham na Zidane ambaye alikuwa jukwaani akiangalia mechi hiyo.

Ancelotti hata hivyo alisema kwamba kinachotokea sasa ni soka la zama hizi ambalo linahitaji mchezaji mwenye nguvu zinazohitajika kama ilivyo kwa Bellingham, ambaye kwa haraka unaweza kumuona katika sehemu kubwa ya uwanja.

“Anatushangaza kila siku na katika kila mechi, si kwamba anatushangaza sisi tu bali anamshangaza kila mtu, Bellingham ni zawadi ya soka, kocha wake na wachezaji wenzake wanafurahia kuwa naye na mashabiki pia wanafurahia lakini kila mmoja anafurahia kuona mchezaji mwenye sifa zake na mwenye mtazamo chanya,” alisema Ancelotti.


Bellingham hadi sasa amefunga jumla ya mabao 15 katika mechi 16 za Real Madrid, na zaidi ya hilo ana rekodi ya kufunga goli katika kila mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya aliyocheza hadi sasa.

The post Ancelotti awachambua Bellingham, Zizou first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/30/ancelotti-awachambua-bellingham-zizou/feed/ 0
Bellingham ailiza Barca, Ancelotti amshangaa https://www.greensports.co.tz/2023/10/29/bellingham-ailiza-barca-ancelotti-amshangaa/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/29/bellingham-ailiza-barca-ancelotti-amshangaa/#respond Sat, 28 Oct 2023 21:14:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8269 Madrid, HispaniaKocha Carlo Ancelotti ameshangazwa na kiwango cha ufungaji mabao cha kiungo Jude Bellingham baada ya mchezaji huyo kufunga mabao mawili Real Madrid ikiwalaza mahasimu wao, Barcelona mabao 2-1.Bellingham kwanza alifunga bao la kusawazisha dakika 68 katika mechi iliyopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Olympic baada ya Ilkay Gundogan kuipa Barca bao la kuongoza mapema […]

The post Bellingham ailiza Barca, Ancelotti amshangaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kocha Carlo Ancelotti ameshangazwa na kiwango cha ufungaji mabao cha kiungo Jude Bellingham baada ya mchezaji huyo kufunga mabao mawili Real Madrid ikiwalaza mahasimu wao, Barcelona mabao 2-1.
Bellingham kwanza alifunga bao la kusawazisha dakika 68 katika mechi iliyopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Olympic baada ya Ilkay Gundogan kuipa Barca bao la kuongoza mapema dakika ya sita.
Kiungo huyo wa England aliongeza bao la pili kwa timu yake katika dakika za nyongeza na kuifanya Real Madrid itoke na pointi tatu muhimu zinazoifanya ishike usukani wa La Liga ikiwa na pointi 28.
“Kwanza alifunga bao lililovutia akawa makini hadi kufunga bao la pili, tunashangazwa, kila mmoja anashangazwa na kiwango chake hasa kiwango cha umakini akiwa mbele,” alisema Ancelotti baada ya mechi hiyo.
“Anaingia kwenye ‘boksi’ lakini leo shuti la bao la kwanza limetushangaza, amefunga bao ambalo limekuwa kivutio mno, kwa sasa ni aina ya mchezaji anayeweza kuleta utofauti,” alisema Ancelotti.
Bellingham kwa sasa amefikisha mabao 10 katika mechi 10 za ligi akiwa kwenye msimu wake wa kwanza na Real Madrid na ndiye kinara wa mabao na kwa mashindano yote hadi sasa ana mabao 13 baada ya kufunga matatu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Anaonekana kama ni mchezaji mkongwe, yuko vizuri, bao lake la kusawazisha lilibadili kabisa kasi ya mchezo, lilimaanisha sisi kupata nguvu zaidi na kusababisha udhaifu kwa Barcelona ambao tayari walikuwa wanacheza vizuri hadi wakati huo,” aliongeza Ancelotti.


Bellingham pia alisifiwa na kiungo mwenzake wa timu hiyo, Luka Modric ambaye alisema kwamba wanamfurahia mchezaji huyo na kuongeza kuwa kwa sasa anaonekana kama amekuwa kwenye timu hiyo kwa kipindi kirefu.
Matokeo mechi za La Liga Jumamosi…
Barcelona 1-2 Real Madrid
Almería 1-2 Las Palmas
Mallorca 0-0 Getafe
Cadiz 2-2 Sevilla

The post Bellingham ailiza Barca, Ancelotti amshangaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/29/bellingham-ailiza-barca-ancelotti-amshangaa/feed/ 0
Bellingham ajipa miaka 10 Real Madrid https://www.greensports.co.tz/2023/10/18/bellingham-ajipa-miaka-10-real-madrid/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/18/bellingham-ajipa-miaka-10-real-madrid/#respond Wed, 18 Oct 2023 08:44:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8141 London, EnglandKiungo wa klabu ya Real Madrid, Jude Bellingham amesema anataka kuwa katika timu hiyo kwa miaka 10 akidai kwamba klabu hiyo imelifikisha soka lake katika kiwango kipya.Bellingham alitoa mchango mkubwa katika ushindi wa mabao 3-1 ambao England uliupata katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Ulaya 2024 (Euro 24) iliyopigwa kwenye dimba […]

The post Bellingham ajipa miaka 10 Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kiungo wa klabu ya Real Madrid, Jude Bellingham amesema anataka kuwa katika timu hiyo kwa miaka 10 akidai kwamba klabu hiyo imelifikisha soka lake katika kiwango kipya.
Bellingham alitoa mchango mkubwa katika ushindi wa mabao 3-1 ambao England uliupata katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Ulaya 2024 (Euro 24) iliyopigwa kwenye dimba la Wembley jana Jumanne.
Kwa msimu huu pekee, Bellingham ameshafunga jumla ya mabao 11 kwa timu ya England na klabu yake katika mechi 13 akiwa pia na asisti sita.
Bellingham aliyejiunga na Real Madrid akitokea Borussia Dortmund kwa ada ya Euro milioni 103, alisema kwamba ameendelea kuwa bora kila wakati anapocheza.
“Ulikuwa usiku mzuri kwetu, sote tunakumbuka kilichotokea miaka michache iliyopita walipokuwa wakicheza nasi, wakati wote malengo huwa ni kupiga hatua, tunaelekea katika njia sahihi na huu ni ushindi muhimu kwetu,” alisema Bellingham.

“Nalipenda soka ninapokuwa nacheza, katika klabu na timu ya taifa napewa uhuru wa kucheza jinsi ninavyoona, tangu mwezi uliopita nimekuwa nikipigania kucheza niwe naingia kwenye ‘box’ na ninapofika nakuwa mwenye hasira,” alisema Bellingham.


Bellingham pia alisema kwamba baada ya uhamisho wake mkubwa wa kujiunga na Real Madrid ukweli ni kwamba kinachofuata ni matokeo katika uchezaji iwe ni kufunga magoli au kutoa asisti au kucheza katika kiwango cha kuipa timu ushindi,” alisema.

The post Bellingham ajipa miaka 10 Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/18/bellingham-ajipa-miaka-10-real-madrid/feed/ 0