Azam FC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 09 May 2026 14:44:37 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Azam FC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Watoza kodi waichapa Azam 4-1 https://www.greensports.co.tz/2026/05/08/watoza-kodi-waichapa-azam-4-1/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/08/watoza-kodi-waichapa-azam-4-1/#respond Fri, 08 May 2026 19:18:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14619 Na mwandishi wetuTimu ya TRA United au Watoza Kodi, imetoa kichapo cha mabao 4-1 kwa Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, leo Ijumaa, Mei 8, 2026.Azam waliuanza mchezo kwa kasi wakionesha dhamira ya kusaka pointi tatu na kasi yao ilizaa matunda mapema dakika ya saba […]

The post Watoza kodi waichapa Azam 4-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya TRA United au Watoza Kodi, imetoa kichapo cha mabao 4-1 kwa Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, leo Ijumaa, Mei 8, 2026.
Azam waliuanza mchezo kwa kasi wakionesha dhamira ya kusaka pointi tatu na kasi yao ilizaa matunda mapema dakika ya saba walipopata bao lao pekee lililofungwa na Japhet Kitambala aliyeitumia pasi ya Sadio Kanoute.
Iliwachukua dakika 12 TRA kusawazisha bao hilo mfungaji akiwa Ally Ng’anzi aliyeyatumia vizuri mapungufu ya safu ya ulinzi ya Azam kuipatia TRA bao la kusawazisha kwa pasi ya Ally Mapaka.
Kuingia bao hilo hakukuwasumbua Azam ambao waliendelea kuonesha uhai ingawa kadri muda ulivyokwenda ndivyo kasi ya TRA ilivyoongezeka na Azam kujikuta wakipachikwa mabao mawili ya haraka haraka.
Mabao hayo yalifungwa na Amy Mapaka katika dakika ya 41 na Mapaka tena akaongeza bao la pili dakika ya 44 na kuifanya TRA iende mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-1.
Karamu ya mabao ya TRA ilikamilishwa dakika ya 64 kwa bao lililofungwa na Ramadhan Chobwedo aliyefumua shuti kali lililomshinda kipa Aishi Manula wa Azam.
Matokeo hayo mbali ya kuvuruga mbio za Azam katika kulisaka taji la ligi hiyo, pia yanakuwa yameivunja rekodi ya Azam ya kutopoteza mechi zake za ligi msimu huu.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa leo, Namungo wakiwa nyumbani Lindi walishindwa kuwadhibiti wageni wao Mashujaa na kujikuta wakitoka sare ya bila kufungana.

The post Watoza kodi waichapa Azam 4-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/08/watoza-kodi-waichapa-azam-4-1/feed/ 0
Azam yaiadhibu Singida Black https://www.greensports.co.tz/2026/04/04/azam-yaiadhibu-singida-black/ https://www.greensports.co.tz/2026/04/04/azam-yaiadhibu-singida-black/#respond Sat, 04 Apr 2026 20:22:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14516 Na mwandishi wetuAzam FC imenyakua pointi tatu muhimu katika Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Singida Black Stars mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa Jumatano Aprili 1, 2026 kwenye Uwanja wa Airtel mjini Singda.Kipigo hicho ni mwendelezo wa matokeo yasiyopendeza kwa Singida Black ambayo ni hivi karibuni tu imetoka kuchezea kichapo kingine cha mabao 3-0 mbele […]

The post Azam yaiadhibu Singida Black first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Azam FC imenyakua pointi tatu muhimu katika Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Singida Black Stars mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa Jumatano Aprili 1, 2026 kwenye Uwanja wa Airtel mjini Singda.
Kipigo hicho ni mwendelezo wa matokeo yasiyopendeza kwa Singida Black ambayo ni hivi karibuni tu imetoka kuchezea kichapo kingine cha mabao 3-0 mbele ya Yanga na hivyo kubakiwa na pointi 25 katika mechi 16.
Kwa upande wa Azam ushindi huo umeendelea kufufua matumaini ya timu hiyo kwenye mbio za kulisaka taji la ligi ikiwa imefikisha pointi 32 katika mechi 16 na kuwasogelea vinara Yanga kwa tofauti ya pointi sita.
Azam ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya 50 mfungaji akiwa ni Lusajo Mwaikenda baada ya kuiwahi krosi iliyochongwa na Idd Suleiman ‘Nado’ ambaye pia alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Dakika 15 baadaye, Azam waliandika bao la pili lililofungwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye aliuwahi mpira akiwa ndani ya eneo la penalti na kupiga shuti dhaifu lililojaa wavuni.
Singida walipambana na katika dakika ya 70 walifanikiwa kupata bao pekee lililofungwa na Lyanga, bao lililotokana na mpira wa adhabu iliyopigwa na Ande Koffi.

The post Azam yaiadhibu Singida Black first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/04/04/azam-yaiadhibu-singida-black/feed/ 0
Azam, Singida mambo mazuri https://www.greensports.co.tz/2026/01/26/azam-singida-mambo-mazuri/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/26/azam-singida-mambo-mazuri/#respond Mon, 26 Jan 2026 19:40:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14294 Na mwandishi wetuJumapili ya Januari 26, 2026 imekuwa siku nzuri kwa Azam FC na Singida Black Stars, kila moja imetoka na ushindi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam ikiilaza Nairobi United na Singida ikiichapa Otôho.Azam wakiwa ugenini waliichapa Nairobi United mabao 2-1 wakati Singida wakiwa nyumbani waliichapa Otoho ya Congo Brazzavile bao 1-0.Azam […]

The post Azam, Singida mambo mazuri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Jumapili ya Januari 26, 2026 imekuwa siku nzuri kwa Azam FC na Singida Black Stars, kila moja imetoka na ushindi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam ikiilaza Nairobi United na Singida ikiichapa Otôho.
Azam wakiwa ugenini waliichapa Nairobi United mabao 2-1 wakati Singida wakiwa nyumbani waliichapa Otoho ya Congo Brazzavile bao 1-0.
Azam waliokuwa ugenini Nairobi, Kenya waliianza vibaya mechi hiyo kwa kuchapwa bao la dakika ya 13 lililofungwa na Dancan Omala akiitumia vizuri pasi ya Michael Karamor.
Iliwachukua dakika nne wawakilishi hao wa Tanzania kusawazisha bao hilo kupitia kwa Jephte Kitambala ambaye alifumua shuti baada ya kuinasa pasi ya Yoro Diaby.
Timu hizo ziliendelea kupambana kila moja ikisaka bao la kuongoza lakini walikuwa ni Azam waliopata bao la ushindi dakika ya 78, bao lililotokana na shuti la Himid Mao na mpira kugonga mwamba kabla ya kumgonga kipa wa Nairobi United, Ernest Mohamed kabla ya kujaa wavuni.
Nao Singida walineemeka kwa bao pekee la Elvis Rupia na kutoka kifua mbele kwa ushindi huo mwembamba ambao ulitosha kuwatoa Otoho vichwa chini.

The post Azam, Singida mambo mazuri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/26/azam-singida-mambo-mazuri/feed/ 0
Azam yaiadhibu Simba https://www.greensports.co.tz/2026/01/09/azam-yaiadhibu-simba/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/09/azam-yaiadhibu-simba/#respond Fri, 09 Jan 2026 19:34:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14260 Na mwandishi wetuKocha mpya wa Simba, Steve Barker ameonja machungu ya kufungwa mara ya kwanza baada ya timu yake kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kupokea kichapo cha bao 1-0 mbele ya Azam FC.Katika mechi hiyo iliyopigwa Alhamisi Januari 8, 2026, bao pekee lililoizamisha Simba lilifungwa na Lameck Lawi katika dakika ya 73 […]

The post Azam yaiadhibu Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mpya wa Simba, Steve Barker ameonja machungu ya kufungwa mara ya kwanza baada ya timu yake kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kupokea kichapo cha bao 1-0 mbele ya Azam FC.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Alhamisi Januari 8, 2026, bao pekee lililoizamisha Simba lilifungwa na Lameck Lawi katika dakika ya 73 na kuwaondoa Simba mashindanoni.
Matokeo hayo ni pigo la kwanza kwa Barker ambaye amejiunga na Simba Desemba mwaka jana akitokea Stellenbosch ya Afrika Kusini na hadi sasa tayari ameiongoza timu hiyo katika mechi tatu na kati ya hizo ameshinda mbili.
Wakati Simba ikiaga kwneye Kombe la Mapinduzi, Azam imefuzu hatua ya fainali ya michuano hiyo ya kila mwaka na sasa inasubiri kucheza mechi ya fainali dhiddi ya mshindi wa mechi kati ya Yanga na Singida Black Stars.
Barker amekabidhiwa jukumu la kuinoa Simba baada ya kutimuliwa kwa Dimitar Pantev, bado ana kibarua kingine kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika katika hatua ya makundi pamoja na Ligi Kuu NBC.
Simba sasa inarejea Dar es Salaam ikijiandaa kwa ligi kuu wakati kwenye ligi ya mabingwa itakuwa na kibarua Januari 23 mwaka huu dhidi ya Esperance ya Tunisia.

The post Azam yaiadhibu Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/09/azam-yaiadhibu-simba/feed/ 0
Azam yairarua Simba 2-0 https://www.greensports.co.tz/2025/12/10/azam-yairarua-simba-2-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/10/azam-yairarua-simba-2-0/#respond Wed, 10 Dec 2025 18:49:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14158 Na mwandishi wetuSimba imekutana na kipigo cha kwanza katika Ligi Kuu NBC baada ya kulala kwa mabao 2-0 mbele ya Azam FC katika mechi iliyopigwa Jumapili Novemba 7, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.MAtokeo hayo mabaya yamekuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu timu hiyo iachane na kocha wake, Dimitar Pantev baada ya […]

The post Azam yairarua Simba 2-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imekutana na kipigo cha kwanza katika Ligi Kuu NBC baada ya kulala kwa mabao 2-0 mbele ya Azam FC katika mechi iliyopigwa Jumapili Novemba 7, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
MAtokeo hayo mabaya yamekuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu timu hiyo iachane na kocha wake, Dimitar Pantev baada ya kufanya vibaya katika mechi mbili za hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba kwa sasa ipo chini ya kocha Suleiman Matola ambaye amekabidhiwa jukumu hilo na katika mechi yake hiyo ya kwanza mambo yamekwenda vibaya.
Simba ilionesha uhai na kujengeka matumaini ya timu hiyo kuendeleza wimbi la ushindi katika ligi hiyo lakini kadri muda ulivyokwenda ndivyo mapungufu ya timu hiyo yalipojidhihirisha.
Baada ya kushambuliana mara kadhaa huku kila timu ikitaka kulandika bao la kwanza, kasi hiyo iliendelea kwa kipindi chote cha kwanza na timu kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana kabla ya mambo kuiharibikia Simba katika kipindi cha pili.
Azam waliandika bao la kwanza dakika ya 81 mfungaji akiwa ni Japhet Kitambala aliyeuwahi mpira katika eneo la hatari na kufumua shuti lililojaa wavuni.
Simba wakionekana kushtushwa na bao hilo la jioni walipambana lakini kwa mara nyingine nyota ya Azam ndiyo iliyong’ara baada ya timu hiyo kuandika bao la pili na la ushindi lililofungwa na Idd Nado katika dakika ya 89.

The post Azam yairarua Simba 2-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/10/azam-yairarua-simba-2-0/feed/ 0
Azam yaipa KMKM dozi ya 7-0 https://www.greensports.co.tz/2025/10/25/azam-yaipa-kmkm-dozi-ya-7-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/10/25/azam-yaipa-kmkm-dozi-ya-7-0/#respond Sat, 25 Oct 2025 17:21:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14026 Na mwandishi wetuAzam FC imetinga kwa kishindo hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika ikiichakaza KMKM mabao 7-0 na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 9-0 baada ya ushindi wa mabao 2-0 iliyoupata katika mchezo wa awali.Ikiwa nyumbani kwenye dimba la Azam Complex Jumamosi hii Oktoba 24, Azam ilianza kuhesabu bao la kwanza dakika ya […]

The post Azam yaipa KMKM dozi ya 7-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Azam FC imetinga kwa kishindo hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika ikiichakaza KMKM mabao 7-0 na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 9-0 baada ya ushindi wa mabao 2-0 iliyoupata katika mchezo wa awali.
Ikiwa nyumbani kwenye dimba la Azam Complex Jumamosi hii Oktoba 24, Azam ilianza kuhesabu bao la kwanza dakika ya 22 kwa bao la Idd Nado alipoinasa pasi ya Feisal Salum au Fei Toto.
Dakika nne baada ya bao hilo, Azam waliongeza bao la pili safari hii Nado kwa mara nyingine alihusika kwa kupiga krosi ambayo Jephte Kitambala aliitumia vyema kuipatia Azam bao hilo.
Dakika ya 29, Kitambala aliipatia Azam bao la tatu safari hii kwa pasi ya Fei Toto kabla ya kukamilisha bao la nne, mabao ambayo yalidumu kwa dakika zote 45 za kipindi cha kwanza.
KMKM ilikianza kipindi cha pili kivingine ikifanya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji lakini mabadiliko hayo hayakuweza kuwazuia Azam kuendelea na kasi yao ya kusaka mabao.
Kasi hiyo ilizaa mabao ya Abdul Sopu aliyefunga mawili pamoja na Paschal Msindo aliyekamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la saba na la mwisho.
Kwa ushindi huo Azam sasa wanaisubiri kwa hamu Novemba 3 ya mwaka huu, siku ambayo droo ya kupanga makundi ya timu zilizofuzu hatua hiyo itakapofanyika na timu hiyo kuwajua wapinzani wake.

The post Azam yaipa KMKM dozi ya 7-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/10/25/azam-yaipa-kmkm-dozi-ya-7-0/feed/ 0
Azam, Yanga mwanzo mzuri https://www.greensports.co.tz/2025/09/25/azam-yanga-mwanzo-mzuri/ https://www.greensports.co.tz/2025/09/25/azam-yanga-mwanzo-mzuri/#respond Thu, 25 Sep 2025 15:07:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13950 Na mwandishi wetuAzam FC imeianza Ligi Kuu NBC vizuri kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex kwa kuichapa Mbeya City mabao 2-0 wakati Yanga nayo ikianza kwa kuinyuka Pamba Jiji mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.Mechi hizo za mwanzo za ligi hiyo zimechezwa Jumatano hii Septemba 24, 2025 ambapo Azam chini ya kocha […]

The post Azam, Yanga mwanzo mzuri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Azam FC imeianza Ligi Kuu NBC vizuri kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex kwa kuichapa Mbeya City mabao 2-0 wakati Yanga nayo ikianza kwa kuinyuka Pamba Jiji mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mechi hizo za mwanzo za ligi hiyo zimechezwa Jumatano hii Septemba 24, 2025 ambapo Azam chini ya kocha wao mpya, Florent Ibenge walianza kuziona nyavu za Mbeya City kwa bao la dakika ya 32 lililofungwa na Nassor Saadun.
Bao hilo lilitokana na shambulizi lililotokana na mpira wa kona lililoanzishwa na Feisal Salum au Fei Toto na mpira kumfikia Abdul Sopu aliyetoa pasi iliyozaa bao hilo lililodumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili Azam walikianza kwa kasi na kuandika bao la pili katika muda usiozidi dakika moja baada ya kuanza kipindi hicho mfungaji akiwa Fei Toto aliyeitumia pasi ya mchezaji bora wa mechi hiyo, Baraket lhmidi.
Kwa upande wa Yanga wao walianza kuzichana nyavu za Pamba dakika ya 45 kwa bao la nyota wao mpya, Lassine Kouma aliyefunga kwa kichwa baada ya kuruka juu na kuuwahi mpira wa kona iliyochongwa na Edmund John.
Kipindi cha pili kocha wa Yanga, Romain Folz alifanya mabadiliko kadhaa yaliyoonekana kuipa uhai timu hiyo na kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na mchezaji bora wa mechi hiyo, Maxi Nzengeli dakika ya 61 akiitumia pasi ya aliyekuwa beki wa Simba, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Junior’.
Kasi ya Yanga iliendelea ambapo wapinzani wao Pamba Jiji wakajikuta wakiwa na kazi ngumu ya kujihami na hata walipojaribu kufanya mashambulizi hayakuweza kuleta athari zozote kwenye lango la Yanga.
Ikiwa imebakia dakika moja mpira kumalizika, Yanga waliandika bao la tatu lililofungwa na Mudathir Yahya ambaye aliitumia krosi iliyochongwa na Pacome Zouzoua.

The post Azam, Yanga mwanzo mzuri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/09/25/azam-yanga-mwanzo-mzuri/feed/ 0
Yanga yaitandika Azam 2-1 https://www.greensports.co.tz/2025/04/10/yanga-yaitandika-azam-2-1/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/10/yanga-yaitandika-azam-2-1/#respond Thu, 10 Apr 2025 19:36:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13236 Na mwandishi wetuYanga imeendelea na makali yake kwenye Ligi Kuu NBC baada ya kuinyuka Azam FC mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa leo Alhamisi, Aprili 10, 2025 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.Ushindi huo ni hatua muhimu kwa Yanga katika mbio zake za kulitetea taji la ligi hiyo kwa kuwa Azam ni moja ya […]

The post Yanga yaitandika Azam 2-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imeendelea na makali yake kwenye Ligi Kuu NBC baada ya kuinyuka Azam FC mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa leo Alhamisi, Aprili 10, 2025 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Ushindi huo ni hatua muhimu kwa Yanga katika mbio zake za kulitetea taji la ligi hiyo kwa kuwa Azam ni moja ya timu ambazo zilizoaminika kuwa na ubora wa kuizua Yanga lakini imekwama.
Yanga walianza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 10 mfungaji akiwa Pacome Zouzoua kabla ya kuongeza la pili dakika ya 34 lililofungwa na Prince Dube ambaye pia aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo.
Juhudi za Azam kusawazisha mabao hayo hazikuweza kuzaa matunda badala yake timu hiyo iliishia kupata bao pekee la kufutia machozi lililofungwa na Lusajo Mwaikenda katika dakika ya 82.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuendelea kushikilia usukani wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 67 katika mechi 25.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizopigwa leo, Coastal Union ikiwa nyumbani Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani iliichapa Singida B kwa mabao 2-1.
Kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mambo yaliendelea kuwa magumu kwa Tabora United baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Mashujaa wakati JKT Tanzania ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ilitoka sare ya mabao 2-2 na Namungo FC.

The post Yanga yaitandika Azam 2-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/10/yanga-yaitandika-azam-2-1/feed/ 0
Simba, Azam zatoka sare 2-2 https://www.greensports.co.tz/2025/02/24/simba-azam-zatoka-sare-2-2/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/24/simba-azam-zatoka-sare-2-2/#respond Mon, 24 Feb 2025 18:47:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13050 Na mwandishi wetuSimba na Azam FC zimetoka uwanjani kwa sare ya mabao 2-2 katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa leo Jumatatu, Februari 24, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.Azam waliuanza mchezo kwa kasi na kufanya shambulizi katika dakika ya kwanza lililozaa bao mfungaji akiwa ni Gibril Sillah aliyeitumia pasi ya Idd Nado.Mpira […]

The post Simba, Azam zatoka sare 2-2 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba na Azam FC zimetoka uwanjani kwa sare ya mabao 2-2 katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa leo Jumatatu, Februari 24, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Azam waliuanza mchezo kwa kasi na kufanya shambulizi katika dakika ya kwanza lililozaa bao mfungaji akiwa ni Gibril Sillah aliyeitumia pasi ya Idd Nado.
Mpira uliozaa bao ulitokana na makosa ya Fabrice Ngoma ambaye aliporwa mpira ukiwa katika miliki yake kabla ya kumkuta Sillah ambaye shuti lake la kwanza liliokolewa na kipa Mussa Camara kabla ya kumrudia mfungaji aliyeujaza wavuni.
Wakicheza kwa kujiamini Simba walianza kuliandama lango la Azam na kupata bao la kusawazisha lililofungwa na Elly Mpanzu katika dakika ya 26.
Bao hilo lilitokana na juhudi za Kibu Denis ambaye aliinasa pasi ya Shomari Kapombe akiwa nje kidogo ya eneo la 18 la Simba, akaambaa na mpira na kuvuka kidogo eneo la kati ya uwanja kabla ya kumpasia Mpanzu.
Dakika ya 75 Simba waliandika bao la pili lililofungwa kwa kichwa na Abdulrazak Hamza akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Jean Ahoua, adhabu ambayo mwamuzi Ahmed Arajiga aliitoa baada ya Kibu kuchezewa rafu.
Matumaini ya Simba kutoka na pointi zote tatu yalizimwa na Zidane Sereri aliyeingia akitokea benchi katika dakika 10 za mwisho na kufunga bao la kusawazisha.
Bao hilo lilitokana na pasi ndefu ya Feisal Salum ‘Fei Toto’ pasi ambayo haikutarajiwa kama ingemkuta mfungaji lakini ilitosha kuibua shangwe kwa mashabiki wa Azam.
Kwa matokeo hayo, Simba inaendelea kubaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 51 katika mechi 20 wakiwa nyuma ya Yanga wanaoshika usukani wa ligi hiyo wakiwa na pointi 55 katika mechi 21.

The post Simba, Azam zatoka sare 2-2 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/24/simba-azam-zatoka-sare-2-2/feed/ 0
Azam yashika usukani ligi kuu https://www.greensports.co.tz/2024/12/02/azam-yashika-usukani-ligi-kuu/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/02/azam-yashika-usukani-ligi-kuu/#respond Mon, 02 Dec 2024 12:37:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12298 Na mwandishi wetuAzam FC imeichapa Dodoma Jiji mabao 3-1 na kuchupa hadi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC baada ya kufikisha pointi 30 katika mechi 13 ilizocheza hadi sasa.Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, wenyeji Dodoma Jiji ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya saba baada ya […]

The post Azam yashika usukani ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Azam FC imeichapa Dodoma Jiji mabao 3-1 na kuchupa hadi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC baada ya kufikisha pointi 30 katika mechi 13 ilizocheza hadi sasa.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, wenyeji Dodoma Jiji ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya saba baada ya Yanick Bangala kujifunga.
Iliwachukua dakika nne, Azam kusawazisha bao hilo kupitia kwa Nassor Saaduni na kuongeza bao la pili muda mfupi kabla ya timu kwenda mapumziko kwa bao la penalti lililofungwa na Feisal Salum au Fei Toto.
Kama ilivyokuwa kwa Azam, Dodoma Jiji nao waliwazawadia Azam bao la bure baada ya nyota wake Dickson Mhilu kujifunga katika dakika ya 60.
Azam pamoja na ushindi huo kuwawezesha kushika usukani lakini wanafuatiwa kwa karibu na Simba wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 28 na Yanga wanaoshika nafasi ya tatu na pointi zao 27.
Simba na Yanga pia zimecheza mechi 11 hadi sasa wakati Azam imecheza mechi 13 hivyo timu hiyo inaweza kushushwa kileleni wakati wowote vinginevyo iendelee kushinda huku ikiziombea Simba na Yanga zipoteze mechi zao.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa Jumapili, bao pekee la George Mpole liliiwezesha Pamba Jiji kutoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ken Gold.
Mechi kati ya Coastal Union na Prisons ilishindwa kuchezwa baada ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha kujaa maji kutokana na mvua na mechi hiyo sasa inachezwa Jumatatu.

The post Azam yashika usukani ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/02/azam-yashika-usukani-ligi-kuu/feed/ 0