Aubameyang - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 09 Jan 2026 19:36:21 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Aubameyang - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Serikali Gabon yaifuta timu ya taifa https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/serikali-gabon-yaifuta-timu-ya-taifa/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/serikali-gabon-yaifuta-timu-ya-taifa/#respond Sun, 04 Jan 2026 06:17:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14244 Libreville, GabonSerikali nchini Gabon imechukua uamuzi mgumu wa kuifuta timu ya taifa baada ya kufanya vibaya kwenye fainali za Afcon zinazoendelea nchini Morocco.Sambamba na hilo, serikali hiyo pia imemuondoa katika kikosi hicho mshambuliaji mkongwe wa timu hiyo, Pierre-Emerick Aubameyang pamoja na kumfuta kazi kocha mkuu wa timu hiyo, Thierry Mouyouma na kulivunja benchi zima la […]

The post Serikali Gabon yaifuta timu ya taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Libreville, Gabon
Serikali nchini Gabon imechukua uamuzi mgumu wa kuifuta timu ya taifa baada ya kufanya vibaya kwenye fainali za Afcon zinazoendelea nchini Morocco.
Sambamba na hilo, serikali hiyo pia imemuondoa katika kikosi hicho mshambuliaji mkongwe wa timu hiyo, Pierre-Emerick Aubameyang pamoja na kumfuta kazi kocha mkuu wa timu hiyo, Thierry Mouyouma na kulivunja benchi zima la ufundi.
Vipigo mfulululizo vimeifanya timu hiyo iage mapema fainali za Afcon ikianza kwa kuchapwa bao 1-0 na mahasmu wao Cameroon kabla ya kukutana na kichapo cha mabao 3-2 mbele ya Msumbiji.
Uamuzi huo wa Serikali ya Gabon umechukuliwa ikiaminika sababu ikiaminika kuwa ni kutofurahishwa na mwenendo mzima wa timu hiyo kwenye Afcon na inadaiwa hatua nyingine zitafuata baada ya uamuzi huo.

“Kwa kuzingatia madhara ya jumla ya mwenendo wa timu, serikali imeamua kulivunja benchi zima la ufundi kuifuta timu ya taifa hadi uamuzi mwingine utakapofikiwa na kuwaondoa katika timu hiyo wachezaji Bruno Ecuélé Manga na Pierre-Emerick Aubameyang,”ilieleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Waziri wa Michezo wa Gabon, Simplice-Desire Mamboula.


Aubameyang (pichani juu) na Ecuele Manga ambao awali walijiuzulu kuichezea timu hiyo kabla ya kubadili maamuzi na kuitwa katika kikosi hicho, kila mmoja wao alikuwa nahodha katika mechi mbili za awali za Afcon.
Kitendo cha Aubameyang ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 36, kurudi katika timu hiyo kiliwashangaza baadhi ya watu kwa kuwa alikuwa akijiuguza baada ya kuumia wakati akiitumikia timu ya Marseille ya Ufaransa kabla ya kuanza kwa fainali za Afcon.
Kwa upande wake, Aubameyang alijitetea akisema kwamba anadhani matatizo ya timu ya taifa ya Gabon ni makubwa kuliko kumuangalia yeye mtu mmoja.
Uamuzi huo wa serikali hata hivyo huenda ukaiingiza nchi hiyo katika mgogoro na Fifa kwa kuwa kanuni za Fifa haziruhusu serikali kujiingiza na kuchukua hatua katika masuala yahusuyo soka.

The post Serikali Gabon yaifuta timu ya taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/serikali-gabon-yaifuta-timu-ya-taifa/feed/ 0
Aubameyang avamiwa, afungwa pingu https://www.greensports.co.tz/2022/08/29/aubameyang-avamiwa-afungwa-pingu/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/29/aubameyang-avamiwa-afungwa-pingu/#respond Mon, 29 Aug 2022 12:47:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2610 Barcelona, HispaniaMshambuliaji wa Barcelona, Pierre-Emerick Aubameyang amevamiwa nyumbani kwake na kupigwa na majambazi waliokuwa na silaha mbalimbali zikiwamo za chuma.Klabu ya Barcelona imethibitisha kutokea kwa uvamizi huo Jumatatu hii ambapo Aubameyang na mkewe walifungwa pingu kwa muda wa tukio hilo ingawa hakuna kati yao aliyeachwa na majeraha makubwa.Mapema Jumatatu hii, majambazi hao walivunja na kuingia […]

The post Aubameyang avamiwa, afungwa pingu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Mshambuliaji wa Barcelona, Pierre-Emerick Aubameyang amevamiwa nyumbani kwake na kupigwa na majambazi waliokuwa na silaha mbalimbali zikiwamo za chuma.
Klabu ya Barcelona imethibitisha kutokea kwa uvamizi huo Jumatatu hii ambapo Aubameyang na mkewe walifungwa pingu kwa muda wa tukio hilo ingawa hakuna kati yao aliyeachwa na majeraha makubwa.
Mapema Jumatatu hii, majambazi hao walivunja na kuingia nyumbani kwa mwanasoka huyo anayeishi na mkewe na watoto wake wawili jijini Barcelona kwenye nyumba ambayo ipo umbali wa mita 200 kutoka katika nyumba ambazo bado zinamilikiwa na mastaa wa zamani wa Barcelona, Lionel Messi na Luis Suarez ambao makazi yao yanalindwa na kampuni maalum za ulinzi.
Aubameyang alikuwa ndio kwanza amerudi nyumbani kwake baada ya Jumapili timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Real Valladolid katika mechi ya La Liga, mechi ambayo mchezaji huyo alikaa benchi.
Kwa mujibu wa habari za ndani, majambazi hao wanadaiwa kumlazimisha mchezaji huyu kufungua kabati ambalo lilikuwa na vito mbalimbali vya thamani ambavyo ni kati ya vitu walivyoondoka navyo na hakuna mtu aliyekamatwa wakati polisi wakiendelea na uchunguzi.
Aubameyang amevamiwa ikiwa ni siku chache zimepita baada ya mchezaji mwenzake wa timu hiyo, Robert Lewandowski kuporwa saa wakati akiingia mazoezini. Saa hiyo iliyoporwa kwenye gari la mchezaji huyo thamani yake inadaiwa kufikia Euro 70,000.

The post Aubameyang avamiwa, afungwa pingu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/29/aubameyang-avamiwa-afungwa-pingu/feed/ 0
Keown ashangaa Arteta kumtema Aubameyang https://www.greensports.co.tz/2022/08/13/keown-ashangaa-arteta-kumtema-aubameyang/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/13/keown-ashangaa-arteta-kumtema-aubameyang/#respond Sat, 13 Aug 2022 12:33:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2365 London, EnglandNyota wa zamani wa Arsenal, Martin Keown amesema anashindwa kumuelewa kocha Mikel Arteta kwa kitendo chake cha kukubali kumuondoka, Pierre-Emerick Aubameyang, mchezaji ambaye Keown anasema angekuwa Harry Kane wa Arsenal.Matatizo ya kinidhamu yalidaiwa kumuandama Aubameyang akiwa Arsenal na kujikuta akiporwa unahodha wa timu hiyo kabla ya kucheza mechi yake ya mwisho katika klabu hiyo, […]

The post Keown ashangaa Arteta kumtema Aubameyang first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Nyota wa zamani wa Arsenal, Martin Keown amesema anashindwa kumuelewa kocha Mikel Arteta kwa kitendo chake cha kukubali kumuondoka, Pierre-Emerick Aubameyang, mchezaji ambaye Keown anasema angekuwa Harry Kane wa Arsenal.
Matatizo ya kinidhamu yalidaiwa kumuandama Aubameyang akiwa Arsenal na kujikuta akiporwa unahodha wa timu hiyo kabla ya kucheza mechi yake ya mwisho katika klabu hiyo, Desemba mwaka jana dhidi ya Everton na hatimaye kutimkia Barcelona.
Mtu wa kwanza kumlaumu Arteta kwa uamuzi huo alikuwa ni beki wa zamani wa timu hiyo, Sokratis Papastathopoulos ambaye alisema kwamba anadhani uamuzi huo haukuwa sahihi na sasa Keown anasema kwamba anadhani Arteta alitakiwa kuendelea kuwa na Aubameyang katika klabu hiyo.
Akifafanua Keown alisema, :Nafikiri alikuwa na sababu za kumuondoa ambazo ni za muda mfupi lakini mwisho wa siku iliathiri timu kwa sababu Arsenal haikuwa ikipata mabao mengi.”
“Ni kweli kwamba unatakiwa kuiheshimu hadhi ya klabu ya soka lakini bado kulikuwa na uhitaji wa kuwamo kwenye Ligi ya Mabingwa mbele ya Spurs. Yule (Aubameyang) ni Harry Kane wetu.
“Nafikiri ni uamuzi mpana wa kocha na bado tuko katika safari ya kuona kama aliloamua litafanya kazi, labda tungembakisha hadi mwisho wa msimu, kwa sasa Jesus (Gabriel) amepata nafasi na Aubameyang anabaki kuwa historia, lakini magoli ni mengi ambayo Arsenal wameyakosa, bado yako katika fikra zangu, nafikiri mchezaji (Aubameyang) angeweza kusamehewa.

The post Keown ashangaa Arteta kumtema Aubameyang first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/13/keown-ashangaa-arteta-kumtema-aubameyang/feed/ 0
Chelsea yamgeukia Aubameyang https://www.greensports.co.tz/2022/08/04/chelsea-yamgeukia-aubameyang/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/04/chelsea-yamgeukia-aubameyang/#respond Thu, 04 Aug 2022 12:01:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2129 London, EnglandKlabu ya soka ya Chelsea inajipanga kumsajili nahodha wa zamani wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang ambaye kwa sasa anaichezea Barcelona.Mpango huo ukifanikiwa itakuwa ni kumrudisha mshambuliaji huyo kwenye Ligi Kuu England baada ya kuondoka Arsenal takriban miezi saba iliyopita na kujiunga na Barcelona akiwa mchezaji huru baada ya kutokea tofauti kati yake na kocha Mikel […]

The post Chelsea yamgeukia Aubameyang first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Klabu ya soka ya Chelsea inajipanga kumsajili nahodha wa zamani wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang ambaye kwa sasa anaichezea Barcelona.
Mpango huo ukifanikiwa itakuwa ni kumrudisha mshambuliaji huyo kwenye Ligi Kuu England baada ya kuondoka Arsenal takriban miezi saba iliyopita na kujiunga na Barcelona akiwa mchezaji huru baada ya kutokea tofauti kati yake na kocha Mikel Arteta wa Arsenal.
Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel ndiye anayedaiwa kutoa ushawishi wa kumsajili mchezaji huyo akitaka kuungana naye kwa mara nyingine baada ya kuwa pamoja Borussia Dortmund na anaamini atasaidia kuimarisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Baada ya kumsajili Raheem Sterling kutoka Man City na kuondoka kwa Romelu Lukaku, Chelsea haijasajili mshambuliaji wa hadhi na hivyo Aubameyang ametajwa kuwa mtu sahihi katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Nguvu ya kumsajili mchezaji huyo pia inachangiwa na tajiri wa klabu hiyo, Todd Boehly ambaye vyombo vya habari vinaripoti kuwa jina la Aubameyang pia limejadiliwa mbele ya tajiri huyo.
Aubameyang mwenye miaka 33 sasa, huenda asiwe na tabu ya kurudi England hasa baada ya Barcelona kumsajili Robert Lewandowski kutoka Bayern Munich na hivyo klabu hiyo huenda isiwe na tatizo la kumuachia mchezaji huyo kama mazungumzo yatakwenda vizuri.
Msimu wa 2021/22 ambao ameukuta nusu akiwa Barcelona, Aubameyang, nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Gabon, amefunga mabao 13 katika mechi 23, rekodi ambayo si mbaya kwa mshambuliaji ambaye amecheza nusu ya msimu.

The post Chelsea yamgeukia Aubameyang first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/04/chelsea-yamgeukia-aubameyang/feed/ 0