Atletico Madrid - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 06 May 2026 19:39:53 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Atletico Madrid - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mataji EPL, ligi ya mabingwa yanukia Arsenal https://www.greensports.co.tz/2026/05/06/mataji-epl-ligi-ya-mabingwa-yanukia-arsenal/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/06/mataji-epl-ligi-ya-mabingwa-yanukia-arsenal/#respond Wed, 06 May 2026 19:39:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14605 London, EnglandArsenal hatimaye imefuzu kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu ifanye hivyo mara ya mwisho mwaka 2006 yaani miaka 20 iliyopita.Ushindi huo unaiweka Arsenal katika nafasi ya kulipigania au hata kulibeba taji hilo pamoja na lile la Ligi Kuu England au EPL ambapo pia timu hiyo inashika usukani.Arsenal imepata […]

The post Mataji EPL, ligi ya mabingwa yanukia Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Arsenal hatimaye imefuzu kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu ifanye hivyo mara ya mwisho mwaka 2006 yaani miaka 20 iliyopita.
Ushindi huo unaiweka Arsenal katika nafasi ya kulipigania au hata kulibeba taji hilo pamoja na lile la Ligi Kuu England au EPL ambapo pia timu hiyo inashika usukani.
Arsenal imepata nafasi hiyo baada ya kupata ushindi wa nyumbani Emirates wa bao 1-0 dhidi ya Atletico Madrid Jumanne, Mei 5, 2026 huku bao hilo pekee likifungwa na Bukayo Saka katika dakika ya 44.
Kwa ushindi huo Arsenal inakuwa imefuzu fainali kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya sare ya bao 1-1 katika mechi ya awali na sasa inasubiri kucheza mechi ya fainali itakayopigwa Mei, 20, 2026 mjini Budapest.
Mpinzani wa Arsenal katika fainali hiyo atakuwa ni mshindi wa mechi ya Bayern Munich na PSG, mechi inayochezwa Jumatano Mei 6, 2026.
Nje ya subira na shauku ya kucheza fainali, kinachosubiriwa zaidi na mashabiki wa Arsenal si sherehe za kufikia hatua ya fainali bali ni kuiona timu yao ikibeba taji la michuano hiyo.
Mwaka 2006 timu hiyo ilipofikia hatua ya fainali ilizimwa na Barcelona ya kina Ronaldinho, Samuel Eto’o, Iniesta, Xavi na wengineo ambao waliibwaga Arsenal na kubeba taji hilo.
Safari hii mashabiki Arsenal hawaamini kama kilichotokea 2006 kitajirudia, wanaamini katika kushinda si kushindwa, imani hiyo hiyo pia inawaongoza katika mbio za taji la EPL ambalo mara ya mwisho walilibeba mwaka 2004.

The post Mataji EPL, ligi ya mabingwa yanukia Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/06/mataji-epl-ligi-ya-mabingwa-yanukia-arsenal/feed/ 0