Asec - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 24 Feb 2024 11:24:32 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Asec - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Simba, Asec hakuna mbabe https://www.greensports.co.tz/2024/02/24/simba-asec-hakuna-mbabe/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/24/simba-asec-hakuna-mbabe/#respond Sat, 24 Feb 2024 11:24:31 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9873 Na mwandishi wetuSimba imetoka sare ya 0-0 na Asec Mimosas katika mechi ya Kundi B ya Ligi ya Mabingwa Afrika, matokeo yanayoifanya Simba ilazimike kushinda mechi ijayo na Jwaneng Galaxy ili kufuzu hatua ya mtoano.Matokeo ya mechi hiyo iliyopigwa Ijumaa hii kwenye Uwanja wa Houphouet-Boigny mjini Abidjan, yanazifanya timu tatu zilizobaki katika kundi hilo za […]

The post Simba, Asec hakuna mbabe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imetoka sare ya 0-0 na Asec Mimosas katika mechi ya Kundi B ya Ligi ya Mabingwa Afrika, matokeo yanayoifanya Simba ilazimike kushinda mechi ijayo na Jwaneng Galaxy ili kufuzu hatua ya mtoano.
Matokeo ya mechi hiyo iliyopigwa Ijumaa hii kwenye Uwanja wa Houphouet-Boigny mjini Abidjan, yanazifanya timu tatu zilizobaki katika kundi hilo za Simba, Jwaneng na Waydad kila moja kuwa na nafasi ya kusonga mbele kuungana na Asec ambayo tayari imefuzu.
Asec ndiyo inayoshika usukani katika kundi hilo ikiwa na pointi 11 ikifuatiwa na Simba inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi sita wakati Jwaneng ni ya tatu ikiwa na pointi nne na Wydad inaburuza mkia na pointi tatu.
Jwaneng na Wydad zitaumana Jumamosi hii, mechi ambayo Jwaneng itakuwa nyumbani na kama ikishinda itafikisha pointi saba.
Kwa mantiki hiyo mechi ya Simba na Jwaneng itakayopigwa Machi 2 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ndiyo itakayoamua nafasi ya Simba kusonga mbele au kuziaga fainali hizo, Simba itatakiwa kushinda.
Jwaneng licha ya kuwa nyuma ya Simba kwa pointi lakini si timu ya kubeza hata kidogo, ushindi wa mechi yake na Wydad au sare vyote vitaiweka Simba pagumu na kuwa na ulazima wa kushinda mechi ya Machi 2.
Hata kama Jwaneng itafungwa na Wydad, bado Simba itahitaji kuwa na ulazima wa kupambana ili kupata ushindi katika mechi na Jwaneng kwani kucheza mechi kwa lengo la kutafuta sare pia ni jambo gumu.
Jwaneng akifungwa na Wydad halafu akaifunga Simba, Jwaneng atasonga mbele kwa kuizidi Simba kwa pointi moja.

The post Simba, Asec hakuna mbabe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/24/simba-asec-hakuna-mbabe/feed/ 0
Simba, Asec zatoka sare https://www.greensports.co.tz/2023/11/25/simba-asec-zatoka-sare/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/25/simba-asec-zatoka-sare/#respond Sat, 25 Nov 2023 19:42:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8630 Na mwandishi wetuSimba imeanza na sare ya bao 1-1 mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.Wenyeji Simba ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 44 mfungaji akiwa ni Saido Ntibazonkiza ambaye alifunga […]

The post Simba, Asec zatoka sare first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imeanza na sare ya bao 1-1 mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Wenyeji Simba ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 44 mfungaji akiwa ni Saido Ntibazonkiza ambaye alifunga bao hilo kwa mkwaju ya panelti baada ya beki mmoja wa Asec kuunawa katika eneo la hatari mpira uliopigwa na Kibu Denis.
Serge Pokou aliisawazishia Asec bao hilo katika dakika ya 77 akineemeka na ushirikiano kutoka kwa William Sankara.
Simba katika mechi hiyo ilifanya mabadiliko matano ikiwaingiza, Clatous Chama, John Bocco, Luis Miquissone na Moses Phiri kuchukua nafasi za Ntibazonkiza, Che Malone, Kibu na Jean Baleke, mabadiliko ambayo hata hivyo hayakuweza kuipa bao timu hiyo..
Wakati Simba iliyokuwa nyumbani ikiishia kugawana pointi na timu hiyo ya Ivory Coast, katika michuano hiyo hiyo, jana Ijumaa mambo hayakuwa mazuri kwa mahasimu wao Yanga waliokuwa ugenini Algeria dhidi ya CR Belouizdad baada ya kuchapwa mabao 3-0.

The post Simba, Asec zatoka sare first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/25/simba-asec-zatoka-sare/feed/ 0