Arteta - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 20 Apr 2025 08:42:54 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Arteta - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Arteta amkumbuka Pep kabla ya kuitoa Real Madrid https://www.greensports.co.tz/2025/04/17/arteta-amkumbuka-pep-kabla-ya-kuitoa-real-madrid/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/17/arteta-amkumbuka-pep-kabla-ya-kuitoa-real-madrid/#respond Thu, 17 Apr 2025 09:53:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13269 Madrid, HispaniaBaada ya kuitoa Real Madrid katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutua nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amemkumbuka mwalimu wake Pep Guardiola.Arsenal jana Jumatano ilifuzu hatua ya nusu fainali kwa kuichapa Real Madrid mabao 2-1 katika mechi ya pili ya robo fainali […]

The post Arteta amkumbuka Pep kabla ya kuitoa Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Madrid, Hispania
Baada ya kuitoa Real Madrid katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutua nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amemkumbuka mwalimu wake Pep Guardiola.
Arsenal jana Jumatano ilifuzu hatua ya nusu fainali kwa kuichapa Real Madrid mabao 2-1 katika mechi ya pili ya robo fainali baada ya kushinda kwa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza.
Real Madrid ikiwa nyumbani Santiago Bernabeu ikilala kwa mabao ya Bukayo Saka ambaye pia alikosa penalti na Gabriel Martinelli aliyefunga la pili wakati bao pekee la Real Madrid likifungwa na Vinicius Junior.
Akimzungumzia Guardiola, Arteta alisema alimpigia simu mapema kocha huyo ambaye alidai anaendelea kufurahia ukaribu wao kikazi baada ya kufanya naye kazi Man City kwa miaka mitatu.

“Nilimpigia simu mapema (jana Jumatano) kwa sababu niko hapa na yeye namshukuru, nikiwa mchezaji na baadaye kocha amekuwa akinipa hamasa, nimekuwa na miaka minne mizuri pamoja naye na nitaendelea kumshukuru wakati wote,” alisema Arteta.


Kwa ushindi huo, Arsenal sasa inasubiri kuumana na PSG ya Ufaransa katika mechi ya kwanza ya nusu fainali itakayopigwa Aprili 29.
Akizungumzia mambo yajayo ya timu yake katika hatua waliyofikia, Arteta alisema kwa sasa wataendeleza wimbi la ushindi kwa sababu ari yao ipo vile vile.
“Kwa sasa tunatakiwa kuendelea kufanya tulichokifanya (ushindi) kwa sababu nadhani bado tuna ari ile ile,” alisema Arteta.
Arteta alisema jukumu lao ni kuwafanya watu wao wawe na furaha na anaamini watu hao wanajivunia wachezaji na timu na kilichobaki sasa ni wao kuangalia mambo ya mbele zaidi ya walipofikia sasa.
Naye Saka aliyepiga penalti kwa staili ya panenka na kukosa, alisema jambo hilo hutokea na kwamba alijaribu kufanya kitu tofauti lakini ikashindikana baada ya kipa Thibaut Courtois kuwa makini.
Kwa Arsenal hii inakuwa mara ya kwanza kufikia nusu fainali ya ligi ya mabingwa tangu mwaka 2009 wakati kwa Real Madrid wanakosa hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2020.

The post Arteta amkumbuka Pep kabla ya kuitoa Real Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/17/arteta-amkumbuka-pep-kabla-ya-kuitoa-real-madrid/feed/ 0
Majeruhi Arsenal wamtesa Arteta https://www.greensports.co.tz/2025/04/02/majeruhi-arsenal-wamtesa-arteta/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/02/majeruhi-arsenal-wamtesa-arteta/#respond Wed, 02 Apr 2025 16:22:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13190 London, EnglandArsenal wamefurahia kurejea dimbani kwa mshambuliaji wao Bukayo Saka aliyekuwa majeruhi kwa takriban miezi mitatu lakini hapo hapo wamepata pigo jingine baada ya kuumia kwa beki wao wa kati Gabriel.Saka amerejea na kufunga bao jana Jumanne katika mechi dhidi ya Fulham, mechi ambayo Arsenal ilitoka na ushindi wa mabao 2-1 na kujinyakulia pointi tatu […]

The post Majeruhi Arsenal wamtesa Arteta first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Arsenal wamefurahia kurejea dimbani kwa mshambuliaji wao Bukayo Saka aliyekuwa majeruhi kwa takriban miezi mitatu lakini hapo hapo wamepata pigo jingine baada ya kuumia kwa beki wao wa kati Gabriel.
Saka amerejea na kufunga bao jana Jumanne katika mechi dhidi ya Fulham, mechi ambayo Arsenal ilitoka na ushindi wa mabao 2-1 na kujinyakulia pointi tatu muhimu.
Haikushangaza kwa mashabiki wa Arsenal kumpa heshima Saka kwa kumshangilia kwa kusimama mara baada ya jina lake kutajwa uwanjani japo hali ni tofauti kwa kocha Mikel Arteta.
Kwa Arteta ushindi huo na kurejea kwa Saka ilikuwa furaha ya muda tu, hali bado tete, wachezaji majeruhi wanaendelea kumpa mtihani wa kupanga kikosi chake.
Kuhusu Gabriel, beki wa kati Mbrazil alipata matatizo ya misuli kipindi cha kwanza katika mechi ya jana na hivyo ni wazi ataikosa mechi ya pili ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid Jumanne ijayo.
Hali ni hiyo hiyo kwa mshambuliaji Kai Havert ambaye msimu huu umekuwa wa hovyo kwake baada ya kupatwa na matatizo ya misuli.
Kama hiyo haitoshi, beki Jurrien Timber naye alilazimika kukaa pembeni katika mechi ya jana dhidi ya Fulham akikabiliwa na tatizo la goti kama ilivyo kwa Ricardo Calafiori na Ben White ambao kila mmoja ana tatizo la goti.
Arteta ana kazi kubwa ya kufanya licha ya kuwa na wachezaji wake muhimu ni majeruhi, kazi mbili zilizo mbele yake zote ni ngumu.
Kwanza katika Ligi Kuu England (EPL) timu yake inashika nafasi ya pili, anatakiwa kuishusha kileleni Liverpool inayoshika usukani wakati kwenye Ligi ya Mabingwa mtihani wa robo fainali dhidi ya Real Madrid si mdogo.

The post Majeruhi Arsenal wamtesa Arteta first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/02/majeruhi-arsenal-wamtesa-arteta/feed/ 0
Kiwango Arsenal chamkera Arteta https://www.greensports.co.tz/2025/02/23/kiwango-arsenal-chamkera-arteta/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/23/kiwango-arsenal-chamkera-arteta/#respond Sun, 23 Feb 2025 12:48:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13038 London, EnglandKocha wa Arsenal, Mikel Arteta amewalaumu wachezaji wake kwa kutocheza katika kiwango cha kuwapa ushindi katika mechi ya jana Jumamosi dhidi ya West Ham ambayo walilala kwa bao 1-0.Bao pekee la Jarrod Bowen dakika ya 44 lilitosha kuifanya West Ham iliyokuwa ugenini kutoka na ushindi huku Arteta akilalamikia kiwango cha timu yake iliyoambulia mashuti […]

The post Kiwango Arsenal chamkera Arteta first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amewalaumu wachezaji wake kwa kutocheza katika kiwango cha kuwapa ushindi katika mechi ya jana Jumamosi dhidi ya West Ham ambayo walilala kwa bao 1-0.
Bao pekee la Jarrod Bowen dakika ya 44 lilitosha kuifanya West Ham iliyokuwa ugenini kutoka na ushindi huku Arteta akilalamikia kiwango cha timu yake iliyoambulia mashuti mawili tu ya maana langoni mwa wapinzani wao.
Matokeo hayo yanairudisha nyuma Arsenal katika mbio za kuishusha Liverpool kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England (EPL) ikiwa nafasi ya pili na sasa imezidiwa na Liverpool kwa tofauti ya pointi nane.
Liverpool inaweza kuongeza tofauti hiyo ya pointi na kuwa kubwa zaidi iwapo itashinda mechi yao ya leo Jumapili dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Man City.
Kutokana na janga la wachezaji majeruhi, Arsenal jana ilicheza bila ya Kai Havertz, Gabrieli Martinelli, Gabrieli Jesus na Bukayo Saka hivyo timu kutokuwa na mshambuliaji tegemeo badala yake kiungo Mikel Merino akabeba jukumu hilo.
Alipoulizwa kama kukosekana mshambuliaji mwenye sifa na tegemeo kama ndiko kulikoikwaza Arsenal, Arteta alipingama vikali na mtazamo huo.

“Hapana, hapana nalikataa hilo moja kwa moja kwa sababu hapa nazungumzia kiwango cha wachezaji na timu ambayo tumecheza nayo nikiwamo mimi,” alisema Arteta.


Arteta pia alisema kwamba ingawa timu yake ilijitahidi kumiliki mpira na kupiga mashuti lakini hakuona kama ilikuwa katika kiwango kilichohitajika hasa kwa kuwa walipoteza mipira mingi na kuwapa nafasi wapinzani wao kuwakimbiza.

The post Kiwango Arsenal chamkera Arteta first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/23/kiwango-arsenal-chamkera-arteta/feed/ 0
Arteta adai kukatishwa tamaa https://www.greensports.co.tz/2025/02/04/arteta-adai-kukatishwa-tamaa/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/04/arteta-adai-kukatishwa-tamaa/#respond Tue, 04 Feb 2025 19:36:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12974 London, EnglandKocha wa Arsenal, Mikel Arteta amedai kukatishwa tamaa baada ya timu hiyo kutofanya usajili wowote katika dirisha dogo ingawa amepongeza nidhamu ya timu.Awali zilikuwapo habari kwamba Arsenal ingesajili mshambuliaji baada ya Gabriel Jesus kupata matatizo ya misuli mwishoni mwa mwezi uliopita wakati Bukayo Saka naye akiwa na tatizo linalofanana na hilo na wote wakishindwa […]

The post Arteta adai kukatishwa tamaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amedai kukatishwa tamaa baada ya timu hiyo kutofanya usajili wowote katika dirisha dogo ingawa amepongeza nidhamu ya timu.
Awali zilikuwapo habari kwamba Arsenal ingesajili mshambuliaji baada ya Gabriel Jesus kupata matatizo ya misuli mwishoni mwa mwezi uliopita wakati Bukayo Saka naye akiwa na tatizo linalofanana na hilo na wote wakishindwa kuiwakilisha timu hiyo.
Arteta alisema dhamira yao ilikuwa wazi kwamba baada ya dirisha la usajili kufunguliwa walitakiwa kuangalia fursa za kusajili ili kuimarisha kikosi kwa kusajili wachezaji ambao wangekuwa msaada kwa timu.
Arteta ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja kabla ya Arsenal kujitupa dimbani kuikabili Newcastle katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la EFL itakayopigwa kesho Jumatano.

“Kutokana na wachezaji kuwa majeruhi tulijipa matumaini, hatujayafikia, imetukatisha tamaa lakini hapo hapo tunafahamu kwamba tulitakiwa kusajili aina fulani ya wachezaji na tunatakiwa pia kuwa na nidhamu katika hilo, nafikiri la la nidhamu tuko sawa,” alisema Arteta.


Arteta alisema kuna mchezaji ambaye waliamini angewafanya wawe bora zaidi ingawa alifafanua kuwa katika masuala ya kifedha pia kuna mambo mengi ambayo ni lazima wayasimamie na ndiyo yaliyowafikisha walipofika na kuanzia hapo wanajaribu kuwa bora zaidi.
Arsenal ambayo mwishoni mwa wiki iliyopita iliibugiza Man City mabao 5-1, kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu England (EPL) ikiwa imezidiwa na vinara wa ligi hiyo, Liverpool kwa tofauti ya pointi sita.

The post Arteta adai kukatishwa tamaa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/04/arteta-adai-kukatishwa-tamaa/feed/ 0
Webb aitetea penalti iliyomkera Arteta https://www.greensports.co.tz/2025/01/08/webb-aitetea-penalti-iliyomkera-arteta/ https://www.greensports.co.tz/2025/01/08/webb-aitetea-penalti-iliyomkera-arteta/#respond Wed, 08 Jan 2025 18:20:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12601 London, EnglandBosi wa waamuzi England, Howard Webb amesema mwamuzi Anthony Taylor alikuwa sahihi kutoa penalti katika mechi ya Arsenal na Brighton iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.Tukio lililozaa penalti hiyo lilitokana na beki wa Arsenal, William Saliba kucheza nduvyo sivyo wakati wakiwania mpira na Joao Pedro katika mechi hiyo iliyopigwa Jumamosi iliyopita.Baada ya mechi hiyo […]

The post Webb aitetea penalti iliyomkera Arteta first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Bosi wa waamuzi England, Howard Webb amesema mwamuzi Anthony Taylor alikuwa sahihi kutoa penalti katika mechi ya Arsenal na Brighton iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.
Tukio lililozaa penalti hiyo lilitokana na beki wa Arsenal, William Saliba kucheza nduvyo sivyo wakati wakiwania mpira na Joao Pedro katika mechi hiyo iliyopigwa Jumamosi iliyopita.
Baada ya mechi hiyo kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alieleza kusikitishwa na uamuzi huo akidai hakuwahi kuona tukio la aina hiyo katika maisha yake wakati kocha wa Brighton, Fabian Hurzeler alisema kwamba kwake anadhani ilikuwa penalti ya wazi.
Kwa upande wake Webb, mwamuzi maarufu wa zamani aliyejijengea heshima England na duniani, alisema anaunga mkono uamuzi wa Taylor kutoa penalti.
Webb alifafanua kwamba tukio lililotokea si tu lilikuwa kosa bali halikuwa la kawaida kwa wachezaji wote wawili kuwania mpira wa juu na beki wa Arsenal kuchelewa kuupiga kichwa na kusababisha adhabu iliyotolewa.

“Unachokiona katika mazingira yaliyojitokeza ni wachezaji wawili kwenda juu kuuwahi mpira, Pedro anaupiga mpira kichwa na Saliba haupigi mpira kichwa anakwenda kwenye kichwa cha Pedro akiwa amechelewa,” alisema Webb.


Webb alisema kwamba inapotokea mchezaji akaonekana wazi anaucheza mpira au anaupiga mbali kwa kichwa hapo utakuwa unazungumzia jambo jingine lakini hicho si kilichotokea.

The post Webb aitetea penalti iliyomkera Arteta first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/01/08/webb-aitetea-penalti-iliyomkera-arteta/feed/ 0
Arteta aitaka Barca ya Iniesta, Xavi Arsenal https://www.greensports.co.tz/2024/12/06/arteta-aitaka-barca-ya-iniesta-xavi-arsenal/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/06/arteta-aitaka-barca-ya-iniesta-xavi-arsenal/#respond Fri, 06 Dec 2024 06:32:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12352 London, EnglandKocha wa Arsenal, Mikel Arteta ameikumbuka Barca iliyokuwa bora eneo la kiungo chini ya Iniesta, Xavi na Sergio Bosquets na kujiaminisha kuwa Bukayo Saka na Martin Odegaard wanaweza kutengeneza safu bora ya kiungo kama hiyo.Ødegaard aliyekuwa majeruhi akisumbuliwa na enka amerudi akiwa bora na kuifanya Arsenal iwe moto, ikishinda mechi tatu katika wiki huku […]

The post Arteta aitaka Barca ya Iniesta, Xavi Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
London, England
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta ameikumbuka Barca iliyokuwa bora eneo la kiungo chini ya Iniesta, Xavi na Sergio Bosquets na kujiaminisha kuwa Bukayo Saka na Martin Odegaard wanaweza kutengeneza safu bora ya kiungo kama hiyo.
Ødegaard aliyekuwa majeruhi akisumbuliwa na enka amerudi akiwa bora na kuifanya Arsenal iwe moto, ikishinda mechi tatu katika wiki huku Saka naye akitoa mchango mkubwa katika mafanikio hayo.
Msimu uliopita, Ødegaard aligawa pasi nyingi zaidi kwa Saka (320) hali ambayo imeonesha namna wachezaji hao wanavyojuana na wanavyokwenda vizuri katika mbio za kuipatia mafanikio Arsenal.
Alipoulizwa kuhusu wachezaji wawili wanavyocheza kwa kuelewana, Arteta aliwalinganisha na magwiji wa Barca, ambao mbali na mafanikio yaliyoonekana kwenye klabu pia waliisaidia timu yao ya taifa ya Hispania hadi kubeba Kombe la Dunia na Kombe la Ulaya au Euro.
“Wanaweza kuwa bora katika namna hiyo kwa sababu wao ni viungo washambuliaji na mawinga,” alisema Arteta kuhusu Saka na Ødegaard.
Arteta hata hivyo alisema kwamba pia aliwahi kuwaona mabeki wa kati wenye kucheza kwa maelewano, viungo wa kati lakini wakati wote amekuwa mwenye kuwafikiria Xavi, Iniesta na Busquets kwa kuwa walikuwa wa kipekee.
Katika siku za karibuni, kiungo mwingine wa Arsenal, Jorginho alisema kwamba Saka ana uwezo wa kuingia katika mbio za kuwania tuzo ya Ballon d’Or kama tu atakuwa mwenye kujiamini katika hilo.

The post Arteta aitaka Barca ya Iniesta, Xavi Arsenal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/06/arteta-aitaka-barca-ya-iniesta-xavi-arsenal/feed/ 0
Arteta ajipa matumaini ya taji EPL https://www.greensports.co.tz/2024/05/20/arteta-ajipa-matumaini-ya-taji-epl/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/20/arteta-ajipa-matumaini-ya-taji-epl/#respond Mon, 20 May 2024 18:05:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11050 London, EnglandBaada ya Man City kubeba taji la Ligi Kuu England (EPL), kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amewakikishia mashabiki wa timu hiyo kwamba mwishowe timu yao italibeba taji hilo.Arteta pia ametaka timu hiyo kutoridhika kwa kushika nafasi ya pili na kuhakikisha wanalibeba baada ya kulikosa katika hatua ya mwisho kwa misimu miwili mfululizo.Arsenal jana Jumapili […]

The post Arteta ajipa matumaini ya taji EPL first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Baada ya Man City kubeba taji la Ligi Kuu England (EPL), kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amewakikishia mashabiki wa timu hiyo kwamba mwishowe timu yao italibeba taji hilo.
Arteta pia ametaka timu hiyo kutoridhika kwa kushika nafasi ya pili na kuhakikisha wanalibeba baada ya kulikosa katika hatua ya mwisho kwa misimu miwili mfululizo.
Arsenal jana Jumapili iliifunga Everton mabao 2-1 ushindi ambao haukuiwezesha timu hiyo kubeba taji la EPL baada ya Man City iliyokuwa ikiongoza ligi hiyo kwa pointi mbili nayo kutoka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya West Ham.
Baada ya mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Emirates, Arteta alizungumza na mashabiki na kuwataka kutokata tamaa na kuendelea kuiunga mkono timu na kubwa ni kutoridhika baada ya timu hiyo kushika nafasi ya pili.

“Huu sasa ni wakati wa kupumzika, na kutafakari na tafadhali endeleeni kuiunga mkono timu, kuipa hamasa, msiridhike kwa sababu tunataka mafanikio zaidi ya haya na tunakwenda kuyapata,” alisema Arteta.


Alipoulizwa ni kwa nini anajiamini namna hiyo, Arteta alisema kwamba kama watafanya wanachotakiwa kukifanya na kuyakaribia mafnikio mwishowe watabeba taji.
“Ni lini? Sijui lakini kama tutaendelea kupambana na kuwa karibu na taji mwisho wa siku tutafanikiwa kulibeba,” alisema Arteta.
Arsenal imemaliza ligi ikiwa na pointi 89 ambazo ni nyingi kwa rekodi za ligi hiyo lakini imezidiwa pointi mbili na Man City ambao pia wameweka rekod ya kubeba taji hilo kwa mara ya nne mfululizo.

The post Arteta ajipa matumaini ya taji EPL first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/20/arteta-ajipa-matumaini-ya-taji-epl/feed/ 0
Ndoto za Arteta kubeba taji EPL zipo hai https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/ndoto-za-arteta-kubeba-taji-epl-zipo-hai/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/ndoto-za-arteta-kubeba-taji-epl-zipo-hai/#respond Sat, 18 May 2024 17:17:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11015 London, EnglandKocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema ndoto zake za kubeba taji la Ligi Kuu England (EPL) kesho Jumapili zipo hai wakati huu akijiandaa kwa mechi ya mwisho iliyobeba hatma ya timu yake katika taji hilo.Mabingwa watetezi, Man City wanashika usukani wa ligi hiyo wakiwazidi Arsenal walio nafasi ya pili kwa pointi mbili wakati Jumapili […]

The post Ndoto za Arteta kubeba taji EPL zipo hai first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema ndoto zake za kubeba taji la Ligi Kuu England (EPL) kesho Jumapili zipo hai wakati huu akijiandaa kwa mechi ya mwisho iliyobeba hatma ya timu yake katika taji hilo.
Mabingwa watetezi, Man City wanashika usukani wa ligi hiyo wakiwazidi Arsenal walio nafasi ya pili kwa pointi mbili wakati Jumapili timu hizo kila moja itacheza mechi yake ya mwisho ya kufunga msimu.
Arsenal ili itwae taji hilo italazimika kushinda mechi hiyo dhidi ya Everton wakati huo huo ikiombea mabingwa watetezi Man City wapoteze au walau watoke sare mechi yao dhidi ya West Ham.
“Tulitaka kuwa katika nafasi hii, tumeshinda yote hadi kufikia hapa katika siku nzuri mbele ya watu wetu hapo Jumapili tukiwa na matumaini katika fursa hii kubwa kwamba tutabeba taji mwisho wa mechi hii,” alisema Arteta.

“Tuna uwezekano wa kuifurahia siku hii nzuri ya Jumapili, siku ambayo ndoto zetu bado zipo hai na bado tunaamini inawezekana, haya ndiyo mambo ya soka,” alisema Arteta.


Arteta anaelewa Man City ndiyo iliyo juu katika mbio za kulisaka taji hilo lakini ameamua kuweka nguvu na umakini katika mechi na Everton akiamini lolote linaweza kutokea katika mechi ya Man City na West Ham.
Artete ambaye amewahi kuwa mchezaji Arsenal hakuwahi kulibeba taji la EPL wakati huo na sasa anaamini litakuwa jambo kubwa kufanya hivyo na hiyo ni moja ya ndoto zake.
Mara ya mwisho Arsenal kubeba taji la EPL ilikuwa msimu wa 2003-04 wakati Man City inawania kuweka rekodi ya kulibeba taji hilo kwa mara ya nne mfululizo.

The post Ndoto za Arteta kubeba taji EPL zipo hai first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/ndoto-za-arteta-kubeba-taji-epl-zipo-hai/feed/ 0
Akili ya Arteta yawaza taji EPL tu https://www.greensports.co.tz/2024/05/11/akili-ya-arteta-yawaza-taji-epl-tu/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/11/akili-ya-arteta-yawaza-taji-epl-tu/#respond Fri, 10 May 2024 22:25:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10927 London, EnglandKocha wa Arsenal Mikel Arteta kwa sasa anajiandaa kuivaa Man United katika mechi muhimu ingawa akili ya kocha huyo kwa sasa inawaza kulibeba taji la Ligi Kuu England (EPL) msimu huu.“Ubongo wangu wakati wote unanipeleka mahali ambapo tunabeba taji la ligi kuu, hapo ndipo ulipo ubongo wangu kwa wakati huu,” alisema Arteta.Arsenal kwa sasa […]

The post Akili ya Arteta yawaza taji EPL tu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta kwa sasa anajiandaa kuivaa Man United katika mechi muhimu ingawa akili ya kocha huyo kwa sasa inawaza kulibeba taji la Ligi Kuu England (EPL) msimu huu.
“Ubongo wangu wakati wote unanipeleka mahali ambapo tunabeba taji la ligi kuu, hapo ndipo ulipo ubongo wangu kwa wakati huu,” alisema Arteta.
Arsenal kwa sasa inashika usukani wa EPL ikiwa imeizidi Man City inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi moja na wanaweza kutupwa nafasi ya pili kama Man City watashinda mechi yao ya kesho Jummosi dhidi ya Fulham.
Arsenal nayo inaweza kurejea kileleni iwapo itatoka na ushindi katika mechi yake ya Jumapili dhidi ya Man United, timu ambayo kwa sasa mambo yake si mazuri kwenye ligi hiyo.
Arteta hata hivyo alionekana mwenye kuyajua mazingira hayo aliposema kwamba hali ipo wazi na wanalazimika kuwa makini na wanachokifanya ili kuwa katika nafasi nzuri na hicho ndicho kitu wanachokifanya kwa sasa.
Baada ya mechi dhidi ya Man United itakayopigwa kwenye dimba la Old Trafford, Arsenal itakuwa mwenyeji wa Everton katika mechi yao ya mwisho itakayopigwa Mei 19 wakati Man City itakuwa na mechi Jumanne dhidi ya Tottenham kabla ya kumaliza ligi kwa mechi dhidi ya West Ham.

“Tuko katika safari ya kujaribu kuwakamata, ni jambo zuri kwa wakati wote inapotokea kuna mtu anayekupa changamoto ya kwenda mbali zaidi na zaidi,” alisema Arteta.


Arteta alisema kwamba historia ya Man City imekuwa ni ya kubeba mataji na wamekuwa wapinzani wa kipekee kwa miaka takriban 15 iliyopita na Arsenal wanachotaka ni kubadili hali hiyo.

The post Akili ya Arteta yawaza taji EPL tu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/11/akili-ya-arteta-yawaza-taji-epl-tu/feed/ 0
Arteta aitangazia vita City hadi mwisho https://www.greensports.co.tz/2024/04/29/arteta-aitangazia-vita-city-hadi-mwisho/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/29/arteta-aitangazia-vita-city-hadi-mwisho/#respond Mon, 29 Apr 2024 07:30:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10780 London, EnglandKocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema timu yake ipo tayari kukabiliana na Man City hadi mwisho katika kulisaka taji la Ligi Kuu England (EPL) lakini akaowaonya wachezaji wake kutobweteka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Tottenham Hotspurs.Arsenal jana Jumapili iliwachapa mahasimu wao wa London, Spurs mabao 3-2 na kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa […]

The post Arteta aitangazia vita City hadi mwisho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema timu yake ipo tayari kukabiliana na Man City hadi mwisho katika kulisaka taji la Ligi Kuu England (EPL) lakini akaowaonya wachezaji wake kutobweteka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Tottenham Hotspurs.
Arsenal jana Jumapili iliwachapa mahasimu wao wa London, Spurs mabao 3-2 na kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa EPL ikiwa imefikisha pointi 80 dhidi ya 79 za Man City.
Ushindi dhidi ya Spurs hata hivyo nusura upotee kwani timu hiyo ilianza kwa kuongoza kwa mabao 3-0 kabla ya Spurs kujibu mapigo kipindi cha pili na kupata mabao mawili.
Arsenal ilineemeka kwa bao la kujifunga la Pierre-Emile Højbjerg na mabao yao mengine mawili yalifungwa na Bukayo Saka na Kai Havert wakati yale ya Spurs yalifungwa na Romero na Son Heung-min aliyefunga kwa penalti.
Arteta aliulizwa baada ya mechi hiyo kama ushindi huo ni ushahidi kuwa wachezaji wake wapo tayari kupambania taji la EPL naye akajibu kwamba hilo ni ukweli asilimia 100 na ameliona hilo tangu mwanzo wa msimu.

“Wananipa sababu ya kuamini hilo kila baada ya siku, tuko katika mwelekeo sahihi, shauku ya kilicho mbele yetu ni nzuri, sote tunatarajia kwamba watapigania hadi mwisho,” alisema Arteta.


Alifafanua kuwa hitimisho huwa linapatikana matokeo yanavyokuwa na iwapo Spurs wangeweza kusawazisha na kuwa 3-3 katika dakika za lala salama hapo kusingekuwa na utayari wa kubeba taji la ligi.
Wakati, Arteta akijipa matumaini, Man City nayo imeendeleza mapambano baada ya kuichapa Nottingham Forest mabao 2-0 na hivyo kuzidi kuisogelea Arsenal kileleni na zaidi ya hilo, timu hiyo imezidiwa mchezo mmoja na Arsenal.
Mabao ya Man City yalifungwa na Josko Gvardiol na mshambuliaji Erling Haaland ambaye amekuwa akiandamwa na majeraha katika siku za hivi karibuni.
Kwa upande wake kocha wa Man City, Pep Guardiola alisema wachezaji wake hawakuwa na presha yoyote katika mechi hiyo licha ya Arsenal kupata ushindi wa 3-2 dhidi ya Spurs.
“Presha inakuwa kwa namna unavyocheza, kama ukicheza vizuri na kutawala mchezo hapo watu watasema hauna presha, na kama ukicheza vibaya watu watasema ni shauri ya presha,” alisema Pep.

The post Arteta aitangazia vita City hadi mwisho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/29/arteta-aitangazia-vita-city-hadi-mwisho/feed/ 0