Anthony Joshua - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 09 Mar 2024 08:39:44 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Anthony Joshua - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Joshua amchakaza Ngannou mapema https://www.greensports.co.tz/2024/03/09/joshua-amchakaza-ngannou-mapema/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/09/joshua-amchakaza-ngannou-mapema/#respond Sat, 09 Mar 2024 08:39:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10098 Riyadh, Saudi ArabiaBondia Anthony Joshua amemchakaza kwa KO ya raundi ya pili mpinzani wake, Francis Ngannou katika pambano la ngumi za uzito wa juu lililofanyika usiku wa jana Ijumaa mjini Riyadh.Ngannou alikumbana na kipigo hicho kwa ngumi ya mkono wa kushoto iliyomkuta chini ya kidevu kabla ya kuanguka chini na kujikuta akipoteza fahamu.Baada ya kuanza […]

The post Joshua amchakaza Ngannou mapema first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Bondia Anthony Joshua amemchakaza kwa KO ya raundi ya pili mpinzani wake, Francis Ngannou katika pambano la ngumi za uzito wa juu lililofanyika usiku wa jana Ijumaa mjini Riyadh.
Ngannou alikumbana na kipigo hicho kwa ngumi ya mkono wa kushoto iliyomkuta chini ya kidevu kabla ya kuanguka chini na kujikuta akipoteza fahamu.
Baada ya kuanza kuhesabiwa na kukaa sawa, Ngannou, mwenye umri wa miaka 37 ilidhihirika wazi kwamba asingeweza kuendelea na pambano hilo hasa baada ya watu wa huduma ya kwanza kuanza kumpa msaada.
Katika pambano hilo, Joshua alianza kuonesha makali yake raundi ya kwanza baada ya kumchapa Ngannou ngumi kali ya mkono wa kulia ambayo ilimyumbisha lakini aliweza kusimama imara na kuendelea na pambano.
Johua, 34 katika raundi ya pili aliendeleza makali yake kwa kumchapa Ngannou ngumi nyingine ambayo ilimpiga kisawasawa kwenye sehemu ya sikio la upande wa kushoto.


Ngumi hiyo kali hata hivyo haikumtetemesha sana Ngannou ambaye alionekana kuwa imara na kuendelea na pambano lakini alikutana na ngumi nyingine kali ya mkono wa kulia iliyotosha kumfanya alambe sakafu na kushinda kuendelea na pambano.
Unapoelekea kwenye kuutafuta ubingwa wakati wote unatakiwa kuwa makini, huyu ni mimi ambaye nilijitoa kwa ajili ya mpango huo,” alisema Joshua baada ya ushindi huo.
“Nilipomuona Ngannou kwenye pambano na Tyson Fury nilijisemea, kumbe huyu jamaa anaweza kupigana, nahitaji ‘kitu cha aina hii’,” alisema Joshua.
Baada ya kipigo hicho, Ngannou aliibukia kwenye mitandao ya kijamii akitumia akaunti yake ya Twitter au X kuwaomba radhi mashabiki wake kwa madai kwamba amewaangusha lakini akawataka wasikate tamaa.

“Samahani jamani, nimewaangusha, leo ilikuwa siku mbaya kwenye ofisi yangu lakini kesho itakuwa siku nyingine, asanteni kwa mapenzi yenu,” alisema Ngannou.


The post Joshua amchakaza Ngannou mapema first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/09/joshua-amchakaza-ngannou-mapema/feed/ 0
Joshua ampiga KO Helenius https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/joshua-ampiga-ko-helenius/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/joshua-ampiga-ko-helenius/#respond Sun, 13 Aug 2023 19:48:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7370 London, EnglandBondia Anthony Joshua amefanikiwa kumchapa Robert Helenius kwa KO ya raundi ya saba, katika pambano la uzito wa juu lililofayika kwenye Ukumbi wa O2 London, usiku wa kuamkia leo Jumapili.Katika pambano hilo awali ilikuwa vigumu kutabiri nani angeibuka mshindi kwa namna mabondia hao walivyolianza pambano kabla ya Joshua kumsukumizia Helenius ngumi moja kali iliyomuangusha […]

The post Joshua ampiga KO Helenius first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Bondia Anthony Joshua amefanikiwa kumchapa Robert Helenius kwa KO ya raundi ya saba, katika pambano la uzito wa juu lililofayika kwenye Ukumbi wa O2 London, usiku wa kuamkia leo Jumapili.
Katika pambano hilo awali ilikuwa vigumu kutabiri nani angeibuka mshindi kwa namna mabondia hao walivyolianza pambano kabla ya Joshua kumsukumizia Helenius ngumi moja kali iliyomuangusha chini.
Kwa ushindi huo Joshua sasa anajiandaa kwa pambano linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa ngumi duniani dhdi ya bondia Deontay Wilder, pambano ambalo limepangwa kufanyika Januari mwakani.
Akiuzungumzia ushindi wake kwa Helenius, Joshua alisema ngumi ni mchezo unaokutaka mwenye kubadilika. “Unalazimika kubadili mazingira, ni lazima uwe katika uhalisia huo ili usiwahiwe, nimemaliza kazi yangu usiku huu.”
Katika hali ambayo iliibua hofu kidogo, mara baada ya kipigo hicho Helenius alihitaji kuwekewa oxygen kidogo wakati akiwa chini lakini muda mfupi baadaye akawa sawa na kusimama mwenyewe bila ya msaada wa mtu yeyote na kisha akampongeza Joshua kwa ushindi.

Helenius ambaye ni bondia kutoka Finland, alilazimika kupigana na Joshua baada ya mpinzani wa awali, Dillian Whyte wa Uingereza kuamua mwenywe kujitoa mara baada ya kufanyiwa vipimo.
Baada tu ya kuanza kwa pambano hilo katika sekunde chache za mwanzo alikuwa ni Helenius aliyewahi katikati ya ulingo na kumsukumizia Joshua ngumi ya mkono wa kushoto ambayo hata hivyo haikuwa na madhara kwa Joshua.
Mabondia hao baada ya hapo walikuwa wakicheza kwa kuogopana, hakuna ngumi zozote za maana walizorushiana jambo ambalo pia lilionekana kuwakera mashabiki ambao baadhi yao walianza zomeazomea wakitaka kuona ngumi za uhakika zinapigwa badala ya kuogopana na kuviziana.
Katika raundi ya nne, Joshua alionekana kama kuwatuliza mashabiki aliporusha ngumi ya nguvu ya mkono wa kushoto ambayo ilimrudisha nyuma mpinzani wake lakini hakuonekana kusumbuliwa sana na ngumi hiyo.
Akionekana mwenye kujiamini, katika raundi ya tano, Helenius alianza kumrushia ngumi za hapa na pale Joshua na kushangiliwa na baadhi ya mashabiki.
Ngumi za haraka za raundi ya saba na moja ya nguvu ya mkono wa kulia ndizo zilizomlambisha sakafu Helenius na hapo hapo mwamuzi Victor Loughlin kuamua kumaliza pambano kabla ya kumtangaza Joshua kuwa mshindi.

The post Joshua ampiga KO Helenius first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/13/joshua-ampiga-ko-helenius/feed/ 0
Joshua, Fury kuzipiga Desemba https://www.greensports.co.tz/2022/09/08/joshua-fury-kuzipiga-desemba/ https://www.greensports.co.tz/2022/09/08/joshua-fury-kuzipiga-desemba/#respond Thu, 08 Sep 2022 10:31:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2732 London, UingerezaBondia Anthony Joshua amekubali kuzichapa na Tyson Fury ambaye ni bingwa wa ngumi za uzito wa juu duniani anayeshikilia mkanda wa WBC ingawa atalipwa asilimia 40 wakati Fury atalipwa asilimia 60 ya mapato ya pambano hilo.Promota wa Fury, Eddie Hearn alisema kwamba pambano hilo litafanyika katika Uwanja wa Principality, Cardiff Desemba 17 ingawa awali, […]

The post Joshua, Fury kuzipiga Desemba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, Uingereza
Bondia Anthony Joshua amekubali kuzichapa na Tyson Fury ambaye ni bingwa wa ngumi za uzito wa juu duniani anayeshikilia mkanda wa WBC ingawa atalipwa asilimia 40 wakati Fury atalipwa asilimia 60 ya mapato ya pambano hilo.
Promota wa Fury, Eddie Hearn alisema kwamba pambano hilo litafanyika katika Uwanja wa Principality, Cardiff Desemba 17 ingawa awali, Fury alisema kwamba alipanga pambano hilo lifanyike Novemba 26 kwenye Uwanja wa Wembley au Desemba 3 kwenye Uwanja wa Principality lakini ilishindikana.
Uamuzi wa Fury kukubali kuzichapa na Joshua unakuwa ni tofauti na msimamo wake wa awali alipodai kwamba alitaka kuzichapa na Oleksandr Usyk, bingwa wa uzito wa juu anayeshikilia mkanda unaotambuliwa na WBA-IBF-WBO baada ya bondia huyo kumshinda Joshua kwa pointi katika pambano lao la Agosti 20.
Pambano hilo lilishindikana baada ya kutangaza kutoshiriki pambano lolote la ngumi kwa mwaka 2022 na hivyo kumfanya Fury amgeukie Joshua akisema pambano lake na Joshua litaitwa ‘Battle of Britain’ ambapo Joshua alijibu Jumatatu hii akisema kwamba atakuwa tayari kwa pambano hilo.
Akifafanua kuhusu pambano hilo Jumatano hii, Hearn alisema, “Nimewasiliana nao na kuwaambia kwamba tumekubaliana mgao utakuwa ni 60-40 tunataka hilo lirekebishwe katika pambano la marudiano, kwa sababu wewe ndiye bingwa unahitaji mgao mkubwa, jambo ambalo nadhani ni sahihi.
Akizungumzia zaidi kuhusu mgawo huo Fury alisema, “Nafikiri asilimia 60-40 ni zaidi ya uungwana, sikutaka kwenda kuwapa ofa ya asilimia 20 kama ambavyo wangeweza kufanya kwangu badala yake nilikuwa nataka hasa hili pambano liwepo.”
“Tayari nimeshampiga Deontay Wilder na hivyo kuna mtu mmoja na mtu huyo ni AJ (Anthony Joshua) muinua vitu vizito, kwa hiyo ni kwa nini nisimpe asilimia 40 ili asipate sababu na sasa ngoja tuwe na pambano linaloandaliwa kwa ajili ya umma wa Uingereza.
Fury na Joshua ilikuwa wapigane mwaka 2020 baada ya mapromota kudai kwamba thamani ya pambano lao inaweza kufikia Pauni 200 milioni lakini Fury alichukua uamuzi tofauti kwa kuamua kuzichapa na Deontay Wilder wakati Joshua akapanda ulingoni dhidi ya Usyk na kupoteza pambano kwa bondia huyo kutoka Ukraine.

The post Joshua, Fury kuzipiga Desemba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/09/08/joshua-fury-kuzipiga-desemba/feed/ 0