Andre Onana - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 04 Apr 2026 20:23:42 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Andre Onana - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mshahara wa Onana pasua kichwa https://www.greensports.co.tz/2026/04/01/mshahara-wa-onana-pasua-kichwa/ https://www.greensports.co.tz/2026/04/01/mshahara-wa-onana-pasua-kichwa/#respond Wed, 01 Apr 2026 18:02:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14509 Manchester, EnglandKlabu ya Manchester United kwa sasa ipo njia panda kuhusu mambo ya baadaye ya kipa wao, Andre Onana ambaye mshahara wake unatarajia kupaa baada ya Septemba mwaka jana kumtoa kwa mkopo katika klabu ya Trabzonspor ya Uturuki.Ongezeko la mshahara wa kipa huyo wa kimataifa wa Cameroon litachangiwa na timu hiyo kufuzu kushiriki michuano ya […]

The post Mshahara wa Onana pasua kichwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Klabu ya Manchester United kwa sasa ipo njia panda kuhusu mambo ya baadaye ya kipa wao, Andre Onana ambaye mshahara wake unatarajia kupaa baada ya Septemba mwaka jana kumtoa kwa mkopo katika klabu ya Trabzonspor ya Uturuki.
Ongezeko la mshahara wa kipa huyo wa kimataifa wa Cameroon litachangiwa na timu hiyo kufuzu kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kwa mujibu wa makubaliano, kipa huyo anatarajia kurudi Man United baada ya msimu huu.
Mpango wa kipa huyo kwenda Trabzonspor kwa msimu huu ulifanikishwa kama sehemu ya mkakati wa kumpunguzia mshahara baada ya Man United kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2025-26 na hakukuwa na makubaliano ya kumfanya apate usajili wa kudumu kwenye timu hiyo ya Uturuki.
Kwa mantiki hiyo, Onana anatarajia kurudi Man United na kwa kuwa timu hiyo ipo nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu England, upo uwezekano mkubwa wa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya na mshahara wa Onana unatarajia kurudi katika kiwango chake cha zamani.
Mazingira yaliyopo yanasababisha uwezekano wa kummalizia Onana mshahara wake kama kutakuwa na mpango mwingine wa kujadili mkataba mwingine ingawa hapo hapo Man United ipo katika mkakati wa kupunguza gharama za mishahara.
Onana, 29, nyota wa zamani wa Inter Milan, alisajiliwa Man United mwaka 2023 wakati wa kocha Erik ten Hag na amebakisha miaka miwili katika mkataba wake wa sasa na Man United.
Shauku kubwa ya Onana ni kurudi Man United kupigania namba ingawa kipa namba moja wa sasa, Senne Lammens anaonekana kumvutia kocha Michael Carrick ambaye hana mpango wa kusajili kipa mwingine badala yake anapiga hesabu za kumpata mbadala wa kipa namba mbili wa timu hiyo, Altay Bayindir.

The post Mshahara wa Onana pasua kichwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/04/01/mshahara-wa-onana-pasua-kichwa/feed/ 0
Onana atimkia Uturuki https://www.greensports.co.tz/2025/09/12/onana-atimkia-uturuki/ https://www.greensports.co.tz/2025/09/12/onana-atimkia-uturuki/#respond Fri, 12 Sep 2025 19:28:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13894 Manchester, EnglandKlabu ya Man United imethibitisha kuwa kipa wao, Andre Onana (pichani) amejiunga na klabu ya Trabzonspor ya nchini Uturuki kwa mkopo wa mwaka mmoja.Uamuzi wa Onana kujiunga na klabu hiyo inayocheza Ligi Kuu Uturuki au Super League, umekuja baada ya kuwa katika kikosi cha Man United kwa kipindi cha miaka miwili ambacho kimekuwa na […]

The post Onana atimkia Uturuki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Klabu ya Man United imethibitisha kuwa kipa wao, Andre Onana (pichani) amejiunga na klabu ya Trabzonspor ya nchini Uturuki kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Uamuzi wa Onana kujiunga na klabu hiyo inayocheza Ligi Kuu Uturuki au Super League, umekuja baada ya kuwa katika kikosi cha Man United kwa kipindi cha miaka miwili ambacho kimekuwa na hali ya kupanda na kushuka kwa umahiri wake.
Habari za ndani zinadai kuwa katika mkataba wa Onana kucheza Trabzonspor ada yake haikuwekwa wazi na hakuna kipengele kinachompa nafasi ya kusajiliwa moja kwa moja hivyo baada ya mwaka mmoja atarudi Man United.
Zaidi ya hilo, katika mkataba huo kwa kipindi chote atakachokuwa Trabzonspor, Man United haitowajibika kumlipa chochote kipa huyo ambaye pia huidakia timu ya taifa ya Cameroon.
Uamuzi wa Onana kukubali kuondoka Man United unaaminika kuwa umetokana na kitendo cha klabu hiyo kumsajili kipa Senne Lammens kutoka Antwerp katika siku za mwisho za usajili licha ya Onana kuahidi kubaki kwa lengo la kupigania nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Onana, 29, alijiunga na Man United mwaka 2023 akitokea Inter Milan ya Italia kwa ada iliyofikia Dola 59 milioni huku akipewa matumaini makubwa ya kuwa kipa tegemeo lakini kwa kipindi chote mwenendo wake umekuwa wa kupanda na kushuka ubora.
Taarifa fupi ya Man United ilieleza, “Kipa wa Manchester United, Andre Onana amejiunga na klabu ya Trabzonspor kwa mkopo katika kipindi chote cha msimu wa 2025-26.”
Onana ambaye amejiunga na Trabzonspor wakati wa siku za mwisho za dirisha la usajili Uturuki yaani Ijumaa hii Seotemba 12, 2025, akiwa Man United ameichezea timu hiyo mara 102 na kuiwezesha kubeba Kombe la FA mwaka 2024 wakati huo kocha akiwa Erik ten Hag.

The post Onana atimkia Uturuki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/09/12/onana-atimkia-uturuki/feed/ 0
Matic: Onana kipa wa hovyo https://www.greensports.co.tz/2025/04/14/matic-onana-kipa-wa-hovyo/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/14/matic-onana-kipa-wa-hovyo/#respond Mon, 14 Apr 2025 06:53:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13240 Lyon, UfaransaKiungo wa zamani wa Man United, Nemanja Matic (pichani) amemtaja kipa wa timu hiyo, Andre Onana kuwa ni mmoja wa makipa wa hovyo katika historia ya klabu hiyo.Matic, 36, alikuwa akijibu kauli iliyotolewa na Onana ambaye pia ni kipa wa timu ya taifa ya Cameroon ambaye alisema Man United ni bora kwa mbali kuizidi […]

The post Matic: Onana kipa wa hovyo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Lyon, Ufaransa
Kiungo wa zamani wa Man United, Nemanja Matic (pichani) amemtaja kipa wa timu hiyo, Andre Onana kuwa ni mmoja wa makipa wa hovyo katika historia ya klabu hiyo.
Matic, 36, alikuwa akijibu kauli iliyotolewa na Onana ambaye pia ni kipa wa timu ya taifa ya Cameroon ambaye alisema Man United ni bora kwa mbali kuizidi klabu ya Lyon ya Ufaransa.
Onana alitoa kauli hiyo siku kadhaa kabla ya timu hizo kuumana katika robo fainali ya Europa, mechi ambayo iliisha kwa sare ya 2-2 na sasa timu hizo zitarudiana Alhamisi ijayo.
Akizungumzia kauli hiyo, Matic ambaye aliichezea Man United kati ya mwaka 2017 hadi 2022, alisema anapenda kuheshimu kila mtu lakini inapotokea mtu kutoa kauli kama za Onana unatakiwa kuwa na majibu yake.
Matic aliongeza kwa kusema kwamba inapotokea wewe kuwa mmoja wa makipa wa hovyo katika historia ya Man United ni lazima uwe makini na kile unachokisema.
“Kama angekwua ni Van der Sar, (Peter) Schmeichel au (David) De Gea anayesema hayo ningejiuliza mimi mwenyewe lakini ni lazima uwe na sifa za kutoa kauli kama hizo,” alisema.
Matic ambaye akiwa Man United aliichezea timu hiyo mara 128, mwaka jana alijiunga na Lyon baada ya kuzichezea timu za Rennes pia ya Ufaransa na Roma ya Italia.
Akiwa Man United alibeba taji la Ligi Kuu England mara mbili pamoja na taji la FA na EFL kwa miaka minne aliyokuwa na klabu ya Chelsea.
Kwa upande wa Onana alijiunga na Man United mwaka 2023 akitokea Inter Milan ya Italia na hadi sasa taji pekee alilofanikiwa kulibeba ni lile la FA.
Kipa huyo hivi karibuni amejikuta akilaumiwa kwa kufanya makosa ya kizembe mojawapo ni kitendo chake cha kuchelewa kugawa mipira baada ya kuidaka.

The post Matic: Onana kipa wa hovyo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/14/matic-onana-kipa-wa-hovyo/feed/ 0
Onana awapinga mashabiki Man United https://www.greensports.co.tz/2025/04/08/onana-awapinga-mashabiki-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/08/onana-awapinga-mashabiki-man-united/#respond Tue, 08 Apr 2025 13:01:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13227 Manchester, EnglandKipa wa Man United, André Onana amesema hatoruhusu maamuzi yake uwanjani yatokane na presha za mashabiki baada ya kushutumiwa kwa kukaa na mpira muda mrefu.Onana amejikuta akitupiwa lawama na baadhi ya mashabiki wa Man United ambao wanaamini kipa huyo ana tabia ya kukaa na mpira muda mrefu wakati timu yake inapokuwa na nafasi ya […]

The post Onana awapinga mashabiki Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kipa wa Man United, André Onana amesema hatoruhusu maamuzi yake uwanjani yatokane na presha za mashabiki baada ya kushutumiwa kwa kukaa na mpira muda mrefu.
Onana amejikuta akitupiwa lawama na baadhi ya mashabiki wa Man United ambao wanaamini kipa huyo ana tabia ya kukaa na mpira muda mrefu wakati timu yake inapokuwa na nafasi ya kufanya shambulizi.
Kuna wakati kipa huyo amejikuta akipigiwa kelele na mashabiki na wengine kuguna na moja ya matukio ya kukumbukwa ni kwenye mechi ya Jumapili dhidi ya Man City iliyoisha kwa sare ya 0-0.
Akijibu malalamiko hayo ya mashabiki, Onana ambaye pia ni kipa wa timu ya taifa ya Cameroon alisema hawezi kuharakisha kufanya maamuzi kama hajafikiri maamuzi hayo kuwa ni sahihi au la.
Onana alisema kinachofanywa na mashabiki hakiwezi kuathiri maamuzi yake awapo uwanjani kwa sababu maamuzi ambayo anafanya ni kwa ajili ya kuisaidia timu.

“Kuna wakati nafanya maamuzi sahihi na kuna wakati nafanya makosa, ninapoona wachezaji wangu wanahitaji kupumzika lazima nijipe muda, ninapoona kuna uhitaji wa kuharakisha mchezo nafanya haraka,” alisema Onana.


Aliongeza kwamba kuna wakati hasa kipindi cha pili timu pinzani wakiwa wanamiliki mpira kwa kiasi kikubwa kuliko wao hapo analazimika kuwapa nafasi wachezaji wake wapumue.
Baada ya kutoka sare na mahasimu wao wa Manchester, Man United wtaaeleke Ufaransa ambapo keshokutwa Alhamisi wataikabili Lyon katika robo fainali ya Europa Ligi.

The post Onana awapinga mashabiki Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/08/onana-awapinga-mashabiki-man-united/feed/ 0
Onana alikoroga Man United https://www.greensports.co.tz/2024/04/28/onana-alikoroga-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/28/onana-alikoroga-man-united/#respond Sun, 28 Apr 2024 09:40:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10764 Manchester, EnglandKipa wa Man United, Andre Onana amefanya makosa yaliyozaa penalti katika dakika ya 87 na kuifanya timu yake itoke sare ya 1-1 na Burnley katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) jana Jumamosi.Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Old Trafford, Man United ilipata bao la kuongoza dakika ya 79 lililofungwa na Antony lakini […]

The post Onana alikoroga Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kipa wa Man United, Andre Onana amefanya makosa yaliyozaa penalti katika dakika ya 87 na kuifanya timu yake itoke sare ya 1-1 na Burnley katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) jana Jumamosi.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Old Trafford, Man United ilipata bao la kuongoza dakika ya 79 lililofungwa na Antony lakini dakika tatu kabla ya kutimia dakika 90, Burnley walipata bao la penalti iliyopigwa na Zeki Amdouni.
Man United katika mechi hiyo ingawa haikuonesha ubora lakini juhudi za Antony ziliibua matumaini ya kutoka uwanjani na pointi tatu kabla mambo hayajaharibika baada ya Onana kumchezea rafu mchezaji wa Burnley wakati akiokoa hatari iliyoelekezwa langoni mwake.
Rafu hiyo ilionekana baada ya matumizi ya VAR na ndipo Amdouni aliyeingia kipindi cha pili akafunga bao baada ya kumchanganya Onana aliyeruka upande tofauti na mpira ulipokwenda.
Matokeo hayo yanakuwa faraja kubwa kwa Burnley ambayo inapambana kujinasua na janga la kushuka daraja ikiwa imejitenga na janga hilo kwa tofauti ya pointi mbili huku Man United ikijiweka pagumu kusaka tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Burnley inayonolewa na mchezaji wa zamani wa Man City, Vincent Kompany wiki ijayo itakuwa na kibarua dhidi ya Newcastle wakati mechi yake ya mwisho ya msimu itacheza na Nottingham timu nyingine iliyo katika hatari ya kushuka daraja.
Matokeo ya mechi za EPL Jumamosi…
West Ham 2-2 Liverpool
Fulham 1-1 Crystal Palace
Man Utd 1-1 Burnley
Newcastle 5-1 Sheff Utd
Wolves 2-1 Luton
Everton 1-0 Brentford
Aston Villa 2-2 Chelsea

The post Onana alikoroga Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/28/onana-alikoroga-man-united/feed/ 0
Miezi 6 migumu kwa Onana Man United https://www.greensports.co.tz/2024/03/02/miezi-6-migumu-kwa-onana-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/02/miezi-6-migumu-kwa-onana-man-united/#respond Sat, 02 Mar 2024 13:23:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9981 Manchester, EnglandKipa namba moja wa Man United, Andre Onana amesema kwamba hakuwa mwenye raha katika miezi sita ya kwanza katika klabu hiyo.Onana alijiunga na timu hiyo katika usajili wa dirisha kubwa majira ya kiangazi mwaka jana akitokea Inter Milan kwa ada ya Pauni 47 milioni, amehusishwa na makosa kadhaa katika mechi za nusu ya kwanza […]

The post Miezi 6 migumu kwa Onana Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kipa namba moja wa Man United, Andre Onana amesema kwamba hakuwa mwenye raha katika miezi sita ya kwanza katika klabu hiyo.
Onana alijiunga na timu hiyo katika usajili wa dirisha kubwa majira ya kiangazi mwaka jana akitokea Inter Milan kwa ada ya Pauni 47 milioni, amehusishwa na makosa kadhaa katika mechi za nusu ya kwanza ya msimu huu.
Moja ya makosa anayotajwa kuyafanya kipa huyo, ndiyo yaliyochangia timu hiyo kutolewa mapema kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ingawa amekiri kwamba kwa sasa ameanza kujiona yuko salama na mwenye amani.
“Tayari nimeshajijua mimi ni kipa wa aina gani, imenichukua miezi sita au saba kutoweza kucheza vizuri, kushindwa tu kujisikia vizuri,” alisema Onana.
“Kilikuwa kipindi kigumu kwangu, kwa sasa najiona niko sawa, wakati ule kila kitu kilikuwa kipya, ilikuwa jambo gumu kwangu kwa sababu nyingi tu, ilikuwa nchi mpya, kwa sasa najiona niko sawa, kwangu muhimu ni kuwa sawa na mwenye furaha, hapo nitaanza kung’ara,” alisema Onana.
Akiwa katika msimu wake wa mwisho na Inter Milan kabla ya kutua Man United, Onana aliiwezesha timu hiyo kufikia hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Juni mwaka jana.
Msimu huu hata hivyo mambo yamekuwa magumu kwa Man United katika michuano hiyo, timu hiyo imeishia hatua ya makundi huku Onana akibebeshwa lawama kwa makosa aliyoyafanya katika mechi dhidi ya Bayern Munich na Galatasary hadi timu hiyo kumaliza katika kundi lake ikiwa mkiani.

The post Miezi 6 migumu kwa Onana Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/02/miezi-6-migumu-kwa-onana-man-united/feed/ 0
Onana kukosa mechi ya kwanza Afcon https://www.greensports.co.tz/2024/01/11/onana-kukosa-mechi-ya-kwanza-afcon/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/11/onana-kukosa-mechi-ya-kwanza-afcon/#respond Thu, 11 Jan 2024 07:46:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9257 Manchester, EnglandKipa wa Man United na timu ya taifa ya Cameroon, Andre Onana anatarajia kukosa mechi ya kwanza ya Afcon dhidi ya Guinea ili apate nafasi ya kuichezea Man United katika mechi na Tottenham.Onana alipewa ruhusa na mabosi wa Shirikisho la Soka Cameroon na kutokuwamo kwenye ziara ya timu hiyo nchini Saudi Arabia ili aweze […]

The post Onana kukosa mechi ya kwanza Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kipa wa Man United na timu ya taifa ya Cameroon, Andre Onana anatarajia kukosa mechi ya kwanza ya Afcon dhidi ya Guinea ili apate nafasi ya kuichezea Man United katika mechi na Tottenham.
Onana alipewa ruhusa na mabosi wa Shirikisho la Soka Cameroon na kutokuwamo kwenye ziara ya timu hiyo nchini Saudi Arabia ili aweze kucheza mechi ya Man United ya Kombe la FA dhidi ya Wigan iliyochezwa Jumatatu iliyopita.
Baada ya ruhusa hiyo, kipa huyo pia anatarajia kuendelea kuchelewa kwenye timu yake ya taifa ili aweze kuwa golini katika mechi dhidi ya Tottenham itakayopigwa Jumapili ijayo kwenye dimba la Old Traffod.
Katika mechi hiyo, bilionea mpya wa Man United, Sir Jim Ratcliffe kwa mara ya kwanza tangu anunuea hisa asilimia 25 za klabu hiyo, atakuwa jukwaani Old Traffod akiishuhudia timu yake.
Baada ya mechi hiyo ya Old Trafford ndipo Onana atakapoungana na timu ya Cameroon na habari za ndani zinadai kuwa mabosi wa soka Cameroon wamempa ruhusa kuchelewa na hivyo atakuwa kikosini saa kadhaa baada ya mechi ya kwanza ya Afcon dhidi ya Guinea itakayochezwa Januari 15.
Kwa mantiki hiyo, Onana ataanza kuiwakilisha Cameroon kwenye Afcon katika mechi mbili za hatua ya makundi dhidi ya Senegal itakayopigwa Januari 19, na dhidi ya Gambia, Januari 23.
Baada ya hapo uwapo wa Onana kwenye Afcon utategemea kama Cameroon itasonga mbele kwenye michuano hiyo.

The post Onana kukosa mechi ya kwanza Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/11/onana-kukosa-mechi-ya-kwanza-afcon/feed/ 0
Onana ajipanga kuchelewa Afcon https://www.greensports.co.tz/2023/12/29/onana-ajipanga-kuchelewa-afcon/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/29/onana-ajipanga-kuchelewa-afcon/#respond Fri, 29 Dec 2023 18:44:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9073 Manchester, EnglandKipa wa Man United, Andre Onana anadaiwa kuanza mazungumzo na mabosi wa soka wa Cameroon ili achelewe kadri iwezekanavyo kujiunga na timu ya taifa kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).Onana yumo ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon kinachojiandaa na fainali za Afcon zitakazoanza kutimua vumbi Januari 13 mwakani […]

The post Onana ajipanga kuchelewa Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kipa wa Man United, Andre Onana anadaiwa kuanza mazungumzo na mabosi wa soka wa Cameroon ili achelewe kadri iwezekanavyo kujiunga na timu ya taifa kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).
Onana yumo ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon kinachojiandaa na fainali za Afcon zitakazoanza kutimua vumbi Januari 13 mwakani nchini Ivory Coast na kufikia tamati Februari 11.
Awali Onana alisema yupo tayari kuiwakilisha Cameroon kwenye fainali hizo lakini habari za ndani zinadai kwamba kipa huyo anachotaka ni kuhakikisha anachelewa kuondoka Man United.
Katika maandalizi yake ya Afcon, Cameroon inatarajia kuweka kambi Saudi Arabia na kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Zambia, mechi ambayo itapigwa Januari 9 mwakani.
Baada ya kutambua ratiba hiyo, Onana anahaha kuhakikisha anaiwakilisha Man United katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Wigan, mechi ambayo itapigwa Januari 8 mwakani.
Kwa maana hiyo, Onana ni kama vile yuko tayari kuikosa mechi na Zambia badala yake anachotaka ni kuwa na timu hiyo kwenye mechi ya kwanza ya Afcon dhidi ya Guinea, mechi itakayochezwa Januari 15 mwakani.
Januari 14 mwakani, Man United itakuwa na mechi ya Ligi Kuu England (EPL) dhidi ya Tottenham na Januari 27, siku ambayo mechi za hatua ya mtoano za Afcon zitaanza, Man United huenda ikawa uwanjani siku hiyo katika mechi nyingine ya Kombe la FA.
Baada ya hapo Man United itakuwa na mechi nyingine za EPL, Februari Mosi dhidi ya Wolves, Februari 4 dhidi ya West Ham na Februari 11 dhidi ya Aston Villa.
Suala la Onana kuchelewa kujiunga na timu ya Cameroon kama likiwezekana bado atazikosa mechi kadhaa za Man United vinginevyo ataziwahi iwapo Cameroon itatolewa mapema tofauti na hivyo nafasi yake atapewa kipa namba mbili wa Man United, Altay Bayindir.
Suala la Onana huenda pia likaibua utata na kocha wa Cameroon, Rigobert Song ambaye amemuacha katika timu hiyo mshambuliaji wa Bayern Munich, Eric-Maxim Choupo Moting baada ya mchezaji huyo kukosekana katika mechi tatu zilizopita.
Wakati wa fainali za Kombe la Dunia za Qatar zilizofanyika Novemba na Desemba mwaka 2022, Onana alitangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Cameroon kabla ya kubadili uamuzi huo Septemba mwaka huu.
Katika Afcon, Cameroon imepangwa Kundi C na baada ya mechi yake na Guinea itakuwa na kibarua kingine dhidi ya mabingwa watetezi Senegal na kumalizia mechi za makundi kwa kuumana na Gambia.
Kikosi kamili cha Cameroon ni kama ifuatavyo: Makipa, Andre Onana (Man United), Devis Epassy (Abha Club), Simon Ngapandouetnbu (Marseille) na Fabrice Ondoa (Nimes)
Mabeki: Oumar Gonzalez (Al Raed), Harold Moukoudi (Athens), Tolo Nouhou (Seattle Sounders), Junior Tchamadeu (Stoke City), Enzo Tchato (Montpellier), Darling Yongwa (Lorient) Malcom Bokele (Bordeaux), Christopher Wooh (Stade Rennais) na Jean-Charles Castelletto (Nantes),
Viungo: Olivier Ntcham (Samsunspor), Wilfried Nathan Doualla (Victoria United), Ben Elliott (Reading), Olivier Kemen (Kayserispor), Andre-Frank Zambo Anguissa (Napoli) na Yvan Neyou (Leganes),
Washambuliaji: Francois-Regis Mughe (Marseille), Vincent Aboubakar (Besiktas), Leonel Ateba (Dynamo Douala), Frank Magri (Toulouse), Faris Pemi Moumbagna (Bodo/Glimt), Georges-Kevin Nkoudou (Damac), Karl Toko Ekambi (Abha Club) na Clinton Njie (Sivasspor).

The post Onana ajipanga kuchelewa Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/29/onana-ajipanga-kuchelewa-afcon/feed/ 0
Djemba Djemba ampa somo Onana https://www.greensports.co.tz/2023/12/20/djemba-djemba-ampa-somo-onana/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/20/djemba-djemba-ampa-somo-onana/#respond Wed, 20 Dec 2023 08:44:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8948 Yaounde, CameroonKiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon na Man United, Eric Djemba Djemba (pichani) amesema kipa wa Man United na timu ya taifa ya Cameroon, Andre Onana lazima afikirie soka lake pale anapoamua kukosa baadhi ya mechi za Ligi Kuu England (EPL).Onana atakosekana katika EPL kwa takriban mwezi mmoja kama atajiunga na […]

The post Djemba Djemba ampa somo Onana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Yaounde, Cameroon
Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon na Man United, Eric Djemba Djemba (pichani) amesema kipa wa Man United na timu ya taifa ya Cameroon, Andre Onana lazima afikirie soka lake pale anapoamua kukosa baadhi ya mechi za Ligi Kuu England (EPL).
Onana atakosekana katika EPL kwa takriban mwezi mmoja kama atajiunga na timu ya taifa ya Cameroon kwenye fainali za Afcon zitakazoanza Januari mwakani nchini Ivory Coast.
Septemba mwaka huu, Onana alitangaza kufuta uamuzi wake wa awali wa kustaafu kuichezea timu ya Cameroon, kwa sasa anapitia kipindi kigumu Man United baada ya kuwa katika msimu mgumu ambapo timu hiyo imetolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na katika EPL mambo si mazuri.
“Moja ya tatizo kwake ni kwamba hata akicheza vizuri kwa kipindi hiki bado atakuwa nje kwa mwezi mmoja kwa ajili ya Afcon,” alisema Djemba Djemba na kuongeza kuwa Onana pia anaweza akajiharibia nafasi yake ya kuwa kipa namba moja wa Cameroon kama atabaki Man United kipindi cha Afcon.

“Anajua kwamba kama akienda kwenye Afcon anaweza akapoteza nafasi yake Manchester United, anatakiwa kuamua kipi bora kwake, anachotakiwa ni kufanya kile kilicho bora kwa soka lake,” alisema Djemba Djemba.


Fainali za Afcon zitaanza rasmi kutimua vumbi Januari 13 na kufikia tamati Februari 11 ambapo Onana akienda huko atakosa zaidi ya mechi nne za EPL za Man United kutegemea na nafasi ya Cameroon kwenye Afcon kama itafika mbali au itaishia hatua ya makundi.
Onana (pichani chini) alisajiliwa Man United Julai mwaka huu kwa ada ya Pauni 47 milioni akitokea Inter Milan lakini amejikuta akilaumiwa kwa makosa yaliyoigharimu timu hasa kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray na Bayern Munich.


“Kila mtu anaijua Manchester United, ni moja ya timu kubwa duniani, unapojiunga Manchester United hawakupi muda” alisema Djemba Djemba aliyewahi kuichezea timu hiyo baada ya kujiunga nayo mwaka 2003, alicheza mechi 39 chini ya kocha mkongwe, Sir Alex Ferguson.
Djemba Djemba alisema tatizo la Onana katika timu hiyo linachangiwa na uchezaji wake wa kutoa pasi karibu na eneo lake jambo ambalo halipendelewi Man United.
“Ni kipa mmoja au wawili wa Manchester City wanaocheza kwa staili hiyo ya kutoa pasi, wana kocha Pep Guardiola, anapenda kipa wa aina hiyo ambaye anacheza zaidi kwa miguu,” alisema Djemba Djemba.
“Kwa Manchester United ukiwa kipa mzuri kwa kutumia mikono yako watakusajili, hawatajali kama huna tabia ya kutumia miguu kutoa pasi, Onana amejikuta akilaumiwa kwa sababu Manchester United ni timu kubwa,” alisema Djemba Djemba.

The post Djemba Djemba ampa somo Onana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/20/djemba-djemba-ampa-somo-onana/feed/ 0
Ten Hag amkingia kifua Onana https://www.greensports.co.tz/2023/11/30/ten-hag-amkingia-kifua-onana/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/30/ten-hag-amkingia-kifua-onana/#respond Thu, 30 Nov 2023 12:33:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8689 Istanbul, UturukiKocha wa Man United, Erik ten Hag amekataa kumlaumu kipa wake, Andre Onana licha ya kufanya makosa mawili yaliyosababisha timu hiyo itoke sare ya mabao 3-3 na Galatasaray katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.Katika mechi hiyo ya Kundi A, Man United ilikuwa mbele kwa mabao 2-0 na baadaye kuongoza kwa 3-1 kabla Onana hajafanya makosa […]

The post Ten Hag amkingia kifua Onana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Istanbul, Uturuki
Kocha wa Man United, Erik ten Hag amekataa kumlaumu kipa wake, Andre Onana licha ya kufanya makosa mawili yaliyosababisha timu hiyo itoke sare ya mabao 3-3 na Galatasaray katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika mechi hiyo ya Kundi A, Man United ilikuwa mbele kwa mabao 2-0 na baadaye kuongoza kwa 3-1 kabla Onana hajafanya makosa mawili yaliyofanya ubao usomeke 3-3.
Matokeo hayo yanazidi kuiweka Man United katika wakati mgumu kuweza kufuzu hatua ya mtoano kwani hadi sasa timu hiyo inaburuza mkia katika kundi lake huku Onana akilaumiwa kwa kukosa umakini wa kudhibiti mipira ya mbali iliyopigwa na Hakim Ziyech.
Ten Hag hata hivyo alipoulizwa na waandishi kuhusu Onana kwanza alijibu kwa kifupi, “Yuko sawa.” na baada ya hapo akasisitiza kwamba si kosa la mtu mmoja.

“Kama nilivyopata kusema si suala la mtu mmoja, ni kweli kwamba makosa ya mtu mmoja mmoja kwenye soka yanaweza kubadili mambo na mtu anabeba lawama lakini wakati wote ni suala la timu,” alisema Ten Hag.


Ten Hag alisema kwamba timu yake ni nzuri, wachezaji wote katika kikosi ni wazuri na wanahitaji kupewa heshima kwa kuichezea Manchester United, kwa sababu ni wachezaji mahiri na hilo linawahusu wachezaji wote.
Man United bado haijatoka katika mbio za kusaka tiketi ya hatua ya mtoano (16 bora) ya Ligi ya Mabingwa licha ya kushinda mechi moja tu kati ya tano, nafasi ya kusonga mbele ipo japo ndogo.
Matokeo mechi za jana Jumatano Ligi ya Mabingwa Ulaya…
Galatasaray 3-3 Man Utd
Sevilla 2-3 PSV Eindhoven
Bayern Munich 0-0 FC Copenhagen
Arsenal 6-0 Lens
Real Madrid 4-2 Napoli
Sporting Braga 1-1 Union Berlin
Benfica 3-3 Inter Milan
Real Sociedad 0-0 RB Salzburg

The post Ten Hag amkingia kifua Onana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/30/ten-hag-amkingia-kifua-onana/feed/ 0