Ancelotti - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 22 Apr 2025 16:15:04 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ancelotti - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ancelotti: Lolote lawezekana https://www.greensports.co.tz/2025/04/22/ancelotti-lolote-lawezekana/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/22/ancelotti-lolote-lawezekana/#respond Tue, 22 Apr 2025 15:36:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13305 Madrid, HispaniaKocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amezungumzia mambo yake ya baadaye katika klabu hiyo akisisitiza lolote linawezekana wakati huu timu yake ikichuana na Barcelona kuwania mataji ya La Liga na Kombe la Mafalme.Ancelotti amekuwa katika kipindi kigumu tangu timu yake itolewe na Arsenal kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa […]

The post Ancelotti: Lolote lawezekana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Madrid, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amezungumzia mambo yake ya baadaye katika klabu hiyo akisisitiza lolote linawezekana wakati huu timu yake ikichuana na Barcelona kuwania mataji ya La Liga na Kombe la Mafalme.
Ancelotti amekuwa katika kipindi kigumu tangu timu yake itolewe na Arsenal kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kipigo cha jumla cha mabao 5-1.
Real Madrid imeachwa na Barcelona kwa tofauti ya pointi nne katika La Liga zikiwa zimebaki mechi sita kabla ya kufikia tamati ya kwa ligi hiyo, pia Jumamosi itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya timu hiyo kwenye Kombe la Mfalme.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo Jumanne, Aprili 22, 2025 kabla ya kuumana na Getafe kwenye La Liga, Ancelotti alisema timu yake inaweza kubeba mataji yote hayo mawili.
Kuhusu presha ya nafasi yake ya ukocha, Ancelotti ambaye mkataba wake na Real Madtid unaishia 2026 alisema hali hiyo na yote yanayoendelea ni kama kichocheo kwake.
Kocha huyo badala yake aliwapa mashabiki wa timu hiyo habari njema kuhusu mshambuliaji Kylian Mbappe aliyeumia enka akisema anaendelea vizuri na anaweza kucheza mechi ya fainali ya Kombe la Mfalme.

“Katika soka lolote linawezekana, je mnashangazwa na mambo yote yanayotokea, hakuna kinachonishangaza mimi, kama ninavyosema wakati wote, naipenda hii kazi, nilipenda nilivyokuwa hapa awamu ya kwanza (2013 hadi 2015) napenda hii awamu ya pili kuanzia 2021 na nataka awamu hii iendelee kadri inavyowezekana,” alisema Ancelotti.


Ancelotti pia alisema kwamba ikifika siku ambayo kazi yake itafikia mwisho atakuwa mwenye kushukuru na kuvua kofia yake katika klabu hiyo kwani hiyo ndiyo hali halisi.
Kocha huyo Mtaliano amejijengea heshima kwa kuiwezesha Real Madrid kubeba mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini msimu huu umekuwa mgumu huku habari ya kutimuliwa kwake ikipamba moto siku hadi siku.

The post Ancelotti: Lolote lawezekana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/22/ancelotti-lolote-lawezekana/feed/ 0
Ancelotti: Real Madrid tupo shwari https://www.greensports.co.tz/2025/04/20/ancelotti-real-madrid-tupo-shwari/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/20/ancelotti-real-madrid-tupo-shwari/#respond Sun, 20 Apr 2025 08:41:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13283 Madrid, HispaniaKocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amekana kuwapo mgogoro wa chinichini katika klabu hiyo huku akiweka wazi kwamba mambo yake ya baadaye yatajadiliwa mwisho wa msimu huu.Nafasi ya Ancelotti imekuwa mjadala katika siku za karibuni hasa baada ya timu hiyo kuishia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kutolewa na Arsenal.Real […]

The post Ancelotti: Real Madrid tupo shwari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amekana kuwapo mgogoro wa chinichini katika klabu hiyo huku akiweka wazi kwamba mambo yake ya baadaye yatajadiliwa mwisho wa msimu huu.
Nafasi ya Ancelotti imekuwa mjadala katika siku za karibuni hasa baada ya timu hiyo kuishia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kutolewa na Arsenal.
Real Madrid ikiwa nyumbani Santiago Bernabéu Jumatano iliyopita ililala kwa mabao 2-1 mbele ya Arsenal hiyo ni badaa ya kulala ugenini kwa mabao 3-0 na hivyo kutolewa katika michuano hiyo kwa jumla ya mabao 5-1.
Kocha huyo Mtaliano tangu ajiunge kwa mara ya pili na Real Madrid mwaka 2021 ameweza kujiwekea rekodi nzuri ya kubeba mataji ya La Liga mara mbili na Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili.
Msimu huu hata hivyo umekuwa mgumu kwa Ancelotti, timu yake imetolewa kwenye ligi ya mabingwa, michuano ambayo ina hadhi ya juu Ulaya na dunia kote wakati huo huo inahaha kubeba taji la La Liga.
Real Madrid msimu huu imepoteza mechi kadhaa katika namna ambayo haikutarajiwa, wiki ijayo itacheza mechi ya fainali Kombe la Mfalme, taji inalotakiwa ilipiganie walau itoke na kitu msimu huu.

“Nimezungumza na wachezaji na viongozi, sote tunafikiria katika mtazamo mmoja ambao ni kuendelea kupigania mataji yaliyobaki,” alisema Ancelotti.


Ancelotti alisisitiza kwamba hakuna mgogoro wowote na klabu na kwamba wote wapo katika safari moja na yeyote anayesema kuna mgogoro na klabu au rais (Florentino Perez) huyo hasemi ukweli.
Mkataba wa Ancelotti na Real Madrid unafikia ukomo mwaka 2026 ingawa kumekuwapo habari kwamba klabu hiyo inataka kuachana na kocha huyo ambaye pia inadaiwa anawindwa kwa udi na uvumba kwenye timu ya taifa ya Brazil.

The post Ancelotti: Real Madrid tupo shwari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/20/ancelotti-real-madrid-tupo-shwari/feed/ 0
Ancelotti kortini, adaiwa kukwepa kodi https://www.greensports.co.tz/2025/04/02/ancelotti-kortini-adaiwa-kukwepa-kodi/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/02/ancelotti-kortini-adaiwa-kukwepa-kodi/#respond Wed, 02 Apr 2025 19:48:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13194 Madrid, HispaniaKocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti ameiambia mahakama moja nchini Hispania leo Jumatano Aprili 2, 2025 kwamba hakuwahi hata kufikiria kufanya kosa la ukwepaji kodi.Ancelotti anatuhumiwa kukwepa kodi inayofikia Dola 1.08 milioni, kodi inayotokana na haki za matangazo ya picha kwa mwaka 2014 na 2015 alipokuwa kocha wa Real Madrid kwa mara ya kwanza.“Kwangu […]

The post Ancelotti kortini, adaiwa kukwepa kodi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti ameiambia mahakama moja nchini Hispania leo Jumatano Aprili 2, 2025 kwamba hakuwahi hata kufikiria kufanya kosa la ukwepaji kodi.
Ancelotti anatuhumiwa kukwepa kodi inayofikia Dola 1.08 milioni, kodi inayotokana na haki za matangazo ya picha kwa mwaka 2014 na 2015 alipokuwa kocha wa Real Madrid kwa mara ya kwanza.
“Kwangu mimi kila kitu kilikuwa katika utaratibu, sikuwahi hata kufikiria kukwepa kodi,” alisema Ancelotti baada ya kufika mahakamani hapo kwa mara ya kwanza.
Kocha huyo mkongwe aliwasili mahakamani akiwa na mtoto wake wa kiume, mmoja wa wasaidizi wake pamoja na rafiki yake wa kike na alitumia dakika zipatazo 40 kujitetea.
Ancelotti alisema alipojiunga na Real Madrid Julai 2013 alipewa mshahara wa Euro milioni sita na klabu ilitoa mgawanyo wa mshahara huo na yeye akafikisha taarifa hizo kwa mshauri wake wa masuala ya kodi aliyekuwa Uingereza.

“Sikuwa mwenye kulipa umuhimu wowote suala la haki za picha, makocha hawana umuhimu katika hilo, ni wachezaji ndio wenye umuhimu nalo, nilichokiangalia ni kujiingizia malipo ya Euro milioni sita katika kipindi cha miaka mitatu,” alisema Ancelotti.


Ancelotti alifafanua kuwa hakuwahi kujua kwamba kuna kitu ambacho hakikuwa sawa na hakuarifiwa kwamba alikuwa anachunguzwa.
Katika shauri hilo waendesha mashtaka wanataka mtuhumiwa huyo afungwe jela miaka minne na miezi tisa pamoja na kutozwa faini ya Euro milioni 3.2.
Madai ya waendesha mashtaka hao ni kwamba kwa mwaka 2014 hadi 2015, Ancelotti anadaiwa kutoa taarifa kwenye ofisi za kodi kuhusu mshahara pekee aliokuwa akilipwa na klabu hiyo na kuweka kando haki za picha.
Kocha ambaye alirudi tena kuinoa Real Madrid mwaka 2021 na kuendelea na kibarua hicho hadi sasa, anaingia katika orodha ya makocha na wachezaji mastaa wanaochunguzwa nchini Hispania kwa makosa ya ukwepaji kodi.
Wengine ni Cristiano Ronaldo na Diego Costa ambao kesi zao zilimalizwa nje ya mahakama na kutakiwa kulipa faini kubwa, pia yumo kocha wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso ambaye alikataa kumaliza suala lake nje ya mahakama.

The post Ancelotti kortini, adaiwa kukwepa kodi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/02/ancelotti-kortini-adaiwa-kukwepa-kodi/feed/ 0
Ancelotti: Ni pigo kubwa https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/ancelotti-ni-pigo-kubwa/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/ancelotti-ni-pigo-kubwa/#respond Sun, 02 Mar 2025 09:16:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13076 Madrid, HispaniaKocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amekiri timu yake imepata pigo kubwa katika mbio za kusaka taji la La Liga baada ya kufungwa mabao 2-1 na Real Betis jana Jumamosi.Katika mechi hiyo, Real Madrid ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa naBrahim Díaz lakini Betis walisawazisha kupitia kwa Johnny Cardoso na kuzifanya timu ziende […]

The post Ancelotti: Ni pigo kubwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amekiri timu yake imepata pigo kubwa katika mbio za kusaka taji la La Liga baada ya kufungwa mabao 2-1 na Real Betis jana Jumamosi.
Katika mechi hiyo, Real Madrid ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na
Brahim Díaz lakini Betis walisawazisha kupitia kwa Johnny Cardoso na kuzifanya timu ziende mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Kipindi cha pili, nyota wa zamani wa Real Madrid, Isco aliifungia Betis bao la pili kwa penalti na kuifanya Real Madrid ipoteze pointi tatu na kujiweka pagumu katika mbio za kulisaka taji hilo dhidi ya timu za Barcelona na Atlético Madrid.
Akizungumzia matokeo hayo, Ancelotti alisema mechi ilikuwa mbaya kwao licha ya kuanza vizuri lakini hawakuweza kuendelea na kasi yao hivyo kushindwa na timu ambayo ilicheza vizuri na ilikuwa haki yao kushinda.

“Hili ni pigo kubwa, lazima tuchukue hatua, kupoteza mechi katika hatua hii ya msimu ni pigo, hatukufanya vizuri, tulipoteza mpira mara 27 katika kipindi cha kwanza, hicho ni kiasi kikubwa,” alisema Ancelotti.


Ancelloti pengine baada ya kuona mambo yanakuwa magumu dakika ya 75 alimtoa Kylian Mbappe na kumuingiza Endrick, mabadiliko ambayo hayakuweza kubadili matokeo ya mchezo huo.
Kocha huyo hata hivyo baadaye alisema kwamba Mbappe alikuwa na tatizo la jino na hata mazoezi hakufanya vizuri na alimtoa na kumuingiza Endrick ili kuepusha matatizo zaidi.
Real Madrid kwa sasa inapigania mataji matatu, Jumatano iliyopita ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Real Sociedad katika nusu fainali ya Copa del Rey na keshokutwa Jumanne itacheza mechi ya hatua ya 16 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid.

The post Ancelotti: Ni pigo kubwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/ancelotti-ni-pigo-kubwa/feed/ 0
Ancelotti hana hofu na Mbappe https://www.greensports.co.tz/2024/08/25/ancelotti-hana-hofu-na-mbappe/ https://www.greensports.co.tz/2024/08/25/ancelotti-hana-hofu-na-mbappe/#respond Sun, 25 Aug 2024 20:18:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11815 Madrid, HispaniaKocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema kitendo cha mshambuliaji wake mpya, Kylian Mbappe kushindwa kuzifumania nyavu katika mechi mbili mfululizo za La Liga hakimsumbui.Mbappe amejiunga na Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitano huu ukiwa msimu wake wa kwanza na ingawa mambo hayajawa mazuri kwenye La Liga, tayari ameifungia timu hiyo bao katika […]

The post Ancelotti hana hofu na Mbappe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema kitendo cha mshambuliaji wake mpya, Kylian Mbappe kushindwa kuzifumania nyavu katika mechi mbili mfululizo za La Liga hakimsumbui.
Mbappe amejiunga na Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitano huu ukiwa msimu wake wa kwanza na ingawa mambo hayajawa mazuri kwenye La Liga, tayari ameifungia timu hiyo bao katika mechi ya Uefa Super Cup dhidi ya Atalanta mapema mwezi huu.
Usajili wa Mbappe Real Madrid ulikuwa gumzo duniani kote lakini bado hajaanza kutema cheche zake na Jumapili katika mechi na Real Valladolid licha ya Real Madrid kushinda kwa 3-0 lakini Mbappe alitupwa benchi dakika ya 86.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Ancelotti alipingana na hoja kwamba Mbappe anashindwa kufunga kwa sababu anacheza nafasi ya mshambuliaji wa kati badala ya pembeni.
“Hapana, sidhani kama kuna hilo tatizo hata kidogo, Mbappe ni mshambuliaji wa kipekee, ana kasi na anakwenda vizuri hata asipokuwa na mpira,” alisema Ancelotti.
Akifafanua zaidi kuhusu Mbappe katika mechi na Valladolid, Ancelotti alisema mshambuliaji huyo alipata nafasi tatu na anaamini katika nafasi hizo ataweza kufunga kama ambavyo amekuwa akifunga mara zote na hadhani kama ili kufunga ni lazima acheze kushoto au kulia.
Katika hatua nyingine, Ancelotti pia alimpongeza Endrick ambaye amesaini timu hiyo msimu huu mara baada ya kufikisha miaka 18.
Alisema kwamba mchezaji huyo ni hazina na akiwa kwenye lango ameonesha uwezo wake wote, anamiliki vizuri mpira na anapiga mashuti vizuri.

The post Ancelotti hana hofu na Mbappe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/08/25/ancelotti-hana-hofu-na-mbappe/feed/ 0
Ancelotti ataka wachezaji Madrid wale bata https://www.greensports.co.tz/2024/08/25/ancelotti-ataka-wachezaji-madrid-wale-bata/ https://www.greensports.co.tz/2024/08/25/ancelotti-ataka-wachezaji-madrid-wale-bata/#respond Sat, 24 Aug 2024 21:07:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11804 Madrid, HispaniaKocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema ratiba ngumu ya msimu huu inawafanya wafikirie kuwapa muda wa mapumziko mchezaji mmoja mmoja ili kuwaepusha na uchovu uliopitiliza.Real Madrid ilizianza mbio za msimu wa 2024-25 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Atalanta katika Uefa Super Cup kabla ya kuivaa Mallorca katika mechi ya kwanza ya […]

The post Ancelotti ataka wachezaji Madrid wale bata first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema ratiba ngumu ya msimu huu inawafanya wafikirie kuwapa muda wa mapumziko mchezaji mmoja mmoja ili kuwaepusha na uchovu uliopitiliza.
Real Madrid ilizianza mbio za msimu wa 2024-25 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Atalanta katika Uefa Super Cup kabla ya kuivaa Mallorca katika mechi ya kwanza ya La Liga.
Wachezaji wa Real Madrid katika msimu huu wanatarajia kupambana kuwania mataji saba kuanzia La Liga, Kombe la Mfalme, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uefa Super Cup, Spanish Super Cup, Kombe la Dunia la Klabu na mashindano mapya ya kuwania taji la mabara.
Michuano ya Kombe la Dunia la Klabu yailiyofanyiwa mabadiliko yanatarajia kuanza majira ya kiangazi nchini Marekani ingawa siku maalum ya kuanza michuano hiyo pamoja na viwanja yote hayo bado hayajawekwa wazi na hiyo maana yake ni kwamba msimu huu kwa Real Madrid utafikia ukomo Juni 2025.

“Kuna mambo tunayafanyia tathmini, wachezaji wanahitaji kupumzika, wanahitaji kulfurahia maisha (kula bata), tunafikiria wakati msimu ukiendelea tunaweza kumpa mchezaji mmoja mmoja wiki ya kupumzika,” alisema Ancelotti.


Akifafanua zaidi Ancelotti alisema mchezaji anaweza asionekane kwenye mechi kwa wiki moja na akapewa muda huo ili apumzike na familia yake na kwamba jambo hilo litafanywa zaidi kwa wachezaji walio kwenye timu za taifa na ushauri wa jopo la madaktari wa timu utazingatiwa.
Ancelotti katika hilo alimtolea mfano mshambuliaji wa timu hiyo ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Brazil, Vinicius Junior ambaye alisema kwa kalenda ya mchezaji huyo ni muhimu akawa na muda wa mapumziko katikati ya msimu.

The post Ancelotti ataka wachezaji Madrid wale bata first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/08/25/ancelotti-ataka-wachezaji-madrid-wale-bata/feed/ 0
Ancelotti akataa kumhusisha Mbappe na sare https://www.greensports.co.tz/2024/02/19/ancelotti-akataa-kumhusisha-mbappe-na-sare/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/19/ancelotti-akataa-kumhusisha-mbappe-na-sare/#respond Mon, 19 Feb 2024 07:01:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9797 Madrid, HispaniaKocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amekataa kumhusisha mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe na matokeo ya sare ya bao 1-1 ambayo timu hiyo imeyapata mbele ya Rayo Vallecano.Real Madrid inayoshika usukani katika Ligi Kuu Hispania au La Liga, sare hiyo imefanya tofauti yake na Girona inayoshika nafasi ya pili kuwa pointi sita huku Real […]

The post Ancelotti akataa kumhusisha Mbappe na sare first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amekataa kumhusisha mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe na matokeo ya sare ya bao 1-1 ambayo timu hiyo imeyapata mbele ya Rayo Vallecano.
Real Madrid inayoshika usukani katika Ligi Kuu Hispania au La Liga, sare hiyo imefanya tofauti yake na Girona inayoshika nafasi ya pili kuwa pointi sita huku Real Madrid ikiwa mbele kwa mchezo mmoja.
Katika mchezo huo, Real Madrid iliyokuwa ugenini ilikuwa ya kwanza kupata bao la dakika ya tatu lililofungwa na Joselu na Vallecano kusawazisha dakika ya 27 kwa penalti iliyotiwa kimiani na mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid, Raul de Tomas.
Baada ya mechi hiyo, Ancelotti aliulizwa iwapo habari ya usajili wa Mbappe Real Madrid ilichangia kuivuruga timu yake na kusababisha matokeo hayo kwa kuwafanya wachezaji wakose umakini, kocha huyo alijibu kwa kuhoji, “Ni lini hasa tumeanza kukosa umakini?”
“Tulianza mechi vizuri na kufunga bao la mapema, baada ya Rayo kupata penalti mchezo ulibadilika, ushindani ulizidi, ilikuwa ni kupambana zaidi na mechi kusimama mara kwa mara, ni matokeo ya sare ambayo hatuyafurahii lakini tutaendelea kupambana, tumejiweka pazuri,” alisema Ancelotti.

“Tunatakiwa kushinda kila mechi lakini ili ushinde taji la ligi ni muhimu pale unapokosa ushindi usipoteze kabisa mchezo, kuna wakati sare inaumiza lakini kwa upande mwingine inaweza kuwa ni hatua nzuri ya kutuwezesha kubeba taji la ligi,” alisema Ancelotti.


Katika mechi hiyo, Real Madrid pia ilipata pigo baada ya mchezaji wake Carvajal kulimwa kadi nyekundu katika dakika za majeruhi kwa kumchezea rafu, Eduardo Camavinga.
Matokeo ya mechi za La Liga jana Jumapili
Rayo Vallecano 1-1 Real Madrid
Granada 1-1 Almería
Mallorca 1-2 Real Sociedad
Real Betis 0-0 Alaves

The post Ancelotti akataa kumhusisha Mbappe na sare first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/19/ancelotti-akataa-kumhusisha-mbappe-na-sare/feed/ 0
Ancelotti afuta mpango wa kuinoa Brazil https://www.greensports.co.tz/2023/12/30/ancelotti-afuta-mpango-wa-kuinoa-brazil/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/30/ancelotti-afuta-mpango-wa-kuinoa-brazil/#respond Sat, 30 Dec 2023 20:10:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9083 Madrid, HispaniaKocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti hatimaye amedhihirisha kwamba hana mpango wa kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Brazil baada ya kuongeza mkataba na Real Madrid.Ancelotti alihusishwa na mipango ya kusaini mkataba kuinoa timu ya Brazil lakini habari zilizopatikana leo Jumamosi ni kwamba kocha huyo ameongeza mkataba na Real Madrid hadi mwaka 2026.“Real […]

The post Ancelotti afuta mpango wa kuinoa Brazil first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti hatimaye amedhihirisha kwamba hana mpango wa kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Brazil baada ya kuongeza mkataba na Real Madrid.
Ancelotti alihusishwa na mipango ya kusaini mkataba kuinoa timu ya Brazil lakini habari zilizopatikana leo Jumamosi ni kwamba kocha huyo ameongeza mkataba na Real Madrid hadi mwaka 2026.
“Real Madrid na Carlo Ancelotti wamefikia makubaliano ya kuongeza mkataba hadi Juni 30, 2026,” ilieleza taarifa ya Real Madrid.
Julai mwaka huu ilielezwa kwamba kocha huyo mwenye umri wa miaka 64 alikuwa anaandaliwa kuwa kocha wa kwanza wa kigeni kuinoa timu ya Brazil lakini hatua yake ya kuongeza mkataba inalifanya suala hilo kuwa gumu au ambalo halina nafasi.
Katika kumuandalia Ancelotti nafasi hiyo, Shirikisho la Soka Brazil (CBF) lilimtangaza Fernando Diniz kuwa kocha wa muda huku matumaini yakiwa ni kumsubiri Ancelotti achukue jukumu hilo kwenye fainali za Copa America 2024.
Inadaiwa kwamba Ednaldo Rodriguez ambaye alikuwa rais wa CBF wakati huo alifanya mazungumzo kadhaa na Ancelotti ambaye naye aliwahi kunukuliwa akisema kazi ya kuinoa Real Madrid itakuwa ya mwisho kwake kwenye kazi ya ukocha wa soka.
Hoja ya Rodriguez kumtaka Ancelotti ainoe timu ya taifa ya Brazil hata hivyo ilikumbana na upinzani kwa kilichodaiwa kwamba kumchukua kocha kutoka nje ya Brazil ni kuwadharau makocha wazawa.
Hoja nyingine zilidai kwamba Ancelotti haujui utamaduni wa soka la Brazil na hivyo isingekuwa sahihi kumpa kibarua cha kuinoa timu hiyo.
Mipango ya kumpa kibarua Ancelotti imechangiwa na matokeo yasiyopendeza ya timu ya taifa ya Brazil hasa kwenye fainali za Kombe la Dunia za 2022 na ikaonekana umuhimu wa kutafuta kocha kutoka nje ya taifa hilo na ndipo jina la Ancelotti lilipochomoza.

The post Ancelotti afuta mpango wa kuinoa Brazil first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/30/ancelotti-afuta-mpango-wa-kuinoa-brazil/feed/ 0
Ancelotti kuanza kibarua Brazil 2024 https://www.greensports.co.tz/2023/07/06/ancelotti-kuanza-kibarua-brazil-2024/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/06/ancelotti-kuanza-kibarua-brazil-2024/#respond Thu, 06 Jul 2023 20:52:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6836 Rio de Janeiro, BrazilRais wa Shirikisho la Soka Brazil, Ednaldo Rodrigues amesema kwamba kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti atakabidhiwa majukumu ya kuinoa timu ya Taifa ya Brazil mwaka 2024.Brazil ambao ni mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia wanaamini kocha huyo Mtaliano atakuwa na timu hiyo kwenye fainali za Copa America Juni mwakani.Akimzungumzia kocha […]

The post Ancelotti kuanza kibarua Brazil 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Rais wa Shirikisho la Soka Brazil, Ednaldo Rodrigues amesema kwamba kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti atakabidhiwa majukumu ya kuinoa timu ya Taifa ya Brazil mwaka 2024.
Brazil ambao ni mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia wanaamini kocha huyo Mtaliano atakuwa na timu hiyo kwenye fainali za Copa America Juni mwakani.
Akimzungumzia kocha wa sasa wa timu hiyo, Fernando Diniz, Rodrigues alisema kocha huyo atafanya kazi yake hadi mwaka 2024 wakati huo huo akiendelea na majukumu yake ya sasa katika klabu ya Fluminense.
Tangu kujiuzulu kwa Tite baada ya Brazil kutolewa katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia Desemba mwaka jana, timu hiyo haijawa na kocha wa kudumu ambapo hivi karibuni imekuwa ikinolewa na Ramon Menezes katika mechi za kirafiki.
Ancelotti ambaye mkataba wake na Real Madrid unafikia ukomo Juni 2024, kama mpango wa kuinoa timu hiyo utafanikiwa atakuwa kocha wa kwanza asiye raia wa Brazil kuinoa timu hiyo tangu mwaka 1965.
Na ingawa kiongozi mkuu wa soka la Brazil amejiaminisha kuhusu Ancelotti lakini hadi sasa hakujawa na taarifa yoyote rasmi kutoka kwa kocha huyo au klabu ya Real Madrid kuhusu mpango huo japo habari hiyo imekuwa ikizungumzwa kwa takriban miezi sita sasa.

The post Ancelotti kuanza kibarua Brazil 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/06/ancelotti-kuanza-kibarua-brazil-2024/feed/ 0
Brazil yamkomalia Ancelotti https://www.greensports.co.tz/2023/05/29/brazil-yamkomalia-ancelotti/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/29/brazil-yamkomalia-ancelotti/#respond Mon, 29 May 2023 18:06:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6354 Rio de Janeiro, Brazi;Brazil bado ina matumaini ya kumshawishi kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti ili akabidhiwe jukumu la kuinoa timu ya taifa hilo inayoongoza kwa kubeba Kombe la Dunia mara tano.Ancelotti alianza kuhusishwa na Brazil Desemba mwaka jana mara baada ya timu hiyo kukwama katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia ikitolewa […]

The post Brazil yamkomalia Ancelotti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazi;
Brazil bado ina matumaini ya kumshawishi kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti ili akabidhiwe jukumu la kuinoa timu ya taifa hilo inayoongoza kwa kubeba Kombe la Dunia mara tano.
Ancelotti alianza kuhusishwa na Brazil Desemba mwaka jana mara baada ya timu hiyo kukwama katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia ikitolewa kwa mikwaju ya penalti na Croatia.
Baada ya Brazil kutolewa kwenye michuano hiyo iliyofanyika Qatar, aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Tite aling’atuka na ndipo jina la Ancelotti lilipochomoza ikiaminika kuwa anafaa kupewa jukumu hilo.
Ancelotti hata hivyo alijiweka kando na mjadala huo ingawa nchini Brazil nako kukaibuka mjadala wa kama ni sahihi timu hiyo kunolewa na kocha ambaye si raia mzawa wa Brazil.
Katika mjadala huo wapo wanaodhani huu ni wakati sahihi kwa Brazil kuwa na kocha wa kigeni baada ya mambo kutokuwa mazuri ingawa pia wapo wanaoamini si sahihi kufanya hivyo kwani timu hiyo inahitaji Mbarazil anayelijua vizuri soka la nchi hiyo na mahitaji yake.
Ancelotti hata hivyo ameonekana kutoichangamkia kazi ya kuinoa Brazil na hivi karibuni baada ya Real Madrid kutolewa katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, alinukuliwa akisema kwamba amehakikishiwa kuwa ataendelea kuinoa klabu hiyo iliyotwaa taji hilo msimu uliopita.
Tangu kuondoka kwa Tite, Brazil bado haijachagua kocha wa kudumu huku kukiwa na habari kwamba mabosi wa shirikisho la soka nchini humo yaani CBF safari hii wanataka kumpa kazi kocha kutoka nje ya taifa hilo.

The post Brazil yamkomalia Ancelotti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/29/brazil-yamkomalia-ancelotti/feed/ 0