Amorim - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 03 Apr 2025 18:53:01 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Amorim - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Amorim: Fernandes haondoki https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/amorim-fernandes-haondoki/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/amorim-fernandes-haondoki/#respond Tue, 01 Apr 2025 19:31:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13186 Manchester, EnglandKocha wa Man United, Ruben Amorim amesema kwamba hatomruhusu kiungo wake nyota, Bruno Fernandes kuihama timu hiyo wakati wa usajili wa dirisha kubwa la Majira ya Kiangazi.Kauli hiyo imekuja huku kukiwa na habari kwamba Amorim yuko katika mkakati mzito wa kukisuka kikosi chake akijiandaa kwa msimu ujao ambao anatarajia kuuanza tangu mwanzo.Wakati Amorim akiwa […]

The post Amorim: Fernandes haondoki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man United, Ruben Amorim amesema kwamba hatomruhusu kiungo wake nyota, Bruno Fernandes kuihama timu hiyo wakati wa usajili wa dirisha kubwa la Majira ya Kiangazi.
Kauli hiyo imekuja huku kukiwa na habari kwamba Amorim yuko katika mkakati mzito wa kukisuka kikosi chake akijiandaa kwa msimu ujao ambao anatarajia kuuanza tangu mwanzo.
Wakati Amorim akiwa na mpango huo, Fernandes amekuwa akitajwa katika mipango ya kuhamia Real Madrid lakini kocha wake amemwambia wazi kiungo huyo Mreno kuwa yumo katika mipango ya baadaye Man United.
Amorim alitoa kauli hiyo Jumatatu kwenye mkutano na waandishi wa habari alipoulizwa kuhusu habari za Fernandes kuhama ambapo alijibu kwa kifupi, “Hapana, hicho kitu hakitatokea.”
Kocha huyo alifafanua kuwa Fernandes hatokwenda popote kwa sababu tayari ameshamwambia kuhusu jambo hilo.
Msimu huu umekuwa wa hovyo kwa Man United ikiwa nafasi ya 13 kwenye Ligi Kuu England (EPL) ngawa Fernandes ameendelea kuonesha ubora wake akiwa ameifungia timu hiyo mabao 16 na kutoa asisti 16 katika mashindano yote.
Fernandes, 30, alijiunga na Man United mwaka 2020 na kwa sasa mkataba wake na klabu hiyo unafikia ukomo mwaka 2027 ingawa kuna kipengele kinachompa nafasi ya kuongeza mwaka mmoja.

The post Amorim: Fernandes haondoki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/amorim-fernandes-haondoki/feed/ 0
Amorim: Sitopewa muda mrefu kama Arteta https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/amorim-sitopewa-muda-mrefu-kama-arteta/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/amorim-sitopewa-muda-mrefu-kama-arteta/#respond Sat, 08 Mar 2025 11:21:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13093 Manchester, EnglandKocha wa Man United, Ruben Amorim amesema uongozi wa klabu hiyo hautompa muda wa kutosha kuifanyia maboresho timu kama ambavyo klabu ya Arsenal imempa kocha wao, Mikel Arteta.Arteta alikabidhiwa rasmi majukumu ya kuinoa Arsenal Desemba 2019 akichukua nafasi ya Unai Emery na kuanzia kipindi hicho hadi sasa ameweza kuifanya timu hiyo kuwa miongoni mwa […]

The post Amorim: Sitopewa muda mrefu kama Arteta first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Manchester, England
Kocha wa Man United, Ruben Amorim amesema uongozi wa klabu hiyo hautompa muda wa kutosha kuifanyia maboresho timu kama ambavyo klabu ya Arsenal imempa kocha wao, Mikel Arteta.
Arteta alikabidhiwa rasmi majukumu ya kuinoa Arsenal Desemba 2019 akichukua nafasi ya Unai Emery na kuanzia kipindi hicho hadi sasa ameweza kuifanya timu hiyo kuwa miongoni mwa timu tishio katika mbio za kusaka mataji.
Kwa upande wake Amorim ambaye huu ni msimu wake wa kwanza Man United, haamini kama na yeye atapata muda kama wa Arteta ambaye matunda ya kazi yake yameanza kuonekana.
Tangu akabidhiwe jukumu la kuinoa Arsenal, Arteta ameiwezesha timu hiyo kubeba taji la FA mwaka 2020 lakini ameendelea kuhaha kulisaka taji la Ligi Kuu England na ingawa hajafanikiwa, ubora wa kikosi chake unaonekana.
Arteta pia tangu ajiunge na Arsenal timu ambayo aliwahi kuichezea miaka ya nyuma, imemchukua misimu mitatu kuirudisha timu hiyo katika fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Sitoweza kupewa muda kama ambao Arteta amekuwa nao, naiona Arsenal ni klabu tofauti kwa mapana na namna kwa ambavyo Arteta anakabiliana na mambo inatia hamasa kwa kila mtu,” alisema Amorim.

Arsenal, kesho Jumapili itakuwa ugenini Old Trafford kuikabili Man United, timu ambayo inakabiliwa na janga la wachezaji wao tegemeo kuwa majeruhi, wachezaji hao ni Mason Mount, Luke Shaw na Lisandro Martinez.
Kwa upande mwingine Arsenal imeonekana kuwa moto kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Jumanne iliyopita iliinyuka PSV Eindhoven mabao 7-1 wakati siku mbili baadaye, Man United iliambulia sare ya bao 1-1 mbele ya Real Sociedad katika Europa Ligi.

The post Amorim: Sitopewa muda mrefu kama Arteta first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/amorim-sitopewa-muda-mrefu-kama-arteta/feed/ 0
Amorim awaambia wachezaji Man United wajiandae kuondoka https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/amorim-awaambia-wachezaji-man-united-wajiandae-kuondoka/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/amorim-awaambia-wachezaji-man-united-wajiandae-kuondoka/#respond Sun, 02 Mar 2025 09:09:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13072 Manchester, EnglandKocha wa Man United, Ruben Amorim amewaambia wazi wachezaji wake kuwa wengi wao watalazimika kuachwa mwishoni mwa msimu katika mpango wa kuipangua na kuisuka upya timu hiyo.Mazingira magumu ya kifedha ya klabu hiyo kwa kipindi hiki yanamaanisha kwamba ili waweze kusajili wachezaji wapya lazima wapate pesa baada ya kuuza wachezaji walionao sasa.Katika hilo, Amorim […]

The post Amorim awaambia wachezaji Man United wajiandae kuondoka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man United, Ruben Amorim amewaambia wazi wachezaji wake kuwa wengi wao watalazimika kuachwa mwishoni mwa msimu katika mpango wa kuipangua na kuisuka upya timu hiyo.
Mazingira magumu ya kifedha ya klabu hiyo kwa kipindi hiki yanamaanisha kwamba ili waweze kusajili wachezaji wapya lazima wapate pesa baada ya kuuza wachezaji walionao sasa.
Katika hilo, Amorim ameweka wazi kuwa atalazimika kuwa mkweli kwa wachezaji wake kama anaona wanafaa kuendelea kuwa nao katika klabu hiyo ya Old Trafford.
Amorim hata hivyo alisema kwamba kwa sasa hawawezi kuzungumzia suala la wachezaji kuachwa kwa kuwa bado wana mechi nyingi za kucheza lakini jambo hilo lipo wazi.
Kocha huyo pia alifafanua kwamba anadhani jambo hilo ni muhimu kwa sababu kila mmoja anafahamu katika soka kuna wakati unabaki na kuna wakati unalazimika kuondoka.

“Unapokuwa mkweli kwa mwenzako hapo anaweza kukubaliana na hali, mwanzoni ni vigumu lakini wataelewa, kwa hiyo nipo wazi na mkweli kwa wachezaji wangu na tayari wanafahamu kwamba kuna watalaolazimika kuondoka mwishoni mwa msimu,” alisema Amorim.


Ukosefu wa fedha unadaiwa kumfanya Amorim, kocha mwenye umri wa miaka 40 aione kazi yake kuwa ngumu na sasa amejikuta njia panda kutokana na ukubwa wa majukumu aliyonayo.
Amorim ambaye alijiunga na Man United Novemba mwaka jana akitokea Sporting CP ya Ureno hata hivyo alisema kwamba alitambua ukubwa wa majukumu yanayomkabili na ugumu alionao katika kuweka mambo sawa.

The post Amorim awaambia wachezaji Man United wajiandae kuondoka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/amorim-awaambia-wachezaji-man-united-wajiandae-kuondoka/feed/ 0
Amorim: Lazima tuuze wachezaji https://www.greensports.co.tz/2025/02/15/amorim-lazima-tuuze-wachezaji/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/15/amorim-lazima-tuuze-wachezaji/#respond Sat, 15 Feb 2025 11:56:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13015 Mancheste, EnglandKocha wa Man United, Ruben Amorim amesema klabu yao italazimika kuuza wachezaji kama watataka kununua mchezaji yeyote wakati wa dirisha kubwa la usajili Majira ya Kiangazi.Mambo hayaendi vizuri kwa Man United katika Ligi Kuu England (EPL) msimu huu na upo uwezekano mkubwa wa timu hiyo kutoshiriki mashindano yoyote ya klabu barani Ulaya msimu ujao.Hali […]

The post Amorim: Lazima tuuze wachezaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Mancheste, England
Kocha wa Man United, Ruben Amorim amesema klabu yao italazimika kuuza wachezaji kama watataka kununua mchezaji yeyote wakati wa dirisha kubwa la usajili Majira ya Kiangazi.
Mambo hayaendi vizuri kwa Man United katika Ligi Kuu England (EPL) msimu huu na upo uwezekano mkubwa wa timu hiyo kutoshiriki mashindano yoyote ya klabu barani Ulaya msimu ujao.
Hali hiyo hata hivyo haikuwafanya kujiimarisha kwa usajili mkubwa katika dirisha dogo la Januari badala yake walitumia Pauni 25 milioni tu kumsajili beki Patrick Dorgu.
Habari za ndani zinadai kwamba baada ya kupata hasara ya mamilioni ya Pauni katika miaka ya hivi karibuni, uimara wa klabu kuichumi unawalazimu kujibana katika matumizi.
Alipoulizwa kuhusu mpango wa kukiimarisha kikosi na suala zima la kubana matumizi, Amorim alisema kinachotakiwa kufanyika ni kuuza wachezaji ili kuweza kununua wengine.
Amorim hata hivyo alisisitiza kwamba wanachokiangalia kwa sasa ni namna ya kushinda mechi zilizo mbele yao na baada ya hapo akili yao itaanza kuangalia nini cha kufanya kwenye usajili.
Mpango mwingine uliopo katika klabu hiyo ni kuboresha timu za vijana ili kuwa na idadi ya kutosha ya wachezaji ambao baadaye watacheza kwenye kikosi cha kwanza au watauzwa badala ya kutegemea kununua wachezaji bei mbaya kutoka klabu nyingine.
Dalili njema zilizoanza kuonekana katika mpango huo ni kwenye kikosi cha Man United cha vijana chini ya miaka 18 ambacho Jumatano kilifuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la FA kwa vijana baada ya kuichapa Chelsea mabao 5-1.
Katika mechi hiyo nyota anayeonekana kuwa na kipaji Chido Obi alionesha uwezo wake baada ya kufunga mabao matatu (hat trick) peke yake.

The post Amorim: Lazima tuuze wachezaji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/15/amorim-lazima-tuuze-wachezaji/feed/ 0
Amorim atetea usajili mdogo Man United https://www.greensports.co.tz/2025/02/06/amorim-atetea-usajili-mdogo-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/06/amorim-atetea-usajili-mdogo-man-united/#respond Thu, 06 Feb 2025 19:29:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12989 Manchester, EnglandKocha wa Man United, Ruben Amorim amesema uamuzi wa kutosajili wachezaji zaidi katika dirisha dogo la Januari ni wake licha ya kwamba utawaweka katika mazingira magumu.Hadi dirisha dogo la usajili linafungwa mapema wiki hii, Man United imefanya usajili wa wachezaji wiwili tu, beki wa kushoto Patrick Dorgu, 20, kutoka Lecce ya Italia na beki […]

The post Amorim atetea usajili mdogo Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man United, Ruben Amorim amesema uamuzi wa kutosajili wachezaji zaidi katika dirisha dogo la Januari ni wake licha ya kwamba utawaweka katika mazingira magumu.
Hadi dirisha dogo la usajili linafungwa mapema wiki hii, Man United imefanya usajili wa wachezaji wiwili tu, beki wa kushoto Patrick Dorgu, 20, kutoka Lecce ya Italia na beki wa kati Ayden Heaven, 18, kutoka Arsenal.
Baada ya kumtoa kwa mkopo Marcus RAshford aliyejiunga na Aston Villa na kumruhusu Antony kujiunga na Real Betis, ilitarajiwa timu hiyo pia ingejiimarisha kwa kusajili japo mshambuliaji mmoja.
Amorim hata hivyo baada ya dirisha la usajili kufungwa alisema kwamba walifanya kila wawezalo ili kuimarisha kikosi kwa kusajili zaidi lakini wameshindwa kuongeza wachezaji wengine.
“Tumechukua uamuzi mgumu lakini ni kwa sababu tunahitaji kitu tofauti katika timu, hadhi na sifa tofauti, ulikuwa ni uamuzi wangu kufanya hivyo,” alisema Amorim.
Kocha huyo alifafanua kwamba anachokiona ni kuwa klabu inajipa muda ingawa wanajua mahitaji ya wakati huu ya timu lakini hakuna anayetaka kufanya makosa ya siku za nyuma.

“Katika kipindi cha usajili majira ya kiangazi tutaona itakavyokuwa, lakini kama nilivyosema kwa hakika tunakuwa makini katika usajili kwa sababu kuna makosa tuliyofanya siku za nyuma,” alisema Amorim.


Keshokutwa Ijumaa, Man United itaumana na Leicester City kwenye dimba la nyumbani Old Trafford katika mechi ya raundi ya nne ya Kombe la FA, mechi ambayo huenda wachezaji wapya, Dorgu na Heaven watapata nafasi ya kuiwakilisha timu yao mpya kwa mara ya kwanza.

The post Amorim atetea usajili mdogo Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/06/amorim-atetea-usajili-mdogo-man-united/feed/ 0
Amorim: Bora mzee wa miaka 63 kuliko Rashford https://www.greensports.co.tz/2025/01/27/amorim-bora-mzee-wa-miaka-63-kuliko-rashford/ https://www.greensports.co.tz/2025/01/27/amorim-bora-mzee-wa-miaka-63-kuliko-rashford/#respond Mon, 27 Jan 2025 20:40:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12937 Manchester, EnglandKocha wa Man United, Ruben Amorim amesema kwamba anadhani ni afadhali kumpa nafasi kwenye benchi la timu hiyo mtu mwenye umri wa miaka 63 badala ya Marcus Rashford.Amorim ameitetea hoja yake hiyo kwa madai kwamba anachokiona kwa mchezaji huyo ni kwamba hajaonesha kujituma kwa kiwango cha juu kila siku.Rashford amekuwa akitengwa katika kikosi cha […]

The post Amorim: Bora mzee wa miaka 63 kuliko Rashford first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man United, Ruben Amorim amesema kwamba anadhani ni afadhali kumpa nafasi kwenye benchi la timu hiyo mtu mwenye umri wa miaka 63 badala ya Marcus Rashford.
Amorim ameitetea hoja yake hiyo kwa madai kwamba anachokiona kwa mchezaji huyo ni kwamba hajaonesha kujituma kwa kiwango cha juu kila siku.
Rashford amekuwa akitengwa katika kikosi cha Man United kwa takriban wiki sita sasa na Jumapili iliyopita aliachwa kwenye kikosi cha timu hiyo kilichocheza na Fulham na kutoka na ushindi wa bao 1-0 katika Ligi Kuu England (EPL).
Rashford amejikuta katika kipindi kigumu na haitoshangaza akaihama timu hiyo katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili ambalo litafungwa rasmi Februari 3, 2025.

“Wakati wote sababu imeendelea kuwa hiyo hiyo, mazoezi ya kujituma kwa namna ambayo nawaona wachezaji wakifanya kwa maisha yao, ni jambo la kila siku, ni kwa kila hatua inayohusika,” alisema Amorim.


Amorim alisisitiza kwamba kama mambo hayatabadilika na yeye hatobadilika, hali itabaki kuwa hivyo hivyo kwa kila mchezaji ambaye hatajitoa kwa kiwango cha juu na kufanya kwa usahihi mambo ambayo yanawahusu wachezaji kwa kila siku.
Katika hatua nyingine Amorim alisema anaweza pia kumpa nafasi kwenye benchi kocha wa makipa, Jorge Vital kuliko nafasi hiyo kumpa mchezaji ambaye hajitumi kwa kiwango cha juu kila siku.


Wakati hali ikiwa hivyo, katika siku za karibuni, Rashford amekuwa akihusishwa na timu kadhaa zikiwamo AC Milan ya Italia ingawa mpango huo unaonekana kukwama baada ya timu hiyo kumsajili Kylie Walker.
Barca nayo ilidaiwa kuwa katika mpango wa kumsajili Rashford kwa mkopo lakini mpango huo utategemea kama baadhi ya wachezaji wataachwa na yeye kupata nafasi.
Timu nyingine ambazo zimewahi kuhusishwa na mipango ya kutaka kumsajili Rashford ni PSG ya Ufaransa na Napoli ya Italia.

The post Amorim: Bora mzee wa miaka 63 kuliko Rashford first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/01/27/amorim-bora-mzee-wa-miaka-63-kuliko-rashford/feed/ 0
Amorim akiri mambo magumu https://www.greensports.co.tz/2024/12/23/amorim-akiri-mambo-magumu/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/23/amorim-akiri-mambo-magumu/#respond Mon, 23 Dec 2024 08:58:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12483 Manchester, EnglandKocha wa Man United, Ruben Amorim amesema timu yake ipo katika kipindi kigumu baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Bournemouth jana Jumapili ikiwa nyumbani Old Trafford.Man United sasa inakuwa imepoteza mechi mbili mfululizo baada ya kulala kwa mabao 4-3 mbele ya Tottenham Hotspur Alhamisi iliyopita katika Kombe la Carabao.Kipigo dhidi ya Bournemouth pia kinakuwa […]

The post Amorim akiri mambo magumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Manchester, England
Kocha wa Man United, Ruben Amorim amesema timu yake ipo katika kipindi kigumu baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Bournemouth jana Jumapili ikiwa nyumbani Old Trafford.
Man United sasa inakuwa imepoteza mechi mbili mfululizo baada ya kulala kwa mabao 4-3 mbele ya Tottenham Hotspur Alhamisi iliyopita katika Kombe la Carabao.
Kipigo dhidi ya Bournemouth pia kinakuwa kipigo chao cha pili mfululizo kwenye dimba la Old Trafford baada ya hapo kabla kulala kwa mabao 3-2 mbele ya Nottingham Forest.
Amorim alifafanua kwamba wapo katika kipindi kigumu lakini ni lazima kukabiliana nacho na kujiandaa kwa ajili ya mechi inayofuata.

“Ni jukumu langu kuiandaa timu, kweli tunahitaji kuwa bora, kwa sasa kila kitu kigumu kwetu, kwa klabu ya Manchester United kufungwa mabao 3-0 nyumbani ni jambo gumu kwa kila mtu, ukweli ni kwamba hata mashabiki inawaumiza na kuwachosha,” alisema Amorim.

Baada ya kipigo kwenye mechi yao dhidi ya Spurs, Amorim alionekana mwenye kuwalaumu wachezaji wake kwa namna walivyokuwa na mipango mibaya ya kuutawala mchezo baada ya kufungwa mabao mawili katika dakika nane za mwanzo za kipindi cha pili.
Hali ilikuwa inayofanana na hiyo katika mechi yao na Bournemouth ambao waliwafunga Man United mabao mawili katika dakika tatu za mwanzo za kipindi cha pili.

The post Amorim akiri mambo magumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/23/amorim-akiri-mambo-magumu/feed/ 0
Amorim kocha mkuu Man United https://www.greensports.co.tz/2024/11/02/amorim-kocha-mkuu-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2024/11/02/amorim-kocha-mkuu-man-united/#respond Sat, 02 Nov 2024 09:29:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12219 Manchester, EnglandKlabu ya Manchester United hatimaye imemteua Ruben Amorim (pichani) kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo akichukua nafasi iliyoachwa na Erik ten Hag aliyetimuliwa.Amorim mwenye umri wa miaka 39 ambaye anatokea Sporting Lisbon ya Ureno, amesaini mkataba unaofikia ukomo Juni 2027 na anatarajia kutua rasmi Old Trafford yalipo makazi ya Man United Novemba 11.Kwa […]

The post Amorim kocha mkuu Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Manchester, England
Klabu ya Manchester United hatimaye imemteua Ruben Amorim (pichani) kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo akichukua nafasi iliyoachwa na Erik ten Hag aliyetimuliwa.
Amorim mwenye umri wa miaka 39 ambaye anatokea Sporting Lisbon ya Ureno, amesaini mkataba unaofikia ukomo Juni 2027 na anatarajia kutua rasmi Old Trafford yalipo makazi ya Man United Novemba 11.
Kwa mantiki hiyo kocha wa muda, Ruud van Nistelrooy aliyekabidhiwa majukumu mara baada ya kutimuliwa kwa Ten Hag Jumatatu iliyopita, ataendelea kufanya kazi hiyo kwa mechi tatu zijazo.
Tetesi kuhusu Amorim zilianza kusikika katika siku za karibuni ambapo kocha mwingine ambaye jina lake pia lilikuwa likitajwa mara kadhaa ni Xavi Hernandez aliyekuwa akiinoa Barcelona.
Amorim anakuwa kocha wa sita wa kudumu wa Man United tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson, kocha ambaye aliinoa klabu hiyo kwa mafanikio kwa kipindi cha miaka 26 kabla ya kung’atuka mwaka 2013.
Sporting walithibitisha Amorim kwenda Man United na kubainisha kwamba klabu hiyo ilikubali kuuvunja mkataba wa sasa wa Amorim na kutoa kiasi cha fedha kama sehemu ya makubaliano hayo.
Amorim anatajwa kuwa mmoja wa makocha wenye umri mdogo ambaye ameanza kuheshimika katika soka Ulaya, mtihani wake wa kwanza katika Ligi Kuu England akiwa kwenye benchi la Man United utakuwa Novemba 24 dhidi ya Ipswich Town.

The post Amorim kocha mkuu Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/11/02/amorim-kocha-mkuu-man-united/feed/ 0