Ally Kamwe - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 21 Apr 2025 12:26:23 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ally Kamwe - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ally Kamwe atozwa faini milioni 5, wengine wafungiwa maisha https://www.greensports.co.tz/2025/04/19/ally-kamwe-atozwa-faini-milioni-5-wengine-wafungiwa-maisha/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/19/ally-kamwe-atozwa-faini-milioni-5-wengine-wafungiwa-maisha/#respond Sat, 19 Apr 2025 19:33:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13281 Na mwandishi wetuKamati ya Maadili ya TFF imemtoza faini ya Sh milioni 5, meneja habari na mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe baada ya kumkuta na hatia katika kosa la kuchochea umma.Maamuzi ya kamati hiyo ambayo yametangazwa leo Jumamosi, Aprili 19, 2025 kwenye taarifa ya TFF, pia yamemkosa na hatia meneja habari na mawasiliano wa Simba, […]

The post Ally Kamwe atozwa faini milioni 5, wengine wafungiwa maisha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kamati ya Maadili ya TFF imemtoza faini ya Sh milioni 5, meneja habari na mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe baada ya kumkuta na hatia katika kosa la kuchochea umma.
Maamuzi ya kamati hiyo ambayo yametangazwa leo Jumamosi, Aprili 19, 2025 kwenye taarifa ya TFF, pia yamemkosa na hatia meneja habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ambaye kama Kamwe wote walikuwa na tuhuma za kuchochea umma.
Wakati Ahmed alishitakiwa na Yanga kwa kosa hilo, Kamwe yeye alishitakiwa na kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi na amepewa onyo na kutakiwa kutofanya kosa hilo kwa kipindi cha miaka miwili.
Taarifa ya TFF haijataja makosa hayo yalifanyika lini lakini inaaminika ni baada ya kuahirishwa mechi baina ya Yanga na Simba ambayo awali ilipangwa kuchezwa Machi 8 mwaka huu.
Baada ya mechi ya Yanga na Simba ambayo ni ya Ligi Kuu NBC kuahirishwa, yaliibuka malumbano baina ya viongozi wa timu hizo kwa kila upande kumtupia lawama mwenzake.
Mwingine aliyekutwa na hatia ya kosa la kuchochea umma ni ofisa habari wa Kagera Sugar, Hamis Mazanzala ambaye pia ametozwa faini ya Sh milioni tano.
Mwingine aliyekumbana na adhabu hiyo ni mwanachama wa klabu ya Simba, Mohamed Hamis Mohamed ambaye kama walivyo wenzake, wote wameanza kutumikia adhabu hizo Aprili 16 mwaka huu.
Wafungiwa maisha
Katika hatua nyingine kamati ya maadili ya TFF imemfungia maisha kujihusisha na soka ndani na nje ya nchi, Shufaa Jumanne Nyamlani ambaye ni mtunza vifaa wa timu ya taifa ya Beach Soccer.
Shufaa ambaye pia alikuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Chama cha Soka Wilaya ya Temeke (Tefa) alishitakiwa na Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) kwa makosa matatu.
Makosa hayo ni kuchochea umma, kutoheshimu maamuzi ya vyombo halali vya usimamizi wa soka na kutaka kuiondoa madarakani kamati ya utendaji ya Tefa na licha ya kuitwa kwa ajili ya shauri lake lakini hakuitikia wito huo.
Mwingine aliyefungiwa maisha ni Salehe Mohamed Salehe aliyekuwa makamu mwenyekiti Tefa ambaye naye alikuwa akituhumiwa kwa makosa kama ya Shufaa lakini naye hakuitikia wito wa kwenda kusikiliza tuhuma zilizokuwa zikimkabili.

The post Ally Kamwe atozwa faini milioni 5, wengine wafungiwa maisha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/19/ally-kamwe-atozwa-faini-milioni-5-wengine-wafungiwa-maisha/feed/ 0
Mgunda amsamehe Ally Kamwe https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/mgunda-amsamehe-ally-kamwe/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/mgunda-amsamehe-ally-kamwe/#respond Tue, 30 May 2023 20:02:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6386 Na mwandishi wetuKocha Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amemsamehe ofisa habari wa Yanga, Ally Kamwe huku akidai kwamba anaamini Yanga ina uwezo wa kubeba Kombe la Shirikisho Afrika iwapo itajipanga vizuri.Yanga itakuwa ugenini Algeria Juni 3 kucheza mechi ya pili ya nusu fainali ambapo Mgunda amesema kwamba timu hiyo ina uwezo wa kushinda mechi hiyo […]

The post Mgunda amsamehe Ally Kamwe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amemsamehe ofisa habari wa Yanga, Ally Kamwe huku akidai kwamba anaamini Yanga ina uwezo wa kubeba Kombe la Shirikisho Afrika iwapo itajipanga vizuri.
Yanga itakuwa ugenini Algeria Juni 3 kucheza mechi ya pili ya nusu fainali ambapo Mgunda amesema kwamba timu hiyo ina uwezo wa kushinda mechi hiyo na kubeba taji licha ya kulala kwa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Mgunda ambaye ni kocha na mchezaji wa zamani wa Coastal Union amesema wanachotakiwa kufanya Yanga ni kuandaa mpango mkakati utakaowawezesha kufunga mabao mawili ya haraka ili kuwavuruga wenyeji wao na kuufanya mchezo kuwa rahisi.
“Bado Yanga ina nafasi ya kubeba ubingwa, naheshimu uwezo wao, naamini kuelekea mchezo wa marudiano itakuwa wameandaa mbinu mbadala itakayowapa matokeo chanya na kubeba ubingwa, wachezaji wa Yanga ni wapambanaji naamini watapambana kuipigania timu yao na taifa,” alisema Mgunda.
Akimzungumzia Kamwe Mgunda alisema hana tatizo lolote na ofisa habari huyo kwani alimuomba msamaha na yeye kama mzazi alimsamehe kama kijana wake wa kumzaa.
Mgunda alisema anajua kijana wake aliteleza na alikuwa katika harakati za kupigania mkate wake hivyo hayo yalishakwisha na anamwombea mafanikio mema katika mechi ya marudiano ya mchezo wao huo wa fainali.

“Sina tatizo na Kamwe sababu namchukulia kama kijana wangu, kizuri amegundua kosa lake na ameomba msamaha na mimi kama mzazi nimeshamsamehe na namtakia mafanikio mema kwenye kazi yake ikiwemo kuchukua ubingwa wa Afrika,” alisema Mgunda.


The post Mgunda amsamehe Ally Kamwe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/30/mgunda-amsamehe-ally-kamwe/feed/ 0