Allasane Diao - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 15 Mar 2024 07:37:43 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Allasane Diao - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Diao kukosa mechi zote za ligi https://www.greensports.co.tz/2024/03/15/diao-kukosa-mechi-zote-za-ligi/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/15/diao-kukosa-mechi-zote-za-ligi/#respond Fri, 15 Mar 2024 07:37:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10198 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa timu ya Azam FC, Allasane Diao (pichani kushoto) anatarajia kuzikosa mechi zote za Ligi Kuu NBC zilizosalia za msimu huu baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa wa goti nchini Afrika Kusini.Diao mwenye mabao matatu mpaka sasa, atakosa mechi 10 za ligi dhidi ya Yanga, Namungo, Mashujaa, Ihefu, Mtibwa Sugar, KMC, Simba, JKT […]

The post Diao kukosa mechi zote za ligi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa timu ya Azam FC, Allasane Diao (pichani kushoto) anatarajia kuzikosa mechi zote za Ligi Kuu NBC zilizosalia za msimu huu baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa wa goti nchini Afrika Kusini.
Diao mwenye mabao matatu mpaka sasa, atakosa mechi 10 za ligi dhidi ya Yanga, Namungo, Mashujaa, Ihefu, Mtibwa Sugar, KMC, Simba, JKT Tanzania, Kagera Sugar na Geita Gold.
Ofisa Habari wa Azam, Thabiti Zacharia alisema Alhamisi hii kuwa Diao amefanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Vincent Palloti ya Cape Town na atakuwa nje kwa kipindi cha miezi saba hadi tisa kuuguza majeraha hayo.
“Tunatarajia kuikosa huduma ya Diao kwa mechi zote za msimu huu zilizosalia baada ya kufanyiwa upasuaji utakaomfanya akae nje kwa muda mrefu.

“Tunashukuru upasuaji ulifanyika kwa mafanikio makubwa, ni pigo kwenye mipango yetu msimu huu lakini tunaamini mwalimu atatumia wachezaji waliopo kuziba pengo lake,” alisema Zacharia.


Wachezaji wengine wa Azam wanaosumbuliwa na majeraha ni Franklin Navaro, Sospeter Bajana, Malickou Ndoye, Ali Ahmada na Abdulai Idrisu.

The post Diao kukosa mechi zote za ligi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/15/diao-kukosa-mechi-zote-za-ligi/feed/ 0
Azam FC yanasa straika mpya https://www.greensports.co.tz/2023/07/04/azam-fc-yanasa-straika-mpya/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/04/azam-fc-yanasa-straika-mpya/#respond Tue, 04 Jul 2023 19:27:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6813 Na mwandishi wetuKlabu ya Azam FC imemtambulisha straika mpya kutoka Senegal, Allasane Diao (pichani) aliyesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu hiyo.Mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka US Goree inayoshiriki Ligi Kuu ya Senegal ametambulishwa na Azam jioni ya leo Jumanne kupitia mitandao yao ya kijamii.Huo unakuwa usajili wa tatu kwa Azam kuelekea msimu ujao wakiendelea […]

The post Azam FC yanasa straika mpya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Azam FC imemtambulisha straika mpya kutoka Senegal, Allasane Diao (pichani) aliyesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu hiyo.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka US Goree inayoshiriki Ligi Kuu ya Senegal ametambulishwa na Azam jioni ya leo Jumanne kupitia mitandao yao ya kijamii.
Huo unakuwa usajili wa tatu kwa Azam kuelekea msimu ujao wakiendelea kujiimarisha kwa ajili ya michuano ya Ligi Kuu NBC na Kombe la Shirikisho Afrika.
Azam FC hivi karibuni ilifanikiwa kuinasa saini za viungo washambuliaji, Djibril Sillah kutoka Raja Casablanca na Feisal Salum au Fei Toto kutoka Yanga SC.
Klabu hiyo hivi karibuni inatarajiwa kwenda nchini Tunisia kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya msimu ujao.

The post Azam FC yanasa straika mpya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/04/azam-fc-yanasa-straika-mpya/feed/ 0