Al Jaish - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 09 Mar 2023 05:46:10 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Al Jaish - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mchezaji Syria afungiwa maisha https://www.greensports.co.tz/2023/03/09/mchezaji-syria-afungiwa-maisha/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/09/mchezaji-syria-afungiwa-maisha/#respond Thu, 09 Mar 2023 05:45:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5449 Damascus, SyriaChama cha Soka cha Syria kumemfungia kucheza soka maisha nahodha wa zamani wa timu ya Taifa, Ahmed Al-Saleh baada ya kumpiga, kumtusi na kumtemea mate mwamuzi.Al-Saleh (pichani juu) ambaye ni beki wa timu ya Al Jaish, baada ya kupewa kadi nyekundu katika mechi ya mwishoni mwa wiki, anadaiwa kumfuata mwamuzi huyo na kumfanyia vitendo […]

The post Mchezaji Syria afungiwa maisha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Damascus, Syria
Chama cha Soka cha Syria kumemfungia kucheza soka maisha nahodha wa zamani wa timu ya Taifa, Ahmed Al-Saleh baada ya kumpiga, kumtusi na kumtemea mate mwamuzi.
Al-Saleh (pichani juu) ambaye ni beki wa timu ya Al Jaish, baada ya kupewa kadi nyekundu katika mechi ya mwishoni mwa wiki, anadaiwa kumfuata mwamuzi huyo na kumfanyia vitendo hivyo kabla ya kuzuiwa na wachezaji wa timu zote mbili.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 33 alifanya kitendo hicho wakati timu yake ikiumana na Al Wathba na sambamba na adhabu hiyo, timu ya Al-Jaish imetozwa faini na kamati ya nidhamu iliyotoa adhabu hiyo na haina ruhusa ya kukata rufaa.
Inadaiwa kwamba hata baada ya kutolewa, mchezaji huyo aliendelea kumtolea lugha chafu mwamuzi wa mchezo huo wakati wakiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

The post Mchezaji Syria afungiwa maisha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/09/mchezaji-syria-afungiwa-maisha/feed/ 0