Al Hilal - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 13 Jan 2025 07:44:10 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Al Hilal - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Yanga yanusa robo fainali Afrika https://www.greensports.co.tz/2025/01/13/yanga-yanusa-robo-fainali-afrika/ https://www.greensports.co.tz/2025/01/13/yanga-yanusa-robo-fainali-afrika/#respond Sun, 12 Jan 2025 21:20:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12627 Na mwandishi wetuYanga imepiga hatua muhimu kuelekea kufuzu robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuilaza Al Hilal ya Sudan bao 1-0 mechi iliyopigwa Jumapili hii usiku nchini Mauritania.Bao hilo peke lililofungwa na Stephane Aziz Ki mapema dakika ya saba linaifanya Yanga kufikisha pointi saba na sasa italazimika kushinda mechi ijayo dhidi ya MC […]

The post Yanga yanusa robo fainali Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imepiga hatua muhimu kuelekea kufuzu robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuilaza Al Hilal ya Sudan bao 1-0 mechi iliyopigwa Jumapili hii usiku nchini Mauritania.
Bao hilo peke lililofungwa na Stephane Aziz Ki mapema dakika ya saba linaifanya Yanga kufikisha pointi saba na sasa italazimika kushinda mechi ijayo dhidi ya MC Alger ili kujikatia tiketi ya robo fainali.
MC Alger yenye pointi nane nayo inapigania nafasi hiyo jambo ambalo linaifanya mechi hiyo itakayopigwa Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kuwa ngumu kwa timu zote.
Aziz Ki anayesifika kwa kufunga mabao ya mashuti ya mbali, alifunga bao hilo baada ya kuinasa pasi ya chinichini aliyopenyezewa na Dickson Job.
Baada ya kuinasa pasi hiyo, Aziz Ki aliambaa kidogo na mpira kabla ya kuuweka sawa kwenye mguu wake wa kushoto na kufumua shuti lililomshinda mlinda mlango wa Al Hilal, Issa Fofana.
Yanga ilikuwa na nafasi ya kuongeza bao la pili katika dakika ya 44 baada ya Aziz Ki kuuwahi mpira uliopigwa vibaya na beki wa Sudan lakini shuti la Aziz Ki lilipaa juu ya lango.
Dakika ya 76, Prince Dube aliunasa mpira akiwa karibu na lango la Al Hilal wakati kipa wa timu hiyo akiwa ametoka lakini Dube akapiga mpira uliookolewa kirahisi.

The post Yanga yanusa robo fainali Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/01/13/yanga-yanusa-robo-fainali-afrika/feed/ 0
Al Hilal ya Saudi Arabia yamtaka Mbappe https://www.greensports.co.tz/2023/07/24/al-hilal-ya-saudi-arabia-yamtaka-mbappe/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/24/al-hilal-ya-saudi-arabia-yamtaka-mbappe/#respond Mon, 24 Jul 2023 11:45:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7089 Riyadh, Saudi ArabiaKlabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia inamtaka mshambuliaji wa PSG ya Ufaransa, Kylian Mbappe (pichani) na ipo tayari kuweka rekodi ya dunia kwa kumsajili kwa ada ya Pauni 259 milioni.Mbappe ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya Ufaransa ana uwezekano mdogo mno kuendelea kuichezea PSG msimu ujao wa 2023-24 unaoanza […]

The post Al Hilal ya Saudi Arabia yamtaka Mbappe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia inamtaka mshambuliaji wa PSG ya Ufaransa, Kylian Mbappe (pichani) na ipo tayari kuweka rekodi ya dunia kwa kumsajili kwa ada ya Pauni 259 milioni.
Mbappe ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya Ufaransa ana uwezekano mdogo mno kuendelea kuichezea PSG msimu ujao wa 2023-24 unaoanza mapema mwezi ujao na tayari ameachwa na timu hiyo katika safari ya maandalizi ya msimu ujao nchini Japan.
Katika siku za karibuni amekuwa akihusishwa zaidi na mipango ya kujiunga na klabu ya Real Madrid ya Hispania kabla ya Al Hilal kumtangazia ofa mpya kubwa hii leo Jumatatu.
Mbappe amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa na PSG na ameshaweka wazi msimamo wake wa kubaki katika klabu hiyo lakini hataki kusaini mkataba mpya wakati huu.
Msimamo huo unapingana na msimamo wa Rais wa PSG, Nasser Al Khelaifi ambaye amemtaka mchezaji huyo achague moja kama anataka kubaki PSG lazima asaini mkataba mpya wakati huu tofauti na hivyo aondoke.
Mbappe mwenye umri wa miaka 24 alijiunga na PSG mwaka 2017 akitokea Monaco kwa ada ya Pauni 166 milioni na tangu wakati huo amekuwa mfungaji tegemeo wa mabao wa timu pamoja na timu ya Taifa ya Ufaransa.
Mchezaji wa mwisho kusajiliwa PSG kwa bei mbaya alikuwa ni Neymar ambaye ada yake ilifikia Pauni 200 milioni mwaka 2017 akitokea Barcelona na kama mpango wa Al Hilal utafanikiwa basi usajili wa Mbappe katika klabu hiyo itakuwa rekodi nyingine ya dunia lakini pia utamfanya Mbappe aungane na mastaa wengine wa soka waliowahi kutamba Ulaya na kwa sasa wanacheza soka Saudi Arabia kina Cristiano Ronaldo, Karim Benzema, Eduardo Mendy na wengineo.

The post Al Hilal ya Saudi Arabia yamtaka Mbappe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/24/al-hilal-ya-saudi-arabia-yamtaka-mbappe/feed/ 0