Al Ahly - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 26 Feb 2026 16:33:57 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Al Ahly - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mechi ya Ahly, FAR Rabat yachunguzwa https://www.greensports.co.tz/2026/02/16/mechi-ya-ahly-far-rabat-kikaangoni/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/16/mechi-ya-ahly-far-rabat-kikaangoni/#respond Mon, 16 Feb 2026 15:13:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14361 Cairo, MisriShirikisho la Soka Afrika (CAF) limelaani matukio yasiyokubalika yaliyojitokeza katika mechi kati ya Al Ahly ya Misti na AS FAR Rabat ya Morocco, mechi iliyochezwa Jumapili, Februari 15, 2026 na suala hilo limefikishwa kamati ya nidhamu.Taarifa ya CAF iliyopatikana leo Jumatatu Februari 16, 2026 imeitaja mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiihusisha na […]

The post Mechi ya Ahly, FAR Rabat yachunguzwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Cairo, Misri
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limelaani matukio yasiyokubalika yaliyojitokeza katika mechi kati ya Al Ahly ya Misti na AS FAR Rabat ya Morocco, mechi iliyochezwa Jumapili, Februari 15, 2026 na suala hilo limefikishwa kamati ya nidhamu.
Taarifa ya CAF iliyopatikana leo Jumatatu Februari 16, 2026 imeitaja mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiihusisha na vitendo hivyo ingawa haikufafanua ni vitendo gani visivyokubalika vilivyojitokeza katika mechi hiyo.
Katika mechi hiyo ya Kundi B, Al Ahly wakiwa nyumbani walitoka sare ya bila kufungana na AS Rabat, mechi ambayo ilichezwa wakati Ahly wakiwa na pointi tisa na tayari walikuwa wamefuzu kucheza robo fainali.
Kwa upande wa AS Rabat ili kufuzu hatua hiyo walihitaji sare ambayo waliipata na hatimaye kufikisha pointi tisa ambazo mpinzani wao mkuu Yanga hakuweza kuzipata licha ya kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 mbele ya JS Kablylie.
Kabla ya mechi hizo za mwisho za kundi hilo, Yanga walikuwa na pointi tano na AS Rabat pointi nane, matarajio ya Yanga yalikuwa ni Ahly ambao ni vinara wa kundi hilo wangepata ushindi na Yanga kumshinda Kabylie.
Matarajio hayo hata hivyo yalikwamishwa na matokeo ya sare ya Al Ahly na AS Rabat na kuufanya ushindi wa Yanga wa mabao 3-0 mbele ya JS Kabylie usiwe na maana yoyote kwa kuwa AS Rabat amefikisha pointi tisa.
Baadhi ya mashabiki hasa wanaoaminika kuwa wa Yanga walianza kutilia shaka mwenendo wa mechi ya AS Rabat na Ahly wengi wao wakiamini kuwa haikuwa na ushindani uliotarajiwa.
CAF katika taarifa yake ilieleza kuwa suala hilo limepelekwa kwenye kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo kwa ajili ya uchunguzi na hatua zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kuhusika katika vitendo hivyo.

The post Mechi ya Ahly, FAR Rabat yachunguzwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/16/mechi-ya-ahly-far-rabat-kikaangoni/feed/ 0
Yanga yakwama Misri, yalala 2-0 https://www.greensports.co.tz/2026/01/24/yanga-yakwama-misri-yalala-2-0/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/24/yanga-yakwama-misri-yalala-2-0/#respond Sat, 24 Jan 2026 11:30:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14282 Alexandria, MisriMambo si mambo kwa klabu ya Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Al Ahly ya Misti, mechi iliyopigwa usiku wa Ijumaa, Januari 24, 2026 kwenye Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.Yanga ambayo ipo Kundi B ilitunguliwa mabao hayo na Mahmoud Hassan Trezeguet, mabao yaliyowafanya wababe hao wa […]

The post Yanga yakwama Misri, yalala 2-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Alexandria, Misri
Mambo si mambo kwa klabu ya Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Al Ahly ya Misti, mechi iliyopigwa usiku wa Ijumaa, Januari 24, 2026 kwenye Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.
Yanga ambayo ipo Kundi B ilitunguliwa mabao hayo na Mahmoud Hassan Trezeguet, mabao yaliyowafanya wababe hao wa Misri na Afrika kuongoza kundi hilo ambalo pia lina timu za JS Kablie ya Algeria na AS FAR Rabat ya Morocco.
Ahly licha ya kuwa wenyeji na kutawala mchezo lakini mechi haikuwa rahisi kwao kwani kwa kipindi chote cha kwanza walipata wakati mgumu kuupenya ukuta wa Yanga kabla ya kuwaotea katika dakika za nyongeza za kipindi hicho kwa bao la Trezeguet.
Mpira uliozaa bao hilo ulitokana na krosi ya Mohamed Hany kutokea na kumkuta Trezeguet aliyeruka juu na kuujaza mpira wavuni kwa kichwa akimuacha kipa wa Yanga, Djigui Diara akiwa hajui la kufanya.
Umakini na mbinu za uwezo wa Ahly kutawala mchezo ulizaa matunda katika dakika ya 75 walipopata bao la pili, safari hii Trezeguet aliunasa mpira akiwa katika eneo la penalti na kuuhamishia kwenye mguu wake wa kulia kabla ya kufumua shuti lililojaa wavuni.
Baada ya matokeo hayo, Al Ahly sasa imefikisha pointi saba ikiwa kinara wa kundi hilo wakati Yanga inabaki katika nafasi ya pili na pointi zake nne ikiwa imeshinda mechi moja na sare moja.

The post Yanga yakwama Misri, yalala 2-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/24/yanga-yakwama-misri-yalala-2-0/feed/ 0
Al Ahly wafalme Ligi ya Mabingwa https://www.greensports.co.tz/2024/05/26/al-ahly-wafalme-ligi-ya-mabingwa/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/26/al-ahly-wafalme-ligi-ya-mabingwa/#respond Sun, 26 May 2024 05:59:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11128 Cairo, MisriTimu ya Al Ahly ya Misri ndio wafalme wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2023-24 baada ya kuilaza Esperance ya Tunisia bao 1-0 katika mechi iliyopigwa Jumamosi hii jioni kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.Ushindi huo unaifanya Ahly kuweka rekodi ya kubeba taji hilo kwa mara ya 12 lakini pia unaifanya timu hiyo […]

The post Al Ahly wafalme Ligi ya Mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Cairo, Misri
Timu ya Al Ahly ya Misri ndio wafalme wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2023-24 baada ya kuilaza Esperance ya Tunisia bao 1-0 katika mechi iliyopigwa Jumamosi hii jioni kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
Ushindi huo unaifanya Ahly kuweka rekodi ya kubeba taji hilo kwa mara ya 12 lakini pia unaifanya timu hiyo iwe imebeba taji hilo kubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika kwa mara ya nne katika kipindi cha miaka mitano.
Ushindi huo pia unaifanya Ahly iweke rekodi ya kucheza mechi 20 za ligi hiyo bila kupoteza lakini pia imeweka rekodi ya kuvutia katika safu yake ya ulinzi ikiwa imefungwa bao moja tu kwa msimu huu.
Esperance katika mechi hiyo iliingia na shauku kubwa ya kubeba taji hilo ikiamini ulikuwa wakati wake sahihi kufanya hivyo ikiwania rekodi ya kulibeba kwa mara tano ikikumbukwa kuwa ilifanya hivyo mara ya mwisho mwaka 2019.
Mambo hata hivyo yaliwaharibikia Esperance mapema dakika ya nne baada ya Roger Aholou kujifunga wakati akiokoa mpira wa kichwa uliopigwa na Ramy Moustafa ukitokana na kona iliyochongwa na Hussein El Shahata.
Ahly waliweza kulilinda vyema bao hilo na hadi dakika 90 zinakamilika walitoka vifua mbele wakineemeka pia na matokeo ya awali katika mechi ya kwanza iliyopigwa mjini Tunis na timu hizo kutoka sare ya bila kufungana.
Uwanja wa Kimataifa Cairo ulilipuka kwa shangwe baada ya wafalme hao wa soka la Afrika kumaliza dakika 90 wakiwa mashujaa na rekodi yao ya kubeba taji hilo kwa mara ya 12.

The post Al Ahly wafalme Ligi ya Mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/26/al-ahly-wafalme-ligi-ya-mabingwa/feed/ 0
Simba nayo yatolewa Ligi ya Mabingwa https://www.greensports.co.tz/2024/04/06/simba-nayo-yatolewa-ligi-ya-mabingwa/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/06/simba-nayo-yatolewa-ligi-ya-mabingwa/#respond Sat, 06 Apr 2024 06:23:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10533 Na mwandishi wetuSimba nayo imeungana na hasimu wake Yanga kwa kuaga fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika katika hatua ya robo fainali baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Al Ahly ya Misri mjini Cairo.Kwa matokeo ya mechi hiyo iliyopigwa usiku wa kuamkia Jumamosi hii, Simba inakuwa imetolewa kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya kulala […]

The post Simba nayo yatolewa Ligi ya Mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba nayo imeungana na hasimu wake Yanga kwa kuaga fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika katika hatua ya robo fainali baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Al Ahly ya Misri mjini Cairo.
Kwa matokeo ya mechi hiyo iliyopigwa usiku wa kuamkia Jumamosi hii, Simba inakuwa imetolewa kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya kulala kwa bao 1-0 katika mechi ya kwanza iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Simba hata hivyo ilionesha upambanaji wa hali ya juu kwa kucheza pasi kadhaa na kulisakama mara kadhaa lango la Ahly na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika matokeo yalikuwa sare ya 0-0.
Mambo yaliwaharibikia Simba dakika mbili baada ya kuanza kipindi cha pili walipofungwa bao la kwanza mfungaji akiwa Amr El Soleiya aliyefunga bao hilo kwa shuti kali akiwa ndani ya 18.
Mpira uliozaa bao hilo ulianzia kwa Maloul aliyemzidi ujanja Shomary Kapombe na kumuunganishia pasi Antony Modeste ambaye alimtengea vizuri El Soleiya naye bila ajizi akaujaza wavuni.
Baada ya bao hilo, Simba iliendelea kupambana ingawa safu yake ya ulinzi ilionekana kushindwa kujipanga hasa upande wa kulia ambapo, Kapombe mara kadhaa alijikuta katika wakati mgumu kukabiliana na wachezaji wa Ahly walioonekana kutumia upande wake zaidi kwa kupeleka mashambulizi.
Dakika ya 64 nusura, Ahly waongeze bao la pili ambalo Modeste alikuwa akielekea kuonana na kipa Ayoub Lakred lakini Henock Inonga akawa makini kumdhibiti.
Dakika moja baada ya kosa kosa hiyo, Kibu Denis aliunganishiwa pasi na Mohamed Hussein na kukimbia kwa kasi na mpira lakini wakati akitaka kuwatoka mabeki wa Ahly alianguka na mwamuzi akampa kadi ya njano kwa kilichoonekana kama alijiuangusha na kuukumbatia mpira.
Wachezaji wa Simba waliendelea kuonesha utulivu wakizuia mashambulizi ya Ahly na kulisogelea lango la timu hiyo lakini mambo yaliwaharibikia kwa mara nyingine dakika moja kabla ya mpira kumalizika walipofungwa bao la pili.
Bao hilo lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Mahmoud Kahraba, penalti ambayo ilitolewa baada ya Che Malone kumpiga kichwa Hussein El Shehata wakati wakiwania mpira wa juu.
Tukio hilo lililotokea ndani ya eneo la 18 la Simba lilisababisha mchezo huo kusimama kwa dakika kadhaa na El Shehata kulazimika kupata huduma ya kwanza huku akionekana kuumia zaidi karibu na sehemu ya jicho la kulia.
Kocha wa Simba, Abdelhak Benchikha katika juhudi za kusaka matokeo aliwatoa Kapombe na Kanoute na kuwaingiza Israel Mwenda na Miquisonne, baadaye akamtoa Kibu na nafasi yake kuingia Willy Onana.
Pia Benchikha aliwatoa Saido Ntibazonkiza ambaye nafasi yake aliingia Jobe Omar na Clatous Chama ambaye nafasi yake aliingia Freddy Koublan.
Hii ni mara ya nne Simba kuishia robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa miaka ya karibuni na sasa timu hiyo kama ilivyo kwa hasimu wake Yanga, wote wanarudi nyumbani kwenye Ligi Kuu NBC na Kombe la FA kusaka tiketi ya kushiriki ligi hiyo kubwa barani Afrika kwa msimu ujao.

The post Simba nayo yatolewa Ligi ya Mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/06/simba-nayo-yatolewa-ligi-ya-mabingwa/feed/ 0
Mahamat ndiye mwamuzi Simba, Ahly https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/mahamat-ndiye-mwamuzi-simba-ahly/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/mahamat-ndiye-mwamuzi-simba-ahly/#respond Thu, 04 Apr 2024 19:43:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10503 Na mwandishi wetuImewekwa wazi kuwa mwamuzi Alhadi Mahamat (pichani) ndiye atakayeamua mechi ya mkondo wa pili wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Al Ahly ya Misri na Simba SC ya Tanzania.Mahamat, 37 raia wa Chad ndiye aliyewahi kuichezesha Yanga pia ilipopoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya CR Belouzdad katika […]

The post Mahamat ndiye mwamuzi Simba, Ahly first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Imewekwa wazi kuwa mwamuzi Alhadi Mahamat (pichani) ndiye atakayeamua mechi ya mkondo wa pili wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Al Ahly ya Misri na Simba SC ya Tanzania.
Mahamat, 37 raia wa Chad ndiye aliyewahi kuichezesha Yanga pia ilipopoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya CR Belouzdad katika mchezo wa hatua ya makundi uliopigwa nchini Algeria.
Mwamuzi huyo sasa ndiye atakayewaamua Simba katika mchezo wao huo utakaounguruma kesho Ijumaa mjini Cairo, Misri kuanzia saa 5 usiku.
Kwa mchanganuo Simba inapaswa kuwa waangalifu kinidhamu kwani mwamuzi huyo katika mechi zake nane zilizopita ametoa kadi za njano 28 ikiwa ni wastani wa kadi tatu kila mchezo huku akitoa kadi nyekundu moja.
Mahamat alitoa kadi nyekundu katika mchezo wa michuano ya African Football League (AFL) baina ya Enyimba na Wydad AC ambao Enyimba ilichapwa bao 1-0, Oktoba 22, mwaka jana.
Katika mchezo huo, Simba inahitaji ushindi ili kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa awali uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam wiki iliyopita.

The post Mahamat ndiye mwamuzi Simba, Ahly first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/mahamat-ndiye-mwamuzi-simba-ahly/feed/ 0
Al Ahly yaitungua Yanga 1-0 https://www.greensports.co.tz/2024/03/02/al-ahly-yaitungua-yanga-1-0/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/02/al-ahly-yaitungua-yanga-1-0/#respond Sat, 02 Mar 2024 13:17:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9978 Na mwandishi wetuYanga imemaliza mechi zake za makundi za Ligi ya Mabingwa Afrika Ijumaa hii kwa kukutana na kipigo cha bao 1-0 mbele ya Al Ahly ya Misri ingawa timu hizo zote zimefuzu hatua ya robo fainali ya ligi hiyo.Kwa matokeo ya mechi hiyo ambayo Yanga ilikuwa ugenini, Ahly ambao ni mabingwa watetezi wa ligi […]

The post Al Ahly yaitungua Yanga 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imemaliza mechi zake za makundi za Ligi ya Mabingwa Afrika Ijumaa hii kwa kukutana na kipigo cha bao 1-0 mbele ya Al Ahly ya Misri ingawa timu hizo zote zimefuzu hatua ya robo fainali ya ligi hiyo.
Kwa matokeo ya mechi hiyo ambayo Yanga ilikuwa ugenini, Ahly ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo wamemaliza mechi za makundi wakiwa kinara katika Kundi B na pointi zao 12 na Yanga imeshika nafasi ya pili baada ya kukusanya pointi nane.
Bao lililoizamisha Yanga lilipatikana dakika moja baada ya kuanza kipindi cha pili mfungaji akiwa ni Hussein Shehata, bao ambalo kwa kiasi kikubwa lilichangiwa na makosa ya safu ya ulinzi ya Yanga.
Yanga licha ya kufungwa bao hilo pekee, ilionesha kandanda safi kuanzia mwanzo hadi mwisho huku kipa wake Djigui Diarra akionesha umahiri kwa kuokoa michomo kadhaa iliyoelekezwa langoni mwake hasa katika kipindi cha pili.
Katika mechi hiyo Yanga ilipata pigo baada ya kiungo wake, Khalid Aucho kuumia na nafasi yake kuingia Aboubakar Salum ‘Sure Boy’ ingawa haikuweza kufahamika mara moja ukubwa wa majeraha aliyopata mchezaji huyo.
Mechi nyingine ya kundi hilo ilizikutanisha CR Belouizdad ya Algeria iliyokuwa ikiumana na Medeama ya Ghana, mechi ambayo iliisha kwa Belouizdad kutoka na ushindi wa mabao 3-0.
Belouizdad ambayo kabla ya mechi hiyo ilikutana na kipigo cha mabao 4-0 mbele ya Yanga, imemaliza mechi zake za makundi ikishika nafasi ya tatu wakati Medeama ikiburuza mkia.

The post Al Ahly yaitungua Yanga 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/02/al-ahly-yaitungua-yanga-1-0/feed/ 0
Yanga, Ahly zagawana pointi https://www.greensports.co.tz/2023/12/02/yanga-ahly-zagawana-pointi/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/02/yanga-ahly-zagawana-pointi/#respond Sat, 02 Dec 2023 18:44:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8717 Na mwandishi wetuYanga leo Jumamosi imegawana pointi moja moja na Al Ahly ya Misri baada ya sare ya bao 1-1 katika mechi ya Kundi D ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.Ahly walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 87 mfungaji akiwa Percy Tau aliyeujaza mpira wavuni kwa kichwa […]

The post Yanga, Ahly zagawana pointi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga leo Jumamosi imegawana pointi moja moja na Al Ahly ya Misri baada ya sare ya bao 1-1 katika mechi ya Kundi D ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Ahly walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 87 mfungaji akiwa Percy Tau aliyeujaza mpira wavuni kwa kichwa baada ya Bakari Nondo Mwamnyeto kuokoa kwa kichwa krosi iliyoelekezwa langoni mwake kabla ya mpira kumkuta mfungaji.
Mwamnyeto alijikuta katika mazingira hayo magumu baada ya Yanga kushambuliwa lakini mpira alioupiga kwa kichwa haukuenda mbali ukawahiwa na Tau ambaye aliujaza wavuni wakati kipa Diarra akiwa mbali kidogo na lango lake.
Baada ya hapo dakika tano ziliongezwa na ndipo Yanga iliponeemeka na muda huo katika dakika ya pili baada ya Pacome Zouazoua kuujaza mpira wavuni kwa shuti kali akiwa amezungukwa na msitu wa mabeki wa Ahly baada ya kuiwahi pasi ya Kennedy Musonda.
Timu zote zilionesha uhai na kujiamini huku zikishindwa kuzitumia nafasi kadhaa katika kipindi cha kwanza, kwa Ahly mchezaji wao tishio, Hussein El Shehata alishindwa kuipatia bao timu yake akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga.
Yanga nayo katika dakika ya 33 ilifanya shambulizi langoni mwa Ahly ambapo Aziz Ki aliuwahi mpira uliombabatiza beki wa Ahly na kupiga shuti la mguu wa kushoto la kimo cha mbuzi lakini mpira ulitoka nje ya lango.
Dakika ya 47, Ahly walifanya shambulizi kali langoni mwa Yanga, shambulizi lililozaa kona tatu ambazo hazikuzaa matunda na dakika nne baadaye Mahmoud Kahraba akiwa karibu na kipa Diarra alishindwa kuipatia Ahly bao.
Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi alifanya mabadiliko kadhaa, kwanza alimtoa Clement Mzize na kumuingiza Kennedy Musonda na Maxi Nzengeli akatoka nafasi yake ikachukuliwa na Zawadi Mauya.
Kwa matokeo hayo Yanga inakuwa imezidi kujiweka pagumu kwani hadi sasa ina pointi moja katika mechi mbili wakati Ahly inayoshika usukani katika kundi hilo imefikisha pointi nne katika mechi mbili.

The post Yanga, Ahly zagawana pointi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/02/yanga-ahly-zagawana-pointi/feed/ 0
Simba ya kibingwa yaaga AFL https://www.greensports.co.tz/2023/10/25/simba-ya-kibingwa-yaaga-afl/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/25/simba-ya-kibingwa-yaaga-afl/#comments Wed, 25 Oct 2023 06:36:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8220 Na mwandishi wetuSimba ya kibingwa imeaga kibingwa michuano mipya ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) ikiangushwa na kanuni ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Al Ahly ya Misri katika mechi iliyopigwa Jumanne hii jioni.Katika mechi ya kwanza iliyopigwa jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita, Simba ilitoka sare ya mabao […]

The post Simba ya kibingwa yaaga AFL first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba ya kibingwa imeaga kibingwa michuano mipya ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) ikiangushwa na kanuni ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Al Ahly ya Misri katika mechi iliyopigwa Jumanne hii jioni.
Katika mechi ya kwanza iliyopigwa jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita, Simba ilitoka sare ya mabao 2-2 na vijogoo hao wa Afrika na ilihitaji ushindi wowote au sare ya zaidi ya mabao matatu ili kusonga hatua ya nusu fainali.
Simba licha ya kuwa ugenini mjini Cairo, Misri kwenye Uwanja wa Cairo, ilicheza soka la kujiamini kwa nidhamu ya hali ya juu ikiziba njia za Ahly na kufanya mashambulizi ya hapa na pale na haikushangaza timu hizo kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana.
Matokeo hayo yaliibua matumaini makubwa kwa mashabiki wa Simba kwamba timu yao ilikuwa ikielekea kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo inayoshirikisha timu nane bora Afrika.
Nidhamu ya kiuchezaji na umakini wa kushambulia uliwafanya Simba wawe wa kwanza kuzitikisa nyavu za Ahly katika dakika ya 68 kwa bao lililofungwa kwa kichwa na Sadio Kanoute.
Kanoute alifunga bao hilo kwa mpira mrefu ulioanzia kwa Shomary Kapombe aliyepiga krosi ambayo iliunganishwa pia kwa kichwa na Jean Baleke kabla ya kumkuta mfungaji.
Bao hilo lilizidi kufufua matumaini ya Simba kuwabwaga vigogo hao wa soka la Afrika lakini mambo yaliharibika dakika nane baadaye, Ahly waliposawazisha bao hilo kupitia kwa Ally Maaloul ambaye aliitumia vizuri krosi ya Mahmoud Kahraba.
Simba kwa ujumla ilionekana kuwa na mpango mzuri katika mechi hiyo, haikuwa timu yenye woga wa kufanya mashambulizi na kutumia muda mwingi kujilinda badala yake ilicheza kwa utulivu, ikifunguka na bila kusahau kujilinda.
Mapema katika dakika ya 11 mipango hiyo ya Siimba ilionekana ilipofanya shambulizi lililoanzia kwa Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ aliyefumua shuti ambalo hata hivyo lilitua mikononi mwa kipa wa Ahly, Mohamed El Shenawy.
Katika kipindi cha kwanza, Simba walijihami vizuri huku wakilisogelea mara kadhaa lango la Ahly wakimtumia zaidi mshambuliaji pekee John Bocco ambaye muda mwingi alicheza akiwa eneo la Ahly ambao pia walikuwa wakitibua vyema mipango ya Simba.
Kwa matokeo hayo, Simba inakuwa imeishia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ingawa italamba kitita cha Sh bilioni 2.5 ambazo zinapewa timu zilizofikia hatua ya robo fainali wakati zitakazofikia nusu fainali zitapewa Sh bilioni 4.3, nafasi ya pili Sh bilioni 7.5 na mshindi Sh bilioni 10.

The post Simba ya kibingwa yaaga AFL first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/25/simba-ya-kibingwa-yaaga-afl/feed/ 1
Simba, Al Ahly zatoka sare AFL https://www.greensports.co.tz/2023/10/20/simba-al-ahly-zatoka-sare-afl/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/20/simba-al-ahly-zatoka-sare-afl/#respond Fri, 20 Oct 2023 17:57:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8172 Na mwandishi wetuSimba imeianza michuano ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) kwa sare ya mabao 2-2 na Al Ahly ya Misri katika mechi ya uzinduzi wa michuano hiyo iliyopigwa leo Ijumaa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.Katika mechi hiyo iliyoshuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Fifa na CAF, wageni Ahly walikuwa wa kwanza kupata […]

The post Simba, Al Ahly zatoka sare AFL first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imeianza michuano ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) kwa sare ya mabao 2-2 na Al Ahly ya Misri katika mechi ya uzinduzi wa michuano hiyo iliyopigwa leo Ijumaa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo iliyoshuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Fifa na CAF, wageni Ahly walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 45 lililofungwa na Slim na kuifanya timu hiyo iende mapumziko ikiwa mbele.
Kipindi cha pili Simba ilikianza kwa kufanya mabadiliko ikiwatoa Muzamir Yassin na nafasi yake kuingia Sadio Kanoute na kumtoa Luis Miquisson na nafasi yake kuchukuliwa na Jean Baleke.
Mara baada ya kuanza kipindi cha pili Ahly walifanya shambulizi langoni mwa Simba kabla ya Simba kujibu mapigo lakini ilikuwa vigumu kuwapenya Ahly waliojazana nyuma kulinda lango lao huku wakijaribu kufanya mashambulizi machache.
Simba wakicheza kwa umakini walifanikiwa kuipenya safu ya ulinzi ya Ahly na kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 53 lililofungwa na Kibu Dennis.
Bao hilo lilianzia kwa pasi ndefu ya Saido Ntibazonkiza na kuunganishwa na Baleke kabla ya kumkuta Clatous Chota Chama ambaye aliurudisha ndani mpira wa juu ambao ulikuwa ukitoka nje na kumkuta mfungaji aliyeujaza wavuni kwa kichwa na mpira kumshinda kipa El Shanawy wa Ahly.
Dakika saba baada ya Simba kusawazisha bao hilo, Kanoute aliongeza bao la pili kwa kichwa akiujaza wavuni mpira wa kona uliopigwa na Saido Ntibazonkiza na mfungaji kumzidi ujanja beki wa Ahly aliyekuwa karibu naye.
Iliwachukua Ahly dakika mbili kuwanyamazisha mashabiki wa Simba waliokuwa katika hali ya furaha baada ya kupata bao la kusawazisha lililofungwa na Mahmoud Kehraba.
Simba iliendelea kuonesha uhai licha ya kufungwa bao hilo na katika dakika ya 75, Ntibazonkiza aliinasa pasi ya Chama na kupiga shuti la mbali ambalo mlinda mlango wa Ahly, El Shanawy alionekana kuudharau mpira ambao uligonga mwamba wa juu na kuwainua vitini mashabiki wa Simba.
Kocha wa Simba, Robertinho aliendelea kufanya mabadiliko akiwatoa Kibu Dennis na nafasi yake kuingia Willy Onana na Shomary Kapombe na nafasi yake kuchukuliwa na Israel Mwenda.
Wakati Simba wakipambana kusaka bao la tatu, Ahly walikuwa wakijihami zaidi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza na kama si umakini wa safu ya ulinzi ya Simb a na kipa Ally Salim timu hiyo ingeweza kupata bao la tatu.
Zikiwa zimebakia dakika chache mpira kumalizika, kocha Robertinho alimtoa Chama na nafasi yake kuingia John Bocco, mabadiliko ambayo hayakubadili matokeo ya mchezo.
Mechi ya leo ambayo ni ya uzinduzi wa michuano mipya ya AFL ilihudhuriwa na Rais wa Fifa, Gianni Infantino na rais wa Caf, Patrice Motsepe.
Wengine waliokuwa uwanjani ni mkurugenzi wa maendeleo ya soka wa Fifa na kocha wa zamani wa Arsenal, Arsenal Wenger, mwamuzi maarufu wa zamani wa Fifa ambaye pia mwenyekiti wa kamati ya waamuzi ya Fifa, Pierluigi Collina na viongozi mbalimbali wa soka barani Afrika.

The post Simba, Al Ahly zatoka sare AFL first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/20/simba-al-ahly-zatoka-sare-afl/feed/ 0
Al Ahly baba wa Afrika https://www.greensports.co.tz/2023/06/12/al-ahly-baba-wa-afrika/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/12/al-ahly-baba-wa-afrika/#respond Mon, 12 Jun 2023 08:48:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6564 Casablanca , MoroccoAl Ahly ya Misri imetwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya bao 1-1 na Wydad Casablanca ya Morocco na hivyo kuweka rekodi ya kubeba mara 11 taji la michuano hiyo mikubwa ya klabu barani Afrika.Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili hii usiku, Ahly walipata bao la kusawazisha katika dakika ya […]

The post Al Ahly baba wa Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Casablanca , Morocco
Al Ahly ya Misri imetwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya bao 1-1 na Wydad Casablanca ya Morocco na hivyo kuweka rekodi ya kubeba mara 11 taji la michuano hiyo mikubwa ya klabu barani Afrika.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili hii usiku, Ahly walipata bao la kusawazisha katika dakika ya 78 lililofungwa kwa kichwa na Mohamed Abdelmoneim kutokana na mpira wa kona uliopigwa na Ali Maaloul.
Kwa matokeo hayo, Ahly imefanikiwa kulibeba taji hilo kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 baada ya ushindi wa mechi ya kwanza ya fainali wa mabao 2-1, mechi iliyopigwa mjini Cairo, Misri.
Ushindi umekuwa tukio kubwa la kuwafuta machozi Ahly ambao msimu uliopita walishindwa kutamba mbele ya vigogo hao wa Morocco walipolala kwa mabao 2-0 katika mechi moja ya fainali iliyopigwa mjini Casablanca.
Kabla ya Abdelmoneim kusawazishia bao, Wydad walikuwa mbele kwa bao ambalo pia lilifungwa na Yahya Attiat katika dakika ya 28, bao ambalo lingetosha kuwapa Wydad taji na kuwafanya waweke rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka Morocco kubeba taji hilo mara mbili mfululizo.
Hata hivyo mwisho wa siku walikuwa ni Ahly waliotoka uwanjani na shangwe wakineemeka na bao la Abdelmoneim na hivyo kuweka rekodi ya kulibeba taji hilo lenye hadhi barani Afrika kwa mara 11.

The post Al Ahly baba wa Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/12/al-ahly-baba-wa-afrika/feed/ 0