Ahmed Ally - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 29 May 2024 19:02:09 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ahmed Ally - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ahmed Ally: Ligi ya Mabingwa bila Simba! https://www.greensports.co.tz/2024/05/29/ahmed-ally-ligi-ya-mabingwa-bila-simba/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/29/ahmed-ally-ligi-ya-mabingwa-bila-simba/#respond Wed, 29 May 2024 19:02:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11166 Na mwandishi wetuMeneja habari na mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally amesema anaamini kutokuwepo kwao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao kuna kitu kitapungua kwenye michuano hiyo msimu ujao.Ally ameyasema hayo leo Jumatano akieleza kwa kifupi kuwa hiyo inatokana na ukubwa wao kwa sasa, ubora, hamasa ya mashabiki na heshima waliyonayo ingawa hayo […]

The post Ahmed Ally: Ligi ya Mabingwa bila Simba! first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Meneja habari na mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally amesema anaamini kutokuwepo kwao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao kuna kitu kitapungua kwenye michuano hiyo msimu ujao.
Ally ameyasema hayo leo Jumatano akieleza kwa kifupi kuwa hiyo inatokana na ukubwa wao kwa sasa, ubora, hamasa ya mashabiki na heshima waliyonayo ingawa hayo hawayatazami sana zaidi ya kujipanga kwa ajili ya ushiriki wa Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.
Simba imeshindwa kukata tiketi ya Ligi ya Mabingwa baada ya kumaliza Ligi Kuu NBC nafasi ya tatu kwa pointi 69 sawa na Azam iliyomaliza ya pili lakini yenyewe ikiwa juu kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga.
“Nimelipokea kwa moyo mkunjufu Kombe la Shirikisho sababu ni michuano halali na rasmi ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) japo hatukupenda kushiriki Shirikisho, malengo yetu ni Ligi ya Mabingwa lakini imekuwa bahati mbaya tumeangukia Shirikisho hatuna budi kushiriki…

“Ingawa Simba tuna heshima yetu kwenye michuano ya Caf hasa Ligi ya Mabingwa kutokana na ukubwa wetu, ‘vibe’ letu, ubora wetu na heshima yetu. Kukosekana Ligi ya Mabingwa kuna kitu kinapungua kwenye michuano hiyo lakini huo si muda wake kwa sasa, kilichopo sasa ni kuona namna gani tunakwenda kutawala Kombe la Shirikisho msimu ujao,” alieleza Ally.


Mara ya mwisho Wekundu hao kushiriki Kombe la Shirikisho ilikuwa msimu wa 2022-23 kabla ya kutolewa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini kwenye hatua ya robo fainali kwa penalti 4-3 baada ya kila timu kushinda bao 1-0 nyumbani kwake.
Timu nyingine iliyoungana na Simba kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo ni Coastal Union iliyomaliza nafasi ya nne wakati vinara Yanga na Azam zitawakilisha nchi katika ya Ligi ya Mabingwa.

The post Ahmed Ally: Ligi ya Mabingwa bila Simba! first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/29/ahmed-ally-ligi-ya-mabingwa-bila-simba/feed/ 0
Simba yaipongeza Yanga https://www.greensports.co.tz/2024/05/15/simba-yaipongeza-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/15/simba-yaipongeza-yanga/#respond Wed, 15 May 2024 07:06:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10970 Na mwandishi wetuMeneja habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amewapongeza mahasimu wao Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu NBC msimu huu ikiwa ni msimu wa tatu mfululizo wanafanya hivyo.Akizungumza Jumanne hii, Ally alisema kwamba anawapongeza Yanga kwa kazi nzuri waliyoifanya na hatimaye kufanikiwa kubeba taji hilo.Ally hata hivyo alisema wanawapongeza lakini wakifahamu […]

The post Simba yaipongeza Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Meneja habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amewapongeza mahasimu wao Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu NBC msimu huu ikiwa ni msimu wa tatu mfululizo wanafanya hivyo.
Akizungumza Jumanne hii, Ally alisema kwamba anawapongeza Yanga kwa kazi nzuri waliyoifanya na hatimaye kufanikiwa kubeba taji hilo.
Ally hata hivyo alisema wanawapongeza lakini wakifahamu wao pia wana mengi ya kujifunza, kujikosoa na kurekebisha kutokana na kutotwaa taji hilo kwa msimu wa tatu mfululizo wakishuhudia likitua Yanga.
“Tuwapongeze kwa kazi nzuri waliyoifanya na hatimaye kupata ubingwa, wameibuka namba moja na hatuna budi kuwapongeza kwa kazi kubwa waliyoifanya.
“Na sisi kama Simba tunayo mengi ya kujilaumu, tunayo megi ya kujifunza ya kujikosoa na ya kurekebisha na inapaswa kukaa chini na kuona wapi tunakosea na huu ni msimu wa tatu tunamaliza bila ubingwa,” alisema Ally.

“Kwa hiyo hii imemalizika kwa maana ya ubingwa lakini inafungua nafasi nyingine ya kupigania nafasi ya thamani iliyobaki kwenye ligi yetu nayo ni nafasi ya pili, sasa hivi tumelingana alama na Azam na tuna kila sababu ya kufanya vizuri ili tuchukue nafasi ya pili katika ligi ya msimu huu,” alisema Ally.


Mpaka Jumatatu, Yanga inatawazwa bingwa baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 3-1, ilifikisha pointi 71 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine huku Azam FC ikiwa na pointi 60 katika nafasi ya pili baada ya mechi 27 na Simba inashika nafasi ya tatu kwa pointi 57 baada ya mechi 26.

The post Simba yaipongeza Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/15/simba-yaipongeza-yanga/feed/ 0
Sapraizi ya kipa mpya Simba Day https://www.greensports.co.tz/2023/08/04/sapraizi-ya-kipa-mpya-simba-day/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/04/sapraizi-ya-kipa-mpya-simba-day/#respond Fri, 04 Aug 2023 20:08:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7233 Na mwandishi wetuBaada ya kuwapo kitendawili cha kipa namba moja wa Simba kwa ajili ya msimu ujao, uongozi wa timu hiyo umejinadi kuwa watafanya ‘sapraizi’ ya utambulisho wa kipa wao mpya kwenye Tamasha la Simba Day.Meneja Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameeleza kwa kifupi leo Ijumaa kuwa mashabiki wa timu hiyo hawapaswi kuwa na […]

The post Sapraizi ya kipa mpya Simba Day first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya kuwapo kitendawili cha kipa namba moja wa Simba kwa ajili ya msimu ujao, uongozi wa timu hiyo umejinadi kuwa watafanya ‘sapraizi’ ya utambulisho wa kipa wao mpya kwenye Tamasha la Simba Day.
Meneja Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameeleza kwa kifupi leo Ijumaa kuwa mashabiki wa timu hiyo hawapaswi kuwa na wasiwasi kwani kila kitu kipo tayari na kipa huyo atatambulishwa kwenye tamasha hilo litakalofanyika keshokutwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

“Simba tunakwenda Simba Day tukiwa na wachezaji wote wamekamilika, ikiwemo atakayekuja kuchukua nafasi ya kipa Luis Jefferson naye atatangazwa hapo, ikifika hiyo siku kila kitu kitakuwa hadharani na Wanasimba watamuona kipa wao,” alisema Ally.


Kauli ya Ally imekuja wakagti zipo habari kwamba Simba iko kwenye hatua za mwisho kumnasa kipa anayekipiga nchini Ufaransa ikielezwa jana na leo viongozi wa timu hiyo wamekuwa ‘bize’ kufanya mawasiliano nchini humo kuhakikisha wanamaliza dili hilo mapema.
Wekundu hao wamemgeukia kipa huyo ambaye anafanywa siri kubwa kwa sasa baada ya kuelezwa kumkosa kipa wa Nigeria, John Noble aliyetua Tabora United akitokea Enyimba FC.
Simba inasaka mbadala wa Aishi Manula anayetarajia kuwa nje ya uwanja wa miezi minne baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti nchini Afrika Kusini Mei 30 mwaka huu.
Manula ambaye pia ni kipa namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania au Taifa Stars, aliumia Aprili 7, mwaka huu katika mechi ya Simba dhidi ya Ihefu iliyopigwa kwenye, Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

The post Sapraizi ya kipa mpya Simba Day first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/04/sapraizi-ya-kipa-mpya-simba-day/feed/ 0
Makocha watatu wanukia Simba https://www.greensports.co.tz/2023/06/27/makocha-watatu-wanukia-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/27/makocha-watatu-wanukia-simba/#respond Tue, 27 Jun 2023 19:59:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6731 Na mwandishi wetuKlabu ya Simba imeeleza kuwa imeshakamilisha mchakato wa kuwanasa makocha watatu wapya kwa ajili ya kukamilisha jopo la benchi la ufundi la timu hiyo kwa ajili ya kusaka mafanikio ya msimu ujao.Meneja wa Habari wa Simba, Ahmed Ally (pichani) amesema makocha hao wako vizuri kuziba nafasi tatu zilizoachwa wazi na kocha wa makipa, […]

The post Makocha watatu wanukia Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Simba imeeleza kuwa imeshakamilisha mchakato wa kuwanasa makocha watatu wapya kwa ajili ya kukamilisha jopo la benchi la ufundi la timu hiyo kwa ajili ya kusaka mafanikio ya msimu ujao.
Meneja wa Habari wa Simba, Ahmed Ally (pichani) amesema makocha hao wako vizuri kuziba nafasi tatu zilizoachwa wazi na kocha wa makipa, Zakaria Chlouha, kocha wa viungo, Kelvin Mandla na mtaalam wa viungo, Fareed Cassim.
Ingawa meneja huyo hakuwa tayari kubainisha maelezo mengine juu ya kupatikana kwa makocha hao, alisema mashabiki wa timu hiyo wasiwe na wasiwasi kwani ni makocha wazuri, wenye weledi mkubwa wa utendaji wa kazi zao.

“Kwa sasa tumeshapata wataalamu wote hao watatu kwa maana pia ya kocha wa viungo ambaye yuko vizuri sana, na ubingwa unaanzia kwenye utimamu wa wachezaji, kama una wachezaji legelege maana yake hawatakuwa na uwezo wa kumudu dakika 90 au watakuwa na majeraha kila wakati,” alisema Ally.


Alisema wana imani na makocha hao, wanafahamu kiu ya mashabiki na wapenzi wa Simba ya kuhitaji mafanikio kuanzia msimu ujao hivyo nao wamefanya jambo stahiki katika hilo.
Ally pia alisema kuwa bado wanaendelea na mazungumzo na wachezaji wengine ambao wataachana nao na kwamba hawajamaliza zoezi hilo licha ya kwamba wameshawatema wachezaji saba hadi sasa.

The post Makocha watatu wanukia Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/27/makocha-watatu-wanukia-simba/feed/ 0