Ahly Tripoli - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 22 Sep 2024 16:41:27 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ahly Tripoli - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Simba yairarua Ahly Tripoli 3-1 https://www.greensports.co.tz/2024/09/22/simba-yairarua-ahly-tripoli-3-1/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/22/simba-yairarua-ahly-tripoli-3-1/#respond Sun, 22 Sep 2024 16:15:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11933 Na mwandishi wetuSimba imefuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuichapa Ahly Tripoli ya Libya mabao 3-1 katika mechi iliyopigwa Jumapili hii jioni Septemba 22, 2024 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.Ahly walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 17 lililofungwa na mshambuliaji hatari wa timu hiyo, Paciencia Mabululu, bao lililowaduwaza mashabiki […]

The post Simba yairarua Ahly Tripoli 3-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imefuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuichapa Ahly Tripoli ya Libya mabao 3-1 katika mechi iliyopigwa Jumapili hii jioni Septemba 22, 2024 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Ahly walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 17 lililofungwa na mshambuliaji hatari wa timu hiyo, Paciencia Mabululu, bao lililowaduwaza mashabiki wa Simba na kuwafanya wasielewe nini kilichowakuta.
Kibu Dennis aliwatuliza mashabiki hao katika dakika ya 36 baada ya kusawazisha bao hilo akiitumia vizuri pasi ya kichwa ya Che Malone Fondoh, bao ambalo liliwarudisha Simba katika ubora wao.
Wachezaji wa Simba waliendelea kulisakama lango la Ahly ambao ni kama walianza kujichanganya na Simba kuutumia mwanya huo kuandika bao la pili lililofungwa na Lionel Ateba dakika ya 45.
Ahly baada ya kuona mambo yanakwenda ndivyo sivyo walianza kufanya mabadiliko ikiwamo kumuingiza mshambuliaji wao mahiri Ahmed Arawa aliyechukua nafasi ya Ghaelin Shelel.
Simba nao walijiimarisha kwa mabadiliko kadhaa kwa kuwatoa Yusuf Kagoma, Kibu, Joshua Mutale na Jean Ahoua na nafasi zao kuingia Donald Ngoma, Okejepha Augustine, Edwin Balua na Kelvin Kijili.
Mabadiliko hayo yalikuwa na maana kubwa kwa Simba ambao waliandika bao la tatu lililofungwa na Balua katika dakika ya 90 baada ya kuambaa na mpira na kufumua shuti la chinichini lililomshinda kipa.
Dakika ya 61 Simba ilipata bao lililofungwa na Ateba baada ya Ahoua kumchambua kipa wa Ahly, Ayman Abdullah na kumpasia Ateba lakini bao lilikataliwa kwa madai kuwa mpira uliomfikia Ahoua kutoka kwa Deborah Fernandes ulizaa tukio la kuotea.
Ahly walilitikisa lango la Simba baada ya kufungwa bao la pili wakitaka kuwasazisha, Mabululu aliunasa mpira uliotokana na kona na kuupiga kwa juu lakini kipa wa Simba, Mussa Camara aliyekuwa tayari amehama upande, alionesha umahiri wake kwa kuuwahi mpira huo na kuokoa huku akiwalaumu mabeki wake kwa uzembe.
Baada ya mechi hiyo Ahly walianza kumzonga mwamuzi wakimlaumu tukio ambalo lilimfanya mwamuzi huyo atoe kadi nyekundu ambayo alimpa mshambuliaji wa timu hiyo, Mabululu.
Kwa matokeo hayo, Simba sasa inasubiri kucheza hatua ya makundi ikiwa imefuzu kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya sare ya bila kufungana katika mechi ya kwanza iliyochezwa juma lililopita mjini Tripoli, Libya. Wakati huo huo Simba pia inapata zawadi ya Sh milioni 15 zinazotokana na ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya Sh milioni tano kwa kila bao linalofungwa kwenye mechi ya ushindi ya michuano hiyo.

The post Simba yairarua Ahly Tripoli 3-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/22/simba-yairarua-ahly-tripoli-3-1/feed/ 0
Simba, Ahly Tripoli zatoka sare https://www.greensports.co.tz/2024/09/15/simba-ahly-tripoli-zatoka-sare/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/15/simba-ahly-tripoli-zatoka-sare/#respond Sun, 15 Sep 2024 19:47:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11915 Na mwandishi wetuSimba imeanza kwa sare ya 0-0 na Ahly Tripoli katika mechi yake ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika iliyopigwa leo Jumapili mjini Tripoli, Libya.Wachezaji wa Ahly walikuwa wakishangiliwa kwa nguvu na mashabiki wao walioujaza uwanja, waliuanza mchezo kwa kutawala vyema dakika 20 za kipindi cha kwanza kwa pasi nyingi dhidi ya Simba.Pasi […]

The post Simba, Ahly Tripoli zatoka sare first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imeanza kwa sare ya 0-0 na Ahly Tripoli katika mechi yake ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika iliyopigwa leo Jumapili mjini Tripoli, Libya.
Wachezaji wa Ahly walikuwa wakishangiliwa kwa nguvu na mashabiki wao walioujaza uwanja, waliuanza mchezo kwa kutawala vyema dakika 20 za kipindi cha kwanza kwa pasi nyingi dhidi ya Simba.
Pasi za Ahly katika kipindi hicho zilizalisha mashambulizi kadhaa ambayo yalianzia pembeni hasa kupitia kwa Mohamed Abdusalam na mshambuliaji wa kati, Christopher Mabululu ambaye alilichachafya mara kadhaa lango la Simba.
Katika kipindi hicho mabeki wa Simba wakiongozwa na mlinda mlango Mussa Camara na beki wa kati Che Malone Fondoh walifanikiwa kuyadhibiti mashambulizi hayo kabla ya Simba kuanza kujibu mapigo.
Mashambulizi ya Simba yaliitikisa Ahly hasa kuanzia dakika ya 30 baada ya Jean Ahoua kuunasa mpira akiwa karibu na eneo la kati na kumchungulia kipa wa Ahly aliyetoka kidogo katika eneo lake kabla ya kufumua shuti la juu ambalo bado kidogo liipatie Simba bao.
Kipindi cha pili, Simba ilijiimarisha kwa kocha Fadlu Davids kufanya mabadiliko akianza kuwatoa Ateba na baadaye Joshua Mutale na nafasi zao kuingia Valentino Mashaka na Kibu Dennis ambao walizidi kuipa uhai Simba katika eneo la ushambuliaji na baadaye kumtoa Edwin Balua na nafasi yake kuingi Augustine Okehefa.
Ahly nao hawakuwa nyuma katika kusaka bao ambapo Fondoh alilazimika kufanya juhudi binafsi kuutoa mpira mbele ya mshambuliaji wa Ahly ambaye alikuwa akielekea kukutana na kipa wa Simba kabla ya kuanguka chini na kuanza kulalamika akitaka timu yake ipewe penalti.
Tukio hilo lilizua tafrani ya muda mfupi kwa wachezaji wa Ahly kumzonga mwamuzi ambaye hata hivyo alishikilia msimamo wake wa kuipa timu hiyo kona akikataa kwamba Fondoh alicheza rafu ndani ya eneo la penalti.
Simba waliendelea kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Ahoua na Deborah Fernandes na nafasi zao kuingia Chamou Karaboué na Donald Ngoma wakati Ahly nao wakati huo huo walimuingiza mshambuliaji wao tishio Ahmed Akrawa ambaye alikuwa akiimbwa na mashabiki wa timu hiyo.
Mshambuliaji huyo aliongeza uhai kwenye safu ya ushambuliaji na dakika chache kabla ya kutimua dakika 90, nusura aipatie timu hiyo bao baada ya kuunganisha krosi iliyotokea upande wa kulia wa Ahly lakini mpira alioupiga kwa kichwa uligonga mwamba na kurudi uwanjani.
Matokeo ya mechi hiyo yanaweza kuwa msaada kwa Simba kusonga mbele kama wataweza kuutumia vyema uwanja wa nyumbani katika mechi ya marudiano itakayopigwa wikiendi ijayo.

The post Simba, Ahly Tripoli zatoka sare first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/15/simba-ahly-tripoli-zatoka-sare/feed/ 0