Afcon 2027 - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 04 Jul 2024 06:08:36 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Afcon 2027 - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ndumbaro akagua CCM Kirumba https://www.greensports.co.tz/2024/07/04/ndumbaro-akagua-ccm-kirumba/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/04/ndumbaro-akagua-ccm-kirumba/#respond Thu, 04 Jul 2024 06:08:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11508 Na mwandishi wetuWaziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro, amekagua hali ya Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza uliopo kwenye mpango wa kufanyiwa ukarabati mkubwa kwa ajili ya michuano ya Afcon 2027.Ndumbaro amefanya ukaguzi huo Jumanne hii akiwa ameambatana na Mbunge wa llemela, Angelina Mabula ambapo amekagua eneo la kuchezea, vyumba vya kubadilishia nguo […]

The post Ndumbaro akagua CCM Kirumba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro, amekagua hali ya Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza uliopo kwenye mpango wa kufanyiwa ukarabati mkubwa kwa ajili ya michuano ya Afcon 2027.
Ndumbaro amefanya ukaguzi huo Jumanne hii akiwa ameambatana na Mbunge wa llemela, Angelina Mabula ambapo amekagua eneo la kuchezea, vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji, sehemu za maliwato na eneo la watu mashuhuri.
Ndumbaro amesema mpango wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ni kufanya ukarabati mkubwa wa uwanja huo ambao utatumika kama uwanja wa mazoezi wakati wa Afcon 2027.
Fainali za Afcon 2027 ambazo hushirikisha nchi za mataifa ya Afrika kwa mwaka 2027 zitafanyika katika nchi majirani Afrika Mashariki za Tanzania, Kenya na Uganda .
Kwa Tazania viwanja vingine vitakavyokarabatiwa ni Jamhuri Morogoro, Uwanja wa Majimaji-Songea, Mkwakwani-Tanga na Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

The post Ndumbaro akagua CCM Kirumba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/04/ndumbaro-akagua-ccm-kirumba/feed/ 0
Mawaziri waunda kamati Afcon, Chan https://www.greensports.co.tz/2024/05/07/mawaziri-waunda-kamati-afcon-chan/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/07/mawaziri-waunda-kamati-afcon-chan/#respond Tue, 07 May 2024 19:48:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10877 Na mwandishi wetuWaziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Tabia Mwita wameunda Kamati ya Taifa ya Maandalizi ya michuano ya CHAN 2024 na AFCON 2027 chini ya uenyekiti wa Leodegar Tenga.Kamati hiyo imetangazwa baada ya kikao cha jana Jumatatu mjini Dodoma kilichohusisha wizara hizo […]

The post Mawaziri waunda kamati Afcon, Chan first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Tabia Mwita wameunda Kamati ya Taifa ya Maandalizi ya michuano ya CHAN 2024 na AFCON 2027 chini ya uenyekiti wa Leodegar Tenga.
Kamati hiyo imetangazwa baada ya kikao cha jana Jumatatu mjini Dodoma kilichohusisha wizara hizo mbili, kikiwa ni maalum kwa ajili ya kujadili maandalizi ya michuano hiyo ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa Afcon ikishirikiana na nchi za Kenya na Uganda.
Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo ni Ayoub Mahmoud, katibu ni Neema Msitha, katibu msaidizi ni Said Marine wakati wajumbe ni Wallace Karia, Suleiman Jabir, Nehemia Mchechu, Wilfred Kidao, Ally Mayay, Ameir Makame, Naima Shaame, Mohamed Abdulaziz na Madundo Mtambo.
Wengine ni Aboubakar Bakhresa, Jacqline Kawishe, Gilead Teri, Ramadhan Dau, Hassan Mabena, Abdul Nsekela, Jumanne Muliro, Abdul Mhinte, Saleh Ally, Hamad Abdallah, Johnson Pallangyo na Kheri Ally.
Mbali na uteuzi huo, pia kikao hicho kilijadili ukarabati wa miundombinu ambayo itatumika katika michuano hiyo kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar kwa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na wakaguzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

The post Mawaziri waunda kamati Afcon, Chan first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/07/mawaziri-waunda-kamati-afcon-chan/feed/ 0
Tanzania yataja viwanja Afcon 2027 https://www.greensports.co.tz/2023/09/29/tanzania-yataja-viwanja-afcon-2027/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/29/tanzania-yataja-viwanja-afcon-2027/#respond Fri, 29 Sep 2023 17:01:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7888 Na mwandishi wetuSiku mbili baada ya Tanzania, Uganda na Kenya kutangazwa kuwa waandaaji wa fainali za Kombe la Mataifa Afrika 2027 (Afcon), imewekwa wazi kuwa kwa Tanzania vitatumika viwanja vitatu katika michuano hiyo.Akizungumza leo Ijumaa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania, Ally Mayay alisema viwanja vitakavyotumika ni Benjamin Mkapa, Dar es […]

The post Tanzania yataja viwanja Afcon 2027 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Siku mbili baada ya Tanzania, Uganda na Kenya kutangazwa kuwa waandaaji wa fainali za Kombe la Mataifa Afrika 2027 (Afcon), imewekwa wazi kuwa kwa Tanzania vitatumika viwanja vitatu katika michuano hiyo.
Akizungumza leo Ijumaa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania, Ally Mayay alisema viwanja vitakavyotumika ni Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Uwanja wa Amaan wa Zanzibar na Uwanja wa The Hexagon uliopo Arusha unaotarajia kuanza kujengwa mwanzoni mwa mwaka 2024.
“Viwanja vya mashindano ni vinane kwa nchi hizi tatu, Tanzania tulichagua ule wa Benjamin Mkapa, Uwanja wa Amaan Zanzibar na uwanja mpya wa Arusha. Ni uwanja wa kisasa ambao unajengwa nje ya mji, Kata ya Olmoti na utakuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 30,000 waliokaa,” alisema Mayay.
Uwanja wa Mkapa ndio mkubwa zaidi Tanzania na Afrika Mashariki wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 60,000, huku Uwanja wa Amaan ukiwa na uwezo wa kuingiza kuanzia mashabiki 15,000.
Tanzania, Uganda na Kenya ambazo zimeita umoja huo Pamoja Bid zilishinda kwenye kinyang’anyiro hicho juzi kwa kuzibwaga nchi za Misri, Senegal na Botswana wakati Algeria ilijitoa kwenye ushindani huo dakika za mwisho.

The post Tanzania yataja viwanja Afcon 2027 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/29/tanzania-yataja-viwanja-afcon-2027/feed/ 0
Tanzania, Kenya, Uganda wenyeji Afcon 2027 https://www.greensports.co.tz/2023/09/27/tanzania-kenya-uganda-wenyeji-afcon-2027/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/27/tanzania-kenya-uganda-wenyeji-afcon-2027/#respond Wed, 27 Sep 2023 13:26:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7864 Cairo, MisriWakati Morocco ikitangazwa kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Matafa ya Afrika (Afcon) 2025, nchi majirani Afrika Mashariki za Tanzania, Kenya na Uganda zimeshinda nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali hizo mwaka 2027.Akitangaza ushindi wa nchi hizo, leo Jumatano Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe alisema kwamba fainali za 2027 […]

The post Tanzania, Kenya, Uganda wenyeji Afcon 2027 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Cairo, Misri
Wakati Morocco ikitangazwa kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Matafa ya Afrika (Afcon) 2025, nchi majirani Afrika Mashariki za Tanzania, Kenya na Uganda zimeshinda nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali hizo mwaka 2027.
Akitangaza ushindi wa nchi hizo, leo Jumatano Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe alisema kwamba fainali za 2027 zitakuwa nzuri kutokana na namna ambavyo marais watatu wa nchi za Afrika Mashariki walivyojitoa kwa jili ya fainali hizo.

“Hii inaonesha ni kwa kiasi gani ukanda huu ulikuwa na shauku kubwa ya kuwa wenyeji wa fainali hizi,” alisema Motsepe mara baada ya mkutano wa CAF uliofanyika mjini Cairo.


Tanzania, Kenya na Uganda zimeshinda nafasi hiyo dhidi ya nchi za Senegal, Botswana na Algeria ambayo inadaiwa iliamua kujitoa siku mbili kabla ya kutangazwa kwa mshindi wa kinyang’anyiro hicho.
Kufuzu kwa nchi hizo za Afrika Mashariki ni hatua ya kwanza lakini bado nchi hizo zina kazi ya kuweka miundombinu hasa ya viwanja katika ubora ambao wakaguzi wa CAF watauridhia.

The post Tanzania, Kenya, Uganda wenyeji Afcon 2027 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/27/tanzania-kenya-uganda-wenyeji-afcon-2027/feed/ 0