Afcon 2025 - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 01 Apr 2026 18:17:11 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Afcon 2025 - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Katibu Mkuu CAF aachia ngazi https://www.greensports.co.tz/2026/03/30/katibu-mkuu-caf-aachia-ngazi/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/30/katibu-mkuu-caf-aachia-ngazi/#respond Mon, 30 Mar 2026 19:22:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14505 Cairo, MisriKatibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Veron Mosengo-Omba (pichani) amejiuzulu nafasi hiyo wakati shirikisho hilo likiwa katika mgogoro baada ya Senegal kuvuliwa taji la ubingwa wa Afrika (Afcon 2025).Senegal ambayo iliibuka kinara na kutangazwa mshindi wa taji hilo baada ya kupata ushindi katika mechi ya fainali dhidi ya wenyeji Morocco imevuliwa ushindi […]

The post Katibu Mkuu CAF aachia ngazi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Cairo, Misri
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Veron Mosengo-Omba (pichani) amejiuzulu nafasi hiyo wakati shirikisho hilo likiwa katika mgogoro baada ya Senegal kuvuliwa taji la ubingwa wa Afrika (Afcon 2025).
Senegal ambayo iliibuka kinara na kutangazwa mshindi wa taji hilo baada ya kupata ushindi katika mechi ya fainali dhidi ya wenyeji Morocco imevuliwa ushindi huo na kupewa Morocco sababu ikitajwa kuwa ni kitendo cha timu hiyo kugomea mechi hiyo kwa takriban dakika 17.
Mosengo-Omba, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambaye ameshika wadhifa huo kwa takriban miaka mitano, hata hivyo katika taarifa yake ya kujiuzulu hakutaja suala la Senegal.
Badala yake alisema kwa ufupi tu kuwa ameamua kujiuzulu ili awe na muda wa kutosha kwa ajili ya masuala yake binafsi.

“Kwa hili nimeweza kuvunja uvumi ambao baadhi ya watu wamekuwa nao kwa kiwango kikubwa wakinihusisha mimi, sasa nastaafu kwa amani ya moyo bila matatizo,” alisema Mosengo-Omba.


Naye Rais wa CAF, Dk Patrice Motsepe aliwaambia waandishi wa habari kuwa Mosengo-Omba amejiuzulu kwa lengo la kwenda kusaidia maendeleo ya soka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuombwa na rais wa nchi hiyo, Felix Tshisekedi.
Dk Motsepe alimshukuru Mosengo-Omba kwa mchango wake na kazi aliyoifanya katika maendeleo na mafanikio ya soka la Afrika.
Kwa sasa nafasi ya Mosengo-Omba itashikwa kwa muda na mkurugenzi wa mashindano wa shirikisho hilo, Samson Adamu kutoka Nigeria ambapo Dk Motsepe amesema anaamini Adamu atafanya kazi nzuri na atasaidia kuifanya CAF ipige hatua mbele.
Dk Motsepe pia alisema kwamba makamu wa rais wa CAF wataongoza mchakato wa kumchagua katibu mkuu mpya na baada ya hapo ripoti ya mchakato huo itawasilishwa kwake (Dk Motseppe).

The post Katibu Mkuu CAF aachia ngazi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/30/katibu-mkuu-caf-aachia-ngazi/feed/ 0
CAF yaivua Senegal taji la Afcon https://www.greensports.co.tz/2026/03/19/caf-yaivua-senegal-taji-la-afcon/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/19/caf-yaivua-senegal-taji-la-afcon/#respond Thu, 19 Mar 2026 07:34:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14457 Cairo, MisriBodi ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imeivua timu ya taifa ya Senegal taji la Afcon 2025 kwa kosa la kwenda kinyume na kanuni namba 84 na kuifutia ushindi wa bao 1-0 badala yake imeipa Morocco ushindi wa ‘mezani’ wa mabao 3-0.Senegal imevuliwa taji hilo kwa kosa la kugomea mechi kwa takriban […]

The post CAF yaivua Senegal taji la Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Cairo, Misri
Bodi ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imeivua timu ya taifa ya Senegal taji la Afcon 2025 kwa kosa la kwenda kinyume na kanuni namba 84 na kuifutia ushindi wa bao 1-0 badala yake imeipa Morocco ushindi wa ‘mezani’ wa mabao 3-0.
Senegal imevuliwa taji hilo kwa kosa la kugomea mechi kwa takriban dakika 17, tukio lililotokea katika mechi ya fainali baina ya timu hizo iliyopigwa Januari 18 na timu hiyo kugomea mechi kwa madai kwamba mwamuzi alikuwa akiwabeba wenyeji Morocco.
Uamuzi huo wa CAF umetokana na malalamiko yaliyowasilishwa na Shirikisho la Soka la Morocco ambapo Bodi ya Rufaa ya CAF iliona kuna kosa kwa upande wa Shirikisho la Soka Senegal kupitia timu yao ya taifa.
Katika mechi hiyo ya fainali iliyopigwa mjini Rabat, Senegal walisusia penalti iliyotolewa baada ya El Hadji Malick Diouf kumuangusha Brahim Diaz katika eneo la penalti ingawa Diaz aliyepewa kupiga penalti hiyo alikosa.
Senegal au Simba wa Teranga walizitumia vyema dakika 30 za nyongeza kupata bao pekee na la ushindi dakika ya tatu (93) kwa mpira ulioanzia kwa pasi ya kisigino ya Mane aliyemuunganishia Idrissa Gana Gueye naye kumpasia Pape Gueye aliyeujaza wavuni.
Uamuzi wa CAF kuivua Senegal taji ambalo walilipigania kwa mbinde baada ya mechi iliyochezwa kwa dakika 120, umezua taharuki miongoni mwa wadau wa soka duniani kote.
Mmoja wa watu waliojitokeza hadharani kupinga uamuzi huo ni kiungo wa zamani wa Arsenal, Man City na timu ya taifa ya Ufaransa, Samir Nassir ambaye alionesha kushtushwa na uamuzi huo akisema si sahihi.
Kwa upande mwingine Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Senegal, Abdoulaye Seydou amehoji uhalali wa uamuzi huo ambao wanaona ni kama vile hautokani na taratibu za kisheria badala yake kulikuwa na maelekezo.
Shirikisho hilo linadaiwa kuanza mchakato wa kupinga uamuzi huo kupitia Mahakama ya Kimataifa ya Michezo (CAS) wakati baadhi ya wachezaji wa Senegal wakidai kwamba hawatorudisha medali za ushindi huo huku Idrissa Gueye akisisitiza kwamba mafanikio yao ya kihistoria katika mji wa Rabat hawawezi kuacha yapotee.
Serikali ya Senegal nayo imeingilia kati suala hilo ikisema kwamba uamuzi huo umetokana na makosa ya kutafsiri sheria na hivyo kuja na uamuzi ambao si wa haki.

The post CAF yaivua Senegal taji la Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/19/caf-yaivua-senegal-taji-la-afcon/feed/ 0
Senegal mabingwa Afcon 2025 https://www.greensports.co.tz/2026/01/23/senegal-mabingwa-afcon-2025/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/23/senegal-mabingwa-afcon-2025/#respond Fri, 23 Jan 2026 19:37:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14272 Rabat, MoroccoBaada ya mpambano na dakika 120 za kukata na shoka, hatimaye timu ya taifa ya Sernegal imeibuka kinara wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 baada ya kuwanyuka wenyeji Morocco bao 1-0.Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili Januari 18, 2026, hadi kupata ushindi, Senegal walijikuta katika wakati mgumu wa kususia mchezo wakidai mwamuzi alikuwa […]

The post Senegal mabingwa Afcon 2025 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rabat, Morocco
Baada ya mpambano na dakika 120 za kukata na shoka, hatimaye timu ya taifa ya Sernegal imeibuka kinara wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 baada ya kuwanyuka wenyeji Morocco bao 1-0.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili Januari 18, 2026, hadi kupata ushindi, Senegal walijikuta katika wakati mgumu wa kususia mchezo wakidai mwamuzi alikuwa akiwabeba wenyeji Morocco ingawa baadaye walirudi uwanjani kuendelea na mchezo.
Tukio hilo lilitokea katika dakika za nyongeza (dakika ya 98) kabla ya dakika 90 za kawaida kumalizika baada ya Morocco kupewa penalti iliyotokana na kosa la El Hadji Malick Diouf kumuangusha Brahim Diaz.
Wachezaji wa Senegal kwa ushawishi wa kocha wao, Pape Thiaw waliingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakisusia penalti ambayo hata hivyo Diaz, mpira alioupiga uliokolewa na kipa wa Senegal, Edouard Mendy.
Baadaye Mendy na Sadio Mane walionekana wakiwashawishi wachezaji hao kurudi uwanjani kuendelea na mchezo wakati huo timu zikiwa hazijafungana na ndipo zilipoongezwa dakika nyingine 30.
Senegal au Simba wa Teranga walizitumia vyema dakika 30 za nyongeza kupata bao dakika ya tatu (93) kwa mpira ulioanzia kwa pasi ya kisigino ya Mane aliyemuunganishia Idrissa Gana Gueye naye kumpasia Pape Gueye aliyeujaza wavuni.
Gueye licha ya kufunga bao hilo, pia ametangazwa kuwa nyota wa mchezo na baada ya mechi hiyo alisema kwamba
anajisikia furaha kupata ushindi katika mechi iliyotawaliwa na utata lakini walitulia hasa baada ya Morocco kukosa penalti.
Mane, nyota wa zamani wa Liverpool na Bayern Munich ambaye inaelezwa kuwa hizi ni fainali zake za mwisho za Afcon, akiwa ndiye nahodha katika mchezo huo alionesha ujasiri wa kuwatuliza wenzake na hatimaye juhudi zake zikazaa matunda kwa Senegal kubeba taji.

The post Senegal mabingwa Afcon 2025 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/23/senegal-mabingwa-afcon-2025/feed/ 0
Salah hataki Misri ilewe sifa https://www.greensports.co.tz/2026/01/08/salah-hataki-misri-ilewe-sifa/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/08/salah-hataki-misri-ilewe-sifa/#respond Thu, 08 Jan 2026 19:01:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14257 Rabat, MoroccoNahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah amepuuza habari inayoiweka timu yao katika orodha ya timu zinazopewa nafasi kubwa kubeba taji ya michuano ya Afcon 2025 inayoendelea nchini Morocco.Salah ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya Liverpool ya England, badala yake amesema kwamba wanachofanya katika fainali za Afcon ni kuweka […]

The post Salah hataki Misri ilewe sifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rabat, Morocco
Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah amepuuza habari inayoiweka timu yao katika orodha ya timu zinazopewa nafasi kubwa kubeba taji ya michuano ya Afcon 2025 inayoendelea nchini Morocco.
Salah ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya Liverpool ya England, badala yake amesema kwamba wanachofanya katika fainali za Afcon ni kuweka mkazo kwa kila mechi wanayocheza.
Misri kwa sasa inapambana kusaka taji la nane la Afcon, tayari imefuzu hatua ya robo fainali baada ya kuichapa Benin mabao 3-1 huku Salah akiwa moto kwenye mechi hiyo akifunga bao la tatu na hadi sasa ana mabao matatu katika fainali hizo.
Timu hiyo imeonesha kiwango cha kuvutia katika Afcon 2025 lakini Salah yuko makini katika matarajio makubwa ambayo yanahusishwa na timu hiyo kwa kupewa nafasi kubwa ya kubeba taji.

“Tuna wachezaji wachanga na wengi wao wanacheza soka nyumbani Misri, tunachofanya ni kuipigania nchi yetu na baada ya hapo tutaona tutakapofika, kila mmoja hapa anataka kujitoa katika ubora wake,” alisema Salah.


Katika fainali za Afcon zinazoendelea, Salah hadi sasa amekosa mechi moja ya hatua ya makundi dhidi ya Angola, mechi ambayo Misri walicheza wakiwa tayari wamefuzu hatua ya mtoano (16 bora) na kukutana na Benin.
Uamuzi wa kocha Hossam Hassan kumuweka benchi mchezaji huyo ulionekana kuwa na faida kubwa kwa namna ambavyo alikuwa tishio katika mechi dhidi ya timu sumbufu ya Benin na hatimaye kutoka na ushindi.
Salah pia aliipongeza Benin akisema kwamba Misri ilicheza dhidi ya timu nzuri yenye kocha bora na mfumo mzuri na wana furaha kwa kupata ushindi ingawa anakiri haikuwa kazi rahisi.
.

The post Salah hataki Misri ilewe sifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/08/salah-hataki-misri-ilewe-sifa/feed/ 0
Taifa Stars yafa kiume https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/taifa-stars-yafa-kiume/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/taifa-stars-yafa-kiume/#respond Sun, 04 Jan 2026 19:49:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14252 Rabat, MoroccoUmewahi kusikia hadithi ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kufa kiume, achana na hadithi zote za nyuma, hadithi ya kweli imetokea leo Jumapili Januari 4, 2026 kwa timu hiyo kufungwa bao 1-0 na Morocco kwenye fainali za Afcon 2025.Stars ikiumana na wenyeji Morocco katika mechi ya hatua ya mtoano (16 bora) imekubali […]

The post Taifa Stars yafa kiume first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rabat, Morocco
Umewahi kusikia hadithi ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kufa kiume, achana na hadithi zote za nyuma, hadithi ya kweli imetokea leo Jumapili Januari 4, 2026 kwa timu hiyo kufungwa bao 1-0 na Morocco kwenye fainali za Afcon 2025.
Stars ikiumana na wenyeji Morocco katika mechi ya hatua ya mtoano (16 bora) imekubali kipigo hicho na hivyo kuaga fainali hizo huku ikiweka rekodi ya kipekee kwa kupambana kisawasawa na Morocco ambao ni wenyeji wa fainali hizo.
Matarajio ya Stars kufungwa mabao mengi yalitoweka na hadi dakika 90 zinamalizika Morocco, timu lenye hadhi na heshima yake katika soka, Afrika na duniani kote, ilishikwa kila kona na kujikuta ikiambulia bao hilo pekee.
Morocco ambao kwa ushindi huo wamefuzu hatua ya robo fainali, waliuanza mchezo kwa kufanya mashambulizi na kuongoza kwa umiliki wa mpira kwa zaidi ya asilimia 70 katika kipindi chote cha kwanza lakini nidhamu ya safu ya ulinzi ya Stars ilikuwa kikwazo.
Safu hiyo ya ulinzi ya Stars ilifanikiwa kuwavuruga Morocco mbele ya maelfu ya mashabiki wao ambao licha ya kushangilia kwa muda mwingi, hawakuamini kuona timu zikitoka uwanjani kwenda mapumziko bila kufungana.
Moja ya nafasi ambazo Morocco walizitengeneza lakini hazikuweza kuwapatia bao ni katika dakika ya 24 baada ya Ismail Saibari kuuwahi mpira wa juu na kuujaza wavuni kwa kichwa lakini mwamuzi alikataa bao hilo baada ya kutumia VAR kwa madai kwamba mfungaji aliotea.
Stars ambao wanajivunia rekodi ya kufikia hatua ya mtoano ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza, nao walifanya mashambulizi kadhaa kwa nidhamu ya hali ya juu, mfano katika kipindi hicho Simon Msuva akiwa ndani ya 18 alishindwa kuunganisha vyema krosi ya Seleman Abdallah.
Kipindi cha pili juhudi za Morocco zilizaa matunda dakika ya 63 baada ya kupata bao hilo pekee lililotokana na shuti la chini lililopigwa na mshambuliaji wa Real Madrid, Brahim Diaz na kujaa wavuni huku kipa Hussein Masalanga akiishia kuugusa mpira huo na mkono wake wa kushoto.
Stars, licha ya kufungwa bao hilo lakini waliendelea kuonesha upambanaji bila kujali aina ya mpinzani waliyekuwa wakishindana naye na katika dakika za lala salama, Iddi Nado aliangushwa na beki wa Morocco, Adam Masina wakati akiambaa na mpira kuelekea lango la Morocco.
Kuangushwa kwa mchezaji huyu kuliibua malalamiko kwa wachezaji na benchi la Stars wakitaka wapewe penalti au VAR itumike ili kujua undani wa tukio hilo lakini mwamuzi wa mechi hiyo, Boubou Traore alikataa kutoa penalti.
Wakati Stars ikiziaga fainali hizo ikiwa kifua mbele, Morocco sasa wanasubiri kuumana na mshindi wa mechi kati ya Afrika Kusini na Cameroon katika mechi ya robo fainali.

The post Taifa Stars yafa kiume first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/taifa-stars-yafa-kiume/feed/ 0
Stars wananifikirisha ya Chipolopolo https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/stars-wananifikirisha-ya-chipolopolo/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/stars-wananifikirisha-ya-chipolopolo/#respond Sun, 04 Jan 2026 06:22:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14247 Na Hassan KinguTimu ya taifa ya Morocco imekamilika kila idara, historia yake inatisha, si Afrika tu bali duniani kote, tayari imeonesha ubora wake kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 kwa kufika hatua ya nusu fainali.Unapozungumzia Kombe la Dunia maana yake ni kwamba unazungumzia mashindano makubwa ya soka duniani, Morocco wameonesha ubora wao katika michuano […]

The post Stars wananifikirisha ya Chipolopolo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Hassan Kingu
Timu ya taifa ya Morocco imekamilika kila idara, historia yake inatisha, si Afrika tu bali duniani kote, tayari imeonesha ubora wake kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 kwa kufika hatua ya nusu fainali.
Unapozungumzia Kombe la Dunia maana yake ni kwamba unazungumzia mashindano makubwa ya soka duniani, Morocco wameonesha ubora wao katika michuano hiyo na kuingia katika orodha ya timu tishio.
Morocco ni timu ya kwanza barani Afrika kufikia nusu fainali ya Kombe la Dunia, hii ni rekodi ya kipekee na ya kujivunia si kwa Morocco tu bali hata Shirikisho la Soka Afrika (CAF) linajivunia rekodi hiyo.
Katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) zinazoendelea nchini Morocco, wenyeji hao Morocco ni timu inayopewa nafasi kubwa kama si nafasi ya kwanza kubeba taji hilo au kulibakisha nyumbani.
Morocco hiyo ambayo inatisha Afrika yenye rekodi za kutisha kuanzia kwenye Afcon yenyewe, Jumapili hii ya Januari 4, 2026 itacheza na timu ya taifa ya Tanzania au Taifa Stars, timu ambayo haikuwamo katika timu zinazopewa nafasi ya japo kufikia hatua ya robo fainali.
Si robo fainali tu, Taifa Stars haikuwamo hata katika timu ambazo ungeweza kuzitaja kuwa zitavuka hatua ya makundi, ni timu ambayo ilihusishwa na mechi tatu za makundi na baada ya hapo kurudi nyumbani.
Kilichotokea ni tofauti na matarajio ya wengi, hata baadhi ya mashabiki wachache wa Tanzania ambao pengine hawakupenda kuona timu hiyo inafanikiwa wameshangazwa na hatua ambayo timu imefikia.
Huenda hata wachezaji wenyewe hawakutarajia kama wangefanya vizuri kiasi cha kufuzu kucheza hatua ya mtoano (16 bora) na hilo linathibitishwa na hali ya furaha waliyokuwa nayo baada ya kufuzu kiasi cha kuimba kibao cha ‘Sisi ndio wale wale mliotukataa mkasema hatufiki mbali…’
Kimsingi Taifa Stars iliingia katika Afcon ikiwa kile kinachoitwa ‘underdogs’ unaweza kusema ni timu dhaifu lakini leo imepiga hatua na sasa inasubiri kukabiliana na Morocco au miamba ya soka barani Afrika.

Wanachokutana nacho Stars leo kinanikumbusha tukio la mwaka 2012, timu ya taifa ya Zambia ikiwa chini ya kocha Mfaransa, Renard Herve ililishangaza bara la Afrika, haikuwa timu iliyotajwa au kupewa nafasi ya kufika mbali, mafanikio pekee ambayo ilihusishwa nayo ni kupambana hadi kufika hatua ya robo fainali.
Hali ikawa tofauti, Zambia au Chipolopolo (pichani) ilipiga hatua moja baada ya nyingine ikiwapangua vigogo na mwishowe ikafika fainali na kubeba taji hilo katika michuano iliyofanyika Guinea ya Ikweta na Gabon.
Katika fainali za 2012 kuna ukweli kwamba baadhi ya nchi mahiri katika soka Afrika zilikuwa na matatizo ya kisiasa kuanzia Misri, Libya na Algeria, hapo hapo timu za Nigeria, Afrika Kusini na Cameroon zilishindwa kufuzu.
Kwa baadhi ya wachambuzi hali hiyo ilijengewa hoja kwamba ndio sababu mojawapo ya Zambia kufanya vizuri hadi kubeba taji la michuano hiyo lakini kimsingi kilichowawezesha Zambia kubeba taji ni uwezo na kujiamini kwa wachezaji.
Kujiamini huko ndiko kulikoifanya timu hiyo ipenye hadi kubeba taji katika michuano ambayo pia ilishirikisha mataifa mengine mahiri katika soka la Afrika kuanzia Morocco, Senegal na wenyeji Guinea na Gabon.
Kubwa kuliko yote ni ushindi wao katika mechi ya fainali dhidi ya Ivory Coast, taifa ambalo lina heshima yake katika soka la Afrika na kabla ya mechi ndiyo timu iliyotajwa na wachambuzi na hata wacheza kama kuwa ndiyo ambayo ingebeba taji hilo na kuwa taji lao la nne kwa wakati huo.
Hali hata hivyo ikawa kinyume, Zambia wakaishangaza Afrika, wakawashangaza wachambuzi na wacheza kamari, wakaushangaza ulimwengu kwa kutoka sare na Ivory Coast kabla ya kuwatoa kwenye penalti na kubeba taji.
Sijui ni kwa nini na huenda si mimi peke yangu, historia ya Chipolopolo hadi kuibwaga Ivory Coast na kubeba taji la Afcon 2012 inanifikirisha wakati huu Taifa Stars ikijiandaa kuikabili Morocco.

The post Stars wananifikirisha ya Chipolopolo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/stars-wananifikirisha-ya-chipolopolo/feed/ 0
Serikali Gabon yaifuta timu ya taifa https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/serikali-gabon-yaifuta-timu-ya-taifa/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/serikali-gabon-yaifuta-timu-ya-taifa/#respond Sun, 04 Jan 2026 06:17:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14244 Libreville, GabonSerikali nchini Gabon imechukua uamuzi mgumu wa kuifuta timu ya taifa baada ya kufanya vibaya kwenye fainali za Afcon zinazoendelea nchini Morocco.Sambamba na hilo, serikali hiyo pia imemuondoa katika kikosi hicho mshambuliaji mkongwe wa timu hiyo, Pierre-Emerick Aubameyang pamoja na kumfuta kazi kocha mkuu wa timu hiyo, Thierry Mouyouma na kulivunja benchi zima la […]

The post Serikali Gabon yaifuta timu ya taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Libreville, Gabon
Serikali nchini Gabon imechukua uamuzi mgumu wa kuifuta timu ya taifa baada ya kufanya vibaya kwenye fainali za Afcon zinazoendelea nchini Morocco.
Sambamba na hilo, serikali hiyo pia imemuondoa katika kikosi hicho mshambuliaji mkongwe wa timu hiyo, Pierre-Emerick Aubameyang pamoja na kumfuta kazi kocha mkuu wa timu hiyo, Thierry Mouyouma na kulivunja benchi zima la ufundi.
Vipigo mfulululizo vimeifanya timu hiyo iage mapema fainali za Afcon ikianza kwa kuchapwa bao 1-0 na mahasmu wao Cameroon kabla ya kukutana na kichapo cha mabao 3-2 mbele ya Msumbiji.
Uamuzi huo wa Serikali ya Gabon umechukuliwa ikiaminika sababu ikiaminika kuwa ni kutofurahishwa na mwenendo mzima wa timu hiyo kwenye Afcon na inadaiwa hatua nyingine zitafuata baada ya uamuzi huo.

“Kwa kuzingatia madhara ya jumla ya mwenendo wa timu, serikali imeamua kulivunja benchi zima la ufundi kuifuta timu ya taifa hadi uamuzi mwingine utakapofikiwa na kuwaondoa katika timu hiyo wachezaji Bruno Ecuélé Manga na Pierre-Emerick Aubameyang,”ilieleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Waziri wa Michezo wa Gabon, Simplice-Desire Mamboula.


Aubameyang (pichani juu) na Ecuele Manga ambao awali walijiuzulu kuichezea timu hiyo kabla ya kubadili maamuzi na kuitwa katika kikosi hicho, kila mmoja wao alikuwa nahodha katika mechi mbili za awali za Afcon.
Kitendo cha Aubameyang ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 36, kurudi katika timu hiyo kiliwashangaza baadhi ya watu kwa kuwa alikuwa akijiuguza baada ya kuumia wakati akiitumikia timu ya Marseille ya Ufaransa kabla ya kuanza kwa fainali za Afcon.
Kwa upande wake, Aubameyang alijitetea akisema kwamba anadhani matatizo ya timu ya taifa ya Gabon ni makubwa kuliko kumuangalia yeye mtu mmoja.
Uamuzi huo wa serikali hata hivyo huenda ukaiingiza nchi hiyo katika mgogoro na Fifa kwa kuwa kanuni za Fifa haziruhusu serikali kujiingiza na kuchukua hatua katika masuala yahusuyo soka.

The post Serikali Gabon yaifuta timu ya taifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/serikali-gabon-yaifuta-timu-ya-taifa/feed/ 0
Kocha Nigeria awajia juu wachambuzi https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/kocha-nigeria-awajia-juu-wachambuzi/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/kocha-nigeria-awajia-juu-wachambuzi/#respond Sun, 04 Jan 2026 06:08:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14237 Rabat, MoroccoKocha wa timu ya taifa ya Nigeria, Eric Chelle amewajia juu wachambuzi waliokuwa wakimkosoa baada ya timu yake kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Tunisia kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025.Matokeo hayo ya mechi ya hatua ya makundi yaliibua shutuma dhidi ya Chelle kutokana na mabadiliko ya wachezaji aliyokuwa […]

The post Kocha Nigeria awajia juu wachambuzi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rabat, Morocco
Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria, Eric Chelle amewajia juu wachambuzi waliokuwa wakimkosoa baada ya timu yake kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Tunisia kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025.
Matokeo hayo ya mechi ya hatua ya makundi yaliibua shutuma dhidi ya Chelle kutokana na mabadiliko ya wachezaji aliyokuwa akiyafanya kocha huyo ambapo mashabiki na wachambuzi hawakuyakubali.
Kelele za mashabiki na hoja za wachambuzi zilitokana na mtazamo hasi kuhusu mabadiliko ambayo yalionekana kuibua hofu kwamba Nigeria ingeweza kupoteza ponti tatu katika mechi ambayo walionekana kuitawala vyema.
Chelle (pichani juu) hata hivyo alieleza kushangazwa kwake na mtazamo huo hasa kwa kuwa hakuna ambaye anazungumzia hali ilivyokwa katika mechi hiyo kwa kipindi cha kwanza hadi dakika ya 75 na jinsi kasi ya mchezo ilivyokuwa.
Kocha huyo alisema kwamba watu hawazungumzii kuhusu mbinu na hadhi ya wachezaji au namna ambavyo timu ilikuwa na haki ya kushinda na imepata ushindi mkubwa.

“Katika mechi hii tulikuwa vizuri kwa dakika 75, hadi mwishoni mwa kipindi cha kwanza tulitawala mchezo kwa asilimia 70 na hadi inafika dakika ya 75 tulikuwa timu bora uwanjani kwa hiyo nina furaha na najivunia wachezaji wangu,” alisema Chelle.


Malalamiko mengi yalikwenda kwa kocha kutokana na mipango yake ya kuibadili timu jambo lililoonekana kama kuharibu mpango mzima na kuiruhusu Tunisia itawale na hatimaye kutengeneza nafasi hadi kupata mabao mawili.
Tunisia walianza kwa kupata bao la kwanza kwa mpira wa adhabu kabla ya kupambana na kupata bao la penalti na hatimaye matokeo kuwa 3-2, matokeo ambayo ilidaiwa kwamba yalisababishwa na udhaifu kwenye eneo la ulinzi la Nigeria hali ambayo haikuonekana katika kipindi cha kwanza.
Chelle hata hivyo alitetea uamuzi wake wa kuwaingiza mawinga wawili, Chidera Ejuke na Moses Simon kwa madai kwamba hatua hiyo ilikuwa ni mbinu ya kuikabili timu ya Tunisia ambayo ilibadili mbinu za kiuchezaji.
“Ni kwa sababu walijua mbinu yetu na ndio maana nikafanya mabadiliko, unapokuwa na mawinga wawili hawawezi kwenda eneo hilo lakini walikuwa sahihi kwa sababu walitengeneza bao na kupata jingine kwa penalti,” alisema Chelle.
Chelle hata hivyo alikiri kuwapo udhaifu katika safu ya ulinzi ya timu yake kusisitiza umuhimu wa kufanya maboresho na kukabiliana na presha za dakika za lala salama.
Kocha huyo ambaye Jumatatu timu yake itaikabili Msumbiji katika hatua ya mtoano, hata hivyo alijigamba kwa kufafanua kwamba hakuna timu ambayo inaweza kukabiliana na hali ya presha ya namna ile kwa dakika 90 kama ilivyokuwa timu yake.

The post Kocha Nigeria awajia juu wachambuzi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/04/kocha-nigeria-awajia-juu-wachambuzi/feed/ 0
Stars yaweka historia, yatinga hatua ya mtoano Afcon https://www.greensports.co.tz/2025/12/30/stars-yaweka-historia-yatinga-hatua-ya-mtoano-afcon/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/30/stars-yaweka-historia-yatinga-hatua-ya-mtoano-afcon/#respond Tue, 30 Dec 2025 20:10:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14233 Rabat, MoroccoTimu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa mara ya kwanza imeingia hatua ya mtoano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Tunisia, mechi iliyochezwa leo Jumanne, Desemba 30, 2025.Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kufikia hatua hiyo baada ya kuishia […]

The post Stars yaweka historia, yatinga hatua ya mtoano Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rabat, Morocco
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa mara ya kwanza imeingia hatua ya mtoano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Tunisia, mechi iliyochezwa leo Jumanne, Desemba 30, 2025.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kufikia hatua hiyo baada ya kuishia hatua ya makundi katika fainali zote ilizofuzu kuanzia mwaka 1980 ilipofuzu kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza.
Mechi dhidi ya Tunisia ndiyo ya mwisho kwa Stars katika mechi zake za Kundi C na imemaliza ikiwa nafasi ya tatu nyuma ya Nigeria iliyoshika usukani, Tunisia ya pili na Uganda ikiburuza mkia katika kundi hilo.
Stars imemaliza na pointi mbili, Nigeria tisa na Tunisia nne wakati Uganda haina pointi hata moja na kuiacha Stars ikifuzu kupitia kundi la best loosers na sasa inasubiri kuumana na wenyeji Morocco.
Tunisia ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 42 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na Ismail Gharbi baada ya Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ kumkaba shingoni Hazem Mastouri wa Tunisia aliyekuwa akiuwahi mpira wa juu uliopigwa na Hannibal Mejbri kuelekea kwenye lango la Stars.
Penalti hiyo ilitolewa na mwamuzi Jacques Ndala Ngambo baada ya kujiridhisha kupitia VAR na picha kurudiwa zikimuonesha Bacca alivyomzuia Mastouri kwa kumkaba shingoni ndani ya eneo la penalti na mwamuzi kumpa kadi ya njano beki huyo wa Yanga.
Stars walisawazisha bao hilo dakika ya 54 mfungaji akiwa Feisal Salum au Fei Toto ambaye alifumua shuti la chinichini akiwa nje ya eneo la 18 na kumuacha kipa wa Tunisia, Aymen Dahmen akiruka bila mafanikio.
Tunisia waliuanza mchezo vizuri wakitawala kila eneo na Stars kujikuta wakifanya kazi ya kuzuia mashambulizi na katika dakika ya 11, Gharbi alifumua shuti lililogonga mwamba wa juu kwenye kona na kurudi uwanjani na kuwaacha mashabiki wa Stars wakiwa hawaamini kilichotokea.
Kipa wa Stars, Hussein Masalanga aliruka akijaribu kuufuata mpira huo lakini aliishia kuuangalia kwa macho ukigonga mwamba kabla ya kurudi uwanjani.


Stars nao walianza kujiamini huku Mbwana Samatta na Simon Msuva wakionekana kuwa tishio kwenye lango la Tunisia ambao hatimaye walianza kucheza kwa tahadhari zaidi.
Kocha wa Stars, Miguel Gamondi ambaye timu yake ilianza mchezo kwa kujihami, kipindi cha pili alionekana kubadili mbinu ambazo zilisaidia kuifanya Stars icheze pasi na kulisogelea lango la Tunisia mara kadhaa na haikushangaza kwa timu hiyo kupata bao.
Katika kipindi hicho, Gamondi alianza kwa kumtoa Samatta na nafasi yake kuingia Seleman Mwalimu, baadaye akamtoa Mohamed Hussein Zimbwe na kuingia Paschal Msindo.
Mabadiliko hayo yaliendelea kwa kuwatoa, Fei Toto, Msuva na Haji Mnoga na nafasi zao kuingia Charles M’mombwa, Tarryn Allarakhia na Shomari Kapombe.
Stars sasa ina kazi ngumu ya kuwakabili wenyeji Morocco, mechi ambayo itachezwa Jumapili ijayo ya Januari 4, 2026 wakati siku moja kabla Tunisia wao wataumana na Mali.

The post Stars yaweka historia, yatinga hatua ya mtoano Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/30/stars-yaweka-historia-yatinga-hatua-ya-mtoano-afcon/feed/ 0
Stars, Cranes zatoka sare ya 1-1 https://www.greensports.co.tz/2025/12/27/stars-cranes-zatoka-sare-ya-1-1/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/27/stars-cranes-zatoka-sare-ya-1-1/#respond Sat, 27 Dec 2025 20:50:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14226 Rabat, MoroccoTimu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imetoka sare ya bao 1-1 na Uganda Cranes katika mechi ya Kundi C ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2025) iliyochezwa leo Jumamosi, Desemba 27, 2025.Stars ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 59 kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Simon Msuva na […]

The post Stars, Cranes zatoka sare ya 1-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rabat, Morocco
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imetoka sare ya bao 1-1 na Uganda Cranes katika mechi ya Kundi C ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2025) iliyochezwa leo Jumamosi, Desemba 27, 2025.
Stars ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 59 kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Simon Msuva na kumshinda kipa mkongwe wa Cranes, Dennis Onyango.
Penalti hiyo ilitolewa na mwamuzi baada ya Baba Alhassan wa Cranes, kuunawa mpira uliopigwa na Alphonce Mabula na Alhassan kujichanganya katika harakati za kuokoa na kujikuta akiuzuia mpira huo kwa mkono ingawa kipa wake aliokoa.
Cranes baada ya kufungwa bao hilo walianza kulisakama lango la Stars mara kwa mara huku Stars wakiwa na kazi ya kuzuia kabla ya mambo kuharibika dakika ya 69 baada ya Cranes kupata bao la kusawazisha.
Bao hilo lilitokana na mpira ulioanzia kwa kipa Onyango aliyetoa pasi ndefu kabla ya kupigwa krosi ambayo ilipigwa na Denis Omedi na Uche Ikpeazu akaujaza mpira wavuni kwa kichwa.
Kuingia kwa bao hilo ni kama vile kuliwaamsha Cranes ambao dakika chache baadaye nusura waandike bao la pili baada ya kupata penalti iliyotokana na makosa ya Haji Mnoga aliyemshika mchezaji mmoja wa Cranes lakini mpigaji wa penalti, Allan Okelo akaupaisha mpira.
Cranes ndio waliouanza mpira kwa kasi kwa kupeleka mashambulizi ya mapema yaliyoanzia kwa beki wa kushoto Abdul Aziz Kayondo ambaye alikuwa akipanda na kupiga krosi chonganishi ambazo hata hivyo ziliokolewa na kipa Zubeir Foba.
Stars nao walijibu mapigo na kutengeneza nafasi kadhaa ikiwamo dakika ya 41 baada ya Kelvin John akiwa katika nafasi nzuri lakini mpira alioupiga ulipaa juu ya lango la Cranes.


Katika mechi ya leo, kocha wa Stars Miguel Gamondi alianza kwa kumuweka benchi nahodha Mbwana Samatta kabla ya kumuingiza dakika ya 63 akichukua nafasi ya Kelvin John.
Mechi ya leo ilikuwa na neema mara mbili kwa Msuva kwani licha ya kufunga bao lililoibeba Stars pia ndiye aliyetajwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Kwa matokeo hayo, Stars na Cranes ambazo zimepangwa kundi moja na timu za Nigeria na Tunisia, sasa zitakuwa na kazi ya kuhakikisha zinashinda mechi zao za mwisho zilizobaki ili kufufua matumaini ya kusonga mbele hatua ya mtoano (16 bora).
Timu hizo zimepoteza mechi zao za kwanza, Stars ikilala kwa Nigeria na Cranes mbele ya Tunisia na katika mechi zao za mwisho hatua ya makundi zitakazochezwa Jumanne Desemba 30, 2025, Stars itaivaa Tunisia na Cranes itaumana na Nigeria.

The post Stars, Cranes zatoka sare ya 1-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/27/stars-cranes-zatoka-sare-ya-1-1/feed/ 0