Afcon 2025 - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 28 Jan 2025 12:46:43 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Afcon 2025 - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Stars, Uganda Cranes kundi moja Afcon 2025 https://www.greensports.co.tz/2025/01/27/stars-uganda-cranes-kundi-moja-afcon-2025/ https://www.greensports.co.tz/2025/01/27/stars-uganda-cranes-kundi-moja-afcon-2025/#respond Mon, 27 Jan 2025 20:58:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12940 Na mwandishi wetuTimu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars imepangwa Kundi C ambalo pia ipo timu ya taifa ya Uganda au Uganda Cranes kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2025 zitakazofanyika nchini Morocco.Makundi hayo yamepatikana Jumatatu hii usiku Januari 27, 2025 baada ya droo kufanyika nchini Morocco ambapo mbali na Uganda Cranes, […]

The post Stars, Uganda Cranes kundi moja Afcon 2025 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars imepangwa Kundi C ambalo pia ipo timu ya taifa ya Uganda au Uganda Cranes kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2025 zitakazofanyika nchini Morocco.
Makundi hayo yamepatikana Jumatatu hii usiku Januari 27, 2025 baada ya droo kufanyika nchini Morocco ambapo mbali na Uganda Cranes, timu nyingine zilizopangwa na Stars katika kundi hilo ni Nigeria na Tunisia.
Wenyeji wa fainali hizo Morocco wao wamepangwa Kundi A ambalo pia lina timu za Mali, Zambia na Comoro wakati Kundi B lina timu za Misri, Afrika Kusini, Angola na Zimbabwe.
Katika Kundi D kuna timu za Senegal, DR Congo, Benin na Botswana wakati Kundi E zipo Algeria, Burkina Faso, Guinea ya Ikweta na Sudan na kundi F lina timu za mabingwa watetezi Ivory Coast, Cameroon, Gabon pamoja na Msumbiji.

Fainali za Afcon 2025 zinatarajia kuanza kutimua vumbi Desemba 21, 2025 na kufikia tamati Januari 18, 2026.

The post Stars, Uganda Cranes kundi moja Afcon 2025 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/01/27/stars-uganda-cranes-kundi-moja-afcon-2025/feed/ 0
Stars yafuzu Afcon 2025 https://www.greensports.co.tz/2024/11/20/stars-yafuzu-afcon-2025/ https://www.greensports.co.tz/2024/11/20/stars-yafuzu-afcon-2025/#respond Wed, 20 Nov 2024 08:09:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12281 Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 zitakazofanyika nchini Morocco baada ya kuilaza Guinea bao 1-0. Ushindi huo umepatikana Jumanne hii Novemba 19, 2024 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kwa bao hilo pekee lililofungwa na Simon Msuva. Bao hilo […]

The post Stars yafuzu Afcon 2025 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 zitakazofanyika nchini Morocco baada ya kuilaza Guinea bao 1-0.

Ushindi huo umepatikana Jumanne hii Novemba 19, 2024 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kwa bao hilo pekee lililofungwa na Simon Msuva.

Bao hilo limetosha kuifanya Stars iweke rekodi ya kufuzu fainali hizo zinazoshirikisha nchi za Mataifa ya Afrika kwa mara ya nne kuanzia mwaka 1980, 2018 na 2023.

Msuva alifunga bao hilo dakika ya 60 akimalizia pasi ya juu ya Mudathir Yahya na kuruka kabla ya kuupiga mpira wa kichwa ambao ulimshinda kipa wa Guinea, Mussa Camara ambaye pia anaidakis timu ya Simba.

Ushindi huo umeifanya Stars iliyokuwa Kundi H kufikisha pointing 10 na kushika nafasi ya pili nyuma ya vinara DR Congo wenye pointi 12 wakati Guinea wanabaki na pointi tisa na Ethiopia wamemaliza wakiwa mkiani na pointi yao moja.

Guinea ni dhahiri wameumizwa mno na matokeo hayo kwani walihitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu lakini walijikuta pagumu kwa kipindi kirefu cha mchezo kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya wachezaji wa Stats.

Stars walicheza kwa kujiamini wakikaba na kulishambulia mara kwa mara lango la Guinea ingawa timu hiyo ilikuwa na tatizo katika umaliziaji.

Msuva na Clement Mzize mara kadhaa walilisakama lango la Guinea lakini walikosa umakini katika umaliziaji na kuinyima Stars mabao kabla ya Msuva kurekebisha makosa yake na kuipa Stats ushindi.

Baada ya filimbi ya kumaliza mchezo kupulizwa na mashabiki waliofurika uwanjani kulipuka kwa shangwe, baadhi ya wachezaji wa Guinea walionekana wakimzonga mwamuzi wa mchezo huo katika namna iliyoonesha kutofurahia baadhi ya maamuzi yake.

Stars baada ya ushindi sasa inasubiri kujua itapangwa na timu gani katika Kundi lake kwa ajili ya fainali za Afcon 2025 zitakazofanyika mapema mwakani nchini Morocco.

The post Stars yafuzu Afcon 2025 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/11/20/stars-yafuzu-afcon-2025/feed/ 0
Mechi ya DR Congo, kikwazo muhimu Stars kukivuka https://www.greensports.co.tz/2024/09/29/mechi-ya-dr-congo-kikwazo-muhimu-stars-kukivuka/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/29/mechi-ya-dr-congo-kikwazo-muhimu-stars-kukivuka/#respond Sun, 29 Sep 2024 14:45:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11954 Na mwandishi wetuTimu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ina mechi mbili muhimu dhidi ya timu ya taifa ya DR Congo ili kuthibitisha uwezo wake katika mbio za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2025.Stars iliyo kundi H itaanzia ugenini Oktoba 10 na kurudiana na timu hiyo Oktoba 15 jijini Dar es […]

The post Mechi ya DR Congo, kikwazo muhimu Stars kukivuka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ina mechi mbili muhimu dhidi ya timu ya taifa ya DR Congo ili kuthibitisha uwezo wake katika mbio za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2025.
Stars iliyo kundi H itaanzia ugenini Oktoba 10 na kurudiana na timu hiyo Oktoba 15 jijini Dar es Salaam, mechi ambazo Stars ikishinda zote itajikusanyia pointi sita na hivyo kufikisha jumla ya pointi 10.
Awali timu hiyo ilianza hovyo mechi ya kwanza na Ethiopia kwa sare ya bila kufungana, tena ikiwa kwenye uwanja wa nyumbani kabla ya kupata ushindi katika mechi ya pili ugenini dhidi ya Guinea.
Kwa hiyo ushindi dhidi ya DR Congo kwanza utakuwa umefunika makosa ya awali ya sare ya bila kufungana na Ethiopia lakini pia utadhihirisha uwezo na dhamira ya timu hiyo kufuzu Afcon 2025.
Stars tayari imeshaonesha uwezo ugenini katika mechi na Guinea, ushindi ilioupata wa mabao 2-1 umeonesha kwamba timu hiyo iko vizuri ina uwezo na kilichotokea dhidi ya Ethiopia ni makosa ya kawaida.
Matokeo yoyote mabaya baada ya sare na Ethiopia na ushindi dhidi ya Guinea yatafifisha matumaini ya timu hiyo kuelekea Afcon 2025.
Kwa hiyo mechi mbili za Stars dhidi ya DR Congo zimebeba mwelekeo wa timu hiyo na ndizo zinazoweza kuthibitisha kila kitu kama Stars hii inaelekea kufuzu Afcon 2025 au nafasi yake ni ndogo au haipo.
Matokeo yoyote mabaya dhidi ya DR Congo yanaweza kuwa mwanzo wa kuitoa timu hiyo kwenye mstari au kuiweka katika wakati mgumu na kujikuta ikilazimika kuangalia matokeo ya timu nyingine ili kujua kama inafuzu Afcon 2025 au la.
Stars ikiwa tayari imecheza mechi mbili inatakiwa ihakikishe inashika usukani katika kundi lake yaani Kundi H na hilo litawezekana au kuwa rahisi iwapo itapata matokeo mazuri katika mechi dhidi ya DR Congo.
Baada ya mechi mbili za Stars, DR Congo inaonekana kuwa timu ngumu kwenye kundi la Stars na hivyo ili kujiwekea mazingira mazuri ya kufuzu, mechi na timu hiyo inabaki kuwa kikwazo muhimu cha kukivuka.
Guinea na Ethiopia japo si timu nyepesi lakini tayari Stars imeonesha ina uwezo mkubwa wa kuzifunga katika mechi za marudiano na hatimaye kumaliza mechi zake zote ikiwa na jumla ya pointi 16.
Bila kujali matokeo ya timu nyingine, pointi 16 zinatosha kuifanya Stars iwe katika nafasi nzuri ya kujikatia tiketi ya kushiriki Afcon 2025.
Dr Congo ndio wanaoongoza kundi hilo wakiwa na pointi sita wakifuatiwa na Stars wenye pointi nne na wa tatu ni Ethiopia wenye pointi moja na Guinea wanashika mkia wakiwa hawana pointi hata moja.

The post Mechi ya DR Congo, kikwazo muhimu Stars kukivuka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/29/mechi-ya-dr-congo-kikwazo-muhimu-stars-kukivuka/feed/ 0
Morocco apiga chini ofa za klabu https://www.greensports.co.tz/2024/07/07/morocco-apiga-chini-ofa-za-klabu/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/07/morocco-apiga-chini-ofa-za-klabu/#respond Sun, 07 Jul 2024 09:46:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11542 Na mwandishi wetuKaimu kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’ ameeleza wazi kupiga chini ofa za klabu alizozipata kutokana na majukumu aliyonayo katika kikosi cha Stats.Morocco ameiambia GreenSports kuwa kwa sasa hatofundisha klabu sambamba na kuinoa Stars kama alivyokuwa akifanya awali kwani kuna kitu anataka kukivuna akiwa na timu […]

The post Morocco apiga chini ofa za klabu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kaimu kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’ ameeleza wazi kupiga chini ofa za klabu alizozipata kutokana na majukumu aliyonayo katika kikosi cha Stats.
Morocco ameiambia GreenSports kuwa kwa sasa hatofundisha klabu sambamba na kuinoa Stars kama alivyokuwa akifanya awali kwani kuna kitu anataka kukivuna akiwa na timu hiyo hivyo ameamua kuwekeza huko jumla.
“Ofa zimekuja za hapa Tanzania nyingi tu na chache nje ya nchi lakini nimeamua kuachana nazo sababu kuna kitu nataka kufanya nikiwa na Stars, nataka akili yangu iwe huku kwanza,” alisema Morocco.
Kocha huyo amekuwa akiitumikia Stars huku akizinoa baadhi ya klabu za Ligi Kuu kwa misimu kadhaa kabla ya mwishoni mwa msimu wa 2023-24 kuondoka Geita Gold.
Akizungumzia nafasi ya Taifa Stars katika Kundi H kwenye mechi za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025, alisema nafasi ipo akifafanua mambo kadhaa.
“Kwanza tuna nafasi ya kufuzu kutokana na hamasa na ukuaji wa kiwango wa kikosi chetu, lakini ni muhimu kutokana na uandaaji wetu wa Afcon 2027, lazima tuendelee kuwemo ili ikifika kwetu tuwe tayari kujipigania nyumbani.

“Na makundi yote ni magumu kimsingi, yote yana changamoto lakini tunapaswa kupambana, kujiandaa vya kutosha, kuwa tayari na kuipigania timu na taifa kuipeleka tena Afcon nyingine,” alisema Morocco.


Katika kundi hilo Stars iliyoshiriki michuano hiyo mwaka 1980, 2019 na 2023 itapambana dhidi ya Guinea, DR Congo na Ethiopia katika kuwania nafasi ya timu mbili zitakazofuzu.

The post Morocco apiga chini ofa za klabu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/07/morocco-apiga-chini-ofa-za-klabu/feed/ 0