Adel Zrane - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 02 Apr 2024 20:01:42 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Adel Zrane - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kocha wa viungo Simba afariki ghafla https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/kocha-wa-viungo-simba-afariki-ghafla/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/kocha-wa-viungo-simba-afariki-ghafla/#respond Tue, 02 Apr 2024 20:01:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10481 Na mwandishi wetuKlabu ya APR ya Rwanda imetangaza kufariki dunia kwa aliyekuwa kocha wao wa viungo, Adel Zrane ambaye pia aliwahi kuinoa Simba ya Tanzania hivi karibuni.Kupitia taarifa iliyotolewa jioni ya leo Jumanne na APR kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii imeeleza kusikitishwa na kifo hicho kilichoelezwa kuwa ni cha ghafla:“Kwa masikitiko makubwa tunatangaza […]

The post Kocha wa viungo Simba afariki ghafla first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya APR ya Rwanda imetangaza kufariki dunia kwa aliyekuwa kocha wao wa viungo, Adel Zrane ambaye pia aliwahi kuinoa Simba ya Tanzania hivi karibuni.
Kupitia taarifa iliyotolewa jioni ya leo Jumanne na APR kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii imeeleza kusikitishwa na kifo hicho kilichoelezwa kuwa ni cha ghafla:
“Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha kocha wetu wa viungo, Dr, Adel Zrane,” ilieleza taarifa hiyo ya APR.
Taarifa zaidi kutoka nchini Rwanda zinafafanua kuwa kimekuwa ni kifo cha ghafla kwani kocha Zrane (pichani juu na wachezaji wa Simba) hakuwa mgonjwa na alishiriki katika mechi ya Jumapili iliyopita dhidi ya Rwamagana City na kupata sare ya bao 1-1.
Kocha huyo raia wa Tunisia anayetajwa kuwa na umri wa miaka 31, amewahi kuwa kocha wa viungo wa Simba kuanzia mwaka 2018 chini ya Kocha Patrick Aussems kabla ya kuondoka mitaa ya Msimbazi, Kariakoo mwaka 2021.
Klabu ya Simba nayo ilitoa taarifa yake ambayo ilipatikana kwenye mitandao ya kijamii ikizungumzia kifo cha kocha huyo.

The post Kocha wa viungo Simba afariki ghafla first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/kocha-wa-viungo-simba-afariki-ghafla/feed/ 0