Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 16 Jun 2025 14:42:08 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Rufaa ya Guinea dhidi ya Stars yakwama CAF https://www.greensports.co.tz/2025/06/16/rufaa-ya-guinea-dhidi-ya-stars-yakwama-caf/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/16/rufaa-ya-guinea-dhidi-ya-stars-yakwama-caf/#respond Mon, 16 Jun 2025 14:38:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13623 Na mwandishi wetuKamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imeitupa rufaa iliyowasilishwa kwao na Guinea dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyopatikana leo Jumatatu Juni 16, 2025 ilieleza kuwa Guinea walikata rufaa kupinga uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya CAF kuyatupa malalamiko yao dhidi […]

The post Rufaa ya Guinea dhidi ya Stars yakwama CAF first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imeitupa rufaa iliyowasilishwa kwao na Guinea dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyopatikana leo Jumatatu Juni 16, 2025 ilieleza kuwa Guinea walikata rufaa kupinga uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya CAF kuyatupa malalamiko yao dhidi ya Taifa Stars.
Katika malalamiko yao Guinea waliilalamikia Taifa Stars kwa kumchezesha mchezaji Ibrahim Ame aliyeingia kipindi cha pili katika mechi baina ya timu hizo ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika iliyochezwa Novemba mwaka jana.
Guinea walidai kuwa mchezaji huyo aliingia uwanjani akiwa amevaa jezi yenye namba tofauti na ile iliyoandikwa kwenye orodha rasmi ya wachezaji.
Katika mechi hiyo, Stars walishinda kwa bao 1-0 ambapo Guinea katika hoja zao CAF wamedai kuwa kitendo hicho cha tofauti ya jezi kiliwachanganya kisaikolojia na kuwa sababu ya wao kushindwa mechi hiyo.
Kamati ya Rufaa ya CAF katika maamuzi yake imekubaliana na maamuzi ya Kamati ya Nidhamu kwa madai kwamba hoja za Guinea hazina mashiko kikanuni.

The post Rufaa ya Guinea dhidi ya Stars yakwama CAF first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/16/rufaa-ya-guinea-dhidi-ya-stars-yakwama-caf/feed/ 0
Bayern yashinda 10-0 https://www.greensports.co.tz/2025/06/16/bayern-yashinda-10-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/16/bayern-yashinda-10-0/#respond Mon, 16 Jun 2025 14:34:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13620 California, MarekaniBayern Munich imeanza kwa kishindo michuano ya Fifa ya Klabu ya Dunia kwa kuweka rekodi ya ushindi wa mabao 10-0 dhidi ya Auckland City katika mechi iliyochezwa Jumapili hii Juni 15, 2025.Vinara hao wa Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga waliutawala vyema mchezo huku Jamal Musiala akifunga mabao matatu (hat trick) na Thomas Muller akipachika […]

The post Bayern yashinda 10-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

California, Marekani
Bayern Munich imeanza kwa kishindo michuano ya Fifa ya Klabu ya Dunia kwa kuweka rekodi ya ushindi wa mabao 10-0 dhidi ya Auckland City katika mechi iliyochezwa Jumapili hii Juni 15, 2025.
Vinara hao wa Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga waliutawala vyema mchezo huku Jamal Musiala akifunga mabao matatu (hat trick) na Thomas Muller akipachika mawili.
Bayern chini ya kocha Vincent Kompany walianza kuziona nyavu za wapinzani wao kutoka New Zealand katika dakika ya sita ya mchezo kwa bao la Kingsley Coman.
Dakika sita baadaye Bayern waliongeza bao la pili lililofungwa na Sacha Boey kabla Michael Olise hajapahika bao la tatu alipoinasa krosi ya Muller.
Wakati Auckland City wakitafakari, Coman kwa mara nyingine alitupia mpira kambani na kuifanya Bayern ifikishe mabao manne huku yeye akiwa amefunga la pili.
Muda mfupi kabla ya timu kwenda mapumziko, Muller alifunga bao la tano akiitumia krosi ya Olise kabla Olise hajakamlisha bao la sita na kuzifanya timu ziende mapumzko Bayern wakiwa mbele kwa mabao 6-0.
Kasi ya Bayern kupachika mabao ilipungua kidogo kipindi cha pili lakini hatimaye dakika ya 67 Musiala aliongeza bao la saba .
Musiala ambaye alizikosa mechi sita za Bayern za mwishoni mwa msimu kutokana na kuwa majeruhi, aliandika bao la nane kwa mkwaju wa penalti dakika ya 73 na kukamilisha bao lake la tisa na la tatu kwenye mechi hiyo katika dakika ya 84.
Bao la 10 na la mwisho kwa Bayern lilifungwa na Muller zikiwa zimebakia dakika mbili kumalizika kwa mchezo huo.
Ushindi wa Bayern unaingia kwenye rekodi ya kuwa ushindi wa mabao mengi zaidi katika mashindano hayo baada ya ule wa mwaka 2022 wa Al Hilal kuichapa Al Jazira mabao 6-1.
Katika mechi nyingine vinara wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, PSG ya Ufaransa waliilaza Atletico Madrid mabao 4-0 huku mabao ya washindi yakifungwa na Fabián Ruiz,
Vitinha, Mayulu kwa mkwaju wa penalti na Lee Kang-In.

The post Bayern yashinda 10-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/16/bayern-yashinda-10-0/feed/ 0
TFF yatoa ruksa wanaotaka kumrithi Karia https://www.greensports.co.tz/2025/06/15/tff-yatoa-ruksa-wanaotaka-kumrithi-karia/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/15/tff-yatoa-ruksa-wanaotaka-kumrithi-karia/#respond Sun, 15 Jun 2025 10:23:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13614 Na mwandishi wetuKaria anafaa, Karia hafai, ni mjadala uliotawala ukimhusu Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia lakini hatimaye wanaomjadili wamepewa rasmi ruksa ya kumpinga kwenye sanduku la kura.Mwanamichezo yeyote ambaye hajaridhishwa na uongozi wa Karia pale TFF huu ni wakati wake wa kujitokeza kumpinga katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo badala ya […]

The post TFF yatoa ruksa wanaotaka kumrithi Karia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Karia anafaa, Karia hafai, ni mjadala uliotawala ukimhusu Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia lakini hatimaye wanaomjadili wamepewa rasmi ruksa ya kumpinga kwenye sanduku la kura.
Mwanamichezo yeyote ambaye hajaridhishwa na uongozi wa Karia pale TFF huu ni wakati wake wa kujitokeza kumpinga katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo badala ya kuishia kumjadili.
TFF wametangaza uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo ambao umepangwa kufanyika Agosti 16, 2025 mkoani Tanga hivyo anayejiamini na ana sifa za kuchukua nafasi ya Karia amepewa ruksa hiyo.
Katika uchaguzi huo mbali na nafasi moja ya urais inayoshikiliwa na Karia, nafasi nyingine zitakazogombewa ni ujumbe wa kamati ya utendaji ambazo zipo nafasi sita.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyopatikana Jumamosi hii Juni 14, 2025 na kusainiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kiomoni Kibamba, fomu za kuwania nafasi hizo zitaanza kutolewa Jumatatu yaani Juni 16 2025 kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam na mwisho wa zoezi hilo ni Juni 20, 2025.
Kwa anayetaka nafasi ya urais atalazimika kulipa Sh 500,000 kwa ajili ya fomu hizo wakati wale wa ujumbe wa kamati ya utendaji kila fomu gharama yake ni Sh 200,000.

The post TFF yatoa ruksa wanaotaka kumrithi Karia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/15/tff-yatoa-ruksa-wanaotaka-kumrithi-karia/feed/ 0
Reijnders avikataa viatu vya De Bruyne https://www.greensports.co.tz/2025/06/15/reijnders-avikataa-viatu-vya-de-bruyne/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/15/reijnders-avikataa-viatu-vya-de-bruyne/#respond Sun, 15 Jun 2025 10:21:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13611 Florida, MarekaniKiungo mpya wa Man City, Tijjani Reijnders (pichani) amesema hajajiunga na timu hiyo kwa lengo la kuziba pengo la Kevin De Bruyne ambaye ameihama City na hapo hapo Reijnders akasajiliwa.Reijnders amekiri kuwa De Bruyne ni kati ya wachezaji waliokuwa wakimvutia, amejiunga na Man City kwa ada ya Pauni 46.5 milioni akitokea Ac Milan lakini […]

The post Reijnders avikataa viatu vya De Bruyne first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Florida, Marekani
Kiungo mpya wa Man City, Tijjani Reijnders (pichani) amesema hajajiunga na timu hiyo kwa lengo la kuziba pengo la Kevin De Bruyne ambaye ameihama City na hapo hapo Reijnders akasajiliwa.
Reijnders amekiri kuwa De Bruyne ni kati ya wachezaji waliokuwa wakimvutia, amejiunga na Man City kwa ada ya Pauni 46.5 milioni akitokea Ac Milan lakini ameipinga hoja kwamba yuko Man City kuziba pengo la mchezaji huyo.
De Bruyne ameachana na Man City baada ya kuichezea timu hiyo kwa miaka 10 ambapo Reijnders amekiri kuwa alivutiwa na soka la kiungo huyo pamoja na Andres Iniesta wa Barcelona na Hispania.
Reijnders alisema akiwa Man City atajaribu kuwa yeye na si De Bruyne kwani hajajiunga na timu hiyo kwa lengo la kuziba pengo la kiungo huyo mkongwe wa Ubelgiji.

“Siko hapa kuchukua nafasi yake, lazima nicheze soka langu lakini huwa nachukua vitu kwa wachezaji tofauti pamoja na mazuri wanayoyafanya na kuyaiga yakiwamo ya De Bruyne kwa namna alivyokuwa akiusoma mchezo na kutoa pasi,” alisema Reijnders.


De Bruyne alitamba Man City chini ya kocha Pep Guardiola na aliwahi kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa Ligi Kuu England mara mbili na hatua yake ya kuhama timu hiyo na kusajiliwa Reijnders ilitafsiriwa kwamba City imesajili mbadala wa De Bruyne.
Reijnders, 26, yupo nchini Marekani na Man City kwenye michuano ya Fifa ya Klabu ya Dunia na amekuwa akitajwa miongoni mwa viungo bora wa Serie A huku akipewa nadasi kubwa ya kutamba katika timu hiyo mpya.
Reijnders pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Uholanzi ambayo alianza kuichezea mara ya kwanza mwaka 2023 na hadi sasa ameichezea mara 23 na kuifungia mabao manne.

The post Reijnders avikataa viatu vya De Bruyne first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/15/reijnders-avikataa-viatu-vya-de-bruyne/feed/ 0
Kasongo asimamishwa TPLB, Mnguto ajiuzulu https://www.greensports.co.tz/2025/06/14/kasongo-asimamishwa-tplb-mnguto-ajiuzulu/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/14/kasongo-asimamishwa-tplb-mnguto-ajiuzulu/#respond Sat, 14 Jun 2025 19:39:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13609 Na mwandishi wetuOfisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Almas Kasongo (pichani) amesimamishwa kazi wakati mwenyekiti wa bodi hiyo, Steven Mnguto ametangaza kujiuzulu.Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyopatikana leo Juammosi, Juni 14, 2025 imeeleza kuwa Mnguto amewasilisha TFF barua ya kujiuzulu nafasi yake.Katika taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa […]

The post Kasongo asimamishwa TPLB, Mnguto ajiuzulu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Almas Kasongo (pichani) amesimamishwa kazi wakati mwenyekiti wa bodi hiyo, Steven Mnguto ametangaza kujiuzulu.
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyopatikana leo Juammosi, Juni 14, 2025 imeeleza kuwa Mnguto amewasilisha TFF barua ya kujiuzulu nafasi yake.
Katika taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau hata hivyo haikuwekwa wazi sababu hasa za Mnguto kuamua kujiuzulu nafasi yake.
Kuhusu Kasongo, taarifa hiyo pia haikuweka wazi sababu hasa za TFF kuchukua uamuzi huo badala yake ilielezwa kwa kifupi kuwa Rais wa TFF, Walace Karia ndiye aliyechukua uamuzi wa kumsimamisha kiongozi huyo.
Wakati TFF haikutaja sababu hasa za kusimamishwa na kujiuzulu kwa viongozi hao lakini inadhaniwa kuwa sakata la mechi ya mahasimu wa soka Simba na Yanga ndilo lililochangia.
Mechi baina ya mahasimu hao wa soka nchini imeingia katika sintofahamu baada ya kuahirishwa mara mbili huku mjadala mkubwa ukiibuka miongoni mwa mashabiki wa klabu hizo mbili.
Katika mjadala huo baadhi ya mashabiki waliwalaumu viongozi wa TPLB kuwa ndio waliochangia kuahirishwa kwa mechi hiyo.
Awali mechi hiyo ilipangwa kuchezwa Machi 8 lakini iliahirishwa kwa kilichoelezwa kuwa ni sababu za kiusalama na kupangwa kuchezwa Juni 15, tarehe ambayo ilizidisha mjadala huku Yanga wakishikilia msimamo wa kutocheza.
Hatimaye mechi hiyo iliahirishwa kwa mara nyingine na sasa imepangwa kuchezwa Juni 25, uamuzi ambao pia umeanza kulalamikiwa na kupingwa na mashabiki wanaoaminika kuwa ni wa Simba.

The post Kasongo asimamishwa TPLB, Mnguto ajiuzulu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/14/kasongo-asimamishwa-tplb-mnguto-ajiuzulu/feed/ 0
Pogba kuibukia Monaco https://www.greensports.co.tz/2025/06/14/pogba-kuibukia-monaco/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/14/pogba-kuibukia-monaco/#respond Sat, 14 Jun 2025 19:36:31 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13607 Paris, UfaransaKiungo wa zamani wa Man United, Paul Pogba inadaiwa yuko mbioni kujiunga na klabu ya Monaco ya Ufaransa ikiwa takriban miaka miwili imepita tangu aanze kutumikia adhabu ya kufungiwa kucheza soka.Habari za ndani kutoka klabu ya Monaco zinaeleza kuwa mazungumzo ya awali baina ya Pogba na mabosi wa timu hiyo ya Ligi Kuu Ufaransa […]

The post Pogba kuibukia Monaco first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Paris, Ufaransa
Kiungo wa zamani wa Man United, Paul Pogba inadaiwa yuko mbioni kujiunga na klabu ya Monaco ya Ufaransa ikiwa takriban miaka miwili imepita tangu aanze kutumikia adhabu ya kufungiwa kucheza soka.
Habari za ndani kutoka klabu ya Monaco zinaeleza kuwa mazungumzo ya awali baina ya Pogba na mabosi wa timu hiyo ya Ligi Kuu Ufaransa maarufu Ligi 1 yameanza.
Pogba, 32, kwa kipindi kirefu hajacheza soka la ushindani tangu afungiwe miaka minne na mamlaka za kisheria nchini Italia, adhabu aliyopewa Septemba, 2023 baada ya kubainika kutumia dawa za kuongeza nguvu.
Adhabu ya mchezaji huyo hata hivyo baadaye ilipunguzwa na kuwa ya miezi 18 baada ya kukata rufaa lakini tayari klabu aliyokuwa akiichezea ya Juventus ilikubaliana naye kusitisha mkataba wake.
Tangu wakati huo hadi sasa, Pogba amekuwa nje ya soka la ushindani lakini sasa nyota huyo aliyekuwa katika kikosi cha Ufaransa kilichobeba taji la dunia mwaka 2018 yuko mbioni kujiunga na Monaco akiwa mchezaji huru.
Awali kulikuwa na habari kwamba mchezaji huyo alikuwa akiwindwa na klabu moja ya Saudi Arabia na matarajio ni kwamba angekuwamo kwenye michuano ya Fifa ya Klabu ya Dunia inayotarajia kuanza Jumapili hii nchini Marekani.
Monaco hata hivyo inatajwa kuwa na nia ya dhati ya kumsajili kiungo huyo ambaye alikuwa akitajwa kuwa miongoni mwa viungo bora wa soka kutoka Ufaransa kabla ya kukumbwa na kadhia ya madawa ya kuongeza nguvu.

The post Pogba kuibukia Monaco first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/14/pogba-kuibukia-monaco/feed/ 0
Simba, Yanga sasa ni Juni 25 https://www.greensports.co.tz/2025/06/13/simba-yanga-sasa-ni-juni-25/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/13/simba-yanga-sasa-ni-juni-25/#respond Fri, 13 Jun 2025 18:48:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13602 Na mwandishi wetuHatimaye Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza kuusogeza mbele mchezo wa mahasimu wa soka nchini Yanga na Simba ambao sasa utapigwa Juni 25, 2025 badala ya Juni 15 ya awali.Taarifa hiyo imekuja wakati kukiwa na sintofahamu kuhusu mechi hiyo ambayo awali ilipangwa kuchezwa Machi 8 mwaka huu kabla ya kuahirishwa hadi Juni […]

The post Simba, Yanga sasa ni Juni 25 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Hatimaye Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza kuusogeza mbele mchezo wa mahasimu wa soka nchini Yanga na Simba ambao sasa utapigwa Juni 25, 2025 badala ya Juni 15 ya awali.
Taarifa hiyo imekuja wakati kukiwa na sintofahamu kuhusu mechi hiyo ambayo awali ilipangwa kuchezwa Machi 8 mwaka huu kabla ya kuahirishwa hadi Juni 15 lakini sasa imeahirishwa tena hadi Juni 25.
Kama mechi hiyo itachezwa Juni 25 maana yake itakuwa imepita miezi mitatu na siku 16 tangu tarehe ya awali ya mechi hiyo yenye kuvuta hisia za mashabiki wa soka ndani na hata nje ya nchi.
Taarifa hiyo hata hivyo haikuwa na maelezo marefu badala yake ilitaja tarehe ya mechi na kufafanua kuwa itapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 11 alasiri na TPLB kuzitakia kila la heri timu hizo katika maandalizi ya mechi hiyo.
Haijaweza kueleweka mara moja timu hizo zitakuja na uamuzi gani baada ya tarehe hiyo mpya kutangazwa hasa kwa Yanga ambao awali walisema hawako tayari kucheza na Simba na kuweka masharti kadhaa kwa TPLB na TFF.
Hatua ya TPLB kuahirisha mechi Machi 8 kwa sababu zilizotajwa kuwa ni za kiusalama baada ya Simba kudaiwa kuzuiwa kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi hiyo ilizua mjadala huku Yanga wakitishia kutocheza mechi hiyo katika tarehe nyingine.
Suala hilo liliingiza bungeni na kusababisha malumbano yasiyo rasmi na yaliyo rasmi miongoni mwa wabunge ambapo baadhi wanaoaminika kuwa ni wa Yanga walisisitiza kutocheza mechi hiyo
Juhudi mbalimbali zilifanyika na kuwahusisha viongozi wakiwamo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na viongozi wa serikali kwa lengo la kutaka mechi hiyo ichezwe lakini Yanga walishikilia msimamo wa kutokuwa tayari kucheza.
Kikao cha mwisho kilifanyika hivi karibuni kati ya viongozi wa TPLB na wale wa Yanga lakini mara tu baada ya kikao hicho, msimamo wa Yanga kutocheza mechi hiyo uliwekwa wazi.

The post Simba, Yanga sasa ni Juni 25 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/13/simba-yanga-sasa-ni-juni-25/feed/ 0
Florian Wirtz atua Liverpool https://www.greensports.co.tz/2025/06/13/florian-wirtz-atua-liverpool/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/13/florian-wirtz-atua-liverpool/#respond Fri, 13 Jun 2025 18:44:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13598 Liverpool, EnglandMabingwa wa Ligi Kuu England (EPL) Liverpool, wamekubali kumsajili kiungo mshambuliaji Florian Wirtz (pichani juu) kutoka Bayer Leverkusen ya Ujerumani kwa ada ya Pauni 100 milioni.Ada ya mchezaji huyo ambaye ndio kwanza ana miaka 22, imeweka rekodi kwa klabu ya Liverpool wakati kwa England ni CHelsea iliyoweka rekodi ya juu mwaka 2023 ilipomsajili Enzo […]

The post Florian Wirtz atua Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Liverpool, England
Mabingwa wa Ligi Kuu England (EPL) Liverpool, wamekubali kumsajili kiungo mshambuliaji Florian Wirtz (pichani juu) kutoka Bayer Leverkusen ya Ujerumani kwa ada ya Pauni 100 milioni.
Ada ya mchezaji huyo ambaye ndio kwanza ana miaka 22, imeweka rekodi kwa klabu ya Liverpool wakati kwa England ni CHelsea iliyoweka rekodi ya juu mwaka 2023 ilipomsajili Enzo Fernandez kutoka Benfica kwa ada ya Pauni milioni 107.
Hadi kumpata Wirtz, Liverpool ililazmika kushindana na Chelsea ambao walionesha nia ya kumtaka mchezaji huyo kama ilivyokuwa kwa Bayern Munich ambao nao walitajwa kumtaka.
Wirtz hata hivyo inaaminika aliweka wazi msimamo wake wa kuitaka Liverpool ambao walianza majadiliano na Leverkusen na kufikia muafaka licha ya klabu hiyo kuwasilisha ofa ya awali ya Pauni 126 milioni.
Kabla ya kujiunga na Leverkusen mwaka 2020, Wirtz ambaye pia ameichezea timu ya taifa ya Ujerumani mara 31 na kuifungia mabao saba, aliwahi kuzichezea timu za SV Grün-Weiß na FC Cologne za Ujerumani.
Akiwa na Leverkusen ameifungia timu hiyo mabao 57 katika mechi 197 na mwaka 2024 alitoa mchango mkubwa kwa timu hyo hadi kubeba taji la Ligi Kuu Ujerumani maarufu Bundesliga.
Kwa sasa Liverpool pia ipo katika mpango wa kumsajili beki wa kushoto wa Bournemouth, Milos Kerkez kwa ada inayotajwa kufikia Pauni milioni 45.
Wakati huo huo, klabu ya Real Madrid ya Hispania nayo inadaiwa kukamilisha usajili wa kinda wa River Plate ya Argentina, Franco Mastantuono (pichani chini) ambaye ni kiungo na mshambuliaji.
Mastantuono, 17, kwa sasa yuko nchini Marekani na klabu yake ya River Plate ambayo ataiwakilisha kwenye michuano ya Fifa ya Klabu ya Dunia itakayoanza kutimua vumbi Jumapili Juni 15, 2025 nchini Marekani.

Real Madrid ilionesha nia ya kumtaka nyota huyo takriban miaka miwili iliyopita kabla ya kuamua kukamilisha mpango huo mwaka huu wakati klabu kadhaa Ulaya ikiwamo PSG nazo zikidaiwa kumtolea macho.
Mastantuono ambaye Agosti 14 mwaka huu atatimiza miaka 18, atajiunga rasmi na timu yake hiyo mpya miezi miwili ijayo tayari kwa ajili ya msimu mpya wa 2025-26.
Mchezaji huyo ambaye ni mzaliwa wa jimbo la Buenos Aires, Juni 5 mwaka huu aliichezea kwa mara ya kwanza timu yake ya taifa ya Argentina katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Chile, mechi ambayo Argentina ilishinda kwa bao 1-0.

The post Florian Wirtz atua Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/13/florian-wirtz-atua-liverpool/feed/ 0
Je ni kweli soka linaongozwa na wajinga wajinga? https://www.greensports.co.tz/2025/06/12/je-ni-kweli-soka-linaongozwa-na-wajinga-wajinga/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/12/je-ni-kweli-soka-linaongozwa-na-wajinga-wajinga/#respond Thu, 12 Jun 2025 09:22:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13595 Na Hassan KinguNimeikumbuka kauli ya kocha na beki wa zamani wa Mtibwa Sugar na timu ya taifa ya Tanzania au Taifa Stars, Mecky Maxime aliposema soka linaongozwa na wajinga wajinga.Awali nilimpuuza lakini sasa nafikiria mara mbili mbili na kujiuliza kama nilikuwa sahihi kumpuuza au nilihitaji kutafakari kwa kina kuhusu kauli ile?Kwa kinachoendelea katika soka letu […]

The post Je ni kweli soka linaongozwa na wajinga wajinga? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na Hassan Kingu
Nimeikumbuka kauli ya kocha na beki wa zamani wa Mtibwa Sugar na timu ya taifa ya Tanzania au Taifa Stars, Mecky Maxime aliposema soka linaongozwa na wajinga wajinga.
Awali nilimpuuza lakini sasa nafikiria mara mbili mbili na kujiuliza kama nilikuwa sahihi kumpuuza au nilihitaji kutafakari kwa kina kuhusu kauli ile?
Kwa kinachoendelea katika soka letu nabaki najiuliza zaidi, je kwa kauli ile Maxime alikuwa sahihi au aliitoa tu katika mazingira ya hasira kutokana na mambo yanayowakuta makocha Tanzania?
Kinachoendelea baina ya Yanga, TFF na Simba kinanifanya nizidi kufikiri na kutafakari kwa mapana kama Maxime alikuwa sahihi au la?
Nikianzia Machi 8 mwaka huu, naliangalia tukio siku moja kabla kwa timu ya Simba kuzuiwa kuingia uwanjani kufanya mazoezi kabla ya mechi yao na Yanga, mazoezi ambayo ni utaratibu ulio rasmi na unatambulika hata na sisi tusio viongozi, nazidi kutafakari kwamba je tukio hili nalo si sehemu ya ule ujinga ujinga uliosemwa na Maxime?
Baada ya hapo hisia zinanipeleka katika tukio la kuahirishwa mechi yenyewe, tena kuahirishwa siku ya mechi, saa kadhaa kabla ya mechi, je hili nalo ni sehemu ya ule ujinga ujinga uliozungumzwa na Maxime au la?
Baada ya hapo najiuliza kuhusu tukio la kugomea mechi, nautafuta uharamu na uhalali wake, nakosa jibu lakini sichoki kutafakari na kujifikirisha mwisho wa yote nabaki najiuliza kama huu nao ni sehemu ya ule ujinga ujinga au la?
Sakata la kuahirishwa kwa mechi ya Yanga na Simba na kupangiwa tarehe nyingine yaani Juni 15 limeibua mgomo, huyu anataka mechi huyu hataki, natafakari vijembe na malumbano yanayoendelea hasa mitandaoni na swali langu linabaki lile lile je huu nao ni sehemu ya ujinga ujinga ulioanzia kwa viongozi?
Nawataja viongozi kwa sababu yote haya yanayoendelea yametokana na viongozi, watu ambao wamepewa dhamana ya kuongoza soka letu, mchezo unaopendwa na wengi lakini bahati mbaya sana Maxime amenifikirisha kwamba wengi wao ni wajinga wajinga na mwisho wa yote nabaki na swali lile lile, je ni kweli soka linaongozwa na wajinga wajinga?
Hadi sasa mashabiki wa soka wapo njia panda, mechi kubwa ya Yanga na Simba haijulikani kama ipo au haipo, je ni kweli kwamba mashabiki wamewekwa njia panda kwa sababu viongozi wenye dhamana ni wajinga wajinga?
Si katika sakata hili la mechi ya Yanga na Simba bali yapo mambo mengi ya kwenye soka letu yananifikirisha kuhusu suala zima la ujinga ujinga, kuanzia kwa maamuzi ya matukio mbalimbali yanayojitokeza, waamuzi na uchezeshaji wao, vyote hivi nikivichambua swali la ujinga ujinga linanijia.
Natafakari kuhusu usajili, mchezaji anasajiliwa kutoka nje ya nchi tena kwa bei mbaya lakini akingia uwanjani huoni utofauti anaoleta katika timu, hapo hapo najiuliza kwamba mchezaji huyu si zao la kiongozi mmoja mjinga mjinga aliyemsema Maxime?
Dhana ya wajinga wajinga hainitoki kila ninapojaribu kuachana nayo, namuangalia tena mchezaji huyu huyu aliyesajiliwa kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kwa beki mbaya lakini hana ubora na mwishowe anaishia kusugua benchi.
Mchezaji huyu anasaini mkataba ulio rasmi na unaotambulika kisheria halafu anaachwa kienyeji, anakwenda kulalamika kwenye mamlaka husika analipwa fedha nyingi na klabu, je huo nao si ule ujinga ujinga wa kiongozi mmoja mjinga mjinga aliyemzungumzia Maxime?
Sijachoka kuwaza kuhusu ujinga ujinga aliousema Maxime kwani hata hili sakata la pesa lililobuka hivi majuzi nalo kila nikilitafakari swali la ujinga ujinga au viongozi wajinga wajinga linanijia.
Nimefikia hitimisho la kuja na dhana kwamba huenda kwamba kuna wajinga wajinga wanaodhani kila mtu ni mjinga mjinga kiasi kwamba hata masuala ya pesa nayo yanaibua mjadala unaotoa kila dalili za kupelekana kwenye ujinga ujinga.
Imefikia hatua tunataka kudanganyana kwamba namba nazo zinaweza kuongopa kwamba 50 isomeke 70 na 70 isomeke 50, hili haliwezekani lakini kwa nini limeibuka, na je si kweli kwamba kuna ujinga ujinga mahali?
Kajisemea Bob Marley katika moja ya nyimbo zake ‘You can fool some people sometime but you cant fool all the people all the time’ yaani unaweza kuwadanganya/kuwapumbaza watu fulani kwa wakati fulani lakini huwezi kuwapumbaza/kuwadanganya watu wote kwa wakati wote.’
Huenda sakata linaloendelea sasa ni ishara kwamba tunakaribia kuelewana kwamba mwisho wa wajinga wajinga unakaribia.

The post Je ni kweli soka linaongozwa na wajinga wajinga? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/12/je-ni-kweli-soka-linaongozwa-na-wajinga-wajinga/feed/ 0
Pep amuweka kando Grealish https://www.greensports.co.tz/2025/06/12/pep-amuweka-kando-grealish/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/12/pep-amuweka-kando-grealish/#respond Thu, 12 Jun 2025 09:15:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13592 Manchester, EnglandKocha wa Man City, Pep Guardiola hajampa nafasi kiungo wake wa bei mbaya, Jack Grealish katika wachezaji watakaoshiriki fainali za Kombe la Dunia la Klabu nchini Marekani.Uamuzi wa Pep kumuweka kando kiungo huyo mshambuliaji aliyemnunua kutoka Aston Villa kwa ada iliyotajwa kufikia Euro milioni 100 umefanyika huku nyota wapya waliosajiliwa na kocha huyo wakipewa […]

The post Pep amuweka kando Grealish first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man City, Pep Guardiola hajampa nafasi kiungo wake wa bei mbaya, Jack Grealish katika wachezaji watakaoshiriki fainali za Kombe la Dunia la Klabu nchini Marekani.
Uamuzi wa Pep kumuweka kando kiungo huyo mshambuliaji aliyemnunua kutoka Aston Villa kwa ada iliyotajwa kufikia Euro milioni 100 umefanyika huku nyota wapya waliosajiliwa na kocha huyo wakipewa nafasi.
Pep katika orodha iliyopatikana jana Jumatano aliwajumuisha nyota hao wapya wakiongozwa na Tijjani Reijnders, Rayan Ait-Nouri na Rayan Cherki.
Grealish, 29, alijiunga na Man City Agosti, 2021 na kusaini mkataba wa miaka sita, anamudu vyema nafasi za kiungo mshambuliaji na winga na zipo taarifa kuwa anawindwa na klabu kadhaa za England na Ulaya.
Klabu mojawapo ambayo imeonesha utayari wa kumtaka nyota huyo wa timu ya taifa ya England ni Everton ambayo itachuana kuiwania saini yake na klabu nyingine barani Ulaya.
Pep aliwahi kusema kwamba Grealish yuko huru kuihama timu hiyo kwa lengo la kusaka nafasi ya uhakika katika kikosi cha kwanza kwenye timu nyingine.
Man City imepangwa kuumana na Wydad AC ya Morocco katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia la Klabu itakayopigwa Juni 18 mjini Philadelphia.
Wachezaji wengine ambao Pep amewaacha katika orodha yake ni Kyle Walker ambaye alikuwa AC Milan kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu na James McAtee ambaye anaiwakilisha timu ya vijana chini ya miaka 21 ya England.
Orodha kamili ya wachezaji wa Man City watakaokwenda Marekani ni pamoja na Stefan Ortega, Marcus Bettinelli na Éderson ambao ni makipa.
Mabeki ni Manuel Akanji, Abdukodir Khusanov, Rico Lewis, Vitor Reis, Josko Gvardiol, Rúben Dias, John Stones, Nathan Aké na Rayan Ait-Nouri,
Viungo: Nico Gonzalez, Rodri, Tijjani Reijnders, Matheus Nunes, Ilkay Gündogan, Rayan Cherki, Bernardo Silva, Claudio Echeverri, Phil Foden, Oscar Bobb na Nico O’Reilly na washambuliaji ni Erling Haaland, Savinho, Omar Marmoush na Jeremy Doku.

The post Pep amuweka kando Grealish first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/12/pep-amuweka-kando-grealish/feed/ 0