LigiKuu - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 16 Aug 2024 07:22:06 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg LigiKuu - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mtoto wa Gaucho aelekea Burnley https://www.greensports.co.tz/2024/08/16/mtoto-wa-gaucho-aelekea-burnley/ https://www.greensports.co.tz/2024/08/16/mtoto-wa-gaucho-aelekea-burnley/#respond Fri, 16 Aug 2024 07:22:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11780 London, EnglandJoao Mendes ambaye ni mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Barcelona, Ronaldinho yuko katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Burnley ya England.Kocha wa Burnely, Scott Parker alithibitisha kuwa klabu hiyo ipo katika mpango wa kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka […]

The post Mtoto wa Gaucho aelekea Burnley first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Joao Mendes ambaye ni mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Barcelona, Ronaldinho yuko katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Burnley ya England.
Kocha wa Burnely, Scott Parker alithibitisha kuwa klabu hiyo ipo katika mpango wa kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 ingawa haitaki suala hilo kuwa gumzo kubwa kwenye vyombo vya habari.
Mendes ambaye amekuwa katika akademi ya Barcelona, anatarajia kuwajili Burnley wakati wowote kuanzia sasa baada ya taratibu za awali kukamilika.
Habari za ndani zinadai kwamba mchezaji huyo atasaini mkataba wa miaka miwili na Parker amekiri kwamba kumekuwa na mazungumzo ya karibu baina ya pande mbili husika.

“Hakuna ambacho kimekamilika rasmi kwa wakati huu, ni kweli kwamba kuna jambo linaloendelea, tunamuona kuwa ni mchezaji anayeweza kuwa na maendeleo na anaweza kuwa sahihi lakini kuna mambo ya kusaini mikataba ambayo hayajakamilika,” alisema Parker.


Parker alisema kwamba anavutiwa na jambo hilo kutokana na sifa za baba wa mtoto huyo lakini anadhani haitokuwa sahihi kulifanya jambo hilo kubwa na kumuweka katika hali ya presha mchezaji huyo kwa kuwa nimchezaji ni mwenye kujiunga na timu ili kuendeleza kipaji chake.
Awali Mendes alianza kucheza soka Brazil kabla ya kuhamia katika akademi ya Barcelona mwaka 2023 na kuwa sehemu ya kikosi cha timu ya vijana chini ya miaka 19 cha timu hiyo.
Burnley ambayo imewahi kucheza Ligi Kuu England kwa sasa ini timu inayoshiriki Ligi ya Championship.
Ronaldinho au Gaucho ni mmoja wa wachezaji waliokuwa tishio akitamba katika klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazil.

The post Mtoto wa Gaucho aelekea Burnley first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/08/16/mtoto-wa-gaucho-aelekea-burnley/feed/ 0
Stars, DR Congo kundi moja Afcon 2025 https://www.greensports.co.tz/2024/07/04/stars-dr-congo-kundi-moja-afcon-2025/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/04/stars-dr-congo-kundi-moja-afcon-2025/#respond Thu, 04 Jul 2024 19:53:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11521 Johannesburg, Afrika KusiniTimu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imepangwa Kundi H katika kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025, kundi ambalo pia lina timu za Ethiopia, DR Congo na Guinea.Katika droo iliyofanyika leo jijini Johannesburg, mabingwa watetezi, Ivory Coast wao wamepangwa Kundi G ambalo pia lina timu za Sierra Leone, […]

The post Stars, DR Congo kundi moja Afcon 2025 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Johannesburg, Afrika Kusini
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imepangwa Kundi H katika kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025, kundi ambalo pia lina timu za Ethiopia, DR Congo na Guinea.
Katika droo iliyofanyika leo jijini Johannesburg, mabingwa watetezi, Ivory Coast wao wamepangwa Kundi G ambalo pia lina timu za Sierra Leone, Zambia pamoja na Chad.
Jumla ya timu 48 zitachuana katika mbio za kuwania kufuzu fainali hizo zinazoshirikisha nchi za mataifa ya Afrika ambapo timu hizo zimepangwa katika makundi 12, kila kundi likiwa na timu nne ambapo mbili ndizo zitakazofuzu.
Morocco ambao wapo Kundi B wanakuwa wamefuzu moja kwa moja kama wenyeji na hiyo maana yake ni kwamba timu nyingine mbili katika kundi lake kati ya Gabon, Afrika ya Kati na Lesotho ndizo zitakazofuzu.
Mechi za kuwania kufuzu fainali hizo zitaanza kutimua vumbi Septemba na kuendelea Oktoba hadi Novemba na fainali za Afcon 2025 zitaanza kutimua vumbi Desemba 21 hadi Januari 18 2026 siku ambayo mechi ya mwisho itapigwa na bingwa kupatikana.


Hii itakuwa mara ya kwanza kwa fainali za Afcon kuchezwa Desemba na kuendelea hadi wakati wa Krismasi kipindi ambacho baadhi ya ligi Ulaya zinakuwa na mapumziko mafupi.

The post Stars, DR Congo kundi moja Afcon 2025 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/04/stars-dr-congo-kundi-moja-afcon-2025/feed/ 0
Gamondi afurahia uwanja mzuri https://www.greensports.co.tz/2024/04/27/gamondi-afurahia-uwanja-mzuri/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/27/gamondi-afurahia-uwanja-mzuri/#respond Fri, 26 Apr 2024 21:02:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10754 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema amefurahishwa kurejea kwenye uwanja mzuri na rafiki kuelekea mechi yao ya kesho Jumamosi ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Coastal Union mechi itakayopigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.Gamondi raia wa Argentina, ameyasema hayo baada ya kupata suluhu dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wao […]

The post Gamondi afurahia uwanja mzuri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema amefurahishwa kurejea kwenye uwanja mzuri na rafiki kuelekea mechi yao ya kesho Jumamosi ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Coastal Union mechi itakayopigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Gamondi raia wa Argentina, ameyasema hayo baada ya kupata suluhu dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wao wa mwisho wa ligi uliopigwa kwenye Uwanja wa Jenerali Isamuhyo.
Kocha huyo alisema kwamba uwanja huo haukuwa rafiki kutokana na kuharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini na hivyo kuvuruga mipango yao mingi ya ushindi.
“Tumetoka kucheza mchezo wa kwenye mazingira magumu na tuna njaa ya kupata alama tatu. Hautakuwa mchezo rahisi kwa sababu Coastal ni wazuri kwenye kuzuia mashambulizi, lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mchezo wa kesho,” alisema Gamondi.
“Mechi zinapokuwa karibu sana muda wa maandalizi unakuwa mdogo, jana tumefanya mazoezi ya kurejesha miili sawa kwa wachezaji na leo (Ijumaa) tutapata muda kidogo wa kujiandaa kwa ajili ya mchezo wa kesho na hapo ndipo nitajua wachezaji wa kuwatumia,” alisema Gamondi.
Mchezo wa kesho unahitaji sana ubora wa wachezaji na angalau tunaenda kucheza kwenye uwanja wenye mazingira mazuri, muhimu zaidi kesho ni kuweka mpira wavuni na kuibuka na ushindi,” alisema Gamondi.
Yanga ambayo inaongoza ligi kwa pointi 59 baada ya mechi 23, itaivaa Coastal iliyo kwenye nafasi ya nne na pointi zao 33 baada ya kushuka dimbani mara 23.

The post Gamondi afurahia uwanja mzuri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/27/gamondi-afurahia-uwanja-mzuri/feed/ 0
Gamondi akiri mechi ngumu https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/gamondi-akiri-mechi-ngumu/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/gamondi-akiri-mechi-ngumu/#respond Tue, 02 Apr 2024 20:25:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10489 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kwamba wanafahamu ugumu ulio mbele yao katika mechi dhidi ya Mamemelodi Sundowns lakini watatafuta matokeo ugenini.Kauli ya Gamondi imekuja wakati Yanga ikiwa imetua salama jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwa mchezo huo ambao ni wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Yanga itakipiga na Mamelodi […]

The post Gamondi akiri mechi ngumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kwamba wanafahamu ugumu ulio mbele yao katika mechi dhidi ya Mamemelodi Sundowns lakini watatafuta matokeo ugenini.
Kauli ya Gamondi imekuja wakati Yanga ikiwa imetua salama jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwa mchezo huo ambao ni wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga itakipiga na Mamelodi Aprili 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld, Pretoria ikitafuta sare ya mabao au ushindi wa aina yoyote ili kufuzu hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza baada ya matokeo ya 0-0 kwenye mchezo wa awali uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
“Mchezo ni mgumu, nafikiri mchezo utakuwa na presha inayofanana maana Sundowns wana presha ya kutaka kuingia nusu fainali sababu ni miongoni mwa wanaopewa nafasi ya kutwaa ubingwa.

“Na wao pia wanataka kushinda, washiriki kwenye michuano ya Klabu Bingwa Dunia lakini nategemea utakuwa mchezo wa mbinu na tutapambana kupata bao ugenini sababu kama nafasi tunatengeneza, tunachohitaji kuendelea kushikamana, nikiwaamini vijana wangu, natumai tutaingia nusu,” alisema Gamondi.


Kocha huyo raia wa Argentina pia alizungumzia uwezekano wa mabadiliko ya kikosi katika mchezo huo kutokana na maendeleo mazuri waliyonayo majeruhi wake.
Wachezaji majeruhi wa Yanga ni Pacome Zouzoua, Kouassi Yao na Khalid Aucho ambao wote walikosekana katika mchezo wa kwanza kutokana na kuwa na majeraha mbalimbali.

The post Gamondi akiri mechi ngumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/02/gamondi-akiri-mechi-ngumu/feed/ 0
Pep amvulia kofia Bellingham https://www.greensports.co.tz/2024/03/16/pep-amvulia-kofia-bellingham/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/16/pep-amvulia-kofia-bellingham/#respond Sat, 16 Mar 2024 20:34:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10231 Manchester, EnglandBaada ya Man City kupangwa kucheza na Real Madrid katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kocha wa City, Pep Guardiola ameibuka na kumfisia kiungo wa Real, Jude Bellingham.Timu hizo zitaumana Aprili 9 na kurudiana Aprili 17 ambapo Pep amesema Real ya msimu huu imekuwa tofauti ukilinganisha na msimu uliopita na […]

The post Pep amvulia kofia Bellingham first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Baada ya Man City kupangwa kucheza na Real Madrid katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kocha wa City, Pep Guardiola ameibuka na kumfisia kiungo wa Real, Jude Bellingham.
Timu hizo zitaumana Aprili 9 na kurudiana Aprili 17 ambapo Pep amesema Real ya msimu huu imekuwa tofauti ukilinganisha na msimu uliopita na kumpa pongezi Bellingham kwa mchango wake katika hilo.
Msimu uliopita, City waliwatoa Real katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya sare ya bao 1-1 ugenini Bernabeu, City wakiwa nyumbani Ettihad kwenye mechi ya marudiano waliibuka na ushindi wa mabao 4-0.
Bellingham ambaye alijiunga na Real Julai mwaka jana akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa ada ya dola milioni 112, hadi sasa ameifungia timu hiyo mabao 20 katika mashindano yote.
Pep aliombwa ufafanuzi kuhusu ubora wa kiungo huyo ambapo alisema kwamba mchango wa mchezaji huyo umekuwa mkubwa mno kwenye timu.

“Timu (Real Madrid) imekuwa tofauti na ya msimu uliopita, mchango Bellingham upo wazi na tutajaribu kuangalia nini anafanya ili kumdhibiti,” alisema Pep.


Pep pia alikiri kwamba kupambana na Real wakati wote ni changamoto nzito na hakuna wa kubisha hilo kwa kuwa timu hiyo ni ya kipekee na katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wanaweza kutawala kila kitu kutokana na uzoefu walionao wa siku za nyuma.

The post Pep amvulia kofia Bellingham first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/16/pep-amvulia-kofia-bellingham/feed/ 0
Mchezaji Cameroon adaiwa kudanganya umri, jina https://www.greensports.co.tz/2024/03/13/mchezaji-cameroon-adaiwa-kudanganya-umri-jina/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/13/mchezaji-cameroon-adaiwa-kudanganya-umri-jina/#respond Wed, 13 Mar 2024 05:49:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10159 Yaounde, CameroonCameroon imemsimamisha mchezaji aliyeshiriki fainali za Afcon 2023 na timu hiyo kwa kosa la kudanganya jina na tarehe ya kuzaliwa jambo ambalo pia linaweza kuifanya nchi hiyo ifungiwe.Taarifa ya Shirikisho la Soka Cameroon (Fecafoot) ilimtaja mchezaji huyo kuwa ni Wilfried Nathan Douala akiwa ni miongoni mwa wachezaji waliosimamishwa katika ligi kwa kwenda kinyume na […]

The post Mchezaji Cameroon adaiwa kudanganya umri, jina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Yaounde, Cameroon
Cameroon imemsimamisha mchezaji aliyeshiriki fainali za Afcon 2023 na timu hiyo kwa kosa la kudanganya jina na tarehe ya kuzaliwa jambo ambalo pia linaweza kuifanya nchi hiyo ifungiwe.
Taarifa ya Shirikisho la Soka Cameroon (Fecafoot) ilimtaja mchezaji huyo kuwa ni Wilfried Nathan Douala akiwa ni miongoni mwa wachezaji waliosimamishwa katika ligi kwa kwenda kinyume na taratibu ikiwamo majina kugongana na kudanganya umri.
Cameroon ilitolewa katika raundi ya pili ya fainali za Afcon Januari mwaka huu lakini kabla ya hapo kulikuwa na utata kuhusu hatua ya kocha wa timu hiyo, Rigobert Song kumuita Douala katika timu yake.
Douala ambaye ilidaiwa kwamba alikuwa na miaka 17, alikuwa akiichezea klabu ya daraha la pili ya Victoria United na hakuwa na uzoefu wowote kwenye soka la kimataifa.
Mchezaji huyo aliibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii ambapo watu wengi walikuwa wakihoji kama kweli alikuwa na miaka 17 mara baada ya picha yake kuonekana hadharani mara ya kwanza.
Uchunguzi wa gazeti la kila siku la Le Monde la Ufaransa ulidai kuwa Douala kabla ya hapo aliwahi kucheza kwenye ligi ya nchini Cameroon kwa jina la Alexandre Bardelli na alikuwa na umri zaidi ya miaka 21.
Siku chache kabla ya timu ya Cameroon kuelekea Ivory Coast kwenye fainali za Afcon, gazeti hilo liliwataka maofisa wanaosimamia soka nchini humo kuelezea utata uliojitokeza kuhusu mchezaji huyo lakini hawakusema lolote.
Mchezaji huyo hata hivyo alibaki kwenye timu ya taifa na kwenda kwenye fainali za Afcon nchini Ivory Coast ingawa hakupata nafasi ya kucheza hata mechi moja.
Kanuni za fainali za Afcon zinasema iwapo kutatokea ukiukwaji wa taratibu au udanganyifu wa aina yoyote, chama cha nchi husika kitasimamishwa kushiriki fainali hizo kwa michuano miwili inayofuata.

The post Mchezaji Cameroon adaiwa kudanganya umri, jina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/13/mchezaji-cameroon-adaiwa-kudanganya-umri-jina/feed/ 0
Kocha Morocco ajibebesha lawama Afcon https://www.greensports.co.tz/2024/02/01/kocha-morocco-ajibebesha-lawama-afcon/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/01/kocha-morocco-ajibebesha-lawama-afcon/#respond Thu, 01 Feb 2024 19:10:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9549 Abidjan, Ivory CoastKocha wa timu ya taifa ya Morocco, Walid Regragui amesema anabeba lawama zote za timu hiyo kutolewa kwenye fainali za Afcon hatua ya 16 bora baada ya kufungwa mabao 2-0 na Afrika Kusini.Morocco au Atlas Lion ilishindwa kutamba juzi Jumanne mbele ya Afrika Kusini na kutolewa kimaajabu jambo lililowashangaza wengi kwa kuwa ni […]

The post Kocha Morocco ajibebesha lawama Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Abidjan, Ivory Coast
Kocha wa timu ya taifa ya Morocco, Walid Regragui amesema anabeba lawama zote za timu hiyo kutolewa kwenye fainali za Afcon hatua ya 16 bora baada ya kufungwa mabao 2-0 na Afrika Kusini.
Morocco au Atlas Lion ilishindwa kutamba juzi Jumanne mbele ya Afrika Kusini na kutolewa kimaajabu jambo lililowashangaza wengi kwa kuwa ni moja ya timu zilizopewa nafasi ya kubeba taji hilo.
Timu hiyo ilianza kwa kuadhibiwa kwa bao la Evidence Makgopa dakika takriban 10 baada ya kuanza kipindi cha pili kabla ya Teboho Mokoena kumalizia bao la pili katika dakika za lala salama.
Morocco mbali na nyota wake, Achraf Hakimi kukosa penalti lakini pia ilimaliza mechi na wachezaji 10 baada ya kiungo wake, Sofyan Amrabat kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
“Labda tungeweza kumaliza mechi katika nusu ya kwanza, lakini katika hatua tuliyofikia unaweza kuadhibiwa kwa nafasi yoyote unayoipoteza,” alisema Regragui.

“Penalti umetuuma sana na hakika hatukufanya kila kitu tulichotakiwa kukifanya lakini mimi nabeba lawama zote,’ alisema Regragui.


Matumaini ya Morocco yalikuwa ni kubeba taji la Afcon kwa mara ya kwanza tangu ifanye hivyo mwaka 1976 na mafanikio yao ya kufikia nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 yalifanya matumaini ya kubeba taji hilo kuwa makubwa zaidi.
“Tutajifunza kutokana na mkwamo huu ambao hatukuutarajia, hili ni jambo la kuumiza kwa mashabiki wetu ambao wamekuwa wakituunga mkono kwa kiasi kikubwa,” alisema Regragui.

The post Kocha Morocco ajibebesha lawama Afcon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/01/kocha-morocco-ajibebesha-lawama-afcon/feed/ 0
Bao la Pacome lang’ara Afrika https://www.greensports.co.tz/2023/12/05/bao-la-pacome-langara-afrika/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/05/bao-la-pacome-langara-afrika/#respond Tue, 05 Dec 2023 20:13:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8747 Na mwandishi wetuBao la kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua dhidi ya Al Ahly limechaguliwa kuwa bao bora la wiki la mechi za raundi ya pili hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Mtandao rasmi wa michuano hiyo uliweka video ya bao la Pacome na kuandika: “Ndani ya Tanzania, katikati ya mabeki watatu, bao bora […]

The post Bao la Pacome lang’ara Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Bao la kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua dhidi ya Al Ahly limechaguliwa kuwa bao bora la wiki la mechi za raundi ya pili hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mtandao rasmi wa michuano hiyo uliweka video ya bao la Pacome na kuandika: “Ndani ya Tanzania, katikati ya mabeki watatu, bao bora la wiki la mechi za pili limekwenda kwa Pacome Zouzoua wa Yanga.”
Kiungo huyo alifunga bao hilo kwa shuti kali ndani ya 18 akiwa amezungukwa na msitu wa mabeki wa Al Ahly kwenye dakika za lala salama katika mchezo huo uliochezwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Bao hilo lilipindua matokeo na kuwa sare ya 1-1 na hivyo kuinusuru timu hiyo na kipigo cha pili mfululizo katika mechi za Kundi D baada ya awali kupoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya CR Belouizdad.
Mbali na kufunga bao hilo, kiungo huyo raia wa Ivory Coast alionesha uwezo mkubwa ikiwemo kutengeneza nafasi kadhaa ambazo wenzake walishindwa kuzitumia ipasavyo.
Pacome aloyejiunga na Yanga msimu huu akitokea ASEC Mimosas, anaungana na Mudathir Yahya na Fiston Mayele ambao mabao waliyoifungia timu hiyo msimu uliopita kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika yalishinda tuzo za mabao bora ya wiki.

The post Bao la Pacome lang’ara Afrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/05/bao-la-pacome-langara-afrika/feed/ 0
Safu ya ulinzi yaibeba Namungo https://www.greensports.co.tz/2023/12/05/safu-ya-ulinzi-yaibeba-namungo/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/05/safu-ya-ulinzi-yaibeba-namungo/#respond Tue, 05 Dec 2023 08:00:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8742 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa Namungo, Denis Kitambi ameeleza kuwa miongoni mwa kinachowafanya kuendelea kupata matokeo mazuri kwenye Ligi Kuu NBC ni kuimarika kwa safu yao ya ulinzi.Kitambi (pichani) ameieleza hayo GreenSports Jumatatu hii baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo uliochezwa Jumapili hii kwenye, Uwanja wa Majaliwa, […]

The post Safu ya ulinzi yaibeba Namungo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Namungo, Denis Kitambi ameeleza kuwa miongoni mwa kinachowafanya kuendelea kupata matokeo mazuri kwenye Ligi Kuu NBC ni kuimarika kwa safu yao ya ulinzi.
Kitambi (pichani) ameieleza hayo GreenSports Jumatatu hii baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo uliochezwa Jumapili hii kwenye, Uwanja wa Majaliwa, Lindi.
Huo unakuwa ni ushindi wao wa tatu katika mechi sita za mwisho za Namungo, kati ya mechi hizo wametoka sare mara mbili na kufungwa mara moja.
Katika mechi sita za awali za ligi chini ya kocha Cedric Kaze, Namungo ilipoteza mechi tatu na kutoa sare tatu.
“Kwanza tumepambana kuimarisha safu yetu ya ulinzi, maana kama ikitokea tumeshindwa kufunga basi tusipoteze pointi, hivyo tunaelekea kufanikiwa na sasa tumehamia safu ya ushambuliaji kuhakikisha nako kunakuwa sawa ili timu iwe kamili kimapambano na kutafuta pointi.
“Kingine ni ushindi wetu wa kwanza tulioupata dhidi ya Ihefu hivi karibuni, maana ilikuwa hata tukicheza nyumbani hatuna morali lakini sasa morali imerejea ndio maana tumeshinda tukiwa nyumbani, hivyo bado tunapambana kukaa sawa na tunaamini tunaelekea kuzuri,” alisema Kitambi.
Baada ya ushindi huo wa Jumapili, Namungo sasa imepanda kutoka nafasi ya 12 mpaka nafasi ya nane ikiwa na pointi 14 kibindoni.

The post Safu ya ulinzi yaibeba Namungo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/05/safu-ya-ulinzi-yaibeba-namungo/feed/ 0
Brazil hoi, Neymar abebwa kwenye machela https://www.greensports.co.tz/2023/10/18/brazil-hoi-neymar-abebwa-kwenye-machela/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/18/brazil-hoi-neymar-abebwa-kwenye-machela/#respond Wed, 18 Oct 2023 08:52:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8144 Montevideo, UruguayBaada ya kurushiwa mfuko wa popcorn na mashabiki, mabalaa yamezidi kumuandama mshambuliaji wa Brazil, Neymar ambaye timu yake imelala kwa mabao 2-0 mbele ya Uruguay huku yeye akiumia goti na kutolewa uwanjani kwa machela.Brazil jana Jumanne iliumana na Uruguay katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 lakini Neymar alicheza mechi […]

The post Brazil hoi, Neymar abebwa kwenye machela first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Montevideo, Uruguay
Baada ya kurushiwa mfuko wa popcorn na mashabiki, mabalaa yamezidi kumuandama mshambuliaji wa Brazil, Neymar ambaye timu yake imelala kwa mabao 2-0 mbele ya Uruguay huku yeye akiumia goti na kutolewa uwanjani kwa machela.
Brazil jana Jumanne iliumana na Uruguay katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 lakini Neymar alicheza mechi hiyo kwa dakika 44 kabla ya kuumia.
Richarlison aliingia kuchukua nafasi ya Neymar ambaye baadaye alionekana akiwa amebebwa kwenye machela akitoka uwanjani huku akiwa ameziba uso kwa mikono yake.
Timu ya madaktari wa Brazil haikusema lolote kuhusu kuumia kwa Neymar lakini baadaye daktari wa timu hiyo, Rodrigo Lasmar alisema kwamba baada ya mechi mchezaji huyo alifanyiwa vipimo vya awali na leo Jumatano atafanyiwa vipimo vingine.

“Saa 24 zijazo ni muhimu kuona hali ya goti itakuwaje, kwa sasa ni mapema mno kusema lolote ngoja tusubiri vipimo zaidi na kujua undani, baada ya hapo tutawaarifu,” alisema Lasmar.


Neymar, 31, hakuzungumza lolote na waandishi wa habari lakini baadaye alitumia mitandao ya kijamii kumshukuru Mungu akidai kwamba ndiye anayejua kila kitu na bado ana imani naye.
Mabao ya washindi katika mechi hiyo yalifungwa na Darwin Nunez na Nicolas de la Cruz na kuifanya Brazil kushindwa kutamba katika mechi ya pili mfululizo baada ya sare ya bao 1-1 na Venezuela, mechi ambayo Neymar alirushiwa mfuko wa popcorn (bisi) na shabiki.
Akizungumzia kuumia kwa Neymar, nahodha wa Brazil, Casemiro alisema ana imani mchezaji huyo hajaumia sana kwa sababu ni mchezaji muhimu kwao ingawa amekuwa akiumia mara kwa mara hata anapoanza kupona na kurejea katika ubora wake hujikuta akiumia. Katika mechi nyingine ya kufuzu Kombe la Dunia, Argentina iliichapa Peru mabao 2-0.

The post Brazil hoi, Neymar abebwa kwenye machela first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/18/brazil-hoi-neymar-abebwa-kwenye-machela/feed/ 0