Video - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 30 May 2023 10:07:37 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Video - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Everton yapona, Leicester yashuka daraja https://www.greensports.co.tz/2023/05/28/everton-yapona-leicester-yashuka-daraja/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/28/everton-yapona-leicester-yashuka-daraja/#respond Sun, 28 May 2023 18:22:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6347 London, EnglandTimu za Leicester na Leeds United zimeungana na Southampton kushuka daraja zikiaga rasmi Ligi Kuu England (EPL) baada ya mechi za leo Jumapili ambazo ni za mwisho huku Everton ikiepuka janga hilo.Everton ambayo ilikuwa inachungulia kaburi, ushindi wa bao 1-0 ilioupata mbele ya Bournemouth umekuwa na maana kwa timu hiyo ambayo imefikisha pointi 36 […]

The post Everton yapona, Leicester yashuka daraja first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Timu za Leicester na Leeds United zimeungana na Southampton kushuka daraja zikiaga rasmi Ligi Kuu England (EPL) baada ya mechi za leo Jumapili ambazo ni za mwisho huku Everton ikiepuka janga hilo.
Everton ambayo ilikuwa inachungulia kaburi, ushindi wa bao 1-0 ilioupata mbele ya Bournemouth umekuwa na maana kwa timu hiyo ambayo imefikisha pointi 36 ikishika nafasi ya 17 na hivyo kujihakikishia kucheza EPL msimu ujao.
Msimu wa EPL 2022-23 umehitimishwa rasmi kwa mechi za mwisho kuchezwa leo ambapo timu hizo tatu sasa zitacheza Ligi ya Champioship kuanzia msimu ujao wa 2023-24.


Southampton ambayo ilishaaga EPL siku chache zilizopita, imehitimisha mechi yake ya mwisho leo kwa sare ya mabao 4-4 na Liverpool na hivyo kumaliza ligi ikiwa na pointi 25 na ndiyo inayoshika mkia.
Timu ya Leeds ambayo nayo haikuwa katika nafasi nzuri imemaliza ligi ikiwa nafasi ya 18 na pointi 31 na katika mechi ya leo imelala kwa mabao 4-1 mbele ya Tottenham.
Leicester, ambao ni mabingwa wa EPL msimu wa 2015-16, licha ya kupata ushindi wa mabao 2-1 mbele ya West Ham, ushindi huo haukuweza kuwaokoa na janga hilo na wamemaliza ligi wakiwa nafasi ya 19 na pointi zao 34.
Matokeo ya mechi zote za leo ambazo ni za mwisho kwa msimu wa EPL 2022-23 ni kama ifuatavyo…
Arsenal 5-0 Wolves
Aston Villa 2-1 Brighton
Brentford 1-0 Man City
Chelsea 1-1 Newcastle
Crystal Palace 1-1 Nottm Forest
Everton 1-0 Bournemouth
Leeds 1-4 Tottenham
Leicester 2-1 West Ham
Man Utd 2-1 Fulham
Southampton 4-4 Liverpool

The post Everton yapona, Leicester yashuka daraja first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/28/everton-yapona-leicester-yashuka-daraja/feed/ 0
Haaland aweka rekodi ya tuzo https://www.greensports.co.tz/2023/05/27/haaland-aweka-rekodi-ya-tuzo/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/27/haaland-aweka-rekodi-ya-tuzo/#respond Sat, 27 May 2023 20:43:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6332 Manchester, EnglandStraika wa Man City, Erling Haaland leo Jumamosi ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu akiwa pia ameshinda tuzo ya mchezaji bora kijana na kuwa mchezaji wa kwanza kubeba tuzo zote mbili kwa msimu mmoja.Haaland (pichani) mwenye umri wa miaka 22 amefunga mabao 36 katika mechi 35 msimu huu ambayo pia yameiwezesha Man City […]

The post Haaland aweka rekodi ya tuzo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Straika wa Man City, Erling Haaland leo Jumamosi ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu akiwa pia ameshinda tuzo ya mchezaji bora kijana na kuwa mchezaji wa kwanza kubeba tuzo zote mbili kwa msimu mmoja.
Haaland (pichani) mwenye umri wa miaka 22 amefunga mabao 36 katika mechi 35 msimu huu ambayo pia yameiwezesha Man City kubeba taji la Ligi Kuu England (EPL) kwa mara ya tatu mfululizo.
Kwa idadi hiyo ya mabao anakuwa amevunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na mastraika wa zamani Andy Cole wa Man United na Alan Shearer wa Newcastle waliofikisha mabao 34 katika msimu mmoja takriban miaka 30 iliyopita.
Haaland ambaye katika michuano yote ana mabao 52 msimu huu, bado ana nafasi ya kuongeza idadi ya mabao kesho Jumapili, Man City itakapocheza mechi yake ya mwisho ya EPL dhidi ya Brentford.
Tuzo hizo kwa Haaland zimetolewa baada ya kura zilizopigwa na umma na nyingine kupigwa na manahodha wa timu 20 za EPL na nyingine zikipigwa na wataalamu wa soka.
“Nimepata heshima kwa kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo zote mbili katika msimu mmoja,” alisema Haaland.

“Imekuwa msimu mzuri katika ligi kuu, na kubeba taji wiki iliyopita mbele ya mashabiki wetu kwenye uwanja wa Etihad ni tukio la kipekee kwangu,” aliongeza Haaland.


Mbali na tuzo hiyo, Haaland pia alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ya Chama cha Waandishi wa Habari za Soka baada ya kuweka rekodi kwa kupata asilimia 82 ya kura zilizopigwa.

The post Haaland aweka rekodi ya tuzo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/27/haaland-aweka-rekodi-ya-tuzo/feed/ 0