Sports Mix - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 19 Apr 2025 19:30:35 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Sports Mix - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Adhabu ya Sinner yamshangaza Serena Williams https://www.greensports.co.tz/2025/04/19/adhabu-ya-sinner-yamshangaza-serena-williams/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/19/adhabu-ya-sinner-yamshangaza-serena-williams/#respond Sat, 19 Apr 2025 19:30:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13278 New York, MarekaniNyota wa mchezo wa tenisi wa Marekani, Serena Williams (pichani) amesema kama yeye angekutwa na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu angefungiwa miaka 20 na kunyang’anywa tuzo zote za Grand Slams alizobeba.Serena alitoa kauli hiyo akionekana kushangazwa na adhabu aliyopewa bingwa namba moja wa mchezo huo duniani kwa upande wa wanaume, Jannik […]

The post Adhabu ya Sinner yamshangaza Serena Williams first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Nyota wa mchezo wa tenisi wa Marekani, Serena Williams (pichani) amesema kama yeye angekutwa na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu angefungiwa miaka 20 na kunyang’anywa tuzo zote za Grand Slams alizobeba.
Serena alitoa kauli hiyo akionekana kushangazwa na adhabu aliyopewa bingwa namba moja wa mchezo huo duniani kwa upande wa wanaume, Jannik Sinner ambaye alikutwa na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu na Februari mwaka jana akafungiwa miezi mitatu.
Sinner alikubali kufungiwa miezi mitatu baada ya makubaliano na Wada, taasisi ya kimataifa inayojihusisha kukabiliana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu.
Wada walifikia hatua hiyo baada ya kupinga maamuzi ya tume huru iliyoamua kumfutia Sinner kosa hilo licha ya kupimwa mara mbili na kubainika kuwa alikuwa akitumia dawa hizo.
Serena alisema anampenda Sinner kwani ni shujaa katika mchezo wa tenisi na ingawa yeye amekuwa akishushwa chini sana lakini kwa upande wake hapendi kumshusha mtu hasa kwa kuwa mchezo wa tenisi kwa wanaume unamhitaji Sinner.

“Hata hivyo ukweli ni kwamba ningekuwa mimi ningefungiwa miaka 20 na kunyang’anywa tuzo zangu zote za Grand Slams,” alisema Serena ambaye amewahi kushinda Grand Slams kwa mara 23.


Serena, 43, alisema kwamba wakati wote katika mchezo wa tenisi amekuwa makini kwa kila kitu anachokiingiza mwilini mwake kwa hofu ya kuingia kwenye matatizo.
Katika hali ya dhihaka, Serena alisema kwamba jambo dogo tu lingeweza hata kumpeleka jela na kusikika kila kona katika namna nyingine.

The post Adhabu ya Sinner yamshangaza Serena Williams first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/19/adhabu-ya-sinner-yamshangaza-serena-williams/feed/ 0
Rais wa kwanza mwanamke IOC aahidi kuwalinda wanawake https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/rais-wa-kwanza-mwanamke-ioc-kuwalinda-wanawake/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/rais-wa-kwanza-mwanamke-ioc-kuwalinda-wanawake/#respond Tue, 01 Apr 2025 10:49:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13169 Athens, UgirikiMwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) na rais wa kwanza wa IOC anayetokea Afrika, Kirsty Coventry (pichani juu) ameahidi kuwalinda wanamichezo wanawake.Katika miaka 130 ya historia ya IOC, ndoto ya kumpata rais mwanamke huenda haikuwahi kufikiriwa ukiachilia mbali mwanamke huyo awe ni mwenye kutoka katika bara la Afrika.Mambo […]

The post Rais wa kwanza mwanamke IOC aahidi kuwalinda wanawake first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Athens, Ugiriki
Mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) na rais wa kwanza wa IOC anayetokea Afrika, Kirsty Coventry (pichani juu) ameahidi kuwalinda wanamichezo wanawake.
Katika miaka 130 ya historia ya IOC, ndoto ya kumpata rais mwanamke huenda haikuwahi kufikiriwa ukiachilia mbali mwanamke huyo awe ni mwenye kutoka katika bara la Afrika.
Mambo hata hivyo yamekuwa tofauti kupitia uchaguzi wa IOC uliofanyika Machi mwaka huu nchini Ugiriki kwa Kirsty ambaye pia amekuwa waziri nchini Zimbabwe kuibuka kidedea.
Kwa wananchi wa Zimbabwe ushindi wa Kirsty, unawakumbusha hali ilivyokuwa miaka 20 ilyopita wakati Kirsty ambaye kwa sasa ana miaka 41, aliposhinda medali ya dhahabu katika mchezo wa kuogelea.
Katika Michezo ya Olimpiki nchini Ugiriki miaka 20 iliyopita jina la Kirsty lilitamba na kuibua shangwe Zimbabwe na Afrika alipotwaa medali ya dhahabu katika mchezo wa kuogelea.
Machi 20 mwaka huu, Kirsty amewapa tena furaha wananchi wa Zimbabwe na Afrika kwa baada ya kushinda kiti cha urais wa IOC na sasa anasubiri Juni mwaka huu ili kuanza rasmi majukumu mapya ya ubosi wa IOC akichukua nafasi ya Thomas Bach (pichani chini) .
Ushindi wake ulimkumbusha mwaka 1992 akiwa msichana mdogo wa miaka tisa akiangalia Michezo ya Olimpiki ya Barcelona kwenye televisheni, hakuwahi kuwaza kama ingefika wakati akawa rais wa IOC.

Ushindi wake haujaibua furaha pekee bali pia kuna hali ya mshangao kwa kuwa hakuna au ni wachache mno waliokuwa na matarajio kama angeweza kuibuka kinara na kumrithi Bach.
Akizungumzia mikakati yake ndani ya IOC baada ya ushindi, Kirsty alisema atawalinda wanamichezo wanawake pamoja na kila kipengele cha michezo ya wanawake.
Katika hilo pia amefafanua kwamba hakuna jipya kwani amekuwa akikabiliana na wanaume wabishi tangu akiwa na umri wa miaka 20.
Zaidi ya hilo, Kirsty ameahidi kufanya kazi na mashirikisho ya kimataifa akitaka IOC kujipa jukumu la kiuongozi zaidi kwa kuunda vikosi kazi ambavyo vitafanyia tathmini kila kazi wanayoifanya.
Kirsty pia alikumbushia medali yake ya mwaka 2004 na ushindi wa urais wa IOC kwa kusema kwamba Ugiriki ni nchi yenye bahati kwake.

“Niliheshimiwa kwa mafanikio ya mwaka 2004 hapa Athens, inaonekana Ugiriki ni nchi ya bahati kwangu,” alisema Kirsty.


Kirsty pia alisema kwamba yeye si mwanamke wa kwanza kujitokeza katika kuwania nafasi hiyo na mmoja wao ambaye amesaidia kumpa hamasa ya kuitaka nafasi hiyo ni Anita DeFrantz ambaye alikuwapo wakati wa uchaguzi huo.
Alisema anajivunia kumfanya Anita awe na jambo la kujivunia kwa kuwa amemhamasisha na kumuongoza tangu wakati anaingia katika harakati za Olimpiki mwaka 2013.
“Najua itanichukua muda kidogo kuwa sawa hapa lakini mwanamke kama yeye huwa anafungua njia kwa wanawake wengine kama mimi na nataka nami nifungue njia kwa wanawake wengine vijana hasa kwa kuwa mimi ni mama wa watoto wawili wa kike,” alisema Kirsty.
Kuhusu mume wake
Akimzungumzia mume wake, Kirsty alimsifu kwamba ana mume wa kipekee na kuongeza kwamba kwa pamoja wana jukumu la kufanya maamuzi na wamekuwa ni watu wa kushirikiana.

“Mimi na mume wangu lazima tuwe wenye kufanya maamuzi, hata nilipopewa kazi ya Waziri wa Vijana, Michezo na Sanaa wa Zimbabwe, tulifahamu kwamba tunajitoa kufanya kazi ya kila siku,” alisema Kirsty.


Akizungumzia ushindi wa Kirsty, mtangulizi wake, Bach alisema IOC imempata mtu sahihi katika sehemu sahihi akiamini kuwa ushindi wa kiongozi huyo ni ishara ya mshikamano katika harakati za Olimpiki.

The post Rais wa kwanza mwanamke IOC aahidi kuwalinda wanawake first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/rais-wa-kwanza-mwanamke-ioc-kuwalinda-wanawake/feed/ 0
Stars yafuzu Afcon 2025 https://www.greensports.co.tz/2024/11/20/stars-yafuzu-afcon-2025/ https://www.greensports.co.tz/2024/11/20/stars-yafuzu-afcon-2025/#respond Wed, 20 Nov 2024 08:09:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12281 Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 zitakazofanyika nchini Morocco baada ya kuilaza Guinea bao 1-0. Ushindi huo umepatikana Jumanne hii Novemba 19, 2024 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kwa bao hilo pekee lililofungwa na Simon Msuva. Bao hilo […]

The post Stars yafuzu Afcon 2025 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 zitakazofanyika nchini Morocco baada ya kuilaza Guinea bao 1-0.

Ushindi huo umepatikana Jumanne hii Novemba 19, 2024 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kwa bao hilo pekee lililofungwa na Simon Msuva.

Bao hilo limetosha kuifanya Stars iweke rekodi ya kufuzu fainali hizo zinazoshirikisha nchi za Mataifa ya Afrika kwa mara ya nne kuanzia mwaka 1980, 2018 na 2023.

Msuva alifunga bao hilo dakika ya 60 akimalizia pasi ya juu ya Mudathir Yahya na kuruka kabla ya kuupiga mpira wa kichwa ambao ulimshinda kipa wa Guinea, Mussa Camara ambaye pia anaidakis timu ya Simba.

Ushindi huo umeifanya Stars iliyokuwa Kundi H kufikisha pointing 10 na kushika nafasi ya pili nyuma ya vinara DR Congo wenye pointi 12 wakati Guinea wanabaki na pointi tisa na Ethiopia wamemaliza wakiwa mkiani na pointi yao moja.

Guinea ni dhahiri wameumizwa mno na matokeo hayo kwani walihitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu lakini walijikuta pagumu kwa kipindi kirefu cha mchezo kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya wachezaji wa Stats.

Stars walicheza kwa kujiamini wakikaba na kulishambulia mara kwa mara lango la Guinea ingawa timu hiyo ilikuwa na tatizo katika umaliziaji.

Msuva na Clement Mzize mara kadhaa walilisakama lango la Guinea lakini walikosa umakini katika umaliziaji na kuinyima Stars mabao kabla ya Msuva kurekebisha makosa yake na kuipa Stats ushindi.

Baada ya filimbi ya kumaliza mchezo kupulizwa na mashabiki waliofurika uwanjani kulipuka kwa shangwe, baadhi ya wachezaji wa Guinea walionekana wakimzonga mwamuzi wa mchezo huo katika namna iliyoonesha kutofurahia baadhi ya maamuzi yake.

Stars baada ya ushindi sasa inasubiri kujua itapangwa na timu gani katika Kundi lake kwa ajili ya fainali za Afcon 2025 zitakazofanyika mapema mwakani nchini Morocco.

The post Stars yafuzu Afcon 2025 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/11/20/stars-yafuzu-afcon-2025/feed/ 0
Aliyemchoma moto mwanariadha naye afariki https://www.greensports.co.tz/2024/09/10/aliyemchoma-moto-mwanariadha-naye-afariki/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/10/aliyemchoma-moto-mwanariadha-naye-afariki/#respond Tue, 10 Sep 2024 19:07:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11885 Eldoret, KenyaSiku chache baada ya mwanariadha wa Uganda, Rebecca Cheptegei (pichani) kufariki kwa kuchomwa moto wa petroli, aliyekuwa rafiki yake wa kiume, Dickson Ndiema anayedaiwa kumfanyia ukatili huo naye amefariki dunia leo Jumanne.Rebecca, 33 ambaye aliiwakilisha Uganda kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 hivi karibuni, alichomwa moto Septemba Mosi na kuungua zaidi ya asilimia […]

The post Aliyemchoma moto mwanariadha naye afariki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Eldoret, Kenya
Siku chache baada ya mwanariadha wa Uganda, Rebecca Cheptegei (pichani) kufariki kwa kuchomwa moto wa petroli, aliyekuwa rafiki yake wa kiume, Dickson Ndiema anayedaiwa kumfanyia ukatili huo naye amefariki dunia leo Jumanne.
Rebecca, 33 ambaye aliiwakilisha Uganda kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 hivi karibuni, alichomwa moto Septemba Mosi na kuungua zaidi ya asilimia 70 ya mwili wake kabla ya kufariki dunia siku nne baadaye.
Kifo cha Rebecca kilitokana na mzozo baina yake na Dickson chanzo kikidaiwa kuwa ni mgogoro baina ya wawili hao uliotokana na eneo la ardhi ambayo inadaiwa Rebecca aliinunua na kujenga nyumba.
Baada ya kifo cha Rebbeca ndugu zake na watu mbalimbali walisisitiza kutaka haki itendeke lakini kifo cha Dickson ambaye alikuwa mtuhumiwa mkuu kinazidi kuacha maswali kuhusu tukio hilo.
Wawili hao baada ya wote kuwa na majeraha ya moto walikimbizwa katika Hospitali ya Moi mjini Eldoret wakiwa na hali mbaya ingawa Rebecca ndiye aliyeungua sehemu kubwa ya mwili wake kumzidi Dickson.
Akizungumzia kifo cha Dickson, msemaji wa Hospitali ya Moi, Daniel Lang’at alisema kifo chake kilitokana na majeraha ya kuungua na moto.
Katika Michezo ya Olimpiki, Rebecca alishika nafasi ya 44 na baadhi ya makundi ya watetezi wa haki za wanawake wanahusisha kifo hicho na matukio ya unyanyasaji na unyonyaji wanaofanyiwa wanamichezo wanawake waliopata mafanikio.

The post Aliyemchoma moto mwanariadha naye afariki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/10/aliyemchoma-moto-mwanariadha-naye-afariki/feed/ 0
Mwanariadha aliyechomwa moto afariki dunia https://www.greensports.co.tz/2024/09/05/mwanariadha-wa-uganda-aliyechomwa-moto-kenya-afariki-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/05/mwanariadha-wa-uganda-aliyechomwa-moto-kenya-afariki-dunia/#respond Thu, 05 Sep 2024 13:07:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11873 Eldoret, KenyaMwanariadha wa Uganda aliyeiwakilisha nchi hiyo kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, Rebecca Cheptegei amefariki dunia siku chache baada ya kuchomwa moto na rafiki yake wa kiume.Rebecca, 33, aliungua zaidi ya asilimia 70 ya mwili wake baada ya kuchomwa moto na rafiki yake wa kiume baada ya kuibuka mzozo baina ya wawili hao.Msemaji […]

The post Mwanariadha aliyechomwa moto afariki dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Eldoret, Kenya
Mwanariadha wa Uganda aliyeiwakilisha nchi hiyo kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, Rebecca Cheptegei amefariki dunia siku chache baada ya kuchomwa moto na rafiki yake wa kiume.
Rebecca, 33, aliungua zaidi ya asilimia 70 ya mwili wake baada ya kuchomwa moto na rafiki yake wa kiume baada ya kuibuka mzozo baina ya wawili hao.
Msemaji wa Hospitali ya Moi ya mjini Eldoret, Owen Menach alithibitisha kuwa mwanariadha huyo amefariki leo Alhamisi asubuhi baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo siku chache zilizopita akiwa na hali mbaya na viungo vyake vingi kushindwa kufanya kazi.
Rebecca alishiriki vyema Michezo ya Olimpiki ya Paris akiwa mwakilishi wa Uganda na kumaliza nafasi ya 44 katika mbio za marathon kwa wanawake na umauti umemkuta akiwa hajamaliza hata mwezi mmoja tangu kuiwakilisha Uganda kwenye Olimpiki.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya hospitali hiyo, Joseph Cheptegei ambaye ni baba mzazi wa Rebecca alisema amepoteza mtoto ambaye alikuwa msaada mkubwa kwake na ana matumaini haki itatendeka.
Mapema Jumatatu taarifa ya polisi wa kaunti ya Trans-Nzoia, ilieleza kuwa rafiki wa kiume wa Rebecca alitumia galoni la petroli na kummwagia Rebecca kabla ya kumuwashia moto.
Moto huo hata hivyo uliwaunguza wote wawili na hadi sasa rafiki huyo naye amelazwa katika hospitali hiyo hiyo akiwa katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu.
Awali kiongozi wa eneo lililotokea tukio hilo alisema wawili hao walikuwa na mzozo ambao chanzo chake kinadaiwa ni eneo la ardhi ambalo lina nyumba inayodaiwa kujengwa na Rebecca, nyumba ambayo tukio la moto huo lilitokea.
Shirikisho la Riadha Uganda lilitoa taarifa kupitia mitandao ya kijamii kueleza kusikitishwa na kifo cha Rebecca na kumuombea marehemu apumzike kwa maani huku wakilaani tukio zima la mauaji hayo na kuomba haki itendeke.

The post Mwanariadha aliyechomwa moto afariki dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/05/mwanariadha-wa-uganda-aliyechomwa-moto-kenya-afariki-dunia/feed/ 0
Mwanariadha Uganda achomwa moto Kenya https://www.greensports.co.tz/2024/09/04/mwanariadha-wa-uganda-achomwa-moto-kenya/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/04/mwanariadha-wa-uganda-achomwa-moto-kenya/#respond Wed, 04 Sep 2024 05:58:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11860 Eldoret, KenyaMwanariadha wa Uganda aliyetoka kushiriki Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, Rebecca Cheptegei amechomwa moto na rafiki yake wa kiume nchini Kenya na kuungua zaidi ya asilimia 70 ya mwili wake.Kwa mujibu wa Polisi tukio hilo lilitokea katika jimbo la Trans-Nzoia ambapo Rebecca ambaye alishika nafasi ya 44 katika Olimpiki Paris 2024 alivamiwa Jumapili […]

The post Mwanariadha Uganda achomwa moto Kenya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Eldoret, Kenya
Mwanariadha wa Uganda aliyetoka kushiriki Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, Rebecca Cheptegei amechomwa moto na rafiki yake wa kiume nchini Kenya na kuungua zaidi ya asilimia 70 ya mwili wake.
Kwa mujibu wa Polisi tukio hilo lilitokea katika jimbo la Trans-Nzoia ambapo Rebecca ambaye alishika nafasi ya 44 katika Olimpiki Paris 2024 alivamiwa Jumapili akiwa nyumbani kwake kabla ya kukutana na kadhia hiyo.
Kamanda wa Polisi wa Trans Nzoia, Jeremiah ole Kosiom alisema rafiki wa kiume wa Rebecca akiwa na dumu la mafuta ya petroli alimmwagia na kumchoma baada ya wawili hao kutofautiana.
Katika kadhia hiyo, rafiki wa kiume wa Rebebcca naye alipatwa na majeraha ya moto na kwa sasa wote wawili wanapatiwa matibabu maalum katika hospitali ya Moi iliyopo katika jiji la Eldoret.
Wazazi wa Rebecca walinukuliwa wakisema kwamba mtoto wao alinunua kiwanja maeneo ya Trans Nzoia ili awe karibu na wanariadha wenzake kwa lengo la kurahisisha ufanyaji wa mazoezi katika kituo maalum.
Taarifa ya polisi ilimnukuu kiongozi mmoja wa eneo hilo akisema kwamba kabla ya kadhia hiyo Rebecca na rafiki yake wa kiume walikuwa na mzozo kuhusu ardhi iliyotumika kujenga nyumba hiyo na ndipo baadaye tukio la Rebecca kuchomwa moto lilipojitokeza.
Tukio la Rebecca ni mwendelezo wa matukio ya kikatili dhidi ya wanariadha wa Uganda, mwaka 2023 mwanariadha Benjamin Kiplagat alikutwa amekufa mjini Eldoret akiwa na majeraha yanayodhaniwa kuwa ni ya visu.

The post Mwanariadha Uganda achomwa moto Kenya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/04/mwanariadha-wa-uganda-achomwa-moto-kenya/feed/ 0
Taswa yaandaa Mwambao Marathon https://www.greensports.co.tz/2024/07/02/taswa-yaandaa-mwambao-marathon/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/02/taswa-yaandaa-mwambao-marathon/#respond Tue, 02 Jul 2024 08:23:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11487 Na mwandishi wetuChama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) kimeandaa mbio za marathon zenye lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kutunza mazingira na kumtua mama kuni kichwani.Taarifa ya Taswa iliyotolewa leo Jumanne na kusainiwa na kaimu katibu mkuu wa chama hicho, Imani Makongoro ilieleza kuwa mbio hizo zilizopewa jina […]

The post Taswa yaandaa Mwambao Marathon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) kimeandaa mbio za marathon zenye lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kutunza mazingira na kumtua mama kuni kichwani.
Taarifa ya Taswa iliyotolewa leo Jumanne na kusainiwa na kaimu katibu mkuu wa chama hicho, Imani Makongoro ilieleza kuwa mbio hizo zilizopewa jina la Mwambao Marathon zitafanyika jijini Tanga Septemba 29 mwaka huu.
Mbio hizo zimeandaliwa na Taswa ili kusukuma mbele dhamira ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kutaka hadi 2034 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.
Taswa chini ya mwenyekiti wake, Amir Mhando (pichani) pia inakaribisha mashirika, makampuni, wadau wa mazingira na nishati safi kushirikiana nao katika kuandaa mbio hizo ambazo washiriki watashiriki mbio za kilometa 21, 10 au za kujifurahisha za kilometa tano.
Sambamba na hilo, mkutano mkuu wa wanachama wa Taswa utafanyika Septemba 28 mwaka huu jijini Tanga na kuhusisha wanachama waliolipa ada na mwisho wa kulipa ada na kuthibitisha kushiriki ni Agosti 30 mwaka huu.
Wanachama washiriki wa mkutano huo pia watapata nafasi ya kuhudhuria semina kuhusu umuhimu wa waandishi wa habari za michezo kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Katika semina hiyo pia itatolewa mada maalum kuhusu nafasi ya wanahabari kuelekea fainali za soka za Kombe la Mataifa ya Afrika 2027 au Afcon 2027 ambazo Tanzania itakuwa mwenyeji pamoja na nchi za Kenya na Uganda.

The post Taswa yaandaa Mwambao Marathon first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/02/taswa-yaandaa-mwambao-marathon/feed/ 0
Vipengele vyaongezwa Tuzo BMT https://www.greensports.co.tz/2024/05/17/vipengele-vyaongezwa-tuzo-bmt/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/17/vipengele-vyaongezwa-tuzo-bmt/#respond Fri, 17 May 2024 07:27:03 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10990 Na mwandishi wetuBaraza la Michezo Tanzania (BMT) limesema kuwa Tuzo za BMT zitafanyika Juni 9 mwaka huu huku vipengele viwili vikiongezwa katika tuzo hizo.Mwenyekiti wa kamati ya Tuzo BMT, Mtumbuka Mtambo, amesema vipengele vilivyoongezeka ni tuzo za mwaka 2023 zitakazotolewa ni vipengele vya tuzo ya kocha bora wa mwaka na mwamuzi bora wa mwaka.Alisema kwamba […]

The post Vipengele vyaongezwa Tuzo BMT first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baraza la Michezo Tanzania (BMT) limesema kuwa Tuzo za BMT zitafanyika Juni 9 mwaka huu huku vipengele viwili vikiongezwa katika tuzo hizo.
Mwenyekiti wa kamati ya Tuzo BMT, Mtumbuka Mtambo, amesema vipengele vilivyoongezeka ni tuzo za mwaka 2023 zitakazotolewa ni vipengele vya tuzo ya kocha bora wa mwaka na mwamuzi bora wa mwaka.
Alisema kwamba lengo la kuongeza vipengele hivyo ni katika kuhakikisha wadau wote wa sekta za michezo wanatambulika na kuthaminiwa.
“Mabadiliko mengine ni uwepo wa tuzo za jumla mwaka huu na si za mchezo mmoja mmoja, mabadiliko haya yanalenga kuleta ushindani na ufanisi ikiwa ni pamoja na kuleta usawa wa uthamani wa michezo yote, kadhalika mabadiliko haya yanaongeza thamani ya tuzo hizi kiujumla,” alisema Mtambo.
Naye, mwenyekiti wa BMT, Leodegar Tenga (pichani juu) kuelekea msimu wa pili mfululizo wa utolewaji wa tuzo hizo, alisema kwa kifupi kuwa ni muhimu kuwepo kwa tuzo hizo kwani zinachagiza maendeleo ya michezo katika kila nyanja kuanzia kukuza viwango vya ushindani mpaka uwekezaji.

“Faida za tuzo ni kubwa sana lakini kwa maneno machache ni kuhamasisha, kuchagiza maendeleo ya michezo kwa maana ya kukuza kiwango, kuna kuchagiza uwekezaji kwenye michezo maana bila uwekezaji hali ni ngumu, haiwezekani hata kidogo, nchi zote zilizofanya vizuri zimewekeza,” alisema Tenga.


The post Vipengele vyaongezwa Tuzo BMT first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/17/vipengele-vyaongezwa-tuzo-bmt/feed/ 0
Katibu awapa neno BMT https://www.greensports.co.tz/2024/05/17/katibu-awapa-neno-bmt/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/17/katibu-awapa-neno-bmt/#respond Fri, 17 May 2024 07:12:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10984 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Suleiman Serera (pichani) amelitaka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) liwe na mipango kabambe na imara itakayofanikisha ukuwaji na maendeleo ya michezo nchini.Serera ametoa kauli hiyo alipokutana na kufanya mazungumzo na menejimenti ya baraza hilo ambapo amewataka waendelee kuimarisha ushirikiano na Serikali za Mitaa.Alisema kwamba […]

The post Katibu awapa neno BMT first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Suleiman Serera (pichani) amelitaka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) liwe na mipango kabambe na imara itakayofanikisha ukuwaji na maendeleo ya michezo nchini.
Serera ametoa kauli hiyo alipokutana na kufanya mazungumzo na menejimenti ya baraza hilo ambapo amewataka waendelee kuimarisha ushirikiano na Serikali za Mitaa.
Alisema kwamba kwa kufanya hivyo watakuwa wanapeleka ujuzi na hamasa zaidi ya michezo kwa lengo la kuibua vipaji na kuimarisha afya za Watanzania kwa ujumla.
“Hatuwezi kufanikiwa kwenye eneo la michezo kama hatujashuka kwenye Serikali za Mitaa, hamasa huko chini ni kubwa ila inahitaji muunganiko mzuri na ushawishi kwa ajili ya kuibua na kuendeleza michezo kote nchini katika ufanisi mkubwa zaidi,” alisema Serera.
Serera alisisitiza zaidi kwa kulitaka baraza hilo kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa michezo katika jamii ili kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.
Kikao hicho kilikuwa cha kwanza kai ya Dk Serera na BMT, tangu kuteuliwa kwake katika nafasi hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan.

The post Katibu awapa neno BMT first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/17/katibu-awapa-neno-bmt/feed/ 0
Viza zawakosesha mashindano wanariadha https://www.greensports.co.tz/2024/03/29/viza-zawakosesha-mashindano-wanariadha/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/29/viza-zawakosesha-mashindano-wanariadha/#respond Fri, 29 Mar 2024 15:05:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10439 Na mwandishi wetuTimu ya Taifa ya riadha ya mbio za Nyika imeshindwa kwenda Belgrade, Serbia kushiriki mashindano ya Dunia yatakayoanza leo Ijumaa baada ya baadhi ya wachezaji kukosa visa.Timu hiyo yenye wachezaji tisa, ambayo ilikuwa kambini Ngaramtoni, Arusha kuanzia Machi 22, mwaka huu ilitarajiwa kuondoka juzi Machi 27, mwaka huu lakini imeshindikana kutokana na changamoto […]

The post Viza zawakosesha mashindano wanariadha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Taifa ya riadha ya mbio za Nyika imeshindwa kwenda Belgrade, Serbia kushiriki mashindano ya Dunia yatakayoanza leo Ijumaa baada ya baadhi ya wachezaji kukosa visa.
Timu hiyo yenye wachezaji tisa, ambayo ilikuwa kambini Ngaramtoni, Arusha kuanzia Machi 22, mwaka huu ilitarajiwa kuondoka juzi Machi 27, mwaka huu lakini imeshindikana kutokana na changamoto hiyo.
Wachezaji waliotarajiwa kusafiri kwa wanaume ni Herman Sulle, Boay Dawi, Dectaforce Boniface, Mao Ako na John Nahhay na wanawake ni Hamida Nassoro, Neema Festo, Ernestina Mngolale na Anastazia Dolomongo na kocha Marcelina Gwandu.
Akizungumza leo Ijumaa, Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Silas Isangi (pichani) alikiri kuhusiana na hilo: “Wanariadha walitarajiwa kuondoka tarehe 27 lakini ililazimika kusogeza mbele safari yao hadi tarehe 28 baada ya kuchelewa kupata viza kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu.
Alisema maombi ya viza yalifanyika Machi 8, mwaka huu kwenye ubalozi wa Serbia uliopo Nairobi nchini Kenya lakini mpaka Machi 27 ni wachezaji watano tu waliofanikiwa kukamilisha upatikanaji wa nyaraka hizo.
Alisema ndege ya KLM inatarajia kuondoka kesho Jumamosi saa nne asubuhi, kutoka Tanzania kupitia Entebbe, Uganda hivyo wangechelewa kufika Amsterdam, Uholanzi kwa ajili ya kuunganisha kwenda Serbia.

The post Viza zawakosesha mashindano wanariadha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/29/viza-zawakosesha-mashindano-wanariadha/feed/ 0