Soka - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 23 Apr 2025 17:18:13 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Soka - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mo amshukuru Rais Samia https://www.greensports.co.tz/2025/04/23/mo-amshukuru-rais-samia/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/23/mo-amshukuru-rais-samia/#respond Wed, 23 Apr 2025 17:14:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13309 Na mwandishi wetuRais wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa msaada wake katika klabu hiyo inayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika.Taarifa ya Mo iliyopatikana leo Jumatano Aprili 23, 2025 ilielezea shukrani za klabu hiyo kwa mchango wa usafiri na malazi kuelekea mchezo wao wa […]

The post Mo amshukuru Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa msaada wake katika klabu hiyo inayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika.
Taarifa ya Mo iliyopatikana leo Jumatano Aprili 23, 2025 ilielezea shukrani za klabu hiyo kwa mchango wa usafiri na malazi kuelekea mchezo wao wa marudiano dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini.
Simba itarudiana na timu hiyo Jumapili ijayo katika mechi ya pili ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho ikiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 ilioupata Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Katika taarifa hiyo, Mo ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo, alisema Simba inatambua na kuthamini juhudi za Rais Samia katika sekta ya michezo nchini hasa mchezo wa soka.
Mo alitolea mfano wa goli la mama ambalo huhusisha zawadi ya Sh milioni 10 kwa kila goli linalofungwa kwenye mechi za kimataifa akisema jambo hilo limekuwa chanzo cha hamasa na ari kwa wachezaji na mashabiki.
Sambamba na Rais Samia, Mo pia alitoa shukrani zake kwa Wizara ya Fedha pamoja na Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kwa namna wizara hizo zilivyoratibu safari ya Simba.
Mo pia alitoa shukran kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Reli Tanzania (TRL).
Iwapo Simba itafanikiwa kuitoa Stellenbosch itaumana katika fainali na mshindi wa mechi kati ya RS Berkane na CS Constantine.

The post Mo amshukuru Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/23/mo-amshukuru-rais-samia/feed/ 0
Ancelotti: Lolote lawezekana https://www.greensports.co.tz/2025/04/22/ancelotti-lolote-lawezekana/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/22/ancelotti-lolote-lawezekana/#respond Tue, 22 Apr 2025 15:36:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13305 Madrid, HispaniaKocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amezungumzia mambo yake ya baadaye katika klabu hiyo akisisitiza lolote linawezekana wakati huu timu yake ikichuana na Barcelona kuwania mataji ya La Liga na Kombe la Mafalme.Ancelotti amekuwa katika kipindi kigumu tangu timu yake itolewe na Arsenal kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa […]

The post Ancelotti: Lolote lawezekana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Madrid, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amezungumzia mambo yake ya baadaye katika klabu hiyo akisisitiza lolote linawezekana wakati huu timu yake ikichuana na Barcelona kuwania mataji ya La Liga na Kombe la Mafalme.
Ancelotti amekuwa katika kipindi kigumu tangu timu yake itolewe na Arsenal kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kipigo cha jumla cha mabao 5-1.
Real Madrid imeachwa na Barcelona kwa tofauti ya pointi nne katika La Liga zikiwa zimebaki mechi sita kabla ya kufikia tamati ya kwa ligi hiyo, pia Jumamosi itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya timu hiyo kwenye Kombe la Mfalme.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo Jumanne, Aprili 22, 2025 kabla ya kuumana na Getafe kwenye La Liga, Ancelotti alisema timu yake inaweza kubeba mataji yote hayo mawili.
Kuhusu presha ya nafasi yake ya ukocha, Ancelotti ambaye mkataba wake na Real Madtid unaishia 2026 alisema hali hiyo na yote yanayoendelea ni kama kichocheo kwake.
Kocha huyo badala yake aliwapa mashabiki wa timu hiyo habari njema kuhusu mshambuliaji Kylian Mbappe aliyeumia enka akisema anaendelea vizuri na anaweza kucheza mechi ya fainali ya Kombe la Mfalme.

“Katika soka lolote linawezekana, je mnashangazwa na mambo yote yanayotokea, hakuna kinachonishangaza mimi, kama ninavyosema wakati wote, naipenda hii kazi, nilipenda nilivyokuwa hapa awamu ya kwanza (2013 hadi 2015) napenda hii awamu ya pili kuanzia 2021 na nataka awamu hii iendelee kadri inavyowezekana,” alisema Ancelotti.


Ancelotti pia alisema kwamba ikifika siku ambayo kazi yake itafikia mwisho atakuwa mwenye kushukuru na kuvua kofia yake katika klabu hiyo kwani hiyo ndiyo hali halisi.
Kocha huyo Mtaliano amejijengea heshima kwa kuiwezesha Real Madrid kubeba mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini msimu huu umekuwa mgumu huku habari ya kutimuliwa kwake ikipamba moto siku hadi siku.

The post Ancelotti: Lolote lawezekana first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/22/ancelotti-lolote-lawezekana/feed/ 0
Yanga yaicharaza Fountain Gate mabao 4-0 https://www.greensports.co.tz/2025/04/21/yanga-yaicharaza-fountain-gate-mabao-4-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/21/yanga-yaicharaza-fountain-gate-mabao-4-0/#respond Mon, 21 Apr 2025 18:56:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13296 Na mwandishi wetuYanga imeipa kipigo cha mabao 4-0 Fountain Gate FC katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa leo Jumatatu Aprili 21, 2025 kwenye Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa mjini Manyara.Yanga ilianza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 38 lililofungwa na Clement Mzize ambaye aliyatumia vizuri makosa ya kipa wa Fountain Gate, John Noble kuipatia […]

The post Yanga yaicharaza Fountain Gate mabao 4-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Yanga imeipa kipigo cha mabao 4-0 Fountain Gate FC katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa leo Jumatatu Aprili 21, 2025 kwenye Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa mjini Manyara.
Yanga ilianza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 38 lililofungwa na Clement Mzize ambaye aliyatumia vizuri makosa ya kipa wa Fountain Gate, John Noble kuipatia Yanga bao.
Bao la pili la Yanga lilifungwa na Stephane Aziz Ki ambaye kama ilivyo kwa Mzize naye aliyatumia makosa ya kipa Noble aliyejichanganya wakati akiokoa mpira ulioelekezwa langoni mwake badala yake akamrudishia mfungaji.
Kipindi cha pili kiliendelea kuwa kigumu kwa Fountain Gate baada ya kupachikwa bao la tatu mfungaji akiwa Mzize katika dakika ya 69 akiitumia pasi ya Jonathan Ikangalombo.
Mzize ambaye pia aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo, bao hilo lina maana kubwa kwake kwani sasa amefikisha mabao 13 katika ligi hivyo kuwa kinara akifuatiwa na Jean Ahoua wa Simba mwenye mabao 12 sawa na Prince Dube wa Yanga.
Clatous Chama alikamilisha bao la nne kwa Yanga katika dakika ya 89 akifunga kwa mpira wa adhabu iliyotolewa baada ya Mtenje Albano kumchezea rafu Mzize nje kidogo ya eneo la penalti.
Ushindi huo unaifanya Yanga kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 70 katika mechi 26 ikiiacha Simba nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 katika mechi 22.

The post Yanga yaicharaza Fountain Gate mabao 4-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/21/yanga-yaicharaza-fountain-gate-mabao-4-0/feed/ 0
Simba yailaza Stellenbosch 1-0 https://www.greensports.co.tz/2025/04/20/simba-yailaza-stellenbosch-1-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/20/simba-yailaza-stellenbosch-1-0/#respond Sun, 20 Apr 2025 16:23:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13285 Na mwandishi wetuSimba imeanza vizuri mechi ya kwanza ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuilaza Stellenbosch ya Afrika Kusini bao 1-0 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, leo Jumapili, Aprili 20, 2025.Bao pekee la Simba lilipatikana dakika ya 45 mfungaji akiwa ni Jean Ahoua kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja hadi wavuni […]

The post Simba yailaza Stellenbosch 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Simba imeanza vizuri mechi ya kwanza ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuilaza Stellenbosch ya Afrika Kusini bao 1-0 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, leo Jumapili, Aprili 20, 2025.
Bao pekee la Simba lilipatikana dakika ya 45 mfungaji akiwa ni Jean Ahoua kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja hadi wavuni na kumshinda kipa Oscarine Masuluke.
Bao hilo liliibua utata baada ya wachezaji wa Stellenbosch kugomea wakidai wachezaji wa Simba waliotea hivyo kulazimika kutumia VAR kabla ya kutangazwa kuwa ni bao halali.
Simba waliutawala vyema mchezo huo kwa wachezaji wake kuonesha ubora wao wa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini tatizo la umaliziaji liliendelea kuiathiri timu hiyo.
Moja ya nafasi ya mapema Simba kuipata ni pale Kibu Dennis alipoambaa na mpira akiwa upande wa kushoto wa Stellenbosch na kupiga krosi ambayo Shomari Kapombe alibinuka vyema na kuupiga mpira staili ya tikitaka lakini mpira huo ulipaa nje ya lango.
Kasi ya Simba iliendelea na katika dakika ya 30, Ahoua aliunasa mpira na kumuunganishia Elly Mpanzu ambaye aliukokota kidogo kabla ya kufumua shuti kali la mguu wa kushoto ambalo liliokolewa vyema na kipa wa Stelenbosch.
Baada ya kuona kasi ya Simba inawazidi wachezaji wa Stellenbosch walianza kucheza rafu na mwamuzi kulazimika kuwapa kadi za njano Enyimnaya na Jabaar kwa kuwachezea rafu Mpanzu na Kibu.
Dakika tano baadaye Stellenbosch nao walijibu shambulizi baada ya kipa kuokoa mpira wa kona na kuwasaidia kutengeneza shambulizi lililoelekezwa upande wa kulia wa Simba.
Shambulizi hilo hata hivyo lilikwama baada ya Zimbwe Jr aliyehamia upande huo kumdhibiti mchezaji wa Stellenbosch wakati huo Kapombe anayecheza zaidi upande wa kulia akiwa amehamia upande wa kushoto ambao anacheza Zimbwe.
Kipindi cha pili, Stellenbosch walikianza kwa kufanya mabadiliko kadhaa yaliyoonekana kuwapa uhai na kumuweka katika wakati mgumu kipa Musa Camara wa Simba.


Simba nao walibadilika na kuanza kulisakama lango la wapinzani wao kwa kutengeneza nafasi nyingi ambazo hata hivyo walikwama katika kuzitumia nafasi hizo.
Nafasi mojawapo ya mwisho ni ile waliyoipata ikiwa imebaki dakika moja katika dakika sita za nyongeza baada ya Ahoua kuunganishiwa pasi ya chinichini na Mpanzu naye kumlamba chenga kipa Masuluke lakini shuti alilopiga la mguu wa kushoto lilitoka nje.
Katika mechi hiyo timu zote zilifanya mabadiliko kadhaa, Stellenbosch wakiwatoa De Jong na kumuingiza Bans na Jabaar ambaye nafasi yake aliingia Palace.
Simba iliwatoa Zimbwe na kuingia Valentine Nouma, Kibu akaingia Joshua Mutale, Deborah Fernandes akaingia kuchukua nafasi ya Chamaou Karabou wakati Ateba akaingia kuchukua nafasi ya Steven Mukwala.
Timu hizo zinatarajia kurudiana Aprili 27 nchini Afrika Kusini, mechi ambayo mshindi atajikatia moja kwa moja tiketi ya kucheza mechi ya fainali ya michuano hiyo dhidi ya mshindi wa mechi ya nusu fainali nyingine kati ya CS Constantine na RS Berkane.

The post Simba yailaza Stellenbosch 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/20/simba-yailaza-stellenbosch-1-0/feed/ 0
Ally Kamwe atozwa faini milioni 5, wengine wafungiwa maisha https://www.greensports.co.tz/2025/04/19/ally-kamwe-atozwa-faini-milioni-5-wengine-wafungiwa-maisha/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/19/ally-kamwe-atozwa-faini-milioni-5-wengine-wafungiwa-maisha/#respond Sat, 19 Apr 2025 19:33:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13281 Na mwandishi wetuKamati ya Maadili ya TFF imemtoza faini ya Sh milioni 5, meneja habari na mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe baada ya kumkuta na hatia katika kosa la kuchochea umma.Maamuzi ya kamati hiyo ambayo yametangazwa leo Jumamosi, Aprili 19, 2025 kwenye taarifa ya TFF, pia yamemkosa na hatia meneja habari na mawasiliano wa Simba, […]

The post Ally Kamwe atozwa faini milioni 5, wengine wafungiwa maisha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kamati ya Maadili ya TFF imemtoza faini ya Sh milioni 5, meneja habari na mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe baada ya kumkuta na hatia katika kosa la kuchochea umma.
Maamuzi ya kamati hiyo ambayo yametangazwa leo Jumamosi, Aprili 19, 2025 kwenye taarifa ya TFF, pia yamemkosa na hatia meneja habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ambaye kama Kamwe wote walikuwa na tuhuma za kuchochea umma.
Wakati Ahmed alishitakiwa na Yanga kwa kosa hilo, Kamwe yeye alishitakiwa na kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi na amepewa onyo na kutakiwa kutofanya kosa hilo kwa kipindi cha miaka miwili.
Taarifa ya TFF haijataja makosa hayo yalifanyika lini lakini inaaminika ni baada ya kuahirishwa mechi baina ya Yanga na Simba ambayo awali ilipangwa kuchezwa Machi 8 mwaka huu.
Baada ya mechi ya Yanga na Simba ambayo ni ya Ligi Kuu NBC kuahirishwa, yaliibuka malumbano baina ya viongozi wa timu hizo kwa kila upande kumtupia lawama mwenzake.
Mwingine aliyekutwa na hatia ya kosa la kuchochea umma ni ofisa habari wa Kagera Sugar, Hamis Mazanzala ambaye pia ametozwa faini ya Sh milioni tano.
Mwingine aliyekumbana na adhabu hiyo ni mwanachama wa klabu ya Simba, Mohamed Hamis Mohamed ambaye kama walivyo wenzake, wote wameanza kutumikia adhabu hizo Aprili 16 mwaka huu.
Wafungiwa maisha
Katika hatua nyingine kamati ya maadili ya TFF imemfungia maisha kujihusisha na soka ndani na nje ya nchi, Shufaa Jumanne Nyamlani ambaye ni mtunza vifaa wa timu ya taifa ya Beach Soccer.
Shufaa ambaye pia alikuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Chama cha Soka Wilaya ya Temeke (Tefa) alishitakiwa na Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) kwa makosa matatu.
Makosa hayo ni kuchochea umma, kutoheshimu maamuzi ya vyombo halali vya usimamizi wa soka na kutaka kuiondoa madarakani kamati ya utendaji ya Tefa na licha ya kuitwa kwa ajili ya shauri lake lakini hakuitikia wito huo.
Mwingine aliyefungiwa maisha ni Salehe Mohamed Salehe aliyekuwa makamu mwenyekiti Tefa ambaye naye alikuwa akituhumiwa kwa makosa kama ya Shufaa lakini naye hakuitikia wito wa kwenda kusikiliza tuhuma zilizokuwa zikimkabili.

The post Ally Kamwe atozwa faini milioni 5, wengine wafungiwa maisha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/19/ally-kamwe-atozwa-faini-milioni-5-wengine-wafungiwa-maisha/feed/ 0
Simba yaingia mkataba wa bilioni 38 https://www.greensports.co.tz/2025/04/17/simba-yaingia-mkataba-wa-bilioni-38/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/17/simba-yaingia-mkataba-wa-bilioni-38/#respond Thu, 17 Apr 2025 09:50:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13266 Na mwandishi wetuKlabu ya Simba imetangaza kuingia mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya Sh bilioni 38 za Kitanzania na Kampuni ya Jayrutty Investment ambayo itahusika na mauzo ya jezi na mambo mengine.Hafla ya kusaini mkataba huo ilifanyika Jumatano hii Aprili 16, 2025 na kuhudhuriwa na viongozi wa Simba na wadau mbalimbali wa michezo akiwamo […]

The post Simba yaingia mkataba wa bilioni 38 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Klabu ya Simba imetangaza kuingia mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya Sh bilioni 38 za Kitanzania na Kampuni ya Jayrutty Investment ambayo itahusika na mauzo ya jezi na mambo mengine.
Hafla ya kusaini mkataba huo ilifanyika Jumatano hii Aprili 16, 2025 na kuhudhuriwa na viongozi wa Simba na wadau mbalimbali wa michezo akiwamo naibu waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’.
Menyekiti wa kamati ya tenda ya Simba, Seif Muba alisema kwamba walipokea barua nyingi za maombi ya tenda hiyo lakini ofa ya Jayrutty imewashawishi kuwapa tenda hiyo.
Muba alisema kwa mantiki hiyo wamekubali kuwapa Jayrutty haki ya matumizi ya nembo ya klabu ya Simba kwa vile mbali na fedha kuna manufaa mengine mengi kwa klabu yao.
Alisema awali kampuni nane zilijitokeza lakini ni sita ndizo zilizowasilisha madokezo yao na kila kitu kilikuwa wazi kabla ya Jayrutty kushinda tenda hiyo na tayari wameweka kiasi cha Sh bilioni 38.
Akizungumzia mkataba huo, Mkurugenzi wa Jayrutty Investment, Joseph Rwagasira alizitaja baadhi ya faida ambazo klabu ya Simba itazipata kupitia mkataba huo kwa kipindi chote cha miaka mitano.
Rwegasira alisema jambo la kwanza watakalofanya ni kuijengea klabu hiyo uwanja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki kati ya 10,000 hadi 12,000 na watafanya hivyo katika uwanja wa klabu hiyo uliopo Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Alisema kwamba mbali na ujenzi huo lakini pia kila mwaka watatoa Sh milioni 100 kwa ajili ya soka la vijana, sh milioni 100 nyingine kwa maandalizi ya msimu na kiasi kingine kama hicho kwa ajili ya tamasha la Simba Day.
Sambamba na hilo, Jayrutty pia watatoa Sh milioni 450 kwa kila mwaka fedha ambazo zitakwenda kwa wachezaji wakati jezi za klabu hiyo sasa zitatengenezwa na kampuni kubwa duniani ingawa hakuitaja jina.
Kwa upande wake naibu waziri Mwana FA alisema serikali inapongeza kuingia kwa mkataba huo huku akielezea kuvutiwa zaidi na mpango wa ujenzi wa uwanja.
Mwana FA alisema uwanja huo unaweza kutumiwa kwa mechi za ndani wakati zile za kimataifa zikiendelea kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa ambao pia utakuwa umepunguziwa matumizi.

The post Simba yaingia mkataba wa bilioni 38 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/17/simba-yaingia-mkataba-wa-bilioni-38/feed/ 0
Yanga yaifanyizia Stand Utd, yailaza 8-1 https://www.greensports.co.tz/2025/04/15/yanga-yaifanyizia-stand-utd-yailaza-8-1/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/15/yanga-yaifanyizia-stand-utd-yailaza-8-1/#respond Tue, 15 Apr 2025 19:11:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13252 Na mwandishi wetuYanga imetua kibabe hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho CRDB kwa kuilaza Stand Utd mabao 8-1, mechi iliyochezwa leo Jumanne Aprili 15, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.Bao la kwanza la Yanga lilipatikana dakika ya 15 mfungaji akiwa Stephanie Aziz Ki aliyefunga kwa guu la kulia akiitumia pasi ndefu ya […]

The post Yanga yaifanyizia Stand Utd, yailaza 8-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Yanga imetua kibabe hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho CRDB kwa kuilaza Stand Utd mabao 8-1, mechi iliyochezwa leo Jumanne Aprili 15, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.
Bao la kwanza la Yanga lilipatikana dakika ya 15 mfungaji akiwa Stephanie Aziz Ki aliyefunga kwa guu la kulia akiitumia pasi ndefu ya Maxi Nzengeli na kumpiga chenga kipa Amir Mashenji.
Yanga iliandika bao la pili dakiika saba baadaye mfungaji akiwa ni beki wa kushoto, Nickson Kibabage ambaye aliitumia pasi ndefu ya Aziz Ki.
Bao la tatu la Yanga lilifungwa na Clatous Chama dakika ya 32, bao lililotokana na pasi ya Chama kwa Aziz Ki ambaye alimrudishia mpira Chama ambaye alimpiga chenga beki kabla ya kuujaza mpira wavuni.
Zikiwa zimebakia dakika tano timu kwenda mapumziko Yanga waliandika bao la nne mfungaji akiwa Chama kwa mara nyingine baada ya Aziz Ki kumpigia pasi ndefu na mpira kuwagonga mabeki wa Stand kabla ya kumkuta mfungaji.
Dakika moja kabla ya timu kwenda mapumziko, Stand walionesha uhai na kufanya shambulizi lililoanzia nyuma kabla ya mpira kumkuta Kigi Makasy lakini shuti lake la mguu wa kushoto lilipaa juu ya goli.
Kipindi cha pili, Stand waliendeleza moto wao na hatimaye kupata bao pekee dakika ya 49 lililofungwa na Msenda Senda ambaye aliingia uwanjani kuchukua nafasi ya Kigi.
Senda alionesha uwezo binafsi hadi kufunga bao hilo baada ya kuambaa na mpira kabla ya kumlamba chenga beki wa Yanga, Bakari Mwamnyeto na kufumua shuti lililomshinda kipa Djigui Diarra.
Bao hilo ni kama liliwatia hasira Yanga ambao waliongeza bao la tano dakika ya 51 likifungwa tena na Aziz Ki kwa mpira wa adhabu iliyotolewa baada ya Jonathan Ikangalombo kuchezewa rafu.

Dakika ya 60 Aziz Ki tena aliifungia Yanga bao la sita na la tatu (hat trick) kwake akiutumia mpira ulioanzia kwa Ikangalombo aliyempasia Chama ambaye naye alimpasia mfungaji na kuujaza mpira wavuni.
Aziz Ki ambaye aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo ni kama vile hakutosheka na hat trick baada ya kuifungia Yanga bao la saba na la nne kwake, safari hii akifunga kwa shuti la mbali.
Yanga walikamilisha karamu ya mabao kwa bao la nane lililofungwa na Kennedy Musonda ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Prince Dube, Musonda alifunga bao hilo kwa pasi ya Farid Mussa ambaye naye aliingia badala ya Aziz Ki.
Yanga sasa inasubiri kuumana na JKT Tanzania katika nusu fainali ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Benki ya CRDB wakati mahasimu wao Simba wataumana na Singida Black Stars katika nusu fainali ya pili, mechi ambazo washindi wake watacheza mechi ya fainali.

The post Yanga yaifanyizia Stand Utd, yailaza 8-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/15/yanga-yaifanyizia-stand-utd-yailaza-8-1/feed/ 0
Simba yatua nusu fainali Kombe la Shirikisho CRDB https://www.greensports.co.tz/2025/04/14/simba-yatua-nusu-fainali-fa/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/14/simba-yatua-nusu-fainali-fa/#respond Mon, 14 Apr 2025 06:56:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13243 Na mwandishi wetuSimba imefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho CRDB kwa kuilaza Mbeya City mabao 3-1 katika mechi iliyopigwa Jumapili hii Aprili 13, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.Mbeya City ndio walioanza kwa kuwashtua Simba baada ya kuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 22 lililofungwa na Mudathir […]

The post Simba yatua nusu fainali Kombe la Shirikisho CRDB first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho CRDB kwa kuilaza Mbeya City mabao 3-1 katika mechi iliyopigwa Jumapili hii Aprili 13, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.
Mbeya City ndio walioanza kwa kuwashtua Simba baada ya kuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 22 lililofungwa na Mudathir Abdullah ambaye aliitumia pasi ndefu ya William Daniel.
Baada ya kuinasa pasi hiyo, Abdullah aliwazidi ujanja mabeki wa Simba, Abdulrazak Hamza na Chamou Karabou kabla ya kufumua shuti la mguu wa kushoto lililomshinda kipa Ally Salim na kujaa wavuni.
Simba walionesha utulivu na dakika tatu baadaye walisawazisha bao hilo mfungaji akiwa Fabrice Ngoma ambaye aliinasa krosi ya Ladack Chasambi na kuunganisha mpira huo kwa kichwa hadi wavuni.
Kasi ya Simba iliendelea kuwaweka pagumu Mbeya City ambao walijikuta wakichapwa bao la pili mfungaji akiwa ni Leonel Ateba akiitumia krosi ya Ngoma.
Zikiwa zimebaki dakika mbili timu kwenda mapumziko, Simba waliandika bao la tatu lililofungwa na Joshue Mutale ambaye alionesha juhudi binafsi hadi kufunga bao hilo.
Mutale akiwa na mpira aliwazidi ujanja mabeki kadha wa Mbeya City kabla ya kufumua shuti lililomzidi ujanja kipa wa Mbeya City, Hashim Mussa.
Baada ya mabao hayo Simba waliendelea kutawala mchezo kwa kulisakama lango la Mbeya City na kumuweka katika wakati mgumu kipa Hashim Mussa ambaye alifanya juhudi kuokoa michomo kadhaa ya wachezaji wa Simba.
Simba baada ya ushindi huo wa robo fainali ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Benki ya CRDB, sasa inasubiri kucheza mechi ya nusu fainali na mshindi wa mechi kati ya Singida Black Stars na Kagera Sugar.

The post Simba yatua nusu fainali Kombe la Shirikisho CRDB first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/14/simba-yatua-nusu-fainali-fa/feed/ 0
Yanga yaitandika Azam 2-1 https://www.greensports.co.tz/2025/04/10/yanga-yaitandika-azam-2-1/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/10/yanga-yaitandika-azam-2-1/#respond Thu, 10 Apr 2025 19:36:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13236 Na mwandishi wetuYanga imeendelea na makali yake kwenye Ligi Kuu NBC baada ya kuinyuka Azam FC mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa leo Alhamisi, Aprili 10, 2025 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.Ushindi huo ni hatua muhimu kwa Yanga katika mbio zake za kulitetea taji la ligi hiyo kwa kuwa Azam ni moja ya […]

The post Yanga yaitandika Azam 2-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imeendelea na makali yake kwenye Ligi Kuu NBC baada ya kuinyuka Azam FC mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa leo Alhamisi, Aprili 10, 2025 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Ushindi huo ni hatua muhimu kwa Yanga katika mbio zake za kulitetea taji la ligi hiyo kwa kuwa Azam ni moja ya timu ambazo zilizoaminika kuwa na ubora wa kuizua Yanga lakini imekwama.
Yanga walianza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 10 mfungaji akiwa Pacome Zouzoua kabla ya kuongeza la pili dakika ya 34 lililofungwa na Prince Dube ambaye pia aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo.
Juhudi za Azam kusawazisha mabao hayo hazikuweza kuzaa matunda badala yake timu hiyo iliishia kupata bao pekee la kufutia machozi lililofungwa na Lusajo Mwaikenda katika dakika ya 82.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuendelea kushikilia usukani wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 67 katika mechi 25.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizopigwa leo, Coastal Union ikiwa nyumbani Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani iliichapa Singida B kwa mabao 2-1.
Kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mambo yaliendelea kuwa magumu kwa Tabora United baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Mashujaa wakati JKT Tanzania ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ilitoka sare ya mabao 2-2 na Namungo FC.

The post Yanga yaitandika Azam 2-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/10/yanga-yaitandika-azam-2-1/feed/ 0
Camara shujaa, Simba ikiitoa Al Masry kwa penalti 4-1 https://www.greensports.co.tz/2025/04/10/camara-shujaa-simba-ikiitoa-al-masry-kwa-penalti-4-1/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/10/camara-shujaa-simba-ikiitoa-al-masry-kwa-penalti-4-1/#respond Wed, 09 Apr 2025 22:01:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13229 Na mwandishi wetuKipa Musa Camara ameibuka shujaa kwa kuokoa mikwaju miwili ya penalti na kuiwezesha Simba kufuzu nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuitoa Al Masry ya Misri kwa penalti 4-1.Ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam Jumatano hii Aprili 9, 2025, Simba ilitoka na ushindi wa mabao 2-0 katika dakika […]

The post Camara shujaa, Simba ikiitoa Al Masry kwa penalti 4-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kipa Musa Camara ameibuka shujaa kwa kuokoa mikwaju miwili ya penalti na kuiwezesha Simba kufuzu nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuitoa Al Masry ya Misri kwa penalti 4-1.
Ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam Jumatano hii Aprili 9, 2025, Simba ilitoka na ushindi wa mabao 2-0 katika dakika 90 za kawaida hivyo kuingia kwenye mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kuwa na matokeo ya jumla ya sare ya mabao 2-2.
Sare hiyo ya jumla imekuja baada ya Simba kulala kwa 2-0 katika mechi ya kwanza baina ya timu hizo iliyopigwa, Ismailia, Misri, Jumatano iliyopita.
Mikwaju ya penalti
Simba ndio waliokuwa wa kwanza kupiga penalti iliyopigwa na Jean Ahoua ambaye alikwenda taratibu na kuujaza mpira wavuni kwa shuti la mguu wa kulia lililomshinda kipa, Mahmoud Gad.
Baada ya hapo Camara akaonesha ushujaa wake kwa kuokoa kwa miguu shuti la chinichini lililopigwa na Mido Gaber wakati Simba wakafunga penalti ya pili iliyopigwa kiufundi na Steven Mukwala.
Mukwala alirudi nyuma na kumchambua vyema kipa ambaye alijikuta akiruka upande wake wa kulia na mpira kujaa wavuni upande wa kushoto.
Al Masry walifanikiwa kupata bao katika penalti yao ya pili mfungaji akiwa Ben Youssef wakati Simba nao wakapata bao kwenye penalti ya tatu mfungaji akiwa Kibu Denis.


Camara kwa mara nyingine akaonesha umahiri wake kwa kuokoa penalti ya tatu ya Masry iliyopigwa na Mahmoud Hamada na kipa huyo kuruka upande wa kulia na kuuwahi mpira.
Baada ya hapo Shomari Kapombe akakamilisha hesabu kwa kuifungia Simba penalti ya nne ambayo ilifanya uwanja ulipuke kwa shangwe kutoka kwa mashabiki wa Simba na kuipa Simba ushindi wa 4-1 moja kwa moja hadi nusu fainali.
Kapombe baada ya kufunga penalti hiyo alikimbiliwa na wachezaji wenzake na benchi zima la ufundi na kushangilia na mchezaji huyo ambaye alivua jezi na kubaki na fulana ya ndani iliyoandikwa Jesus 100% yaani Yesu asilimia 100.
Dakika 90 zilivyokuwa
Katika dakika 90 za kawaida, Simba waliandika bao lao la kwanza dakika ya 22 mfungaji akiwa Elly Mpanzu wakati bao la pili lilifungwa na Steven Mukwala dakika ya 32.
Simba kama ilivyokuwa katika mechi ya kwanza baina ya timu hizo, kwa mara nyingine ilifanikiwa kuutawala mchezo na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini tatizo lilikuwa katika umaliziaji.
Kwa jinsi hali ya mchezo ilivyokuwa Simba walikuwa na kila sababu ya kumaliza dakika 90 wakiwa washindi kwa zaidi ya mabao matatu na kusingekuwa na sababu ya kuingia kwenye penalti.

Al Masry kama kawaida yao walionekana kuzidiwa na kutumia mara kwa mara mbinu ya kuchelewesha muda kwa kujiangusha na wakati mwingine kuingia katika mzozo na watu wa huduma ya kwanza.
Kutokana na matukio hayo kujitokeza mara kwa mara, haikushangaza mechi kuchezwa kwa dakika 10 za nyongeza baada ya 90 za kawaida kukamilika.
Rais Samia awapongeza
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kupitia mtandao wa X (Twitter) aliipongeza Simba kwa ushindi huo ambao aliutaja kuwa ni burudani kwa Watanzania wote.
“Pongezi za dhati kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ushindi wenu ni furaha kwa mashabiki wenu na burudani kwa Watanzania wote. Ninawatakia kila la kheri katika nusu fainali,” ilijieleza taarifa hiyo ya rais.
Baada ya ushindi huo, Simba sasa inasubiri kucheza mechi ya nusu fainali na mshindi wa mechi kati ya Zamalek ya Misri na Stellenbosch ya Afrika Kusini.

The post Camara shujaa, Simba ikiitoa Al Masry kwa penalti 4-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/10/camara-shujaa-simba-ikiitoa-al-masry-kwa-penalti-4-1/feed/ 0