Simulizi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 10 Nov 2021 13:41:54 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Simulizi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Usaliti wa tatu -1 https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/usaliti-wa-tatu-1/ https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/usaliti-wa-tatu-1/#respond Wed, 10 Nov 2021 13:41:51 +0000 https://greensports.co.tz/?p=364 Na Jonathan Haule Saa tatu usiku, niko chumbani nimejilazachali kwenye godoro, mwili umejaa uchovu uliotokana na kibarua kizito cha kupakia vifaa vya ujenzi kwenye magari makubwa. Niko katika tafakuri ya maisha, kila nikiifikiria kesho yangu naona ugumu ulio mbele huku dalili za kuukimbia umasikini zikiwa mbali, usingizi nao ulianza kuninyemelea lakini ghafla nashtushwa na mtu […]

The post Usaliti wa tatu -1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na Jonathan Haule

Saa tatu usiku, niko chumbani nimejilazachali kwenye godoro, mwili umejaa uchovu uliotokana na kibarua kizito cha kupakia vifaa vya ujenzi kwenye magari makubwa.

Niko katika tafakuri ya maisha, kila nikiifikiria kesho yangu naona ugumu ulio mbele huku dalili za kuukimbia umasikini zikiwa mbali, usingizi nao ulianza kuninyemelea lakini ghafla nashtushwa na mtu aliyegonga mlango.

Bila ajizi nilimwambia ingia ndani mlango uko wazi, wakati anaingia nilimuangalia kuanzia chini, alikuwa amevaa yeboyebo nyekundu, kaptura ya kaki iliyopauka, fulana nyeusi na mkononi ana kimkoba kilichochakaa, mwili wake umejaa vumbi.

“Shikamoo kaka Dennis,” niliitikia huku nikimuangalia usoni na ndipo nilipogundua kwamba alikuwa ni Ntibashimana kutoka nyumbani Kanyigo, nikamwambia karibu kwa mara nyingine huku nikionyesha tabasamu.

Chumbani kwangu sikuwa na kiti wala meza, Ntibashimana akakaa pembeni yangu kwenye godoro nililokuwa nimelalia, baada ya kumjulia hali na kuongea machache kwa dakika kama 15 hivi nilimwambia aende akaoge kwanza.

Nikamwonyesha chooni ambapo ndiyo bafuni hapo hapo, nikamwonyesha madumu ya maji na ndoo ya bafuni, akatia maji kwenye ndoo na kwenda kuoga.

Ntibashimana akiwa bafuni nilianza kutafakari juu ya ujio wake,nilijiuliza, huyu ametoka kijijini ana ujumbe kutoka kwa wazazi wangu? Wazazi wanataka nirudi Kanyigo?Hata hivyo kwa ujio ule nilijiaminisha kwamba siku ile atalala kwangu lakini pia nilijiuliza je atalala siku hii moja tu au ndio kahamia?

Atayachukuliaje maisha ya kulala kwenye godoro bila kitanda? Vipi maisha ya chumba kimoja tena Tandale, mahali hata gari halifiki, nyumba ziko bila mpangilio, si atashangaa maisha ya Dar es Salaam tuliyokuwa tukiisikia na jinsi yalivyo, si atasema afadhali kijijini, lakinipia amepajuaje na amewezaje kufika hadi hapa Tandale?

Nje ya mawazo hayo nilianza kupata mawazo ya kunifariji, nikajiambia afadhali sasa nina chumba ingekuaje angekutana namiwakati ule nikilala kwenye mapagale na mahali popote usiku uliponikutia.

Vipi kama angekuja wakati ule nina chumba lakini nalala chini kabisa kwenye mkeka, si afadhali sasa hivi nina godoro tena la sita kwa sita? Lakini pia naishi kwenye chumba chenye umeme, japo ndani nina taa moja tu.

Nilijiambia kwa kujifariji kwamba kwangu mimi si sawa kabisa na wale vijana wanaosema kila siku afadhali ya jana badala yake kwangu mimi, kila siku ni bora kuliko jana, kuna hatua nimepiga japo ndogo.

Yote hayo pamoja na kunifariji lakini hayakuacha kunirudisha katika ukweli kwamba bado naishi kimasikini, umasikini nilioukimbia Kanyigo ndio ninaoendelea nao hapa Dar es Salaam.

Tofauti pekee ni kwamba hapa Dar es Salaam karibu kila siku naingiza pesa, hali hiyo ndiyo inayonifanya niseme leo ni bora kuliko jana hasa ninapofananisha na hali ya kule kijijini nilipotoka.

Kule kijijini pesa kuishika ni kwa msimu, kitu pekee rahisi ni chakula kuanzia maziwa kwa sababu tunafuga ng’ombe na mbuzi, mayai kwa sababu tunafuga kuku wa kienyeji, mboga kwa sababu tuna shamba na vinginevyo, kwa ujumla chakula hakijawahi kuwa tatizo kijijini.

Ajabu ni kwamba kila nikiifikiria pesa ninayoipata shilingi 7,500 kwa siku bado ukweli kwamba najiona masikini haujanitoka, tena fedha yenyewe naipata baada ya kufanya kazi ngumu kwa Kadianji, mhindi anayeuza vifaa vya ujenzi kwa jumla kwenye karakana yake kubwa maeneo ya Gongo la Mboto.

Siku pekee ya kupumzika ni Jumapili tu lakini kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi, natoka Tandale saa 12 asubuhi hadi Gongo la Mboto na kurudi jioni saa 12 nikiwa na shilingi 7,500 tu mfukoni.

Muda wote huo kuanzia saa 12, nitapakia kwenye malorina kushushamifuko ya saruji, nondo, mabati, mbao na kila atakachotaka mteja, bila kujali wingi wa wateja, wingi wa mizigo au uzito wa mizigo, ujira wa Kadianji kila siku jioni ni shilingi 7,500 ile ile.

Shilingi 7,500 yenyewe ilianza kuishia kwenye usafiri kamashilingi 1,500 hivi kila siku kwenda na kurudi kazini. Chaikwa Kadianji nibure, unakunywa utakavyo lakini kitafunwa ni pesa yako, hivyo kila siku nilitumia shilingi 1,000 kwa vitafunwa.

Mchana pia Kadianji alitupa chakula bure na hivyo nikawa na gharama ya chakula cha jioni tu ambayo ni shilingi 2,000 kila siku kula kwa mama lishekaribu na kwangu Tandale.

Kwa hali hiyo kila siku akiba pekee niliyoiweka ni shilingi 3,000 tu, hii pesa iliweza kufikia wastani wa shilingi 75,000 kwa kila mwezi.

Akiba hii iliweza kuongezeka kwa baadhi ya sikupale tu Kadianji alipokuwa na kazi za Jumapili na kututaka kwenda kazini, siku hiyo ambayo kimsingi ni ya kupumzika kila kibarua alilipwa shilingi 10,000 badala ya shilingi 7,500.

Akiba pia iliongezeka kwa mimi kujiongeza siku moja moja ambazo nilitembea kwa miguu kwenda ofisini na kurudi nyumbani yaani Gongo la Mboto hadi Tandale, kuna siku nilijiongeza wiki nzima kwa kutopanda daladala na kuokoa shilingi 1,500 kwa kila siku.

Ujira wa Kadianji kwa mwezi pamoja na udogo wake lakini kwa kuweka akiba mwezi wa kwanza tu ilitosha kunipa ujasiri wa kutafuta chumba na kulipa kodi ya mwezi shilingi 20,000 na huo ukawa mwanzo wa kuachana na maisha ya kulala nje.

Mbali na kulipa kodi pia nilinunua mkeka, mto na shuka mbili kwa ajili ya kulalia, madumu ya kuhifadhi maji, suruali mbili, kaptura na fulana mbili na hivyo nikahamia kwenye chumba changu walau nikiwa na nguo za kubadili tofauti na maisha ya kulala nje nikiwa na suruali moja,shati na fulana.

Mwezi uliofuata nilinunua godoro, nilitaka godoro dogo la futi nne kwa sita lakini ujasiri wa kihaya ukanishawishi kununua la futi sita kwa sita. Safari hii nikajiona mtu, badala ya mkeka nikawa sasa nalala kwenye godoro tena la sita kwa sita.

Akiba yangu ya mwezi uliofuatanikawakumbuka baba na mama, kila mmoja nikamtumia shilingi 15,000. Wazazi walifurahi sana wakati naongea nao kwa simu ya jirani, kwanza niliwaambia nimepata kibarua kwa mhindi aitwaye Kadianji maeneo ya Gombo la Mboto japo ujira wangu ni mdogo.

Baada ya hapo ndio nikawaambia nawatumia shilingi 15,000 kila mmoja japo nilijua kwamba pesa ya baba, Mzee Byarugaba yote itaishia kwenye pombe ya lubisi.

Hatua iliyofuata baada ya hapo ni kufungua akaunti benki, nikaachana na tabia ya kuweka pesa mfukoni, nikawa kila mwezi napeleka benki wastani wa shilingi 70,000 huku mahitaji mengine ya kawaida kama kununua umeme wa luku, kula na kulipa kodi ya nyumba nikiyamudu bila matatizo.

Siku moja likanijia wazo la kupika mwenyewe, nikanunua jiko dogo la mtungi mdogo wa gesi, nikawa kila siku usiku au siku za Jumapili nisipoenda kazini napika wali au ugali, napika pia mboga au wakati mwingine nanunua dagaa (misumari ya bati) nakula na ugali.

Huo ukawa utaratibu wangu na hadi napata mgeni wa kwanza, Ntibashimana benki nilikuwa na shilingi 250,000 akiba ya miezi minne, si haba nilijifariji nikiangalia nilipotoka japo niliendelea kuutambua ukweli kwamba bado niko kwenye umasikini.

Nilijiambia kwamba kijijini ni vigumu kuwa na fedha kama hizo, pamoja na kupata mahitaji yote ya lazima lakini kijijini pesa ni ngumu, haipatikani.

The post Usaliti wa tatu -1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/usaliti-wa-tatu-1/feed/ 0