Filamu - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 09 Dec 2021 11:18:15 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Filamu - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Eddie Murphy, kutoka Coming to America sasa Coming 2 America https://www.greensports.co.tz/2021/11/15/eddie-murphykutoka-coming-to-america-sasa-coming-2-america/ https://www.greensports.co.tz/2021/11/15/eddie-murphykutoka-coming-to-america-sasa-coming-2-america/#respond Mon, 15 Nov 2021 13:39:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=456 New York, MarekaniComing to America, unaweza kuitaja kuwa ni kazi ya Eddie Murphy ya mwaka 1988 iliyopikwa vizuri na kudhihirisha umahiri wake katika tasnia ya filamu, pengine katika kuuendeleza umahiri huo, Machi mwaka huu, Murphy ameshiriki katika kazi nyingine iliyopewa jina la Coming 2 America.Katika Coming to America, Murphy anaigiza kwa jina la Akeem, akiwa […]

The post Eddie Murphy, kutoka Coming to America sasa Coming 2 America first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Coming to America, unaweza kuitaja kuwa ni kazi ya Eddie Murphy ya mwaka 1988 iliyopikwa vizuri na kudhihirisha umahiri wake katika tasnia ya filamu, pengine katika kuuendeleza umahiri huo, Machi mwaka huu, Murphy ameshiriki katika kazi nyingine iliyopewa jina la Coming 2 America.
Katika Coming to America, Murphy anaigiza kwa jina la Akeem, akiwa mwana mfalme wa nchi tajiri barani Afrika ya Zamunda, nchi inayoongozwa na Mfalme au King Jaffe Joffer. Akeem licha ya kuwa mtoto wa mfalme lakini hafurahishwi na maisha ya kifahari na kufanyiwa kila kitu na wahudumu wa kwenye familia ya kifalme.
Kibaya zaidi baba yake anaamua kumtafutia mchumba na kumfungisha ndoa jambo ambalo Akeem analikataa akidai kuwa angependa kuwa na mwanamke watakayependana na ambaye atampenda si kwa sababu ya hadhi ya kifalme aliyonayo.
Katika kuhakikisha anatimiza ndoto yake hiyo Akeem akiwa na rafiki yake Semmi wanaamua kwenda New York, Marekani lengo kuu la Akeem likiwa ni kutafuta mchumba, kutafuta uhuru na huko anajitambulisha kama mwanafunzi wa kawaida kutoka bara la Afrika badala ya mwana mfalme huku akiishi maisha ya kawaida katika eneo la watu wa kipato cha chini.
Akiwa katika hafla ya kuchangisha fedha, jicho la Akeem linaangukia kwa mrembo Lissa Mcdowell, mrembo ambaye kwa Akeem anaonekana kukidhi viwango alivyokuwa akivihitaji na hapo anaanza hesabu za kumpata.
Katika harakati hizo anaangukia kufanya kazi katika mgahawa unaomilikiwa na Cleo Mcdowell ambaye ni baba yake Lisa, katika harakati hizo kunatokea visa vingi akiwamo baba yake Lisa kutomkubali Akeem kwa kuwa ni mtu wa hadhi ya chini. Hapo hapo Lisa naye anaonekana kuwa na ukaribu na Darryl Jenks, tozi, mtanashati na mwenye kujipenda.
Wakiwa katika hafla moja, Jenks anafanya kosa ambalo linakuwa msaada kwa Akeem kupenyeza rupia kwa Lisa, Jenks anamtambulisha Lisa kwa wazazi wake akitaka familia hizo mbili zipige picha ya pamoja kwa kuwa yeye na Lisa tayari ni wapenzi ingawa hakumuarifu Lisa chochote kuhusu tukio hilo.
Lisa anachukizwa na jambo hilo, na katika hali ya kushangaza baadaye anajitenga katika hafla ile, hapo hapo Akeem anaitumia fursa hiyo kujisogeza huku akimuuliza sababu ya kujitenga huko, baada ya Lisa kumuelezea kila kitu ndipo Akeem naye anapopata nafasi ya kumuelezea kilichomsibu yeye kwamba katika nchi yao kuna tabia ya kuchaguliwa wachumba.
Vituko, visanga na vichekesho ni vingi katika filamu hii lakini mwisho wa siku, Lisa ananasa katika mikono ya Akeem na kufunga naye ndoa ya kifahari yenye hadhi ya kifalme.
Katika Coming 2 America, Akeem akiwa katika kumbukumbu ya miaka 30 ya ndoa yake na Lisa, anaitwa na baba yake ambaye ni mgonjwa anayesubiri kifo, akiwa na kiongozi wa kiroho, Akeem anakumbushwa kwamba akiwa New York, Semmi aliwarubuni wanawake wawili na katika hali ambayo pengine haikutarajiwa, mmoja wa wanawake hao aliangukia katika ‘himaya’ ya Akeem.
Mwisho wa tukio hilo mtoto wa kiume alizaliwa na kwa mila za Zamunda, mtoto wa kiume ndiye anayerithi ufalme, na kwa bahati mbaya Akeem na Lisa wana watoto wa kike tu hivyo kwa Akeem kurudi New York kumtafuta mtoto wake ni jambo lenye umuhimu wa kipekee .
Uamuzi wa Akeem kurudi New York unatokana na ukweli kwamba bila ya hivyo ukoo wa kifalme utahamia katika taifa jingine ambalo dikteta wa taifa hilo, Jenerali Izzi alikuwa akipambana kuhakikisha Idi, mtoto wake wa kiume mpenda matanuzi anamuoa Meeka ambaye ni mtoto wa Akeem jambo ambalo lingesaidia kumfanya awe na nguvu hadi katika ufalme wa Zamunda.
Coming 2 America ni kazi nyingine ya kuvutia ambayo Murphy ameshiriki vizuri, lakini tofauti yake na Coming to America ni kwamba wakati Coming to America inatoka mwaka 1988, Murphy ndio kwanza alikuwa na miaka 28 lakini Coming 2 America ilipotoka Machi mwaka huu alikuwa na miaka 59 na sasa ana miaka 60.
Mpenzi na mkewe, Lisa wakati Coming to America inatoka alikuwa na miaka 25 na wakati inatoka Coming 2 America Lisa alikuwa na miaka 56 na sasa ana miaka 57. Murphy wakati wa Coming to America hakuwa na mtoto hata mmoja lakini sasa ni baba wa watoto 10 na mtoto wake wa mwisho alizaliwa mwaka 2018 hivyo si ajabu akaendelea kuzaa.
Kwa upande wa Lisa, hakuwa na mtoto wakati Coming to America inatoka lakini kwa sasa hadi Coming 2 America inatoka, Lisa ni mama wa mtoto mmoja tu.

The post Eddie Murphy, kutoka Coming to America sasa Coming 2 America first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2021/11/15/eddie-murphykutoka-coming-to-america-sasa-coming-2-america/feed/ 0