Makala - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 22 Jun 2026 14:51:21 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Makala - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Hapa BMT wametufikirisha kimataifa https://www.greensports.co.tz/2026/06/22/hapa-bmt-wametufikirisha-kimataifa/ https://www.greensports.co.tz/2026/06/22/hapa-bmt-wametufikirisha-kimataifa/#respond Sun, 21 Jun 2026 22:03:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14718 Na Hassan KinguBaada ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuipa tuzo klabu ya soka ya Simba, mashabiki wa soka nchini Tanzania waliingia katika mjadala mzito.Mjadala wenyewe ni wa kuipinga BMT kwa kuipa Simba tuzo kwa kigezo gani, kabla ya kujua kigezo, mjadala ulipamba moto kwa mashabiki wa Simba na Yanga kuzodoana vijiweni na mitandaoni.Mashabiki […]

The post Hapa BMT wametufikirisha kimataifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Hassan Kingu
Baada ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuipa tuzo klabu ya soka ya Simba, mashabiki wa soka nchini Tanzania waliingia katika mjadala mzito.
Mjadala wenyewe ni wa kuipinga BMT kwa kuipa Simba tuzo kwa kigezo gani, kabla ya kujua kigezo, mjadala ulipamba moto kwa mashabiki wa Simba na Yanga kuzodoana vijiweni na mitandaoni.
Mashabiki hasa wa Yanga waliamini timu yao ndiyo iliyokuwa na hadhi ya kupewa tuzo kutokana na mafanikio yake nchini Tanzania kuanzia mataji ya ligi kuu kwa misimu takriban minne na michuano mingine.
Kimsingi mjadala huu haukupaswa kuwapo lakini ulikuwapo kwa sababu ni hulka ya mashabiki wa timu hizi mbili hasimu kulumbana huku kila mmoja akiamini timu yake ndiyo bora kuliko mwenzake.
Nasema mjadala huu haukupaswa kuwapo kwa sababu tulikuwa tunabishana na kulumbana kwa jambo ambalo wengi wetu tulikuwa hatulijui na hatukusumbuka kulijua badala yake tuliendelea kusumbuka kwa kubishana na kulumbana.
Hatukuwa tunajua kigezo ambacho BMT ilitumia kuipa Simba tuzo hiyo, lakini tulichofanya ni kujiaminisha kuwa Yanga ni bora kuliko Simba na Simba ambao pia walikuwa hawajui kigezo cha BMT kuipa timu yao tuzo nao walijiaminisha kuwa timu yao ni bora kuliko Yanga.
Mjadala huu ulikufa baada ya BMT kuweka wazi kigezo kwamba wao waliangalia mafanikio ya timu kimataifa, Simba walikuwa hawajui kuhusu kigezo lakini waliitetea timu yao na Yanga walikuwa hawajui lolote kuhusu kigezo nao waliamini timu yao ni bora kuliko Simba.
Kumbe kilichotokea ni kwamba BMT waliwaza kimataifa wakati sisi akili zetu ziliwaza kishabiki tena jijini Dar es Salaam katika wilaya ya Ilala mitaa ya Msimbazi, Kariakoo na Twiga na Jangwani.
Tungejaribu kuwaza kimataifa kama BMT na kuwa na fikra na mitazamo ya kimataifa, mjadala huu au malumbano haya yasingekuwapo lakini hatukuwaza huko badala yake mawazo yetu yalikuwa Tanzania, si nje ya Tanzania.
Kwa maana nyingine BMT wao waliwaza mambo ya Cairo, Misri yalipo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), waliwaza Rabat-Morocco, Lagos-Nigeria, Abidjan-Ivory Coast, Tunis-Tunisia na kwingineko lakini sisi fikra na mitazamo yetu iliishia kuwaza mitaa ya Jangwani na Twiga na Msimbazi na Kariakoo.
Na ndio maana sasa hivi hatusikii tena mjadala na malumbano kuhusu tuzo ya Simba, ni kwa sababu tulijadili na kulumbana tusichokijua, tumeujua ukweli tumeishia kubaki kimya na kuhamishia mijadala na malumbano yetu katika mambo mengine.
Kumalizika kwa malumbano na mjadala huo ni vyema kukawa somo kwa mashabiki wa soka nchini kuwa wadadisi wa mambo kabla ya kuanza kuyajadili tena kujadili kwa kutumia nguvu nyingi katika kushambuliana.
Ndio, kuitetea timu yako si jambo baya lakini lazima ujue unachotetea au kukipinga, je uko sahihi au unatetea na kupinga usichokijua, unatetea au kupinga tuzo ya Simba bila kujua kigezo ambacho kimetumika kutoa tuzo hiyo!

The post Hapa BMT wametufikirisha kimataifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/06/22/hapa-bmt-wametufikirisha-kimataifa/feed/ 0
Viwanja kufungiwa, wamiliki wajitathmini https://www.greensports.co.tz/2026/05/02/viwanja-kufungiwa-wamiliki-wajitathmini/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/02/viwanja-kufungiwa-wamiliki-wajitathmini/#respond Sat, 02 May 2026 12:51:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14583 Na Hassan KinguUbora wa viwanja vya soka ni eneo muhimu ambalo halipaswi kupuuzwa kwa namna yoyote ile hasa ubora huo unapohusisha eneo la kuchezea yaani pitch.Mashabiki na wapenzi wa soka wanaweza kujadili matatizo yaliyo mengi kuhusu viwanja hasa vile vinavyotumiwa kwa mechi za Ligi Kuu NBC na wakayapuuza baadhi lakini watakuwa wa ajabu wakipuuza hoja […]

The post Viwanja kufungiwa, wamiliki wajitathmini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Hassan Kingu
Ubora wa viwanja vya soka ni eneo muhimu ambalo halipaswi kupuuzwa kwa namna yoyote ile hasa ubora huo unapohusisha eneo la kuchezea yaani pitch.
Mashabiki na wapenzi wa soka wanaweza kujadili matatizo yaliyo mengi kuhusu viwanja hasa vile vinavyotumiwa kwa mechi za Ligi Kuu NBC na wakayapuuza baadhi lakini watakuwa wa ajabu wakipuuza hoja ya ubora wa eneo la kuchezea.
Uwanja unaweza kuwa na vyoo vichache au vyoo ambavyo havipo katika ubora, uwanja unaweza kuwa na tatizo la majukwaa, viti kuharibika na kusababisha mashabiki kusimama, huduma ya maji ikawa ya mashaka, yote hayo yakavumiliwa kwa staili ya funika kombe mwanaharamu apite lakini si tatizo la eneo la kuchezea.
Tatizo la eneo la kuchezea madhara yake ni makubwa na yanatosha kuchangia kupoteza maana nzima ya ushindani kwenye soka, timu inaweza kupoteza mechi kimaajabu au kushindwa kupata ushindi.
Uwanja wenye eneo bovu la kuchezea unapoteza maana halisi ya kuwa uwanja wa soka, mamlaka zisikae kimya kwa uwanja wenye mashimo na miinuko ya ajabu ajabu, usio na majani yaani vipara, hatua lazima zichukuliwe.
Kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia mamlaka za mpira zikivifungia baadhi ya viwanja na kuvifungulia baada ya muda mfupi hatua ambayo inakuwa kero kwa mashabiki wa soka na inawakatisha tamaa hasa pale fungia fungia hiyo inapojirudia mara mbili au hata tatu katika msimu mmoja.
Jaribu kumfikiria shabiki ambaye amejipanga kwenda uwanjani kuangalia mechi baina ya timu yake halafu ghafla uwanja unafungiwa kwa sababu haukidhi vigezo ambavyo havibainishwi kwa mapana kwenye taarifa za mamlaka husika.
Kwa shabiki uamuzi huo ni kero na kero inakuwa kubwa zaidi mechi hiyo inapohamishiwa uwanja mwinghine ambao upo mbali tena wakati mwingine katika mkoa ambao kero si tu kwa shabiki bali kwa uongozi na wachezaji.
Uongozi unajikuta katika gharama nyingine mpya zilizoongezeka za kusafirisha timu wakati kwa wachezaji wanaingizwa katika uchovu wa safari ambao hawakuutarajia na hivyo kuathiri viwanja au ubora wao mchezoni.
Tumesikia fungia fungia hii ya viwanja ikijitokeza katika baadhi ya viwanja vikiwamo vya Jamhuri Morogoro na Dodoma, Sokoine Mbeya, Alli Hassan Mwinyi Tabora, Kirumba Mwanza na kwingineko.
Unaposikia uwanja umefungiwa zaidi ya mara mbili unaanza kujiuliza tatizo nini ambalo haliishi na nani hasa mmiliki wa uwanja huo au viwanja hivyo, jibu unalipata kwamba kuna taaisi moja kubwa inaitwa CCM ambayo inajipambanua kwa sera za maendeleo ya michezo.
Ni vyema sasa taasisi hii ijitathmini na ianze kuweka nguvu katika maboresho ya viwanja vyake ili kuendana na sera yake ya maendeleo ya michezo.
Tofauti na hivyo sera hiyo inakuwa haina maana au haitekelezeki kama eneo muhimu katika maendeleo ya michezo yaani uwanja haupewi thamani yake.

The post Viwanja kufungiwa, wamiliki wajitathmini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/02/viwanja-kufungiwa-wamiliki-wajitathmini/feed/ 0
Simba wasiishie kuwananga Mangungu, Matola https://www.greensports.co.tz/2025/12/14/simba-wasiishie-kuwananga-mangungu-matola/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/14/simba-wasiishie-kuwananga-mangungu-matola/#respond Sun, 14 Dec 2025 18:06:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14171 Hassan KinguSimba haipo vizuri, mwenendo wa timu kiujumla hauridhishi, utata ulianza kuonekana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya timu hiyo kupoteza mechi mbili za hatua ya makundi.Kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Azam FC, tena mabao ya jioni ni jambo jingine lililoongeza machungu na hasira za mashabiki ambao msimu uliopita waliishuhudia timu yao ikifikia […]

The post Simba wasiishie kuwananga Mangungu, Matola first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Hassan Kingu
Simba haipo vizuri, mwenendo wa timu kiujumla hauridhishi, utata ulianza kuonekana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya timu hiyo kupoteza mechi mbili za hatua ya makundi.
Kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Azam FC, tena mabao ya jioni ni jambo jingine lililoongeza machungu na hasira za mashabiki ambao msimu uliopita waliishuhudia timu yao ikifikia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Matarajio ya msimu huu yalikuwa juu, yalianza kuzungumzwa wakati wa usajili, imani ikajengeka timu itafanya vizuri kwenye Ligi Kuu NBC na Ligi ya Mabingwa lakini matumaini yanafifia siku hadi siku.
Katika kupambana kuweka mambo sawa, Simba imeanza au inaendelea kumsaka mchawi wake, mchawi wa siku zote alikuwa Murtaza Mangungu, mwenyekiti wa klabu hiyo, na sasa mchawi mwingine ni kocha Suleiman Matola.
Ingekuwa miaka ya nyuma Mangungu angekuwa tayari ameondolewa kupitia mkutano mkuu lakini zama hizi jambo hilo ni ngumu na huenda lisipate baraka za mamlaka.
Kwa hiyo Mangungu amepenya kwenye mkutano mkuu wa hivi karibuni, licha ya kusakamwa na kuwekwa katika hali tete lakini alikuwa makini dhidi ya jaribio lolote la kumuondoa na mwisho wa siku akamaliza mkutano kimtindo.
Kuhusu suala la Mangungu kilichobaki sasa ni mkutano wa uchaguzi, hapo ndipo atakapoondolewa kupitia kura za wanachama, tofauti na hivyo kuondoka kwake kunabaki kuwa jambo gumu.
Walioamini mkutano ungemng’oa Mangungu wamefeli wasubiri kura na kwenye kura ni kama ataamua kukaa kando vinginevyo ni vigumu kutabiri kama atashinda au atashindwa, hilo litategemea mengi ikiwamo aina ya wapinzani atakaokutana nao au mwenyewe kujiweka kando au kuwekwa kando na katiba.
Kuhusu Matola ambaye naye anatajwa na kuhusishwa na mwenendo mbaya wa Simba hasa baada ya timu hiyo kufungwa na Azam yeye ni tofauti na Mangungu, Matola anaweza kuondoka au kuondolewa wakati wowote.


Uamuzi dhidi ya Matola unahusisha watu wachache na ndio maana imekuwa rahisi kusikia watu kwenye mitandao wakimjadili katika namna mbaya na wengine kudiriki kusema kwamba siku zake ndani ya Simba zinahesabika.
Majina haya mawili kwa siku za karibuni yamekuwa yakitajwa sana hasa mitandaoni wakinangwa na kuonekana ndio msingi wa tatizo ndani ya Simba.
Kwa hali ilivyo mitandaoni kama kuna mtu labda ni mgeni na mambo ya soka la Tanzania na hajui kinachoendelea anaweza kujiambia kwamba ni kwa nini watu hao wawili hawaondoki ili Simba iwe bora.
Kwa upande mwingine napata tabu kuamini kuwa Matola na Mangungu pekee ndio tatizo la Simba badala yake naona kuna mambo muhimu kuyafanyia tafakuri na kuyapatia majibu badala ya kuwajadili na kuwasakama watu hao wawili.
Hao watu wawili wanaotajwa msimu uliopita walikuwa Simba iliyofikia fainali Kombe la Shirikisho Afrika huku matumaini yakiwa juu kwamba timu hiyo ilikuwa na uwezo wa kuweka historia kwa kubeba taji hilo.
Kilichotarajiwa ni kwamba Simba iliyofikia fainali Shirikisho Afrika msimu uliopita ingeendeleza mafanikio msimu huu lakini dalili za jambo hilo hazionekani.
Nionavyo kabla ya kuanza na Mangungu au Matola ambao walikuwa na timu hiyo msimu uliopita ni vyema kujiuliza kuhusu usajili, je timu ya msimu uliopita na hii ya sasa ipi bora?
Hili ni swali au hoja ngumu na ya kiufundi ambayo inahitaji tafakuri kabla ya kuijibu na ndio maana wengi hatuitaki badala yake yanatafutwa maswali au hoja rahisi yenye majibu rahisi kama vile Mangungu tatizo na sasa Matola tatizo.
Baada ya kikosi hoja au swali la pili kwangu ni kuhusu kocha, je Simba wana mpango gani katika kupata kocha mwenye hadhi au uwezo unaolingana na ule wa Fadlu Davids ambaye aliifikisha timu hiyo fainali ya Shirikisho Afrika?.
Fadlu si tu aliifikisha timu fainali bali hata aina ya soka lake ilivutia na ni sababu kubwa ya kuwapo matumaini kwamba Simba ya msimu huu ingekuwa moto chini ya kocha huyo lakini hali imekuwa tofauti, Fadlu ameondoka wakati anahitajika.
Kwa mantiki hiyo badala ya Mangungu na Matola, tafakuri au swali ambalo wana Simba wanapaswa kujiuliza na kutafuta majibu iwe katika hayo mambo mawili, kwanza kikosi na pili kuhusu kocha wa hadhi ya Fadlu.
Kinyume na hapo kwangu naona ni sawa na kujiuliza swali rahisi na kujipa jibu rahisi ambalo katu haliwezi kuisaidia timu.

The post Simba wasiishie kuwananga Mangungu, Matola first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/14/simba-wasiishie-kuwananga-mangungu-matola/feed/ 0
Eti tatizo Simba ni Mangungu https://www.greensports.co.tz/2025/07/13/eti-tatizo-simba-ni-mangungu/ https://www.greensports.co.tz/2025/07/13/eti-tatizo-simba-ni-mangungu/#respond Sun, 13 Jul 2025 20:56:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13724 Na Hassan KinguMsimu wa 2024-25 umeisha, naiangalia Simba iliyofikia fainali Kombe la Shirikisho Afrika, ikafungwa na RS Berkane mabao 2-0 na kushindwa kubeba taji la michuano hiyo.Simba hiyo hiyo, iliyoishia nafasi ya pili Ligi Kuu NBC na kufungwa mabao 2-0 na Yanga, mashabiki wanaamini timu yao imefeli na tatizo ni mwenyekiti wao, Murtaza Mangungu.Ndoto na […]

The post Eti tatizo Simba ni Mangungu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na Hassan Kingu
Msimu wa 2024-25 umeisha, naiangalia Simba iliyofikia fainali Kombe la Shirikisho Afrika, ikafungwa na RS Berkane mabao 2-0 na kushindwa kubeba taji la michuano hiyo.
Simba hiyo hiyo, iliyoishia nafasi ya pili Ligi Kuu NBC na kufungwa mabao 2-0 na Yanga, mashabiki wanaamini timu yao imefeli na tatizo ni mwenyekiti wao, Murtaza Mangungu.
Ndoto na matumaini ya Simba kubeba taji hilo ziliyeyuka kama ambavyo ziliyeyuka ndoto za kubeba taji la Ligi Kuu NBC ambalo liliishia mikononi mwa mahasimu wao Yanga.
Kama hiyo haitoshi, mahasimu wao Yanga wakaendelea kuwapa vipigo kwa mara ya tano mfululizo huku wakilibeba taji la ligi hiyo kwa mara ya nne mfululizo.
Simba ambayo imefikia fainali Kombe la Shirikisho Afrika haikuambulia hata taji moja katika msimu wa 2024-25 huku ni kufeli na wenyewe wanaaminishana kwamba aliyewafelisha ni Mangungu.
Nyimbo za hatumtaki Mangungu zimesikika kwenye mitandao ya kijamii na ukizisikiliza nyimbo hizo unaweza kujiaminisha moja kwa moja kuwa Simba haina tatizo jingine isipokuwa Mangungu. Huu ni uwongo wa wazi.
Kwa mtu asiyefahamu kuhusu Mangungu pia anaweza kudhani kwamba Mangungu ndiye kocha wa timu au ndiye ofisa mtendaji mkuu yaani CEO, kumbe sivyo Mangungu ni mwenyekiti wa klabu.
Mara ya mwisho Simba kufikia hatua ya fainali kwenye michuano ya klabu barani Afrika inayoandaliwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ilikuwa mwaka 1993, miaka takriban 31 iliyopita, tulidhani kwamba kufikia hatua hiyo msimu huu ni mafanikio, hapana ni kufeli na sababu ni Mangungu.
Kwa kilichotokea katika Simba msimu huu baadhi yetu tunaamini tatizo si Mangungu bali tatizo ni lile lile, mafanikio ya Yanga na vipigo mara nne mfululizo.
Klabu hizi mbili zina tabia ya kuteswa na mafanikio ya mmoja wao kiasi cha kujinyima hata kufurahia mafanikio mengine ya kihistoria waliyofikia.


Kuhusu Mangungu ni ama wanachama wamejazwa na maadui zake mitazamo ya kuamini kuwa yeye ndiye tatizo, iwe ni kwa kulipwa au kutolipwa au hawajatafakari kwa kina wanachokizungumza kuhusu kiongozi huyo.
Inawezekana kuna watu wenye nguvu ndani ya Simba ambao hawamtaki Mangungu kwa hiyo hatua iliyofikia Simba katika msimu wa 2024-25 inageuzwa kuwa ni kufeli, tena kufeli kubaya na eneo sahihi la kumshughulikia Mangungu ni hilo.
Si vibaya kusema kwamba Simba imefeli hasa kwa kuwa haijapata taji lakini si sahihi kugeuza nongwa kufeli kwa aina ya msimu huu na kuuaminisha umma uamini kwamba tatizo alikuwa ni Mangungu.
Mtazamo wa Simba kufeli unaweza kuzungumziwa katika kukosa mataji, kufungwa na Yanga lakini huu hauwezi kuwa msimu wa hovyo kwa Simba badala yake unaweza kutajwa kuwa ni msimu ambao Simba imeteleza.
Katika kuteleza huko ni vyema kuangalia matatizo kwa mapana yake badala ya kumuangalia Mangungu na kujiaminisha kwamba ndiye tatizo na labda akiondoka mambo yatakuwa salama, huku ni kumpa Mangungu sifa ambazo hana.
Klabu yenye kocha, CEO, bodi na viongozi wengine lukuki wanaohusika moja kwa moja na maendeleo ya timu, hao wote hawana tatizo isipokuwa mwenye tatizo ni Mangungu pekee, bila shaka atakuwa na nguvu ya kipekee na anaogopwa.
Wakati Simba inasonga mbele hatua moja hadi nyingine kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, mashabiki walikuwa wakijivunia na hakuna aliyewahi kusema kwamba Mangungu ana msaada au amechangia kufikisha Simba ilipofikia.
Ni kama vile Mangungu alikuwa anasubiriwa Simba ishindwe, tena bila kujali imeshindwaje na katika hatua ipi ndipo waanze kumshutumu kwamba hatakiwi na ndiye tatizo.
Badala ya kuhangaika na Mangungu pekee, Simba waanze mipango ya kuboresha kikosi, warekebishe mapungufu yaliyowafanya wafike fainali na wasichukue taji la Shirikisho Afrika, wahakikishe wanakuwa na kikosi kipana kama cha Yanga.
Kama kuna kitu Simba wanatakiwa kujifunza kwa Yanga basi ni kuhakikisha wanakuwa na kikosi kipana na cha ushindani.
Baada ya hapo wasichoke, waendelee kujiuliza, baada ya kushika nafasi ya pili kwenye ligi, msimu ujao watawezaje kubeba taji na kama kuifunga Yanga kwao ndio kila kitu pia waweke mkakati huo.
Huyu Mangungu kama kweli wamemchoka na ndiye tatizo basi wasubiri kumtoa kwenye uchaguzi, mambo ya kupinduana kwa sasa hayana nafasi au yamepitwa na wakati.

The post Eti tatizo Simba ni Mangungu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/07/13/eti-tatizo-simba-ni-mangungu/feed/ 0
Ambani ataweza kuirudisha hadhi ya Leopards? https://www.greensports.co.tz/2025/07/13/ambani-ataweza-kuirudisha-hadhi-ya-leopards/ https://www.greensports.co.tz/2025/07/13/ambani-ataweza-kuirudisha-hadhi-ya-leopards/#respond Sun, 13 Jul 2025 20:39:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13714 Na Hassan KinguMshambuliaji wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Kenya, Boniface Ambani (pichani) amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa AFC Leopards, klabu kongwe na maarufu ya soka Kenya na Afrika Mashariki na Kati.Katika uchaguzi uliofanyika Juni 30, 2025, Ambani aliibuka mshindi na kukabidhiwa kiti kilichokuwa kikishikiliwa na Dan Shikanda kwa kupata kura 1,100 na […]

The post Ambani ataweza kuirudisha hadhi ya Leopards? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Hassan Kingu
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Kenya, Boniface Ambani (pichani) amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa AFC Leopards, klabu kongwe na maarufu ya soka Kenya na Afrika Mashariki na Kati.
Katika uchaguzi uliofanyika Juni 30, 2025, Ambani aliibuka mshindi na kukabidhiwa kiti kilichokuwa kikishikiliwa na Dan Shikanda kwa kupata kura 1,100 na kumshinda Vincent Mutokah aliyepata kura 681.
Ukiizungumzia Leopards unaitaja moja ya klabu kongwe nchini Kenya ambayo imekuwa na uhasama wa muda mrefu na Gor Mahia pia ya nchini humo.
Uhasama wa timu hizi mbili kwa Kenya ni sawa na Yanga na Simba kwa Tanzania au Man United na Man City kwa England, uhasama wao kwenye soka ni wa miaka mingi.
Kwa Leopards au Ingwe na Gor Mahia au K’ogalo, uhasama wao katika soka umebatizwa jina la Mashemeji Derby ni kama kwa hapa Tanzania tulivyo na Dar au Kariakoo Derby kwa Simba na Yanga.
Tofauti na hali ya uhasama ilivyo kwa Dar Derby, nchini Kenya kidogo mambo si mazuri kwa Mashemeji Derby kwa upande wa Leopards, hadhi na heshima ya timu hiyo imeshuka kwa muda mrefu sasa.
Ukweli kwamba Leopards ni kati ya timu zenye rekodi ya kuvutia katika Ligi Kuu Kenya kwa kutwaa taji la ligi hiyo mara 12 bado haufuti ukweli mwingine kwamba hadhi na heshima ya timu hiyo imekuwa chini kwa muda mrefu sasa.
Wakati Leopards wakibeba taji hilo mara 12, mahasimu wao Gor rekodi inaonesha wamebeba taji hilo mara 18 lakini kwa Leopards mara ya mwisho kubeba taji hilo ilikuwa mwaka 1998, kipindi ambacho kocha Mtazania, Sunday Kayuni alikuwa akiinoa timu hiyo.
Tangu hapo Leopards imekuwa ikiziangalia Gor na timu nyingine zikibeba taji hilo kuanzia timu za Ulinzi, Tusker, Oserian Fastac, Mathare United, Sofapaka na POlisi FC.
Si hivyo tu, Leopards pia ilifikia hadi hatua ya kushuka daraja hivyo kuzidi kupoteza hadhi yake kwenye soka la Kenya kabla ya kupambana na kurudi kwa mara nyingine.
Katika mazingira kama hayo, Ambani, mchezaji wa zamani wa timu hiyo na ambaye pia amewahi kucheza soka India na Oman, ana kibarua kuhakikisha hadhi na heshima ya Leopards inarudi katika soka la Kenya na Afrika Mashariki na Kati.
Kazi ya kwanza ni kuhakikisha timu hiyo inabeba taji la ligi kuu na kurudi kwenye michuano ya klabu Afrika na si tu kurudi kama mshiriki bali kurudi kama mshindani kama ilivyokuwa enzi za kina JJ Masiga na wenzake.
Kazi mojawapo kubwa inayomsubiri Ambani ni kuhakikisha timu hiyo inapata ufadhili wa nguvu ambao utamuwezesha kusajili wachezaji wa viwango vya juu.
Katika hilo tayari ana mtaji wa mashabiki kwani Leopards ni kati ya timu zenye mashabiki wengi Kenya lakini mtaji wake wa pili ni nguvu ya wanasiasa katika timu hiyo.
Mmoja wa wanasiasa ambaye anafahamika kwa miaka mingi kuwa shabiki kindakindaki wa Leopards ni Waziri Mkuu Kiongozi wa Kenya na kiongozi wa chama cha siasa cha ANC, Musalia Mudavadi.
Kwa Mudavadi, historia yake na Leopards ni ya kipekee kwani inaanzia kwa baba yake Moses Mudavad ambaye pia alikuwa shabiki na mfadhili wa timu hiyo, huu unaweza kuwa mtaji muhimu wa kwanza kwa Ambani.
Wanasiasa wengine ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuiunga mkono timu hiyo ni Alfred Sambu ambaye pia amewahi kuwa kiongozi, Edwin Sifuna, Ken Lusaka na wengineo.
Makundi hayo mawili ya wanasiasa na mashabiki yanaweza kuwa mtaji mzuri kwa Ambani pamoja na uzoefu wake katka kuhakikisha hadhi na heshima ya Leopards Afrika Mashariki na Kati inarudi kama zamani.
Ambani pia amekuwa mchambuzi wa soka kwa hiyo kuchaguliwa kwake kuiongoza Leopards kwake ni fursa muhimu ya kuyafanyia kazi baadhi ya mambo ambayo amekuwa akiyashauri kupitia vyanzo mbalimbali vya habari.

The post Ambani ataweza kuirudisha hadhi ya Leopards? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/07/13/ambani-ataweza-kuirudisha-hadhi-ya-leopards/feed/ 0
Mwamuzi Dar Derby kawaachia somo waamuzi Tanzania https://www.greensports.co.tz/2025/07/13/mwamuzi-dar-derby-kawaachia-somo-waamuzi-tanzania/ https://www.greensports.co.tz/2025/07/13/mwamuzi-dar-derby-kawaachia-somo-waamuzi-tanzania/#respond Sun, 13 Jul 2025 20:20:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13700 Na mwandishi wetuKwa mara ya kwanza mechi ya watani wa jadi katika soka la Tanzania, Simba na Yanga ilichezeshwa na mwamuzi Amin Mohammed Omar kutoka nchini Misri.Katika mechi hiyo iliyopigwa Juni 25, 2025 na Yanga kutoka na ushindi wa mabao 2-0, bila shaka hakukuwa na matukio yaliyoacha maswali au kuzua mijadala kuhusu ubora wa mwamuzi.Ukiachana […]

The post Mwamuzi Dar Derby kawaachia somo waamuzi Tanzania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kwa mara ya kwanza mechi ya watani wa jadi katika soka la Tanzania, Simba na Yanga ilichezeshwa na mwamuzi Amin Mohammed Omar kutoka nchini Misri.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Juni 25, 2025 na Yanga kutoka na ushindi wa mabao 2-0, bila shaka hakukuwa na matukio yaliyoacha maswali au kuzua mijadala kuhusu ubora wa mwamuzi.
Ukiachana na tukio la kipa wa Simba, Mousa Camara kugongana na kiungo wa Yanga, Pacome Zouzoua na kuzaa penalti iliyozaa bao, hakuna tukio jingine lililozua mijadala, mechi ilikwenda vizuri na kwa utulivu wa hali ya juu.
Mjadala wa tukio la Pacome na Camara, kwa Simba wanaamini haikuwa penalti kwa kuwa kipa aliruka kuufuata mpira wakati Yanga wanaamini ilikuwa penalti kutokana na mgongano uliochangiwa kwa kiasi kikubwa na mruko wa kipa.
Nje ya tukio hilo, mwenendo wa mchezo na jinsi mwamuzi alivyokuwa uwanjani kila eneo na kufuatilia kwa umakini ni kati ya mambo ambayo yameacha somo kwa waamuzi wa Tanzania.
Ukiachana na umakini huo, mwamuzi huyo pia alituonesha namna mwamuzi anavyotakiwa kuutawala mchezo kwa kutokubali kuchezewa au kujaribiwa na wachezaji pale anapoamini kwamba amefanya uamuzi sahihi.
Mfano hakukubali mchezaji kuonesha kwa ishara ya kutoridhika na maamuzi anayoyachukua kwa kujifanya ameonewa au kufanya tukio lolote baada ya filimbi kupulizwa.
Mifano ya hiyo ilijionesha kwa Kibu Denis wa Simba pale mwamuzi alipopuliza filimbi kuashiria mpira umetoka na urushwe kuelekea lango la Simba.
Kibu pengine kwa kutaka kumjaribu, akaonesha kuchukizwa na maamuzi hayo kwa kuudunda mpira chini kwa hasira ili ionekane kama Simba ndio waliotakiwa kurusha mpira huo kuelekea kwa Yanga.
Mwamuzi alimfuata kwa karibu Kibu huku akionekana mwenye hasira na kumuonya kwa ishara ya kukataa kujaribiwa.
Tukio kama hilo pia lilitokea kwa Duke Abuya wa Yanga aliyeanguka chini kama vile aliyechezewa rafu mbaya na kutaka kumshawishi mwamuzi apulize filimbi lakini mwamuzi huyo alimtolea macho na kumpa ishara ya kutotaka kujaribiwa.
Tukio kama hilo linanikumbusa kisa alichowahi kusimulia mchezaji wa zamani wa timu ya Liverpool ya England, Steven Gerard wakati akimsifia mwamuzi Pierluigi Collina wa Italia kwa umakini.
Katika moja ya mechi, Steven Gerard akiwa nahodha Liverpool alijaribu kwa uwongo kujifanya kaumizwa ili kumshawishi mwamuzi apulize filimbi kuibeba timu yake lakini mwamuzi huyo alibaini tukio hilo na kumtolea macho ya ukali huku akimwambia ‘stop fuck around with me’ (acha kuniletea mzaha, au acha kunijaribu).
Kitu hicho pia ndicho nilichokiona kwa Amin Mohammed Omar, hakuruhusu wachezaji wafanye mzaha na kazi yake au wamjaribu.
Clement Mzize wa Yanga aliubutua mpira nje wakati mwamuzi alishapuliza filimbi, Shadrack Boka naye hivyo hivyo alipiga mpira kwa lengo la kufunga goli baada ya mwamuzi kupuliza filimbi kuashiria kuotea.
Katika matukio yote hayo mawili, Amin Mohammed Omar alionesha jinsi asivyotaka masihara kazini, wote akawaonya kwa ishara ya ukali.
Kuyasimamia matukio hayo kama alivyofanya Amin Mohammed Omar ni sababu tosha inayosaidia kulinda hadhi na heshima ya mwamuzi kwa kutokubali kuchezewa, hiyo ni mbali na umakini ambalo ni jambo la lazima kwa mwamuzi yeyote.
Kwa hiyo ni vyema kwa waamuzi wetu mbali na somo la umakini lakini wawapo uwanjani wasikubali kuchezewa au kujaribiwa na wachezaji.

The post Mwamuzi Dar Derby kawaachia somo waamuzi Tanzania first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/07/13/mwamuzi-dar-derby-kawaachia-somo-waamuzi-tanzania/feed/ 0
Kwa nini Fabrice Ngoma? https://www.greensports.co.tz/2025/06/29/kwa-nini-fabrice-ngoma/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/29/kwa-nini-fabrice-ngoma/#respond Sun, 29 Jun 2025 17:51:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13685 Na mwandishi wetuKlabu ya Simba imeachana na kiungo Fabrice Ngoma na hivyo mchezaji huyo hatokuwa na timu hiyo kwenye Ligi Kuu NBC na michuano ya kimataifa kwa msimu ujao wa 2025-26.Kuachwa kwa mchezaji huyo kumewekwa wazi kupitia vyanzo mbalimbali vya habari nchini Tanzania mojawapo ikiwa ni kauli ya mchezaji huyo kuwaaga mashabiki wa timu hiyo.Inaelezwa […]

The post Kwa nini Fabrice Ngoma? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Simba imeachana na kiungo Fabrice Ngoma na hivyo mchezaji huyo hatokuwa na timu hiyo kwenye Ligi Kuu NBC na michuano ya kimataifa kwa msimu ujao wa 2025-26.
Kuachwa kwa mchezaji huyo kumewekwa wazi kupitia vyanzo mbalimbali vya habari nchini Tanzania mojawapo ikiwa ni kauli ya mchezaji huyo kuwaaga mashabiki wa timu hiyo.
Inaelezwa kuwa mkataba wake umefikia ukomo na uongozi hauna nia ya kumuongezea mkataba mpya lakini hadi sasa haijaelezwa wazi ni kwa nini Simba imeachana na nyota huyo kutoka DR Congo.
Uwajibikaji wake katika timu ni kati ya mambo yasiyotia shaka, uwezo wake pia unatosha kumfanya aendelee kuwa na Simba kwa lengo la kuipa mafanikio zaidi timu hiyo katika msimu mpya.
Msimu wa 2024-25, Simba imeishia nafasi ya pili Ligi Kuu NBC lakini imeweka rekodi ya kipekee kwa kufika hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika, michuano ya klabu inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Mara ya mwisho Simba kufikia hatua ya fainali ya michuano ya klabu inayoandaliwa na CAF ilikuwa mwaka 1993, wakati mwaka huu ilishindwa kutamba mbele ya RS Berkane ya Morocco, mwaka 1993 Simba ilishindwa kutamba mbele ya Stellah ya Ivory Coast.
Kutowekwa wazi kwa sababu hasa za kuachwa kwa Ngoma imekuwa chanzo cha mawazo yasiyo rasmi kuibuka kutoka kwa wadau wa soka nchini wakiwamo mashabiki wa Simba na hata mahasimu wao Yanga.
Wapo wanaolalamikia hatua hiyo wakidai kwamba si sahini kwa kuwa Ngoma alihitajika kuendeleza mafanikio ya Simba kwa kpiga hatua zaidi ya walipoishia msimu wa 2024-25.
Hapo hapo kuna ambao tayari wanamhusisha mchezaji huyo na matukio ya kudai posho katika namna isiyo sahihi, wengine wanamhusisha na mzozo wake na kipa Mousa Camara katika moja ya mechi za Simba na je amepata ulaji sehemu nyingine? yote haya ni mambo yanayojadiliwa.
Mwisho wa yote uongozi wa Simba kwa msaada wa benchi la ufundi ndio wanaojua sababu hasa ya kufikia uamuzi huo, kwa sasa tumtakie kila la kheri Ngoma huko aendako.

The post Kwa nini Fabrice Ngoma? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/29/kwa-nini-fabrice-ngoma/feed/ 0
Je ni kweli soka linaongozwa na wajinga wajinga? https://www.greensports.co.tz/2025/06/12/je-ni-kweli-soka-linaongozwa-na-wajinga-wajinga/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/12/je-ni-kweli-soka-linaongozwa-na-wajinga-wajinga/#respond Thu, 12 Jun 2025 09:22:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13595 Na Hassan KinguNimeikumbuka kauli ya kocha na beki wa zamani wa Mtibwa Sugar na timu ya taifa ya Tanzania au Taifa Stars, Mecky Maxime aliposema soka linaongozwa na wajinga wajinga.Awali nilimpuuza lakini sasa nafikiria mara mbili mbili na kujiuliza kama nilikuwa sahihi kumpuuza au nilihitaji kutafakari kwa kina kuhusu kauli ile?Kwa kinachoendelea katika soka letu […]

The post Je ni kweli soka linaongozwa na wajinga wajinga? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na Hassan Kingu
Nimeikumbuka kauli ya kocha na beki wa zamani wa Mtibwa Sugar na timu ya taifa ya Tanzania au Taifa Stars, Mecky Maxime aliposema soka linaongozwa na wajinga wajinga.
Awali nilimpuuza lakini sasa nafikiria mara mbili mbili na kujiuliza kama nilikuwa sahihi kumpuuza au nilihitaji kutafakari kwa kina kuhusu kauli ile?
Kwa kinachoendelea katika soka letu nabaki najiuliza zaidi, je kwa kauli ile Maxime alikuwa sahihi au aliitoa tu katika mazingira ya hasira kutokana na mambo yanayowakuta makocha Tanzania?
Kinachoendelea baina ya Yanga, TFF na Simba kinanifanya nizidi kufikiri na kutafakari kwa mapana kama Maxime alikuwa sahihi au la?
Nikianzia Machi 8 mwaka huu, naliangalia tukio siku moja kabla kwa timu ya Simba kuzuiwa kuingia uwanjani kufanya mazoezi kabla ya mechi yao na Yanga, mazoezi ambayo ni utaratibu ulio rasmi na unatambulika hata na sisi tusio viongozi, nazidi kutafakari kwamba je tukio hili nalo si sehemu ya ule ujinga ujinga uliosemwa na Maxime?
Baada ya hapo hisia zinanipeleka katika tukio la kuahirishwa mechi yenyewe, tena kuahirishwa siku ya mechi, saa kadhaa kabla ya mechi, je hili nalo ni sehemu ya ule ujinga ujinga uliozungumzwa na Maxime au la?
Baada ya hapo najiuliza kuhusu tukio la kugomea mechi, nautafuta uharamu na uhalali wake, nakosa jibu lakini sichoki kutafakari na kujifikirisha mwisho wa yote nabaki najiuliza kama huu nao ni sehemu ya ule ujinga ujinga au la?
Sakata la kuahirishwa kwa mechi ya Yanga na Simba na kupangiwa tarehe nyingine yaani Juni 15 limeibua mgomo, huyu anataka mechi huyu hataki, natafakari vijembe na malumbano yanayoendelea hasa mitandaoni na swali langu linabaki lile lile je huu nao ni sehemu ya ujinga ujinga ulioanzia kwa viongozi?
Nawataja viongozi kwa sababu yote haya yanayoendelea yametokana na viongozi, watu ambao wamepewa dhamana ya kuongoza soka letu, mchezo unaopendwa na wengi lakini bahati mbaya sana Maxime amenifikirisha kwamba wengi wao ni wajinga wajinga na mwisho wa yote nabaki na swali lile lile, je ni kweli soka linaongozwa na wajinga wajinga?
Hadi sasa mashabiki wa soka wapo njia panda, mechi kubwa ya Yanga na Simba haijulikani kama ipo au haipo, je ni kweli kwamba mashabiki wamewekwa njia panda kwa sababu viongozi wenye dhamana ni wajinga wajinga?
Si katika sakata hili la mechi ya Yanga na Simba bali yapo mambo mengi ya kwenye soka letu yananifikirisha kuhusu suala zima la ujinga ujinga, kuanzia kwa maamuzi ya matukio mbalimbali yanayojitokeza, waamuzi na uchezeshaji wao, vyote hivi nikivichambua swali la ujinga ujinga linanijia.
Natafakari kuhusu usajili, mchezaji anasajiliwa kutoka nje ya nchi tena kwa bei mbaya lakini akiingia uwanjani huoni utofauti anaoleta katika timu, hapo hapo najiuliza kwamba mchezaji huyu si zao la kiongozi mmoja mjinga mjinga aliyemsema Maxime?
Dhana ya wajinga wajinga hainitoki kila ninapojaribu kuachana nayo, namuangalia tena mchezaji huyu huyu aliyesajiliwa kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kwa bei mbaya lakini hana ubora na mwishowe anaishia kusugua benchi.
Mchezaji huyu anasaini mkataba ulio rasmi na unaotambulika kisheria halafu anaachwa kienyeji, anakwenda kulalamika kwenye mamlaka husika analipwa fedha nyingi na klabu, je huo nao si ule ujinga ujinga wa kiongozi mmoja mjinga mjinga aliyemzungumzia Maxime?
Sijachoka kuwaza kuhusu ujinga ujinga aliousema Maxime kwani hata hili sakata la pesa lililobuka hivi majuzi nalo kila nikilitafakari swali la ujinga ujinga au viongozi wajinga wajinga linanijia.
Nimefikia hitimisho la kuja na dhana kwamba huenda kuna wajinga wajinga wanaodhani kila mtu ni mjinga mjinga kiasi kwamba hata masuala ya pesa nayo yanaibua mjadala unaotoa kila dalili za kupelekana kwenye ujinga ujinga.
Imefikia hatua tunataka kudanganyana kwamba namba nazo zinaweza kuongopa kwamba 50 isomeke 70 na 70 isomeke 50, hili haliwezekani lakini kwa nini limeibuka, na je si kweli kwamba kuna ujinga ujinga mahali?
Kajisemea Bob Marley katika moja ya nyimbo zake ‘You can fool some people sometime but you cant fool all the people all the time’ yaani unaweza kuwadanganya/kuwapumbaza watu fulani kwa wakati fulani lakini huwezi kuwapumbaza/kuwadanganya watu wote kwa wakati wote.’
Huenda sakata linaloendelea sasa ni ishara kwamba tunakaribia kuelewana kwamba mwisho wa wajinga wajinga unakaribia.

The post Je ni kweli soka linaongozwa na wajinga wajinga? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/12/je-ni-kweli-soka-linaongozwa-na-wajinga-wajinga/feed/ 0
Bao la mkono katikati ya mjadala wa penalti https://www.greensports.co.tz/2024/12/29/bao-la-mkono-katikati-ya-mjadala-wa-penalti/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/29/bao-la-mkono-katikati-ya-mjadala-wa-penalti/#respond Sun, 29 Dec 2024 10:36:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12531 Na Hassan KinguKama ambavyo mashabiki England wanalikumbuka bao la mkono alilowafunga Diego Maradona kwenye fainali za Kombe la Dunia 1986 ndivyo Ibrahim Bacca atakavyoendelea kukumbukwa kwa kufunga bao la mkono katika mechi dhidi ya Tanzania Prisons.Maradona mwenyewe alisema ule ulikuwa mkono wa ‘mungu’ na hadi anafariki dunia baadhi ya mashabiki England walimkumbuka kwa bao hilo […]

The post Bao la mkono katikati ya mjadala wa penalti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Hassan Kingu
Kama ambavyo mashabiki England wanalikumbuka bao la mkono alilowafunga Diego Maradona kwenye fainali za Kombe la Dunia 1986 ndivyo Ibrahim Bacca atakavyoendelea kukumbukwa kwa kufunga bao la mkono katika mechi dhidi ya Tanzania Prisons.
Maradona mwenyewe alisema ule ulikuwa mkono wa ‘mungu’ na hadi anafariki dunia baadhi ya mashabiki England walimkumbuka kwa bao hilo haramu na wengine kusema kwamba amerudi kwenye mkono wa ‘mungu’ (back to the hand of god).
Katika fainali hizo za Kombe la Dunia zilizofanyika Mexico, Argentina walibeba kombe na baada ya hapo hadithi ya bao la mkono iliendelea kwa mashabiki England wakimuona Maradona kama mwanamichezo aliyeikosea heshima soka.
Mabao yote haramu, la Maradona haramu kama ilivyo la Bacca, kesho Yanga ikitwaa ubingwa kwa faida ya bao moja tutaipongeza kwa ubingwa lakini hapo hapo tutasema kuwa walibebwa na bao haramu.
Ni hivyo hivyo wakiwa wameshika nafasi ya pili na kukawa na uwakilishi kwenye michuano ya kimataifa, ikitokea wakawa na faida ya bao moja, tutasema bao haramu limeibeba Yanga.
Kukiwa na ushindani wa tuzo ya mfungaji bora ikatokea Bacca akapambana na kupata mabao kumzidi mpinzani wake kwa tofauti ya bao moja, pia tutasema bao haramu lambeba Bacca hadi kuwa mfungaji bora.
Yanga katika mechi hiyo iliwafunga Prisons 4-0, ushindi huu umesaidia kufifisha mjadala kwa kuwa hata ukiliondoa bao haramu bado Yanga imevuna pointi tatu muhimu na mabao 3-0.
Uharamu wa bao la Bacca hata hivyo upo wazi, haukwepeki hata kidogo licha ya ushindi mnono wa Yanga na Bacca kama mwanamichezo huenda anasikitika kwa kufunga bao haramu.
Ni kama ilivyokuwa kwa mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Barcelona na timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry Henry, huyu mwaka 2009 katika mechi dhidi ya Jamhuri ya Ireland alitumia mkono kuusogeza mpira uliozaa bao na kuiwezesha Ufaransa kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2010.
Henry licha ya bao lake kuwa muhimu bado lilimtesa, alionekana akiwafariji wachezaji wa Jamhuri ya Ireland, kwa kauli yake alikuwa na nia ya kustaafu timu ya taifa kutokana na tukio hilo, alijiona ameukosea heshima mpira na huenda Bacca naye ni hivyo hivyo.
Kwenye mitandao ya kijami kumekuwa na picha inayomuonesha Lionel Messi naye akifunga bao kwa mkono kama kutetea bao la Bacca, hoja dhaifu, kosa la kwanza halihalalishi kosa la pili, yote hayo ni mabao haramu kwenye soka. Nini Messi hata Maradona naye alifunga bao haramu.
Mashabiki wanaweza wakalumbana wawezavyo asubuhi hadi jioni lakini hawawezi au watakuwa vichaa kusema bao la Bacca alilofunga kwa mkono si haramu eti kwa sababu tu Messi naye alifanya hivyo.
Uhalali/uharamu wa penalti ya Simba
Katika mjadala wa bao haramu la Bacca pia kumekuwa na mjadala mwingine kuhusu penalti iliyoipa Simba bao pekee dhidi ya JKT Tanzania, bao lililofungwa na Jean Ahoua.


Penalti hiyo ilitolewa na mwamuzi Keifa Kayombo baada ya beki wa JKT, Mohammed Bakar kumshika beki wa Simba, Shomary Kapombe aliyekuwa akiuwahi mpira ulioelekezwa lango la JKT.
Kabla ya kujadili uhalali au uharamu wa penalti ile, tutajaribu kufikiri ingekuwaje kama mwamuzi huyo asingepuliza filimbi. Bila shaka angeonekana mwamuzi wa ajabu na asiyejua sheria ndogo na ya kawaida katika soka.
Kuna hoja ambayo imeibuka, hoja yenyewe ni kukiri kwamba kosa lilifanyika lakini Kapombe alijipeleka chini kumshawishi mwamuzi kwamba alifanyiwa dhambi lakini alikuza tukio, dhambi ndogo aliifanya kubwa.
Hili linaweza kuwa jambo la kweli lakini ni vipi mwamuzi angeweza kung’amua kwamba Kapombe alikuza tukio la kushikwa na beki kwamba Kapombe angeweza kuweweseka na si kuanguka kama ilivyotokea.
Kimsingi tukio au kosa la Kapombe kushikwa lilifanyika na sote tuliliona na mwamuzi alitakiwa kupuliza filimbi, asingepuliza tungemshangaa, sasa kashikwa kiasi gani na ni kwa nini hakuweweseka badala yake akaanguka, hilo ni suala jingine gumu.
Kibinadamu kuna baadhi ya mambo ni magumu mno kuyang’amua na hivyo la msingi ni kwa wachezaji hasa mabeki kuwa makini na makosa wanayoyafanya hasa kwenye maeneo ya hatari.
Nasema hivyo kwa sababu washambuliaji walio wengi unapomchezea rafu katika eneo hilo anajitahidi kulikuza kwa kumshawishi mwamuzi na mwamuzi si malaika kujua ukubwa wa tukio na uimara wa mfanyiwa tukio kama linaweza kumuangusha au la.
Kapombe huyu huyu naamini angekuwa ameshikwa na kibaka asingeanguka, angekimbia au angekuwa anakimbilia dhahabu yeye na beki wa JKT, pia asingeanguka angeongeza kasi kuiwahi dhahabu.
Ni hivyo hivyo kwa washambuliaji walio wengi ukimgusa kidogo tu eneo la penalti anatumia kosa hilo kupata faida ya penalti na mwamuzi hawezi kuona tukio la beki kumkwatua mshambuliaji akaliacha.
Washambuliaji wengi inaweza kuwa zaidi ya asilimia 90 wanapokwatuliwa kidogo kwenye eneo la penalti hata kama ni tukio la kumfanya ayumbe kidogo na kuendelea kuuwahi mpira hawafanyi hivyo.
Kwa mshambuliaji tukio hilo kwake hulifanya kuwa faida na mwamuzi akijiridhisha mchezaji kakwatuliwa suala la ukubwa wa ukwatuaji ni gumu kulipima, anachoweza kufanya ni kupuliza filimbi kwa sababu kosa limefanyika.
Mpira unapokuwa kwenye kasi kuna makosa ambayo mchezaji hasa mabeki huyafanya bila kujijua, kama vile kumshika mchezaji na ndio maana baadhi yao hujirudi hapo hapo na kuonesha ishara ya mikono kuwa mbali.
Lengo la kufanya hivyo ni kumshawishi mwamuzi asiwaadhibu lakini wakati huo tayari mfanyiwa kosa ameshakwenda chini na mwamuzi ameshaona na kuchukua hatua, na hatua hutegemea na eneo husika la tukio.
Katika mazingira ya matukio ya aina hii tutajadili na kujadili kadri yatakavyokuwa yakitokea lakini mwishowe tutakubali kwamba dhambi imefanyika na ukubwa wa dhambi ataachiwa mwamuzi aamue.

The post Bao la mkono katikati ya mjadala wa penalti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/29/bao-la-mkono-katikati-ya-mjadala-wa-penalti/feed/ 0
Real Madrid hii yenye Mbappe, Vinicius Jr, Bellingham https://www.greensports.co.tz/2024/07/19/real-madrid-hii-yenye-mbappe-vinicius-jr-bellingham/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/19/real-madrid-hii-yenye-mbappe-vinicius-jr-bellingham/#respond Fri, 19 Jul 2024 11:21:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11637 Madrid, HispaniaJulai 16, 2024, Real Madrid inamtambulisha rasmi mshambuliaji wake mpya, Kylian Mbappe ambaye anaongeza nguvu mpya na ya kipekee katika kikosi cha timu hiyo kwenye safu ya ushambuliajiSafu ya ushambuliaji ya Real Madrid yenye Jude Bellingham na Vinicius Junior tayari imeonesha kiwango cha juu msimu uliopita wa 2023-24 hadi kubeba taji la La Liga […]

The post Real Madrid hii yenye Mbappe, Vinicius Jr, Bellingham first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Julai 16, 2024, Real Madrid inamtambulisha rasmi mshambuliaji wake mpya, Kylian Mbappe ambaye anaongeza nguvu mpya na ya kipekee katika kikosi cha timu hiyo kwenye safu ya ushambuliaji
Safu ya ushambuliaji ya Real Madrid yenye Jude Bellingham na Vinicius Junior tayari imeonesha kiwango cha juu msimu uliopita wa 2023-24 hadi kubeba taji la La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa sasa safu hiyo imeongezewa nguvu kwa usajili wa Mbappe, mshambuliaji tishio duniani ambaye amethibitisha hilo kwenye kikosi cha PSG na timu ya taifa ya Ufaransa.
Mbio za Real Madrid kuisaka saini ya Mbappe ni za muda mrefu ingawa bila Mbappe timu hiyo imeendelea kuwa tishio na hapo unaweza kujiuliza itakuwaje timu hiyo ikiwa na Mbappe.
Itakuwaje timu hiyo ikiwa na mshambuliaji anayeshika rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika klabu ya PSG na ambaye kukosekana kwake kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Ufaransa kuliibua sintofahamu wakati wa fainali za Euro 2024.
Juhudi za kuinasa saini ya Mbappe ziliposhindwa kuzaa matunda kabla ya msimu wa 2023-24, kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti alisema kwamba timu yake ilikuwa imekamilika bila ya Mbappe.
Kwa Ancelloti kilichoonekana ni kwamba Mbappe hakuwa mchezaji wa kumsumbua kichwa na akalithibitisha hilo kwa kuiwezesha Real Madrid kubeba taji la La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kauli ya Ancelloti kutoonekana mwenye kusumbuliwa na usajili wa Mbappe pia ilitoa dalili kwamba huenda mchezaji huyo asingesajiliwa Real Madrid kwa kuwa kocha aliamini maisha bila ya mchezaji huyo yanawezekana.
Ukimuweka kando Mbappe, Real Madrid ina watu wengine hatari katika safu hiyo kuanzia kwa Vinicius, Bellingham lakini hapo hapo yupo mshambuliaji wa Kibrazil, Endrick anayesubiriwa kukamilisha usajili.


Orodha hiyo pia ina Arda Guller ambaye ameonesha umahiri wake akiwa na timu ya taifa ya Uturuki kwenye fainali za Euro 2024 naye huenda akapata nafasi ya ndani ya kikosi cha Real Madrid.
Hapo hapo ikumbukwe kwamba Rodrygo naye ni mchezaji mwingine ambaye tayari ameonesha uwezo na bila shaka ana nafasi yake zaidi kwenye kikosi cha timu hiyo katika msimu wa 2024-25 pengine kuliko ilivyokuwa katika msimu ulioisha wa 2023-24.
Kwa wanaojua utamaduni wa Real Madrid, ujio wa Mbappe na mastaa wengine hauwashangazi, ni mwendelezo wa mfumo wa klabu hiyo kusajili wachezaji mastaa wakubwa wa bei mbaya au madogo wenye vipaji vya juu.
Ilikuwa hivyo tangu zama za kina Zinedine Zidane, Luis Figo, David Beckham, Ronaldo de Lima, Roberto Carlos, Kaka, Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na sasa Bellingham, Vinicius Jr na hatimaye Mbappe huku Erling Haaland naye akisubiriwa.
Kwa haraka haraka unaweza kusema kwamba Real Madrid hii yenye Mbappe, Bellingham, Vinicius Jr na wengineo itashinda kila taji lililo mbele yake lakini ukweli wa mchezo wa soka hauko hivyo.
Kutafuta mfumo wa kuwatumia wachezaji hao ni jambo la kwanza gumu ambalo linaweza kumpa tabu Ancelotti kwani kuna wachezaji ambao panga pangua ni lazima wapangwe kwenye kikosi cha kwanza, ikitokea hawajapangwa kunakuwa na tatizo la ndani na wakati mwingine hata nje ya uwanja.
Kazi ngumu nyingine ngumu kwa Ancelotti ni kuwaongoza mastaa hao wa bei mbaya na kutowapa nafasi ya kumpanda kichwani na wachezaji hao kumpa hadhi na nafasi yake ya ukocha, tofauti na hivyo atajikuta pagumu.
Kazi hii ya kuwasimamia mastaa wa bei mbaya ilimshinda Jose Antonio Camacho akiwa kocha wa Real Madrid yenye Zidane, Beckham, Roberto Carlos, Ronaldo de Lima na wengineo, aliamua kujiuzulu na kueleza wazi kuwa ameshindwa kuwaongoza mastaa hao wa bei mbaya.
Tusishangae katikati ya safari ya Real Madrid hii badala ya mataji likatokea jambo kama hilo kwa Ancelotti naye akajikuta akilazimika kujiuzulu.
Sambamba na hilo pia tushishangae katikati ya safari hii tukasikia, Florentino Perez, rais wa Real Madrid amechukua uamuzi mgumu wa kumfuta kazi Ancelotti baada ya kuona mambo yanakwenda kinyume na matarajio yake.

The post Real Madrid hii yenye Mbappe, Vinicius Jr, Bellingham first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/19/real-madrid-hii-yenye-mbappe-vinicius-jr-bellingham/feed/ 0