Mahusiano - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 01 Apr 2025 19:33:36 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mahusiano - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Dani Alves afutiwa kesi ya kubaka https://www.greensports.co.tz/2025/03/29/dani-alves-afutiwa-kesi-ya-kubaka/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/29/dani-alves-afutiwa-kesi-ya-kubaka/#respond Sat, 29 Mar 2025 18:53:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13167 Barcelona, HispaniaBeki wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Dani Alves amefutiwa kesi ya kubaka katika mahakama ya rufaa nchini Hispania.Katika uamuzi huo uliofikiwa Ijumaa hii, mahakama hiyo ya Catalonia imedai kwamba kesi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41, ni yenye mashaka na mambo yenye utata.Februari mwaka jana Alves alihukumiwa […]

The post Dani Alves afutiwa kesi ya kubaka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Beki wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Dani Alves amefutiwa kesi ya kubaka katika mahakama ya rufaa nchini Hispania.
Katika uamuzi huo uliofikiwa Ijumaa hii, mahakama hiyo ya Catalonia imedai kwamba kesi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41, ni yenye mashaka na mambo yenye utata.
Februari mwaka jana Alves alihukumiwa kifungo cha jela miaka minne na nusu baada ya kukutwa na hatia ya kumdhalilisha kijinsia mwanamke mmoja tukio alilodaiwa kulifanya mwaka 2022 katika klabu moja ya usiku mjini Barcelona.
Alves ambaye wakati akicheza soka la ushindani aliichezea timu ya taifa ya Brazil mara 126 aliachiwa kwa dhamana Machi mwaka jana wakati rufaa yake ikisikilizwa.
Katika uamuzi wa kumfutia mashitaka mchezaji huyo mahakama ya rufaa ilieleza kuwa hukumu ya awali katika kesi hiyo ilikuwa na mapungufu, haikuwa na ukweli, utata na yenye mashaka kuhusu tukio zima na matokeo yake.
Mahakama ilifafanua kuwa hoja za mlalamikaji zilitakiwa zichunguzwe kwa kina lakini hazikuwa na ushahidi wa ‘fingerprint’ na ushahidi wa kibaiolojia ambao ungeweza kuzipa nguvu.
Sambamba na hilo mahakama ilifafanua kuwa hoja ya mlalamikaji kwamba alilazimika kwenda bafuni na Alves kwa hofu kwamba marafiki wa Alves wangeweza kumfuata hazina mashiko.
Zaidi ya hilo mahakama hiyo pia ilifafanua kwamba kilichoonekana ni kwamba mlalamikaji aliamua kwa hiyari yake kwenda bafuni kwa lengo la kuwa karibu na mshtakiwa ili kupata nafasi ya kwenda ‘kujirusha naye’.
Mahakama pia ilimfutia Alves zuio alilowekewa likiwamo la kusafiri na makatazo mengine ingawa uamuzi huo bado unaweza kukatiwa rufaa katika mahakama ya juu zaidi.
Wakati wote wa sakata hilo, Alves ambaye ilidaiwa siku aliyodaiwa kufanya tukio hilo alikuwa amelewa, amekuwa akisisitiza kwamba hajafanya kosa lolote na kama kuna jambo alilomfanyia mlalamikaji basi ilikuwa kwa makubaliano.

The post Dani Alves afutiwa kesi ya kubaka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/29/dani-alves-afutiwa-kesi-ya-kubaka/feed/ 0
Wataka kesi ya aliyembusu mchezaji mdomoni isikilizwe upya https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/wataka-kesi-ya-aliyembusu-mchezaji-mdomoni-isikilizwe-upya/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/wataka-kesi-ya-aliyembusu-mchezaji-mdomoni-isikilizwe-upya/#respond Sat, 08 Mar 2025 12:36:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13099 Madrid, HispaniaOfisi ya waendesha mashtaka wa Hispania imetaka kesi ya rais wa zamani wa shirikisho la soka Hispania, Luis Rubiale ya kumbusu mdomoni mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania, Jenni Hermoso isikilizwe upya.Rubiales aliadhibiwa kwa kosa la udhalilishaji kijinsia na kutozwa faini ya dola 10,500 katika kesi ambayo ilikuwa mjadala mkubwa nchini Hispania na […]

The post Wataka kesi ya aliyembusu mchezaji mdomoni isikilizwe upya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Madrid, Hispania
Ofisi ya waendesha mashtaka wa Hispania imetaka kesi ya rais wa zamani wa shirikisho la soka Hispania, Luis Rubiale ya kumbusu mdomoni mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania, Jenni Hermoso isikilizwe upya.
Rubiales aliadhibiwa kwa kosa la udhalilishaji kijinsia na kutozwa faini ya dola 10,500 katika kesi ambayo ilikuwa mjadala mkubwa nchini Hispania na duniani kwa ujumla.
Katika kesi hiyo, Rubiales alishitakiwa kwa kumpiga Jenni busu la mdomoni bila ridhaa yake tukio lililotokea mwaka 2023 mjini Sydney, Australia wakati wa utoaji medali kwa wachezaji wa timu ya Hispania iliyobeba Kombe la Dunia kwa wanawake.
Uamuzi wa mahakama mbali na kumtoza faini Rubiales lakini uliwaachia huru watu wengine watatu waliodaiwa kuwa washirika wa Rubiales ambao pia walidaiwa kutetea na kumshawishi Jenni aseme kwamba alipigwa busu kwa ridhaa yake.
Awali waendesha mashtaka walitaka Rubiales afungwe jela miaka miwili na nusu lakini baada ya adhabu ya faini kutolewa, sasa wamewasilisha rufaa wakitaka kesi isikilizwe upya kwa madai kwamba ushahidi na maswali yao mengi havikufanyiwa kazi.
Katika hoja yao, ofisi ya waendesha mashtaka imedai kwamba faini aliyotozwa Rubiales na fidia ya Euro 3000 alizopewa Jenni vyote ni vya kiwango cha chini mno.
Tukio la busu hilo lilimuweka pagumu Rubiales ambaye pia alifungiwa na Fifa kujihusisha na soka kwa miaka mitatu na ingawa alikata rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo lakini aligonga mwamba.
Rubiales pia alijikuta akishinikizwa kujiuzulu nafasi ya urais katika Shirikisho la Soka Hispania, awali alikataa akidai hana kosa lakini baadaye alikubali baada ya kusakamwa kila kona.
Pamoja na yote, Rubiales ameendelea kusisitiza kwamba kulikuwa na makubaliano kati yake na Jenni kabla ya kumpiga busu hilo lililozua taharuki.

The post Wataka kesi ya aliyembusu mchezaji mdomoni isikilizwe upya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/wataka-kesi-ya-aliyembusu-mchezaji-mdomoni-isikilizwe-upya/feed/ 0
Aliyepigwa busu mdomoni ataka adhabu iwe fundisho https://www.greensports.co.tz/2025/02/24/aliyepigwa-busu-mdomoni-ataka-adhabu-iwe-fundisho/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/24/aliyepigwa-busu-mdomoni-ataka-adhabu-iwe-fundisho/#respond Mon, 24 Feb 2025 18:46:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13048 Madrid, HispaniaMchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso aliyepigwa busu la mdomoni amesema adhabu iliyotolewa kwa Luis Rubiales aliyempiga busu ibaki kuwa somo.Wakati wa utoaji tuzo kwa timu ya wanawake ya Hispania, Jenni alipigwa busu la mdomoni na Rubiales wakati huo akiwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania, tukio ambalo lilizua […]

The post Aliyepigwa busu mdomoni ataka adhabu iwe fundisho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso aliyepigwa busu la mdomoni amesema adhabu iliyotolewa kwa Luis Rubiales aliyempiga busu ibaki kuwa somo.
Wakati wa utoaji tuzo kwa timu ya wanawake ya Hispania, Jenni alipigwa busu la mdomoni na Rubiales wakati huo akiwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania, tukio ambalo lilizua mjadala mkubwa duniani kote.
Hivi karibuni Mahakama Kuu Hispania ilimpa Rubiales adhabu ya faini ya Dola 10,700 kwa kosa la udhalilishaji kijinsia pamoja na marufuku ya kumsogelea Jenni kwa umbali usiozidi mita 200 na kutofanya mazungumzo naye kwa mwaka mmoja.
Rubiales, 47, ambaye alilazimika kujiuzulu nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Hispania, hata hivyo alifutiwa tuhuma za kutumia nguvu na kumlazimisha Jenni aseme kwamba busu hilo alipigwa kwa makubaliano.
Akizungumzia sakata hilo na uamuzi wa mahakama kwa mara ya kwanza, Jenni alitumia mtandao wa Instagram na kusisitiza kwamba uamuzi wa mahakama ni hatua muhimu.
Jenni hata hivyo aliongeza kwa kusema kwamba kwa mazingira yanayowazunguka katika jamii bado kuna mengi yanatakiwa kufanywa.

“Moyo wangu upo kamili pamoja na kila mtu ambaye amekuwa na ataendelea kuwa pamoja nami katika mapambano haya, na sasa yamefikia mwisho,” alisema Jenni.


Ijumaa iliyopita, Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) iliitupa rufaa iliyowasilishwa na Rubiales ya kupinga adhabu ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka mitatu aliyopewa na Fifa.

The post Aliyepigwa busu mdomoni ataka adhabu iwe fundisho first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/24/aliyepigwa-busu-mdomoni-ataka-adhabu-iwe-fundisho/feed/ 0
Aliyembusu mchezaji mdomoni akutwa na hatia https://www.greensports.co.tz/2025/02/20/aliyembusu-mchezaji-mdomoni-akutwa-na-hatia/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/20/aliyembusu-mchezaji-mdomoni-akutwa-na-hatia/#respond Thu, 20 Feb 2025 19:32:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13034 Madrid, HispaniaRais wa zamani wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales amekutwa na hatia katika kesi ya udhalilishaji kijinsia baada ya kumpiga busu la mdomoni mchezaji wa timu ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso.Rubiales alimpiga mchezaji huyo busu lililozua taharuki wakati wa utoaji tuzo mara baada ya Hispania kuibuka mshindi wa fainali za Kombe la […]

The post Aliyembusu mchezaji mdomoni akutwa na hatia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales amekutwa na hatia katika kesi ya udhalilishaji kijinsia baada ya kumpiga busu la mdomoni mchezaji wa timu ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso.
Rubiales alimpiga mchezaji huyo busu lililozua taharuki wakati wa utoaji tuzo mara baada ya Hispania kuibuka mshindi wa fainali za Kombe la Dunia la Wanawake mwaka 2023.
Mahakama Kuu Hispania baada ya kumkuta na hatia katika kosa hilo imetaja adhabu ya faini ya Dola 10,400 kwa kosa hilo lakini imemfutia kosa la kutoa vitisho au ubabe.
Rubiales mara baada ya kutajiwa hukumu hiyo alisema kwamba anajipanga kukata rufaa akiahidi kuendeleza mapambano.
Awali waendesha mashtaka walitaka Rubiales afungwe jela kwa tukio hilo ambalo liliibua mijadala ya udhalilishaji jinsia na haki za wanawake ingawa mwenyewe alidai kwamba Jenni alikubali kupigwa busu.
Jaji mmoja wa mahakama hiyo alisema anauamini ushahidi uliotolewa na Jenni kwa kudai kwamba hakukuwa na makubaliano kati yake na Rubiales kwenye tukio zima la kupigwa busu mdomoni.
Jaji huyo hata hivyo alipinga suala la ubabe au vitisho vya aina yoyote kutumika katika tukio hilo na hivyo hakuona uhalali wowote wa kumpa Rubiales adhabu ya kifungo cha jela.
Rubiales pia ametakiwa kutomsegelea Jenni kwa umbali wa mita 200, pamoja na kutozungumza naye kwa mwaka mmoja.


Wakati kesi ikiendelea, Jenni alisema busu alilopigwa bila ridhaa yake lilimfanya akose raha katika siku ambayo ilikuwa ya furaha ya maisha yake wakati wachezaji wenzake walisema kwamba mwenzao alilia na kujiona mnyonge kwa saa na siku kadhaa.
Katika hatua nyingine Watuhumiwa wengine watatu waliodaiwa kuhusika kwa kutoa vitisho na ushawishi ili suala hilo lisifike mbali wote wamefutiwa mashtaka na kuachiwa huru.
Watuhumiwa hao ni aliyekuwa kocha timu ya wanawake ya Hispania, Jorge Vilda, mkurugenzi wa michezo wa timu ya soka ya wanaume ya Hispania, Albert Luque na mkurugenzi wa masoko wa Shirikisho la Soka Hispania, Ruben Rivera.
Baada ya hukumu kutolewa Chama cha Wanasoka Hispania (AFE) kimesema kwamba hukumu hiyo ni hatua muhimu katika kulinda haki za wanawake na kupigania michezo ambayo haitokuwa na unyanyasaji na ubaguzi.

The post Aliyembusu mchezaji mdomoni akutwa na hatia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/20/aliyembusu-mchezaji-mdomoni-akutwa-na-hatia/feed/ 0
Aliyempiga busu mchezaji adai aliomba kabla https://www.greensports.co.tz/2025/02/11/aliyempiga-busu-mchezaji-adai-aliomba-kabla/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/11/aliyempiga-busu-mchezaji-adai-aliomba-kabla/#respond Tue, 11 Feb 2025 19:13:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13007 Madrid, HispaniaAliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales ameiambia mahakama moja ya Hispania kuwa alimuomba kumpiga busu mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania, Jenni Hermoso kabla ya kufanya tendo hilo.Rubiales aliingia matatani kwa kumpiga busu mdomoni Jenni katika shamrashamra za kutoa tuzo kwa wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania […]

The post Aliyempiga busu mchezaji adai aliomba kabla first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales ameiambia mahakama moja ya Hispania kuwa alimuomba kumpiga busu mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania, Jenni Hermoso kabla ya kufanya tendo hilo.
Rubiales aliingia matatani kwa kumpiga busu mdomoni Jenni katika shamrashamra za kutoa tuzo kwa wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania iliyobeba Kombe la Dunia mwaka 2023.
Sakata hilo lilikuwa mahakamani leo Jumanne ambapo mbali na Rubiales, viongozi wengine watatu wanatuhumiwa kwa kosa la kutaka busu ambalo Rubiales alimpiga Jenni lionekane ni tukio la kawaida na kupuuzwa.
Katika sakata hilo, Rubiales pia anatuhumiwa kwa udhalilishaji wa kijinsia pamoja na wenzake watatu wanaodaiwa kumshawishi, Jenni amtetee Rubiales.
Watuhumiwa hao watatu ni kocha wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake Hispania, Jorge Vilda, mkurugenzi wa zamani wa michezo wa timu ya taifa ya wanaume ya Hispania, Albert Luque na mkurugenzi wa masoko wa Shirikisho la Soka Hispania, Ruben Rivera.
“Nina hakika alinipa ruhusa, kwa wakati ule lilikuwa jambo ambalo ni la kawaida,” alisema Rubiales kuiambia mahakama.
Alipoulizwa kama ana kawaida ya kuwabusu watu kwenye midomo, Rubiales alisema kwamba kwa tukio lilivyokuwa na kutokana na ukweli kwamba amekuwa akimjua Jenni kwa muda mrefu ilimhalalishia kufanya alichokifanya.
Rubiales pia alifafanua kwamba Kombe la Dunia huwa hawashindi kila siku na angeweza kufanya hivyo hata kwa mchezaji wa kiume au hata kwa mmoja wa watoto wake.
Kwa upande wake Jenni alisema hakutoa ruhusa kwa Rubiales kumpiga busu mdomoni wakati Rubiales amekana kufanya kosa lolote na kusisitiza kwamba alichokifanya kilikuwa na ridhaa ya Jenni.
Baada ya tukio la busu hilo, Rubiales alijikuta akisakamwa hadi akalazimika kujiuzulu nafasi ya urais kwenye shirikisho la soka na kufungiwa na Fifa kwa miaka mitatu.
Katika hoja zake za awali, Jenni alisema baada ya kupigwa busu alijiona aliyedharauliwa na kwamba busu hilo lilimtoa katika tukio la furaha ya maisha yake baada ya Hispania kushinda Kombe la Dunia.
Waendesha mashtaka katika shauri hilo wanataka Rubiales afungwe jela kwa miaka miwili na nusu na kutozwa faini ya Dola 51,000 pamoja na kupigwa marufusu kujihusisha na shughuli za michezo.
Kuhusu watuhumiwa wengine watatu, waendesha mashtaka hao wanataka wafungwe jela kwa mwaka mmoja na nusu kwa kila mmoja.

The post Aliyempiga busu mchezaji adai aliomba kabla first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/11/aliyempiga-busu-mchezaji-adai-aliomba-kabla/feed/ 0
Mjengo wa kipa wa Arsenal kupigwa bei https://www.greensports.co.tz/2025/01/01/mjengo-wa-kipa-wa-arsenal-kupigwa-bei/ https://www.greensports.co.tz/2025/01/01/mjengo-wa-kipa-wa-arsenal-kupigwa-bei/#respond Wed, 01 Jan 2025 17:46:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12542 Munich, UjerumaniKipa wa zamani wa Arsenal, Jens Lehmann anadaiwa yuko mbioni kuupiga bei mjengo wake wa kifahari baada ya kuwapo habari za kutibuana na mkewe.Lehman (pichani chini) ambaye pia amewahi kuwa kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani, alikuwa katika kikosi cha Arsenal kilichobeba taji la Ligi Kuu England mwaka 2004 kikiwa chini ya kocha […]

The post Mjengo wa kipa wa Arsenal kupigwa bei first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Kipa wa zamani wa Arsenal, Jens Lehmann anadaiwa yuko mbioni kuupiga bei mjengo wake wa kifahari baada ya kuwapo habari za kutibuana na mkewe.
Lehman (pichani chini) ambaye pia amewahi kuwa kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani, alikuwa katika kikosi cha Arsenal kilichobeba taji la Ligi Kuu England mwaka 2004 kikiwa chini ya kocha Arsene Wenger.
Chanzo kimoja cha habari kimeripoti kuwa kipa huyo amekuwa katika wakati mgumu na mkewe aitwaye Conny ambaye kwa sasa haishi katika mjengo huo.
Lehman mwenye umri wa miaka 55 na Conny mwenye umri wa miaka 52 walifunga ndoa mwaka 1999 lakini ndoa yao imepitia kipindi kigumu na kwa sasa Conny anadaiwa kuwa na mpenzi mwingine ambaye anatajwa kuwa ni kijana mdogo.
Habari zaidi zinadai kwamba kwa kipindi kirefu ndoa ya Lehman na Conny imekuwa katika misukosuko japo wamekuwa wakijitahidi kuonekana mbele ya umma kama kila kitu kipo sawa.
Tangu kuondoka kwa Conny, Lehman amekuwa akiishi peke yake na watoto wao wawili, pamoja na mtoto wa tatu ambaye ni wa Conny katika mahusiano yake ya awali.


Wakala mmoja wa serikali mjini Munich anadaiwa kutangaza mpango wa kupigwa bei kwa mjengo huo ambapo bei yake imetajwa kufikia Pauni 10.7 milioni.
Mjengo huo wa kifahari wenye vyumba sita, una kila kitu cha kwenye nyumba ya kifahari, likiwamo bwawa la kuogelea, sehemu ya mazoezi, sauna na unatazama Ziwa Starnberg la mjini Munich.
Lehmann amekuwa akiandamwa na tatizo la ulevi ambapo aliwahi kukamatwa na polisi mjini Municha kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na kujikuta akinyang’anywa leseni.
Inadaiwa kwamba baadhi ya majirani wamefurahi kusikia habari za kuuzwa kwa mjengo huo kwa kile kinachodaiwa kwamba kipa huyo alikuwa kero mno kwao ikiwamo kugombana nao huku sababu kuu ikitajwa kuwa ni ulevi uliopindukia.
Inadhaniwa kwamba tatizo la ulevi wa Lehman ni sababu mojawapo iliyomfanya Conny aondoke kwenye mjengo huo wa kifahari na kuanza mahusiano na mpenzi wake mpya.

The post Mjengo wa kipa wa Arsenal kupigwa bei first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/01/01/mjengo-wa-kipa-wa-arsenal-kupigwa-bei/feed/ 0
Mbappe asafishwa kesi ya kubaka https://www.greensports.co.tz/2024/12/12/mbappe-asafishwa-kesi-ya-kubaka/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/12/mbappe-asafishwa-kesi-ya-kubaka/#respond Thu, 12 Dec 2024 18:39:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12399 Stockholm, SwedenWaendesha mashitaka wa Sweden leo Alhamisi wametangaza kufuta uchunguzi ulioanzishwa wa tuhuma za kubaka alizokuwa akihusishwa nazo mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe.Kwa mujibu ya taarifa ya waendesha mashitaka hao, uamuzi wa kufuta uchunguzi huo umekuja baada ya kubaini kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuendelea na uchunguzi.Tuhuma hizo zilimhusisha Mbappe ambaye alidaiwa kufanya tukio […]

The post Mbappe asafishwa kesi ya kubaka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Stockholm, Sweden
Waendesha mashitaka wa Sweden leo Alhamisi wametangaza kufuta uchunguzi ulioanzishwa wa tuhuma za kubaka alizokuwa akihusishwa nazo mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe.
Kwa mujibu ya taarifa ya waendesha mashitaka hao, uamuzi wa kufuta uchunguzi huo umekuja baada ya kubaini kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuendelea na uchunguzi.
Tuhuma hizo zilimhusisha Mbappe ambaye alidaiwa kufanya tukio hilo katika hoteli moja ya jijini Stockholm.
Katika tukio hilo ilielezwa kuwa kulikuwa na mtu alihusishwa na tukio la kubaka na wawili waliohusishwa na tukio la udhalilishwaji kijinsia lakini hakujawa na ushahidi wa kutosha kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo na hivyo uchunguzi huo umefutwa.
Taarifa ya waendesha mashitaka hao haikumtaja mtuhumiwa wa kadhia hiyo lakini vyanzo kadhaa vya habari nchini Sweden vilimtaja mshambuliaji huyo wa Real Madrid ambaye alitembelea jiji la Stockholm wakati wa mapumziko mwezi Oktoba.
Chanzo kimoja cha habari kimeeleza kuwa awali wakili wa Mbappe alizipuuza tuhuma hizo akidai kuwa ni za uwongo ingawa baada ya uamuzi wa kufuta uchunguzi, wakili huyo hakutoa taarifa yoyote.
Mbappe ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa, alijiunga na Real Madrid mwanzoni mwa msimu huu akitokea PSG ya Ufaransa.

The post Mbappe asafishwa kesi ya kubaka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/12/mbappe-asafishwa-kesi-ya-kubaka/feed/ 0
Alves amrudishia Baba wa Neymar fedha zake https://www.greensports.co.tz/2024/04/13/alves-amrudishia-baba-wa-neymar-fedha-zake/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/13/alves-amrudishia-baba-wa-neymar-fedha-zake/#respond Sat, 13 Apr 2024 06:54:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10577 Barcelona, HispaniaBeki wa zamani wa klabu za Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Dani Alves ameonesha jeuri ya fedha baada ya kumrudishia baba mzazi wa Neymar Euro 150,000 ambazo alimpa zimsaidie katika kesi ya kubaka inayomkabili.Alves anakabiliwa na kesi ya udhalilishaji kijinsia akidaiwa kubaka msichana katika klabu moja ya usiku mjini Barcelona na tayari […]

The post Alves amrudishia Baba wa Neymar fedha zake first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Beki wa zamani wa klabu za Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Dani Alves ameonesha jeuri ya fedha baada ya kumrudishia baba mzazi wa Neymar Euro 150,000 ambazo alimpa zimsaidie katika kesi ya kubaka inayomkabili.
Alves anakabiliwa na kesi ya udhalilishaji kijinsia akidaiwa kubaka msichana katika klabu moja ya usiku mjini Barcelona na tayari amekutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha jela miaka minne na nusu.
Chanzo kimoja cha habari nchini Ufaransa kupitia wakili wa mchezaji huyo kilithibitisha Alhamisi hii kuwa Alves ambaye kwa sasa yuko nje kwa dhamana amerudisha kiasi hicho cha fedha tangu wiki iliyopita.
Alves, 40, Februari 22 alihukumiwa katika mahakama moja ya juu ya Calatonia baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka msichana huyo, kosa analodaiwa kulifanya usiku mmoja wa Desemba, 2022 baada ya kumnunulia pombe.
Machi 25 mwaka huu Alves alitolewa kwa dhamana baada ya kukidhi masharti ya ikiwamo kutoa kiasi cha Euro 1 milioni huku akiendelea kusikiliza matokeo ya rufaa aliyokata ingawa alisota gerezani miezi 14 tangu kukamatwa kwa kosa linalomkabili.
Alves na Neymar waliwahi kucheza pamoja Barca na timu ya taifa ya Brazil na kwa muda mfupi katika klabu ya PSG na baada ya kukumbwa na mkasa huo, familia ya Neymar kupitia baba yake mzazi iliahidi kumsaidia.
Wakati Alves akipigania kuachiwa huru, waendesha mashtaka wameshikilia msimamo wa kutaka afungwe miaka tisa jela wakati wakili wa msichana anayedaiwa kubakwa anataka mchezaji huyo afungwe miaka 12 jela.
Alves inadaiwa alimbaka msichana huyo baada ya kumnunulia pombe na kumualika katika chumba cha watu maarufu kwenye klabu hiyo ya usiku na kutumia nguvu kufanya kitendo hicho licha ya msichana huyo kumsihi asifanye hivyo lakini hakumsikiliza.

The post Alves amrudishia Baba wa Neymar fedha zake first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/13/alves-amrudishia-baba-wa-neymar-fedha-zake/feed/ 0
Aliyembusu mchezaji adai tatizo ni kuwa mwanaume https://www.greensports.co.tz/2024/04/05/aliyembusu-mchezaji-adai-tatizo-ni-kuwa-mwanaume/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/05/aliyembusu-mchezaji-adai-tatizo-ni-kuwa-mwanaume/#respond Fri, 05 Apr 2024 18:05:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10526 Madrid, HispaniaRais wa zamani wa Shirikisho la Soka Hispania, (RFEF) Luis Rubiales amehoji hatua ya kumshitaki mahakamani kwa kumpiga busu mdomoni mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania, Jenni Hermoso kwamba imekuja kwa sababu yeye ni mwanaume.Rubiales anajiandaa kupanda mahakamani kwa kosa la kumbusu mdomoni mshambuliaji huyo wa Hispania wakati wa hafla ya utoaji tuzo […]

The post Aliyembusu mchezaji adai tatizo ni kuwa mwanaume first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Hispania, (RFEF) Luis Rubiales amehoji hatua ya kumshitaki mahakamani kwa kumpiga busu mdomoni mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania, Jenni Hermoso kwamba imekuja kwa sababu yeye ni mwanaume.
Rubiales anajiandaa kupanda mahakamani kwa kosa la kumbusu mdomoni mshambuliaji huyo wa Hispania wakati wa hafla ya utoaji tuzo baada ya Hispaia kuibwaga England, Agosti mwaka jana na kubeba Kombe la Dunia la Wanawake mjini Sydney, Australia.
Tukio hilo ambalo limeibua mjadala duniani kote lilisababisha Rubiales kujiuzulu nafasi yake ya urais wa RFEF baada ya kushinikizwa kufanya hivyo huku Jenni na wachezaji wenzake wakidai kwamba tukio hilo limewashushia heshima na halikufanyika kwa makubaliano.
Akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni nchini Hispania, Rubiales alikana kufanya kosa lolote na kuongeza kwamba haiwezekani kuumuliza Jenni kuhusu suala hilo badala yake anaulizwa yeye kwa sababu ni mwanaume.

“Mnaweza kuniuliza mimi hilo kwa sababu mimi ni mwanaume,, kwangu mimi hakuna kosa lolote dhidi ya Jenni, kwa yeyote aliyeona picha za tukio lile, siwezi kuelewa iwapo kuna mtu ataliona tukio lile kuwa ni la udhalilishaji kijinsia,” alisema Rubiales.


Rubiales apia alisema kuwa wahanga wa tukio hilo ambalo liligeuka mjadala katika nchi nyingi hasa za Ulaya ni familia yake pamoja na marafiki zake.
Waendesha mashitaka nchini Hispania wanataka Rubiales afungwa miaka miwili na nusu jela kwa makosa mawili anayotuhumiwa ya ubabe akidaiwa alimlazimisha Jenni kumpiga busu pamoja na udhalilishaji kijinsia.
Rubiales ambaye alikuwa beki enzi zake za soka la ushindani, alisema kwamba labda alitakiwa kuwa kimya bila kufurahia baada ya Hispania kushinda bao 1-0 dhidi ya Engla na kubeba Kombe la Dunia.


Ukiachana na sakala hilo, Rubiales pia alikamatwa juzi Jumatano akihusishwa na tuhuma za kupokea rushwa akidaiwa kupewa mgao usio rasmi wakati wa majadiliano ya kuandaa mechi ya Spanish Super Cup nchini Saudi Arabia.
Akizungumzia tuhuma hizo, Rubiales ambaye akaunti zake zimefungiwa alisema kwamba hajawahi kuchukua rushwa katika maisha yake na kuzitaja tuhuma anazohusishwa nazo kuwa ni uwongo.
“Wamefungi akaunti zangu, na kwa sasa siwezi hata kulipia kinywaji, kama kuna uchunguzi unaofanywa basi hapo kuna hisia kwamba sina kosa,” alisema Rubiales.

The post Aliyembusu mchezaji adai tatizo ni kuwa mwanaume first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/05/aliyembusu-mchezaji-adai-tatizo-ni-kuwa-mwanaume/feed/ 0
Aliyembusu mchezaji matatani kwa rushwa https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/aliyembusu-mchezaji-matatani-kwa-rushwa/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/aliyembusu-mchezaji-matatani-kwa-rushwa/#respond Thu, 04 Apr 2024 12:54:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10496 Madrid, HispaniaRais wa zamani wa Shirikisho la Soka Hispania (RFEF) Luis Rubiales anayekabiliwa na kashfa ya kumbusu mdomoni mchezaji wa timu ya taifa, amekamatwa kwa ajili ya uchunguzi unaomhusisha na kashfa ya kupokea rushwa.Rubiales alikamatwa jana Jumatano mara baada ya kuwasili jijini Madrid akitokea Jamhuri ya Dominica ingawa aliachiwa huru muda mfupi baadaye.Habari zinadai kwamba […]

The post Aliyembusu mchezaji matatani kwa rushwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Hispania (RFEF) Luis Rubiales anayekabiliwa na kashfa ya kumbusu mdomoni mchezaji wa timu ya taifa, amekamatwa kwa ajili ya uchunguzi unaomhusisha na kashfa ya kupokea rushwa.
Rubiales alikamatwa jana Jumatano mara baada ya kuwasili jijini Madrid akitokea Jamhuri ya Dominica ingawa aliachiwa huru muda mfupi baadaye.
Habari zinadai kwamba Rubiales alikamatwa kwa tuhuma za kupokea rushwa wakati akiufanyia kazi mpango wa kuandaa mechi ya Spanish Super Cup mjini Riyadh, Saudi Arabia na waendesha mashtaka wanataka afungwe jela miaka miwili na nusu.
Rubiales ambaye amekana kufanya kosa lolote, alikamatwa mara baada ya ndege aliyosafiria kutua Madrid na kupelekwa moja kwa moja polisi kwa gari jeusi akiwa chini ya ulinzi wa maofisa kadhaa.
Chanzo kimoja cha habari Hispania kilieleza kuwa Rubiales anatarajia kufikishwa mahakamani Alhamisi hii huku pia ikidaiwa kwamba wakati akiwa Dominica, polisi waliivamia nyumba yake na kufanya upekuzi.
Ukiachana na sakata hilo jipya la rushwa, Rubiales anakabiliwa na kashfa ya udhalilishaji kijinsia kwa kitendo alichofanya Agosti mwaka jana cha kumbusu mdomoni hadharani mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania, Jenni Hermoso.

Rubiales akionekana mwenye furaha wakati wa hafla za kukabidhiwa tuzo za ushindi wa Kombe la Dunia la Wanawake mjini Sydney, Australia, alimkumbatia kwa nguvu na kumbusu mdomoni Jenni, tukio ambalo lilizua taharuki duniani kote.
Baada ya tukio hilo, Rubiales alijikuta akiandamwa kila kona na kushinikizwa kujiuzulu nafasi yake RFEF jambo ambalo awali alilikataa akidai kulikuwa na makubaliano baina yake na Jenni ingawa baadaye alitangaza kujiuzulu.

The post Aliyembusu mchezaji matatani kwa rushwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/aliyembusu-mchezaji-matatani-kwa-rushwa/feed/ 0